JWTZ anapolalamikia Serikari ya CCM

Easymutant

R I P
Jun 3, 2010
2,564
1,129
Watuwazimatanzania?
Tuko pamoja tangu miaka mitano iliyopita.
Ila kwa mada hii imebidi niweke wazi lila raia mwema katika jamii ya watanzania kuwadhibitishia kuwa mimi binafsi ni mwanajeshi jwtz nimetumikia humu zaidi ya
Miaka 18.
Nina masikitiko makubwa pamoja wanajeshi wenzangu zaidi ya familia 160 ambao ni waanga wa kutimuliwa kwenye kambi ya jwtz sakina arusha kulikofanywa na CCM kitendo ambacho ni kibaya,cha kishenzi,kihuni,ufirahuni,kinyama,dhuluma chenye uvunjifu wa sheria,taratibu,haki na wajibu,chenye kutuondolea thamani kama jeshi na kutuvunjia heshma serikali na kisichovumilika kabisa kwa kutufukuza sakina camp bila kufuata utaratibu kwa madai kuwa eneo ni mali yao,bila kufikiri madhara,kijamii,kiutendaji au kiusalama.
Baada ya kuonekana kulikuwa na adha ya uhaba wa nyumba kwa askari wengi ambapo serikali hii ilishindwa kukidhi haja ya kutekeleza makazi bora kwa wanajeshi ndipo ilipoamriwa jwtz kuishi hapo sakina Arusha.na siyo kama mahali hapa palikuwa na maisha bora kwa askari kama mlishasikia Kibera slams Nairobi pana ahueni.
Kwa ushahidi wa kimazingira CCM inatumia baadhi ya wakubwa maofisa wa vyeo vya juu wenye Double salary slip kwenye chama na serikali,wakati askari tunapata pay slip. Ambao wamekuwa mzigo mkubwa sana kwa jwtz kwa kuleta vikwazo vya kujikwamua kwa jeshi letu kimaendeleo na kuadvance kiteknologia na kusababisha mgawanyo ktk jeshi wa maofsa na askari, na kudai kuwa mwajiriwa halali jwtz ni ofisa na askari ni kibarua.wakati inaeleweka wazi kuwa mtendaji mkuu kijeshi ni askari na mwajibikaji ktk kila idara.
Askari tumefanywa bubu,hatuna sheria ya kutulinda,hakuna pa kuongelea au kulalamika,kila kitu wanatusemea wao na wanayotuwasilishia ni uongo mtupu. Jwtz halitendi haki kwa askari na haya nayaanika wenye uwezo wa kutusaidi myafikishe panapo husika kila jamii y a watanzania ielewe mapungufu haya yasiyovumilika ambayo yamekuwa mzigo kwa askari kwa miaka mingi ili hali serikali inayoongozwa na majizi ccm imeziba masikio na kusinzia kwa kuwatuma hawa vishoka wao wapuuzi wanaotuchafulia jeshi na kutuangamiza askari kwa ten% hata kwenye mavazi.
Ninachotaka kusema tuna hali mbaya na tumefika pabaya kwa sasa na uvumilivu umetushinda na kazi tunafanya basi tu siyo jeshi hili ni volunteer org.
Ukiona umeula jua umeliwa, one day it will be pay day.
Tutaanza wenyewe humuhumu ndo tuende kwa hao bitches ccmnopithecus nyambafffff zenu ddhyuuu.
Crucial cruel massive.?!'-
 
Tafadhari undeni task force kisha muende kwenye public media, jf itawaunga mkono.
 
Tutaanza wenyewe humuhumu ndo tuende kwa hao bitches ccmnopithecus nyambafffff zenu ddhyuuu.
Crucial cruel massive.?!'-

Hii sentensi ya mwisho yamaanisha nini?
 
Mna uhuru wa kuchagua serikali mnayoitaka, itakayowajali kwa kuchagua viongozi wanaotanguliza maslahi ya wananchi kwanza kwa kupiga kura ifikapo hapo 31 Oktoba 2010. Tumieni kura zenu kwa busara!
 
Endeleeni kuvumilia kwani huku uraiani mambo ni mabaya zaidi. Kodi yenu ya pango mnayolipwa ni mshahara wetu wa mwezi. CCM inajitahidi kukufanyeni muwe upande wao na kesi nyingi zinaonyesha wamefanikiwa!
 
Poleni, sasa nguvu zenu elekezeni trhe 31 kwa kuchagua mbivu na si mbichi tena maana haziivi hata usubiri vipi.
 
Umeona dalili za Slaa kuchukua nchi ndo unataka kulipigia jeshi chapuo? Stop that nonsense. Wewe wala huelekei kuitwa askari.
 
kwanini usiache jeshi kama linakushinda badala ya kulalama...njoo mitaani..lakini kumbuka utapoteza fursa ya kupanda daladala bure!
 
kwanini usiache jeshi kama linakushinda badala ya kulalama...njoo mitaani..lakini kumbuka utapoteza fursa ya kupanda daladala bure!

duh.......kazi ipo! maamuzi magumu sana hayo...MAISHA BORA au DALADALA BURE
 
tusifanye utani kama we hapo juu ni mjtz wa kweli basi mtumie ushawishi wenu hapo kambini na kwa marafiki zenu muwaambie watu wamchague slaa mwaka huu, ccm wanawatumia tu nyie wanaofaidi ni akina maormajor, general etc ambao wanalindwa
 
Pole sana mpiganaji wetu. Malalamiko yako hayatofautiani na ya watumisi wengine wa umma na hata askari polisi wanaowalinda wakikoroma usingizini na wake zao. Wanaishi ktk vijumba vya mbavu za mbwa. Lakini bado wanapiga watu mabomu hata wale wanaowatetea. Kulalamika tu hakutoshi. Umma wa wapenda haki wangefurahi sana kuona CCM inabanduliwa madarakani. Tumechokaaaaaa!!!:nono:
 
Back
Top Bottom