Juu ya tuhuma kwa Zitto na kundi lake kutoka kwa Mamuya...

Status
Not open for further replies.
Nini kifanyike basi?tumeshachoka na lawama na shutuma mbalimbali,toeni na solution basi according na katiba
 
Nawasalimia tu wadau. Japo niseme neno tu kuwa wa_CDM turudi kwenye maadili yetu, tukae vikao
tujadiliane tusje ingia ktk mitego ya Nnape na CCm yake. Asanteni.
 
lakini ukizama zaidi huu mgogoro sio mkubwa ila ulichochewa na viongozi wakuu na hapa Mbowe na Slaa hawakosekani kwani walibaki nalo hili huku wakijua madhara yake ni makubwa! sasa wasubiri matokeo yake kwani ccm wamekaa kimya wakitizama wapi kwa kukamata ili wakuze na mwisho wavuruge chama
 
Hiyo nayo ni sehemu ya kugombanisha. Ni mwendelezo uleule wa kuzusha mambo bila aibu. Wagombea katika chama chetu hupendekezwa katika vikao. Niambie ni kikao gani kilinipendekeza na hatimaye nikatemwa.

Ninachojua ni kwamba kuelekea uchaguzi mkuu ujao migogoro mingi itapikwa ndani ya CHADEMA kwa sababu CCM hawana namna ya kushinda uchaguzi ujao zaidi kuhakikisha wanazua migogoro. Wala hili jambo si geni. Walifanikiwa kuutengeneza mgogoro wa NCCR na wakaisambaratisha. Na walitumia njia hiihii wanayotaka kuitumia leo ya kutengeneza makundi mawili, kundi moja lionekane la wazalendo na lingine lionekana la wasaliti. Na lengo ni kwamba ifike mahala kundi linaloonekana ni la wasaliti likimbie chama na hapo mgawanyikao utakuwa umetokea.


Tuwatoe wasiwasi wanachama wa CHADEMA na wapenda mabadiliko kwamba tutayashinda haya mawimbi na tutaingia katika uchaguzi mkuu ujao tukiwa wamoja. Mawimbi ni makali, lakini tumejipanga kuyashinda na tutayashinda. Tutatumia akili zetu zote kuhakikisha kwamba yaliyoikumba NCCR hayatokei tena katika chama chetu. Vikao vya chama ni imara sana na siku zote mambo yamejadiliwa na kuhitimishwa maturely and responsibly.

Dr. ww si muumini wa mambo kujadiliwa kwenye vikao halali vya chama na taratibu kama unavyotaka kuwaaminisha watu. Wewe ni shahidi jinsi gani baazi ya wapenzi na wapenda maendeleo ya CDM nikiwemo mimi tulivyokuwa tuking´aka humu jamvini kuhusu baazi ya wanachadema hususani Zitto alivyokuwa akitoa matamko hatarishi kwa mustakabali wa maendeleo ya Chama nje ya utaratibu na vikao vya chama,mfano lile la kutangaza kugombbea uraisi 2015 (Huu ndio utaratibu na vikao vya chama vinavyomwongoza Zitto?). Uliingia jamvini na kutetea kwa nguvu zote ukiimba na kumalizia na beti ya mwisho ¨Huu ndio ukuaji wa demokrasia ndani ya chama ¨.

Leo hii vijana wamefunguka humu jamvini umesahau ubeti wa mwishi ¨Huu ndio ukuaji wa demokrasia ndani ya chama¨. Kukaa kimya ni uerevu pia ,leo haya yamefika humu kwa vijana wako kuwavua nguo viongozi wewe na Zitto kwa kutokusoma alama za nyakati. Haya mnayoandika humu jamvini ndio mnazidi kujivua nguo bila sababu ya msingi.
 
lakini ukizama zaidi huu mgogoro sio mkubwa ila ulichochewa na viongozi wakuu na hapa Mbowe na Slaa hawakosekani kwani walibaki nalo hili huku wakijua madhara yake ni makubwa! sasa wasubiri matokeo yake kwani ccm wamekaa kimya wakitizama wapi kwa kukamata ili wakuze na mwisho wavuruge chama

[h=1]Huu mgogoro ni mkubwa, bonya hapa:-
Udhibitisho wa kazi maalumu ya ben saanane na hujuma za dr.slaa kwenye siasa za juliana shonza[/h]
 
CHADEMA ipo juu.
hao wanaochafua chama na kutaka kitawanyike anakusiwe na umoja watatawanyika wao, na watashindwa wao sisi tunaojua kuwa CHADEMA Ni mkombozi wa watanzania tunazidi kusonga mbele na tutahakikisha hakuna kitakachozuia ushindi.

Madamu masalia tushawajua na janja yenu tumeijua humtutenganishi ng'oo!
 
By Exaud Mamuya Nawasalimu sana ndugu zangu hapa jamvini,

Kwa kweli tokea asubuhi ya leo nimekuwa nikipitia michango mbalimbali ya wana janvi hapa na kuona ni jinsi gani ambavyo njia ya muongo huwa ni fupi.

Kwanza kabisa napenda kumwambia naibu katibu wangu mkuu ya kwamba asifikiri vijana wa miaka hii ni sawa na wale wa mfumo wa chama kimoja kipindi kile! Ameweza kujitutumua kwa kujaribu kujitetea pasipo kujibu hoja ya msingi.

Bwana Zitto Zuberi Kabwe ulichokifanya hapa ni kujaribu kuwaonyesha wana jamvi ya kuwa hatufahamiani na kuonyesha ya kwamba tunatumika na baadhi ya watu flani pasipo kujibu hoja ya msingi ya kwamba WEWE NI MFADHILI WA KIKUNDI CHA WAASI WA CHADEMA!

Bwana Zitto labda nikukumbushe na nadhani utakuwa unakumbuka vizuri siku ambayo tulikuwa wote pale MOUNT MERU HOTEL Arusha pamoja na RUGE wa Clouse Radio, Shyrose Bhanji na baada ya kuachana mlielekea NAURA SPRING HOTEL kwa ajili ya tamasha la miss Arusha na baada ya pale tulipanga kukutana lakini ulipokuja kuniuliza niko wapi nilikwambia niko TRIPLE A Club na ukaniambia umechoka unaenda kupumzika so tuonane kesho yake lakini kesho yake hatukutafutana tena. Sasa unaposema hunifahamu mimi nakushangaa sana kamanda!

Bwana Zitto ikumbukwe vizuri ya kwamba wewe ndo uliyekuwa UKICHOCHEA MGOGORO WA MADIWANI kwa lengo la kumdhoofisha mh Lema kisiasa na mipango na mikakati yote ilikuwa ikifanywa baina yangu mimi, wewe Dr Kitila Mkumbo pamoja na madiwani waliofukuzwa Chadema.

Wewe ndio uliokuwa ukiwapa moyo madiwani wa Chadema kwamba wagome mpaka dakika za mwisho na wasikubali kuomba msamaha hata mbele ya kukao cha ngazi ya juu cha chama yaani KAMATI KUU na hata ulipokuwa ndani ya kikao cha kamati kuu na madiwani wale wapo nje ya ukumbi wa kikao ulikuwa ukiwasiliana nao kwa sms ambazo walinifowardia baadae.

Nilikubali kukusikiliza kama kiongozi wangu wa juu wa chama na kutekeleza yale yote ya usaliti niliyoyafanya na hata ndiyo maana mara nyingi nilikuwa Dar nikikutana na Mchange, Mwampamba, Juliana Shonza, Gwakisa, Festo Sanga kwa ajili ya kupanga mikakati thabiti ya kuwadhoofisha viongozi wakuu wapigania ukweli ndani ya chama sana sana mh Mbowe na Dr Slaa kwa lengo la kuwagombanisha na kupata upenyo wa wewe kuwa juu kisiasa zaidi yao ( divide and rule).

Na hata Dr Kitila mkumbo alikuwa akitupa kila kitu ili kufanyikisha mkakati wa kuwafanya madiwani wa Arusha wawe juu ya mh Lema zaidi zaidi diwani Estomih Mala awe na nguvu kisiasa zaidi ya Lema.

Na hata report ya uchunguzi wa mgogoro wa madiwani wa Arusha ambao waliokuja kuchunguza alikuwa ni Dr Kitila Mkumbo na Advocate Mabere Marando pamoja na Ester iliwafikia madiwani wa chadema hata kabla ya kufikishwa kamati kuu na ndio maana madiwani wale pamoja na mimi tulikuwa tukilalamika kuna baadhi ya pages ambazo zimenyofolewa zilizokuwa zikionyesha hakuna rushwa yeyote madiwani waliyokutwa nayo. Lakini hii ni kutokana na kupata report kabla ya kuifikisha kwa kikao kilichoazimia kuunda kamati ya kuitafuta na kuiwasilisha.

Hivyo basi pasipo kuwa na kumumunya maneno ni kwamba msaliti namba moja ndani ya Chadema ni Zitto Zuberi Kabwe na hapa hawezi kupinga ukufuatilia kwenye thread niliyoandika na kufuatilia utetezi wake utaona jinsi ambavyo ndio yeye amekuwa akiwafadhili viajana hawa wasaliti ( masalia) kwa kwa kujikita kueneza propaganda za zinazotolewa na ccm za UDINI, UKABILA na UKANDA.

Rai yangu kwako bwana Zitto ni kwamba CHADEMA ni chama kinachopigania HAKI, USAWA na UKWELI, hivyo basi nakusihi urudi katika mstari ulionyooka na uungane na wapigania USAWA wenzako na uachane na njama zote za USALITI.

Na kwa tahadhari tu ni kwamba mimi tayari najihesabu TAYARI NIMESHAKUFA. Hivyo basi vitisho vyote mnavyonitumia ni kwamba haviniogopeshi hata kidogo maana katika kupigania UKWELI na HAKI najua lazima kuna kufa na mimi sintokuwa wa kwanza so niko tayari kufa bro!

Nawasilisha.

Hapo penye RED vipi? Ester..? Ester yupi?
 
Niliisha yasema haya
Chadema kila mchaga anajiona yeye ni mwenyekiti wa taifa
Kama wewe sio mchaga basi ujue hapo wanakutumia kupata wafuasi tu .
Hawa wote wanaomtukana Zito hapa wamejiunga na chadema juzi juzi tu na hata historia ya chadema ilianzia wapi hawaijui. leo hii wanakuja hapa kumtukana mtu aliekipigania chama toka akiwa chuo kikuu na ukiangalia kwa undani utagundua sababu kuu ni kuwa jamaa ni muisilamu na sio mchaga hivyo hatakiwi kwenye chama.
Mie sio mtabiri lakini nawakikishieni hiki chama kimejengwa kwa msingi wa barafu na jua litakapowaka kitabomoka kama vile kimepigwa na bomu la atomiki kwa sababu hakitabaki kitu hata mbowe mwenye atakimbia sijui nani atabaki.
Chadema na uamsho kuna tofauti gani
WOTE WANATOKA POVU KWA MITUSI NA JAZBA tofauti yao ni kuwa chadema ni wakristo wa kichaga na Uamsho ni waisilamu wa kipemba

Sikujua uko so cheap kihivyo kweli usilolijua
 
Haki sawa's Avatar
Senior Member Array

Join Date : 3rd October 2007
Posts : 212

Rep Power : 615

Likes Received
152
Likes Given
0

Default Mpango wa kuhujumu M4C na CHADEMA huu hapa - chukueni hatua..

Leo tarehe 29.08.2012 niko hapa maeneo ya Lumumba Kariakoo , kuna rafiki yangu alinialika mlo wa mchana katika moja ya migahawa ya hapa Lumumba na kuwa kwangu hapa niomekutana na tukio ambalo nimeamua niliweke hadharani kabla halijatokea kwani naamini kabisa kuwa lengo la mpango huu ni kuendelea kutugawa taifa kwa misingi ya Ukabila jambo ambalo sikubaliani nalo kama ambavyo ninapinga kugawa watanzania kwa misingi ya udini .

Mwigulu Nchemba , juzi jumatatu amechapisha tisheti zenye maandishi ya M4C – na ameweka maana kwenye hizo tisheti ambazo bado hazijaanza kugawanywa kuwa ni Movement 4 Chagga na ameweka maandishi makubwa kuwa changia Movement 4 Chagga (M4C), Zipo na zitaanza kugawanywa muda wowote .

Zoezi hili linaendena sambamba na operation ya Mwigulu ya kwenda Igunga eti kuelezea nini kilitokea mahakamani kwa wana Igunga , ziara hii imepangwa kuanza siku ya Jumamosi kwani alikuwa anasubiria FUSSO waliyonunua kwa shilingi milioni arobaini na tisa (49,000,000) na kuitengeneza kama za CDM ikamilike na walinunua vifaa Mlimani City tayari tangu wiki iliyopita.

Lengo la kuweka hapa ni kuwajulisha CDM wajue kuwa kuna mipango hiyo tayari imepangwa na inaendelea kutekelezwa , chukueni hatua .Aidha kuna vijana wenu watatu majina leo nayahifadhi wanafanya vikao vingi sana na Mwigulu na wa mwisho alipofika kwake wiki iliyopita alipewa shilingi laki nane , mara ya kwanza alipewa shilingi milioni tatu na huyu ametangaza rasmi kuwa atajiunga na CCM wakati wowote – fuatilieni waliogombea Bavicha na kushindwa na hata mmoja aliweza kushinda ila anawahujumu nyie CDM.

Sikubaliani na mipango ya kuligawa taifa kwa misingi ya Udini na Ukabila hivyo nitaipinga sana hata kama mtanijua LIWALO NA LIWE.

NI MIMI MPIGA FILIMBI-

Updates za leo jumapili tarehe 02.09.2012

Baada ya taarifa hii kurushwa hapa na mpango mzima kuwekwa hadharani , Mwigulu ameingia kwenye mgogoro mkubwa wa kifamilia na amefikia hatua ya kuwafukuza watoto wa kike aliokuwa anakaa nao nyumbani kwake Basihaya kuwa kuna nyaraka za vikao hazionekani na anaamini kuwa waliotoa taarifa hizi ni pamoja na wao. Hawa ni wale aliowatoa kijijini kwake kwa hoja kuwa atawasaidia kusoma lakini akawa anawafanya kama wake zake pindi mkewe akiwa hayupo .

Mkewe Mwigulu ni Mchagga wa Machame.


Kitendo cha kuwafukuza kikazua mambo mengine makubwa kati yake na watoto hao yakaibuliwa kwani wamemweleza Mkewe ambaye alikuwa msimamizi wa sensa mkoa wa Dodoma kuhusiana na jinsi alivyokuwa akiwalazimisha kufanya nao ngono kipindi akiwa hayupo na hali nyumbani imechafuka .
Kuhusu nyaraka anazodai kuwa zimeondolewa nyumbani kwake ni pamoja na zile za vikao kama bajeti za chama na nyinginezo mbalimbali za vikao mbalimbali vya CC ya CCM , NI lini zitawekwa hadharani nafikiri ni suala la muda tuu.

Fusso mpaka sasa bado ipo Tabata Dampo , inasubirio nini haijajulikana bado, kijana wake aliyemvisha zile t.shirts yaani James naye wamegombana sana kama ilivyo kwa wale vijana watatu wa CDM ambao walikuwa na mpango wa kujiunga na CCM sasa anawaona kama ni mashushushu waliotumwa kwenda kumchimba kwani amewaeleza kuwa haiwezekani kiasi cha pesa alichowapa kiweze kuandikwa bila wao kushiriki katika kutoa taarifa kwani hilo walifanya na mtu mmoja mmoja .

Kwa leo naishia hapo.

Last edited by Haki sawa; 2nd September 2012 at 10:21. Reason: up dates
 
[h=1]Huu mgogoro ni mkubwa, bonya hapa:-
Udhibitisho wa kazi maalumu ya ben saanane na hujuma za dr.slaa kwenye siasa za juliana shonza[/h]

hiyo thread ya huyo juliana inaonekana ndo kombora la nyuklia.sasa haifunguki ni kwangu tu ama pote.Nahisi kama vile wameifunga.
 
nyabhingi,

I expect him to provide evidence to support his careless assertion. I respect him on this forum and elsewhere, but his standard is steadily falling to gutter level. So I will consider his evidence more reliable. I'm out for now!
Sidhani kuwa anaweza kuendelea kujibu haya. I knew this day was coming.

Kuna wakati huwa najiuliza kwanini wanasiasa wanakuwa wabinafsi namna hii. Maana ni sawa na kukata tawi alilokalia. CDM ikiweza kuchukua hatua kwa wasaliti wa chama kama hawa, ndipo nitakapoamini kuwa ni chama mahiri na kina uwezo wa kulinda na kutetea maslahi ya wananchi. Jambo hili ni dogo kwa taasisi inayoaminika kama Chadema, na ni muhimu kwao kuonyesha kuwa wanaweza kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Taifa endapo wataaminiwa kushika dola. Vinginevyo, wananchi wanaweza kukata tamaa na chama hiki mapema sana kabla ya uchaguzi mkuu ujao (2015).

Kila la kheri CDM. Tunasubiri kuona hatua zinazodhihirisha uwezo wenu.
 
Afadhali haya yatokee sasa, Kama mnayo mengine tuwekeeni hapa tujue kinachoendelea nyuma ya pazia. Mwisho wa haya utakuwa mzuri sana kwa chama. Ila pia naisifu inteligensia ya chama kwa kuwa na pandikizi hata kwenye usaliti.

Respect Ben, you ve got a brain bro.
 
Mkuu hio ndio facts... CCM kuna kitu wanakosea, nadhani intel zao zimeanza either kuwa dhaifu au zinawafanyizia wenyewe. wait october na november 2013 utaona wao sasa wanavurumushana

I THINK CCM NA TIMU YAO NDOGO NDANI YA CHADEMA WANA-UNDERESTIMATE POWER YA NEW THINKING AND NEW BLOOD. THEY NEED TO GO BACK TO CHINA AND GET BACK WITH SOMETHING ELSE

Wana uwezo mdogo sana, hata fikra wanahitaji msaada tuta.Sasa kam wanachapisha t-shirt zimeandikwa m4C wanaiita movement for Chaga, bado hakuan amtu ktk CCM ameona kuwa slandering ni ujinga na haramu pia kuwadhalilidha wananchi na haki yao ya kuona upinzani wenye nguvu ili kule ta ushidani. ujue kuna shida CCM hata kutoa tender kwa haki zaidi ya kusoma tuu document ado watendaji wao ni wa hovyo sana.
 
ama kweli mficha huchi hazai, shame on u ZZK nashindwa kuamini mtu unaejpambanua km mwanasiasa kijana machachari kumbe mchawi mkubwa.
ondokeni wote with ur co muende huko CHAUMMA mkafie huko, msomi mkubwa unakuwa msaliti???? ama kweli vijana kuwa viongozi bado sana, tulikuwa tunawaamini vijana kumbe ndio hao wachawi na wazandiki wakubwa.
Mkuu Zitto & co mmejimaliza kaka, thanx GoD leo nimemtamtambua muhuni TUNTEMENKE, ama kweli dunia haina siri!!!
Unakuja mpk kumuhujum na kamanda Lema?? kweli ww ni muuaji wa demokrasia, afadhari rangi yako imejulikana.
 
Huhitaji kumwamini Ben na wala hulazimishwi kumwamini.La muhimu hapa, ni kwamba hisia zetu zinaelekea kuwa kweli kuwa zitto wa 2005-2009 na wa 2010-2012 ni mwingine kabisa.

Young man, the more things change, the more they remain the same. Ww hisia zimeanza kuwa kweli leo kuhusiana na Zitto, wenzio hisia zilianza kuwa kweli toka 2002, wakat Zitto alipokuwa Speaker wa Daruso-UDSM. Unavyompenda Ben ghafla ghafla, ndivyo watu walivyompenda Zitto mwanzon, walimpenda bila kuhoji maswali magum. Read the lines, read btn the lines, and read beyond the lines.
 
Wassira, Nape, Mwigulu, Kina na wengineo sasa naona mnagonga glass kazi nzuri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom