Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mahakama ya kadhi inapingwa (we side B) kwasababu kuu mbili tu:-

(a) Kuingizwa kwenye katiba ya nchi, kutamaanisha kwamba masuala ya taasisi za kidini yanaingizwa moja kwa moja katika ideology ya Serikali yetu.

(b) Uendeshaji wa Mahakama hiyo kuwa chini ya Serikali, yaani kadhi Mkuu, wasaidizi wake na wafanyakazi wengine kuwa watumishi wa Serikali yaani walipwe mishahara, marupurupu ya nyumba, usafiri, ulinzi nk pia gharama za ujenzi wa majengo na ununuzi wa samani. Bila gharama hizo ni kubwa kubebwa na wananchi wa ambao baadhi yao si waislamu (hawafaidiki na mahakama hiyo).

Logic: Waislam waanzishe hiyo mahakama ya kadhi bila kuihusisha Serikali na wao wawe responsible kuiendesha. Mpeni Kikwete break, hali imeshakuwa mbaya.
 
Mahakama ya kadhi inapingwa (we side B) kwasababu kuu mbili tu:-

(a) Kuingizwa kwenye katiba ya nchi, kutamaanisha kwamba masuala ya taasisi za kidini yanaingizwa moja kwa moja katika ideology ya Serikali yetu.

(b) Uendeshaji wa Mahakama hiyo kuwa chini ya Serikali, yaani kadhi Mkuu, wasaidizi wake na wafanyakazi wengine kuwa watumishi wa Serikali yaani walipwe mishahara, marupurupu ya nyumba, usafiri, ulinzi nk pia gharama za ujenzi wa majengo na ununuzi wa samani. Bila gharama hizo ni kubwa kubebwa na wananchi wa ambao baadhi yao si waislamu (hawafaidiki na mahakama hiyo).

Logic: Waislam waanzishe hiyo mahakama ya kadhi bila kuihusisha Serikali na wao wawe responsible kuiendesha. Mpeni Kikwete break, hali imeshakuwa mbaya.

Mkuu ulicho sema ni kweli tupu.

Lakini hapo hapo inakupasa kukumbuka BAKWATA ni chombo cha Serikali na wafanyakazi na ghara nyingi zaidi zinalipwa na hiyo Serikali kuliko waisilamu wenyewe.
Sasa having a KADHI court kwa mtazomo harisi kutaifuta Bakwata na hilo ndilo waisilamu wanalolitaka,na BAHATI MBAYA zaidi sio jambo linalotakiwa na Serikali pamoja na wengine kwa mambo yalifichika (historia)
 
Hapa umetumia mifano mibaya; Mahakama za Kadhi zilikuwepo katika Palestina kabla ya Taifa la Israeli kuundwa 1948. Eneo linalokaliwa sasa na Israeli lilikuwa likikaliwa na waarabu na kwa miaka mingi likiendeshwa kwa sheria za Kiislamu. Hivyo Israeli haikutengeneza uwepo wa Mahakama za Kadhi bali ulizikuta na kuzitambua na kuziwekea mipaka yake.

India vivyo hivyo, Mahakama za Kadhi zilikuwepo kabla ya kuundwa kwa Taifa la India tunavyolifahamu sasa na kabla ya kutengana kwa India na Pakistani. Kuna maeneo ya India ambayo yalikuwa na Waislamu wengi (Pakistani ya wakati huo na majimbo yanayokaribiana nayo kama Kashmir inayogombewa). Waingereza walipoenda huko walizikuta na waliziacha zifanye kazi zake japo kama Waisraeli walizipunguzia nguvu. Baada ya kuundwa kwa India ya sasa, Wahindi waliamua kuwa secular state na hivyo walizipiga marufuku na hata hivi sasa haziko kisheria lakini maamuzi yake katika ngazi za chini yanaachiliwa kusimama.

Afrika ya Kusini na kwenyewe zimetambulikana kwa sababu moja kubwa tu nayo ni kuwa kulikuwa na jamii ya Waislamu kwenye maeneo machache ambao walitaka kuongozwa Kiislamu na baada ya uundwaji wa Katiba mpya ya Afrika ya Kusini vitu vingi viliruhusiwa na hivyo kuifanya Katiba yao kuwa one of the most liberal in the world. Wa South wanafahama juu ya kunyanyaswa na kutengwa na wamejitahidi sana kuondoa kitu chochote kinachomfanya mtu awe duni.

Kwa Kenya nao ni mfano mbaya kwa sababu Mombasa, Lamu, Malindi, Mijikenda n.k na Ukanda wa Pwani ya Afrika ya Mashariki (Tanga, Dar-es-Salaam, Bagamoyo, Kilwa na visiwa vya Zanzibar) ulikuwa na utawala wa Kiislamu kwa miaka mingi. Na Mahakama za Kadhi zilikuwepo kabla hata ya Mjerumani kuja, na zilikuwa zimezama hata sehemu za ndani ambako Uislamu ulikuwa umeenea. HIvyo Mahakama hizo kama ilivyokuwa India na Israeli hazikuanzishwa kwa ruhusa ya Muingereza, zilikubaliwa kuendelea kwani zilikuwepo tayari.

Na hii ndiyo hoja kubwa kwa WAislamu kuwa Mahakama za Kadhi siyo kitu kigeni katika Afrika ya Mashariki, zimewahi kuwepo, na zimewahi kuwepo wakati wa wamisionary wakifanya kazi. Historia inaonesha kuliwahi kutokea migongano lakini leo hii tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuzirudisha mahakama hizi bila kuwa na matatizo yeyote yale.

Hii mifano niliitoa kwako. Hoja yangu si nani alianzisha hizo mahakama bali ni kwa nini zilikubalika katika mazingira hayo. Ukiangalia nchi zote hizi zina significant majority wa dini moja kiasi cha kutoona kuwepo kwa mahakama hizi kama tishio kwa namna walivyotaka wao kuendesha nchi zao. Katika nchi zote hizo waislamu ni minority kwa idadi na kwa nguvu za kiutawala. Hali hii ndiyo iliyokuwepo hata Afrika Mashariki kwa sababu mtawala alijua kuwa sheria ya mwisho itakayotumika ni ile inayoendana na mtazamo na values zake. Si kwa sababu ya wingi wa waislamu Malindi, Lamu na kwingineko bali ni wingi wa wakristu sehemu nyingine za nchi na ukweli kuwa wao ndio waliokuwa na nguvu ndiko kulikoweza na kunakofanya hizi mahakama zikubalike. Hivyo hivyo katika nchi za kiislamu ambako wanajua hawana namna ya kuzidhibiti kutokana na nguvu za dola, hizi mahakama zimekataliwa kwa kuhofia kuwa kuwepo kwake kutawapeleka kwenye theocracy wakati wao (watawala) wanaelemea secularism. Hapa kwetu tuko katika kundi la pili. Kwa vile ni tumeamua kuwa nchi ya demokrasia na si koloni tena uwezekano wa dini moja kuikandamiza nyingine kupitia wingi wao upo. Ndiyo maana wahenga wetu wakaamua kwa makusudi kutenganisha dini na serikali kuanzia kwenye masuala ya elimu hadi ya sheria. Kusema kuwa mahakama hii itawahusu waislamu ni kuwa disingeneous maana hata definition ya nani ni muislamu ina utata. Ni hivi karibuni tu huko Sinza waislamu na wakristu wamegombea kumzika marehemu huku kila mmoja akidai kuwa alikuwa muumini wa dini yake! Sasa itakuwaje katika masuala ya haki?

Mimi naamini kuwa hizi mahakama zinaweza kuwepo tu zikiwa nje ya mfumo wa serikali. Supremacy ya secular serikali ni lazima ilindwe kwa namna yeyote. Ni kujidanganya kuwa hazitajihusisha na masuala ya jinai. Hivyo hivyo kwenye madai ya kuwa zitawahusu waislamu tu.Katika nchi ambayo tumechanganyikana kwa kiasi kikubwa hii itakuwa ngumu kutekeleza.

Tukumbuke hadithi ya ngamia aliyeomba kuingiza kidole tu kwenye hema. Ndugu zetu waislamu hawajaeleza kwa undani kwa nini wanaona sheria na mfumo wa sasa hauwatoshelezi wakati talaka za kiislamu n.k. zinatambulika!

Tusijaribu kukarabati kitu ambacho hakijavunjika. Tutakuja juta.
 
labda kwa kuongezea tu hili la kwako,Qurani ni MOJA tu.
Sasa ukiwa Shia,Sunn na kadhalika utafata hiyo hiyo(imekua ikifatwa toka enzi na enzi na sheria zake hazibadiliki)
Tatizo lina kuja kwenye Tafsili,sasa hapo ndio inakuja umuhimu wa kuwa na KADHI ambaye ni Mjuzi wa sheria hizo za Qurani.

Itakuwa vigumu kwa huyu Kadhi kuonekana kuwa neutral na wale wa madhehebu mengine. Bakwata hawalipwi mshahara na serikali bado wanaonekana ni vibaraka wao sembuse huyo Kadhi?
 
Haya ndugu yangu,

Hata mimi pia nilikua mkristu (lkn sio RC) na sikufahamu kama mahakama hizo zipo.

Alafu........ unataka nikuamini wewe (unaye tumia nick name hapa) au Mbunge aliye zungumza bungeni?

Huna sababu ya kuniamini mimi lakini umeshindwaje/unashindwa nini kutupa jina la hizo mahakama?
 
Mimi naamini kuwa hizi mahakama zinaweza kuwepo tu zikiwa nje ya mfumo wa serikali. Supremacy ya secular serikali ni lazima ilindwe kwa namna yeyote.

Ninauunga mkono huu msimamo kwa 100%,

However, baada ya kuusoma kwa makini sana huu mjadala, ninaamini kwamba wanaodai hii Kadhi's thing nina wasi wasi kuwa wana tatizo kubwa zaidi kuliko madai yao, tatizo lao ni more than Mahakama ya Kadhi kwa hiyo ni afadhali wangesema tu exactly tatizo lao ni nini hasa kuliko kujificha nyuma ya Kadhi's thing, kwa sababu ni celar kabisa kuwa hata wakipewa hiyo mahakama bado kuna siku watakuja na kutudai mengine zaidi,

Kwa sababu mjadala wa wao kudai hiyo kitu unatia wasi wasi on their side wanapolazimisha mifano ya dini zingne kuwa hiyo mahakama, kitu ambacho ukweli ni kwamba hakipo, zaidi ya kina Milingo mimi hata sikujua kuwa Katholic Church wana mahakama, kwa hiyo kudai kwamba mbona Wakristo wanayo pia, kwa kweli ni very cheap argument, kama sio none argument kabisaa,

Wa-Tanzania, tujifunze kuheshimu separation ya State na Religions, Spikia asingeruhusu huu mjadala kufika bungeni, kwa sababu experience iko very clear kuwa mijadala ya namana hii kwenye national level huwa inaishia kuwagwawa wananchi, serikali yetu should stay awaya na this kind of mijadala na kawapa maneno yaliyo clear wanaodai kuwa serikali yetu haiwezi kujihusisha na this kind of debate, na kwamba serikali yetu inaweza kutambua ndoa tu za hiyo mahakama kama na sio anything else,

Kama wataanzisha au hawataanzisha, it is none of serikali yetu businness, under demokrasia makini ni haki yao kuanzisha hizo mahakama lakini serikali yetu haiwajibiki kabisa kuzitambua hizo makahama na serikali should stay away na this kind of debate.

Mkuu Wangu Matuta,

Hoja zako ni nzuri sana na ni kweli under demokrasia ni haki yako kuanzisha hizo mahakama zako za Kadhi, lakini sio haki yako kuilazimisha serikali kuzitambua hizo kadhi's stuff, au kutulazimsha wananchi wote kuwa involved na process ya uanzishaji wake, nendeni muanzishe na muendelee nazo ila keep us yaani society at large out of it!

Thanks.
 
Ninauunga mkono huu msimamo kwa 100%,

However, baada ya kuusoma kwa makini sana huu mjadala, ninaamini kwamba wanaodai hii Kadhi's thing nina wasi wasi kuwa wana tatizo kubwa zaidi kuliko madai yao, tatizo lao ni more than Mahakama ya Kadhi kwa hiyo ni afadhali wangesema tu exactly tatizo lao ni nini hasa kuliko kujificha nyuma ya Kadhi's thing, kwa sababu ni celar kabisa kuwa hata wakipewa hiyo mahakama bado kuna siku watakuja na kutudai mengine zaidi,

Kwa sababu mjadala wa wao kudai hiyo kitu unatia wasi wasi on their side wanapolazimisha mifano ya dini zingne kuwa hiyo mahakama, kitu ambacho ukweli ni kwamba hakipo, zaidi ya kina Milingo mimi hata sikujua kuwa Katholic Church wana mahakama, kwa hiyo kudai kwamba mbona Wakristo wanayo pia, kwa kweli ni very cheap argument, kama sio none argument kabisaa,

Wa-Tanzania, tujifunze kuheshimu separation ya State na Religions, Spikia asingeruhusu huu mjadala kufika bungeni, kwa sababu experience iko very clear kuwa mijadala ya namana hii kwenye national level huwa inaishia kuwagwawa wananchi, serikali yetu should stay awaya na this kind of mijadala na kawapa maneno yaliyo clear wanaodai kuwa serikali yetu haiwezi kujihusisha na this kind of debate, na kwamba serikali yetu inaweza kutambua ndoa tu za hiyo mahakama kama na sio anything else,

Kama wataanzisha au hawataanzisha, it is none of serikali yetu businness, under demokrasia makini ni haki yao kuanzisha hizo mahakama lakini serikali yetu haiwajibiki kabisa kuzitambua hizo makahama na serikali should stay away na this kind of debate.

Mkuu Wangu Matuta,

Hoja zako ni nzuri sana na ni kweli under demokrasia ni hali yako kuanzisha hizo mahakama zako za Kadhi, lakini sio haki yako kuilazimisha serikali kuzitambua hizo kadhi's stuff, au kutulazimsha wananchi wote kuwa involved na process ya uanzishaji wake, nendeni muanzishe na muendelee nazo ila keep us yaani society at large out of it!

Thanks.

.....Hiyo hapo juu imetulia babake
 
Kadhi kwelikweli, nahisi kunawatu katika dini wanaona mambo hayaendi mpaka wapate nguvu ya ziada,ila sidhani kama serikali imeshindwa kazi yake maana kama ni muongozo wa waislam si quran inatosha na mashehe sasa hiyo mahakama ni watu wanataka kuanzisha vitega uchumi maana inaonekana mahakama zinaongoza kwa rushwa so nadhani njaa zinasumbua watu.labda tu! wangesema ni kesi ipi ambayo imeshindwa kutatuliwa na serikari? Waamie uarabuni basi.


Ustaadh,

Hoja zako zote zimenivunja mbavu...wallah.


Cheers...!
 
Jamani haya masuala ya dini kamwe hamtaelewana!

Kweli kabisa. Ebu fikiria, Mahakama ya kadhi inahusi masuala ya kidini. Serikali haina dini, halafu mtu atoke aende akaiombe serikali, ambayo haina dini, ianzishe mahakama ya kidini, itawezekana kweli?
kwani walipoanzisha bakwata walikwenda kuomba ruhusa serikalini? Au hiyo mahakama haiwi mpaka serikali iruhusu? Mi nilidhani kuwa kama suala haliihusu serikali, ni suala rahisi la watu kukaa na kujianzisha mahakama yao waendelee na ustaarabu wao
 
Siku zote, kumekuwa na kesi zinazohusu mambo ya kiislam, na huwa zinatatuliwa bila hata wasiwasi kwasababu kinachotakiwa ni watu kusoma tu, mambo yenyewe yanayolalamikiwa huwa ni machache sana, yanahitaji mashehe.hata hivyo, katika kesi kama hizo, mashehe au viongozi wa kiislam huwa included katika kutafsiri quran na kusaidia kutoa maamuzi. kama kuna kesi yoyote inayohusu mambo ya kiislam(ndoa na mirathi ndo wanacholalamikia), kilichowahi kuamuliwa kinyume na Quran, ongeeni hapa. hakuna hata kesi moja iliyowahi kuamuliwa kinyume na Quran, zote huwa zinazingatia na kila problem katika mambo hayo zilishakuwa exhausted na kuwekwa kwenye maandishi, hivyo kinachofanyika huwa ni kukopi na kupesti tu kulingana na quran inavyosema, na heshima kubwa huwa inazingatiwa katika maamuzi haya ili isiende kinyume na Quran. Sasa sijui wenzetu wanachotaka haswa ninini? kwani mahakama zimeshindwa kuamua kesi zenu? ni kesi zipi mlishawahi kuonewa kwasababu ninyi ni waislam kwamba zimeenda kinyume na dini yenu?, kama kuna muislam humu naomba maelezo ya kunielewesha jamani.
 
Itabidi nimtafute Mudhihir au Malima watueleze kwa kirefu kuhusu suala hili.

Kuna mtu anaitwa Mikidadi, alikuwa Mbunge wa Kibiti kabla ya uchaguzi uliopita, aliwahi kugiombea umufti, nadhani yeye analielewa zaidi suala hili kuliko hao uliowatajka. Mtafute yeye
 
Mkuu ulicho sema ni kweli tupu.

Lakini hapo hapo inakupasa kukumbuka BAKWATA ni chombo cha Serikali na wafanyakazi na ghara nyingi zaidi zinalipwa na hiyo Serikali kuliko waisilamu wenyewe.
Sasa having a KADHI court kwa mtazomo harisi kutaifuta Bakwata na hilo ndilo waisilamu wanalolitaka,na BAHATI MBAYA zaidi sio jambo linalotakiwa na Serikali pamoja na wengine kwa mambo yalifichika (historia)

Mkuu, kuhusu BAKWATA ninaelewa tofauti, nilikaa kimya ili nione watu wanasema nini sasa naona hakuna anayepinga (huenda ni kweli). But i think BAKWATA ni chombo cha Waislam (siyo Serikali) na gharama za kuendesha ni za waislam (siyo kodi za wananchi). Kama ni tofauti basi kunamatatizo Serikalini.
 
Wanabodi,
Mimi nimejaribu sana kukaa mbali na mjadala huu ambao kama nakumbuka vizuri tulikwisha fikia mahala tukaelewana katika mada iliyotangulia kuhusu swala hili hili..
Kwanza nakubaliana sana na Tanzanianjema ambaye kazungumzia ukweli wa wachangiaji hapa.. Wote mnasukumwa na imani zenu za dini badala ya kutazama hoja iliyopo...Ni mawazo yanayobomoa na kuboa kwa sababu hakuna anayezungumzia hoja hii kwa kutazama upande wa pili kutafuta suluhu..

Pili, binafsi sikubaliani na mahakama hii ya kadhi kwa sababu ambazo nitazitaja kama nitaulizwa lakini, kitu kimoja tu ningependa kufahamu kutoka kwa hao wengine ambao mnapinga mahakama ya kadhi...

Nitatoa vitu vichache ambavyo kwanza kisheria vinapingana na katiba. Ikiwa kweli kuna uhuru wa kila dini kuamini ama kuabudu inakuwaje Sheikh mkuu wa waislaam anachaguliwa na serikali tofauti na dini nyinginezo?..Imekuwaje serikali kuingilia maswala ya dini hii badala ya kuwaacha wao wajiendeshe kama dini nyinginezo...je, hili swala la kutakiwa mahakama ya kadhi hakuwezi kuwa ni chimbuko la mfumo huu wa kuhusisha serikali ktk maamuzi ya dini hii inapofikia swala la viongozi wake?..
Wakristu na dini nyinginezo zote zinaweza kumsimamisha Padre ama kiongozi wa dini kwa kupitia uongozi wa kanisa hilo na ikatambuliwa na serikali tena sio yetu tu bali hata nje lakini sio Waislaam ambao wako controlled na serikali toka uongozi hadi chombo cha dini.. Sasa ikiwa serikali imechagua dini moja tu kui control na hamkuona tatizo iweje dini hiyo inapoweka hoja yake iwe tatatizo hali ham question kilichosababisha kuwepo kwa control ya serikali ktk uongozi wa dini hiyo?
Pili, katika moja ya imani za dini hii wanaruhusiwa kuoa wake zaidi ya mmoja, Je, inapofikia mume amefariki, sheria ya nchi yetu inasema vipi kuhusiana na mirathi kati ya wanawake hawa wanne wenye watoto!.who gets what? au ndio anatambuliwa mke wa kwanza na watoto wake...nambieni sheria inasema vipi!

tatu, Ikiwa serikali inatambua hati za ndoa za waislaam, ni kwa kiwango gani mahakama zetu zimejifunza sheria za kiislaam zinazohuaiana na ndoa hizo ikiwa mwanamme/mwanamke atataka talaka..Nijuavyo mimi talaka haiwezi kuwa talaka kama certificate of divorce haijaltolewa na mahakama.. Je, yule mtu anayeandika talaka kama inavyosadikika na wengi humu (sijui talaka tatu) hiyo ndoa haitambuliwi tena kisheria (serikalini)!..Vipi kama wale wanawake wengine wakidai mirathi yao ktk korti zetu huwa kunapita utaratibu gani! Na je hiyo ndivyo inavyotakiwa kulingana na sheria za ndoa za kiislaam maanake wameamua kuzitambua ndoa ni lazima pia sheria za ndoa hizo zifuatwe au sio?...
Kama taifa ni sheria gani za ndoa na mirathi huwa zinafuatwa?...na kwa nini ikiwa kila Mtanzania anaruhusiwa kufunga ndoa ktk kanisa lolote la imani yake bila kuangalia matatizo madogo madogo ambayo yanaweza kujengeka ndani ya imani hizo!...Nijuavyo mimi nchi za magharibi kwa kuepuka matatizo zime adopt uhuru wa mtu kuoa mke mmoja tu (Christianity) hivyo hata ukiwa na dini tofauti inapofikia maswala ya maamuzi hutazamwa watu wawili tu..Kinyume cha hapo ni kuvunja sheria.
Nitarudia kusema binafsi sikubaliani na kuwepo kwa mahakama ya kadhi lakini nina sababu zangu tofauti kabisa na hizi nazoziona hapa!.. sioni maoni yenye kutazama nje ya box isipokuwa imani za dini (ndani ya box) yale yale ya ME, WE, US - against THEM...ndizo zinachangia zaidi.
Naomba majibu yenu kuhusiana na haya machache kabla hatujaendelea..
 
Mkuu Mkandara heshima mbele,

kwa mtazamo wangu nadhani majibu yako yako kwenye Hoja na maswali yako mwenyewe kwenye post yako ila una TATIZWA na maneno yako haya,....."sikubaliani na kuwepo kwa mahakama ya kadhi lakini nina sababu zangu tofauti kabisa na hizi nazoziona hapa!.. "
Kuwa wazi na sababu zako ili tujifunzi at least sisi tunaona usawa wa jambo hili tuone makosa yetu.
Binafsi nina mambo mengi ya kukujibu(ongezea kwenye maelezo yako)ila subiri hapo hapo nina suprise for you.
 
Pili, binafsi sikubaliani na mahakama hii ya kadhi kwa sababu ambazo nitazitaja kama nitaulizwa lakini, kitu kimoja tu ningependa kufahamu kutoka kwa hao wengine ambao mnapinga mahakama ya kadhi...

Nitatoa vitu vichache ambavyo kwanza kisheria vinapingana na katiba. Ikiwa kweli kuna uhuru wa kila dini kuamini ama kuabudu inakuwaje Sheikh mkuu wa waislaam anachaguliwa na serikali tofauti na dini nyinginezo?..Naomba majibu yenu kuhusiana na haya machache kabla hatujaendelea..

Sheikh Mkuu wa waislamu hachaguliwi na Serikali badala yake anachaguliwa na Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) na kuthibitishwa na baraza la maulamaa la BAKWATA!
 
Kwanza mimi binafsi sipingi kuwepo kwa Mahakama ya kadhi bali kwa nguvu zangu zote napinga mahakama hiyo kuwemo ndani ya katiba ya nchi yangu niipendayo ya Tanzania!

kimsingi sielewi mantiki ya waislamu kung'ang'ania mahakama yao hiyo kutambuliwa na katiba ya nchi yetu,na kwa jinsi hoja zao zilivyo inaonyesha kwamba bila ya mahakama hiyo kuwemo ndani ya katiba yetu haiteweza kufanya kazi. kama ni hivyo kwa nini?

kuna watu wanadai kwamba hakutakuwa na madhara kama mahakama hiyo ikianzishwa kwa mujibu wa katiba. binafsi nakumbuka miaka ya nyuma wakati kijana mmoja aliyekuwa anaitwa Michael alipotandikwa bakora huko Zanzibar kwa kuutwika ulabu wakati wa mwezi wa ramadhani!

Lakini nakumbuka pia hukumu ya mahakama moja ya Kadhi huko Nigeria ilipomhukumu mwanamke kunyongwa kwa kupata mimba bila ya kuolewa ingwa mama huyo alijitetea kwamba mimba yenyewe imetokana na kubakwa!

lakini mahakama nyingine kama hiyo huko saudia ilimhukumu mwanamke kupigwa bakora 200 kwa kile kilichoelezwa kujipeleka kubakwa na kushutumu hukumu aliyopewa.

haya yote na mengine mengi yananifanya nikatae kwa nguvu zangu zote mahakama ya kadhi kuigizwa kwenye katiba ya nchi yangu tanzania. kama waislamu wanaitaka si hata kesho wakutane pale kinondoni mtambani na kuchaguana kuiongoza mahakama yao hiyo?
 
Back
Top Bottom