Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Sasa utaona kitu ambacho watu wanataka siyo Kadhi (kwani tayari wapo na wanatambulika kisheria) lakini wanachotaka ni kuwa Kadhi awe Hakimu pia.[/QUOTE]


Nimekusoma Mkuu,

Sasa kwa mtazamo wako unadhani jambo hili ni baya?,na linaweza kuhatarisha amani ya taifa?
 
Mkuu,

Naomba tuelewane,interest za serikali ziko nyingi sio mfano,taking over the rule of law hapana.
Bakwata na serikali wana mahusiano ya karibu sana,mahusiano ambayo yana watia shaka waisilamu walio wengi ikiwemo na mimi,sasa kama kuta kua na siri kati ya Bakwata na Serikali sidhani kama serikali ita kuwa willing kushare hizo siri na chombo ambacho yenyewe haija husika hata kidogo katika kuiunda (yaani kama hiyo bill itapita basi waislamu wataunda chombo chao wao wenyewe na chombo hicho kitakua na mamaraka ya juu zaidi kuliko Bakwata na serikali itabidi itake isitake ishirikiane nacho hicho chombo) nakama hiyo itakuwa basi chombo hicho ndicho kitahusika na walfare ya waisilamu na uisilamu jambo lolote ambalo litaonyesha kuwakandamiza(au interests zao)
waisilamu au uisilamu litapingwa.

Pili Kadhi court haikuandikwa kwenye katiba ,ila serikali kupitia Bunge inatakiwa kuipitisha nakuikubari kama chombo cha Kiisilamu,na hiyo ndiyo nilisema ndio TATIZO kwani baada ya hapo BAKWATA will be out of the picture.
Serikali haitaki kuipoteza bakwata kwa sababu kadha wa kadha ikiwa kubwa ni chombo kilicho undwa na J.K.Nyerere baada ya kuvunja EAMWS kwa sababu zake za KIHISTORIA.

Tatu,ili ibada itimie kwa muisilamu mambo kama ndoa,mirathi,taraka na mfumo mzima wa maisha ya musilamu baada ya swala na dhaka nilazima yafatwe kama ilivyo takiwa ndani ya qurani na wanotaka kufahamu kwani si wote wenye kujua wanenda kwa KADHI ambaye ni msomi wa hari ya juu katika dini kwa maelezo ya ufasaha.

Mwisho,hizo habari za kunyongwa,mijeredi na kupigwa mawe ni Utawara wa SHARIA ambacho ni kitu tofauti na mahakama ya KADHI.


Bado hujanijibu
Ktk QURAN kumeandikwa kadhi lazima iandikwe kisheria ama katiba ya nchi?? kama kutamburika mwkjj tayari ameshakuonyesha ktk katiba inamtambua KADHI ama unataka imtambue zadi kivipi?

Kuhusu BAKWATA mtamsingizi bure MWL kwa vile chombo hicho kilianza wakati wake.Sioni wala sitaki kuamini ya kwamba serikali ina interest na BAKWATA ungesema BUZWAG ningelewa.

Kama ni migogoro ndani ya BAKWATA wala msimtafute mchawi kua ni serikali maana serikali haiwachagulii mtu wa bakwata ila ni waislamu ndio wanachaguana.
Msiwe kama wapinzani kila mgogoro unakua umesababishwa na CCM.

Kama BaKWATA ilisumbuliwa wakati wa MWL basi wakati huu ilitakiwa itulie maana RAIS ni JK,makamu wa Rais ni SHEIN katibu mkuu wa chama kiongozi ni Makamba na mweka hazina alikua RA sijui bado anaendelea.

Kama ni matatizo wala sio mambo ya serikali ila sisemi ndivyo ilivyo nahsi ktk sheria huko zinamsimamo mkali ama watu wanataka maslahi.HUWEZI ni convice Ngumi zinazorushwa na migogoro ktk misikiti mingi hua ni Mkono wa SERIKALI ama MWL ndio aliwaweka hao MASHEH mfano wa kariakoo waliopinduana.

Harafu ktk maelezo yako unataka kutuambia mahakama ya KADHI ktk uislam ipo juu kuliko misikiti.

kwanini hao wasomi waliobobea ktk QURAN mnashindwa kuwaweka wawe masheh wakuu na masheh wamisikiti?Ama wao wapo wanasubiri KADHI tu?
 
FM,

Sitaki kuingia sana kwenye sheria (kwani i know not),ila kwa ufasa katiba yetu inatoa haki kwa vikundi vya dini kutekeleza ibada zao ipasavyo (kama ujuavyo hata Roman Catholic wanazo pia mahakama zao ingawa hazitambuliwi kikatiba kwani haziko registared lkn ndivyo ibada zao au imani yao iavyo hitaji,kwani kwenye waumini mambo mengi yanatokea vifo,ndoa,utengano(devorce),maugomvi na mambo mengi kadha wakadha,inafikia mpaka vedict inatoka Vatican.)

Hivyo hivyo kwa Waislam mambo kama hayo yanatokea wanapaswa kuwa na kitu kama hicho,sasa tatizo linakuja hapa;Bakwata kama chombo SUPPOSELY cha waislamu kilichowekwa na SERIKALI kina kitengo kama hicho cha ku-sattle disputies LAKINI waislam walio wengi hawakiaami chombo hichi(BAKWATA) kwanza walio viongozi sio wasomi wazuri wa qurani na sheria zake wengine WAGANGA (kitu kibaya kabisa kwenye Uislam(shiriki),wengine ndio hivyo hivyo tena sio wasomi kiasi cha kuutukanisha uislam kama dini isiyo ya wasomi .
Kupukana na yote haya wame opt kuwa na KADHI atakeye kua na nguvu kuliko MUFTI wa Bakwata,sasa hili ni tatizo kwa serikalli kwani mamraka atakayo kuwa nayo Kadhi yata hatarisha interests za serikali ambayo inaona bora kuwapo kwa BAKWATA na si KADHI.
Na kwakuwa Bakwata inapata hizo ruzuku kotoka huko serikalini then itahusu fungu hilo liende kwa kadhi alfu yeye a alocate kwa Bakwata hilo ni tishio pia kwani wanajua kwamba wapo waislam wachache in favour of Bakwata.
Na ili kutambulika kisheria na kua mamraka huru lazima ipate barraka za serikali na hicho ndio kigugumizi chote kipo hapo


Hizo mahakama zinaitwaje? Au umeamua kuleta majungu?
 
Bado hujanijibu
Ktk QURAN kumeandikwa kadhi lazima iandikwe kisheria ama katiba ya nchi?? kama kutamburika mwkjj tayari ameshakuonyesha ktk katiba inamtambua KADHI ama unataka imtambue zadi kivipi?

Kuhusu BAKWATA mtamsingizi bure MWL kwa vile chombo hicho kilianza wakati wake.Sioni wala sitaki kuamini ya kwamba serikali ina interest na BAKWATA ungesema BUZWAG ningelewa.

Kama ni migogoro ndani ya BAKWATA wala msimtafute mchawi kua ni serikali maana serikali haiwachagulii mtu wa bakwata ila ni waislamu ndio wanachaguana.
Msiwe kama wapinzani kila mgogoro unakua umesababishwa na CCM.

Kama BaKWATA ilisumbuliwa wakati wa MWL basi wakati huu ilitakiwa itulie maana RAIS ni JK,makamu wa Rais ni SHEIN katibu mkuu wa chama kiongozi ni Makamba na mweka hazina alikua RA sijui bado anaendelea.

Kama ni matatizo wala sio mambo ya serikali ila sisemi ndivyo ilivyo nahsi ktk sheria huko zinamsimamo mkali ama watu wanataka maslahi.HUWEZI ni convice Ngumi zinazorushwa na migogoro ktk misikiti mingi hua ni Mkono wa SERIKALI ama MWL ndio aliwaweka hao MASHEH mfano wa kariakoo waliopinduana.

Harafu ktk maelezo yako unataka kutuambia mahakama ya KADHI ktk uislam ipo juu kuliko misikiti.

kwanini hao wasomi waliobobea ktk QURAN mnashindwa kuwaweka wawe masheh wakuu na masheh wamisikiti?Ama wao wapo wanasubiri KADHI tu?

Utanisamehe Mkuu,

Siwezi kujibu zaidi ya hapa,nadhani hatuelewani.Inaweza kuwa wewe umeshindwa kunielewa mimi au mimi nimeshindwa kukuelewa hoja zako.
Tuweke mstari maneno yako ndio ukweli.
 
Hizo mahakama zinaitwaje? Au umeamua kuleta majungu?

Sijui jina la mahakama hizo Mkuu,

Ila kwa kukusaidia nenda kwanye website ya BUNGE alafu angalia maandiko ya kikao cha Jana asubui kuna yule Mbunge wa huko shinyanga Bibi TEDDY KASELA-BANTU kama sikosei ndio alileta jina la hizo mahakama
 
Utanisamehe Mkuu,

Siwezi kujibu zaidi ya hapa,nadhani hatuelewani.Inaweza kuwa wewe umeshindwa kunielewa mimi au mimi nimeshindwa kukuelewa hoja zako.
Tuweke mstari maneno yako ndio ukweli.


kweli hatuelewani AMANI IWE na NAWE.
 
Sijui jina la mahakama hizo Mkuu,

Ila kwa kukusaidia nenda kwanye website ya BUNGE alafu angalia maandiko ya kikao cha Jana asubui kuna yule Mbunge wa huko shinyanga Bibi TEDDY KASELA-BANTU kama sikosei ndio alileta jina la hizo mahakama

Mkuu hakuna mahakama kama hizo labda unaongelea ushauri wa wazee wa kanisa n.k. Zingekuwepo basi hata jina lingekuwa wazi na sio la kutafuta.
 
Sitaki kubisha.

Lakini kwanini nisibishe?zipo kwani nihuyo mama aliye zisema kama zipo na kuzitaja na angalia katika posts za humu toka jana kuna mtu ameliongelea hilo.
Alafu aftr all si mimi pekee yangu niliye msikia yule mama Mbunge akitoa hoja zake jana labda wewe hukufatilia.
Usilazimishe kila kitu kiende your way.
 
Harafu JK kama anataka URAIS wake ukome ama uwe matatani 2010 yeye akubali KADHI ipitishwe na BUNGE.Huu ni ushauri tu unaweza kuukubali ama kuukataa.

Wajanja watakuja kui CAPTALIZE hiyo isue na kumwaacha JK akigaa gaa. Maana hapo hakutakua tena ni wizi wa kura kama ambavyo imezoereka ,Hapo ulinzi wa kura utakua ni CHADEMA,CCM,CUF,PPT , WAISLAMU na WAKRISTU kiasi kwamba kura haitaibiwa.

Kuna watu wa siasa wanachekelea tu pembeni afanye kosa hilo la karne ili aone KIVUMBI.
 
Sanda Matuta

Sisi ndio wakristu wenyewe tunakwambia hakuna mahakama yaani wewe unamuamini huyo mama ambaye hata sio mkristu?
 
Sanda Matuta

Sisi ndio wakristu wenyewe tunakwambia hakuna mahakama yaani wewe unamuamini huyo mama ambaye hata sio mkristu?

Haya ndugu yangu,

Hata mimi pia nilikua mkristu (lkn sio RC) na sikufahamu kama mahakama hizo zipo.

Alafu........ unataka nikuamini wewe (unaye tumia nick name hapa) au Mbunge aliye zungumza bungeni?
 
Tatizo kubwa ambalo baadhi ya watu wanalo kuhusu Mahakama ya Kazi ni "Jinsi gani itafanya kazi" katika frame ya mfumo wa sheria tulio nao. Mifano inayotolewa hapo juu kwa kweli inaonesha kuwa watu wengi hawajui hata mahakama ya Kadhi ikoje. Naomba nisema yafuatayo:

1. Mahakama ya Kadhi inaweza kuwepo hata kwenye nchi ambayo ni secular (isiyofuata dini). Nchi ambazo mahakama za kadhi zipo ni pamoja na Israeli (ya wayahudi) na India (ya Wahindi). Nchi kama Afrika ya Kusini nayo inazo na sehemu kadhaa za Pakistani utazikuta. Lakini baadhi ya nchi zenye waislamu wengi kama Uturuki na Indonesia hazina mfumo wa Mahakama ya Kadhi ambao tunaweza kusema siyo wenye msimamo mkali kama wa baadhi ya nchi.

2. Mahakama za Kadhi siyo za aina moja (not homogeneous). Kutegemeana na nchi mahakama za kadhi zinatofautiana sana kuanzia uwezo wake, sheria zake, na msimamo wake kuhusu mambo mbalimbali. Kuanzia kuvunjika kwa Uhalifa wa Umma wa Kiislamu, nchi mbalimbali za Kiislamu au jamii mbalimbali za Waislamu zimetengeneza Mahakama za Kadhi kuendana na mazingira yake na mahali pake.

Hivyo Mahakama ya Kadhi ya Israeli siyo sawa na Mahakama ya Kadhi ya Sudan na kwa hakika siyo sawa na Mahakama ya Kadhi ya India (India hazitambuliki kisheria lakini zipo kwenye maeneo yenyewe Waislamu wengi). Hivyo, tunapozungumzia mahakama ya kadhi tusichukulie mfano wa nchi fulani au nchi nyingine kwani hakuna mfano unaokubalika wa uendeshaji wake ambao waislamu wa Tanzania watalazimika kuufuata.

3. Ukizingatia 2 hapo juu utaona basi mahakama za kadhi zinatofautiana hususana linapokuja suala la makosa ya jinai. Kwenye nchi kama Sudan mahakama zao za kadhi ndizo zinaamua mambo yote hata ya jinai, wakati zile za India na Israeli zimeacha makosa yote ya jinai kwenye mikono Serikali. Miaka ile kule Indonesia (Hata Tanzania kabla ya Uhuru) mahakama za kadhi zilitoa maamuzi siyo kwa waislamu tu bali hata kwa wasio waislamu alimradi wanaamua wenyewe kwenda kuamuliwa na mahakama hizo.

Mfano mzuri wa hilo ni mahakama tunazoziona kwenye TV za kina Jaji Judy. Mtu halazimiki kwenda kwenye mahakama hizo za "TV" lakini akitaka kesi yake ya madai (siyo ya jinai) iamuliwe huko basi anatia sahihi fomu kadhaa na kujiweka chini ya maamuzi ya mahakama hizo. Hivyo, endapo mahakama za kadhi zitarudishwa nchini basi kuna uwezekano wa baadhi ya watu wakijua faida ya hukumu ya mahakama hizo kulinganisha na ile ya mahakama za serikali wakaamua kutatua migogoro ya madai chini ya Kadhi.

4. Jambo kubwa ambalo kwa Tanzania linasumbua sana na hapa nakubaliana na wengi ni ulazima wa mahakama hizo aidha kuingizwa kwenye Katiba au kuendeshwa na serikali. Hoja ya watetezi wa mahakama ya kadhi ni kuwa wanataka iwe hivyo ili hukumu zake zitambulike kisheria. Hoja hii inaweza kuwa na nguvu endapo tu wanachotaka ni kuhusiana na masuala ya jinai.

Lakini kama jumuiya ya Waislamu wanaona kuwa ulazima wa mahakama ya Kadhi ni sehemu ya ibada ya Muislamu au kukamilisha din basi wanajikuta kwenye matatizo makubwa kwa sababu endapo serikali isiyo na dini ikaamua kuingiza ibada ya dini moja kwenye Katiba na kutambua ibada hiyo kwa maneno mengine itakuwa imetangaza de facto kuwa serikali hiyo ni ya dini hiyo moja. Na hapa ndipo watu wengine wanatishwa.

5. Naamini kama Waislamu kweli wanataka kuanzisha mahakama ya Kadhi wanaweza kufanya hivyo wao wenyewe na wakishauriana na serikali kuhusu wigo wa upana wa nguvu za kisheria. Kwa vile tumesema kuwa Mahakama ya Kadhi inaweza kuwa hadi kwenye masuala ya jinai basi ni lazima kuwe na mipaka ya aina fulani.

Hapa ndipo naona haja ya serikali kubadilisha Katiba au Sheria na kuweka kipengele kama hiki:

"Taasisi yoyote ya kidini inaruhusiwa kuanzisha utaratibu wake wa kukata mashauri na kutoa haki kwa kuzingatia kanuni kubwa zifuatazo:
1. Haitatoa hukumu kuhusu makosa ya jinai
2. Haitatiooa hukumu kwenye kesi zinazohusisha muumini wa dini zaidi ya moja
3. Haitatoa hukumu kwa mtu yeyote ambaye hayuko tayari kujiweka chini ya taratibu hizo/mahakam hizo.
4. Mtu yeyote anayeamua kukata shauri au kutafuta hukumu kwenye mahakama ya kidini apewe nafasi na haki ya kutambua kuwa uamuzi huo wa kidini hautakatiwa rufaa kwenye mahakama yoyote ya serikali. Mtanzania akianza jambo lolote kwenye mahakama ya dini basi utaratibu wa rufaa ni huo huo wa kidini.
5. Mahakama za kidini hazitaendeshwa, kufadhiliwa, au kwa namna yoyote ile kupata malipo kutoka serikalini. "

Ukiangalia utaona katika nchi ambazo ni secular na zimeruhusu mahakama ya kadhi ni kuwa wingi wa waumini wa dini nyingine (Israel,wayahudi;India, wahindu; Kenya,wakristu; Afrika ya Kusini, wakristu n.k) wanawapa safety net ya kuweza kuhakikisha kuwa haki za wasio waislamu haziwi affected. Hapa kwetu kabla ya uhuru dola ilishikwa na utawala ambao ulikuwa wa kikristu ( Malkia akiwa ndiye kiongozi wa Church of England) kwa hiyo kutokuwa na wasiwasi kuwa wafuasi wake watakuwa affected au hizo mahakama zitakuwa na ubavu wa kwenda nje ya sheria za serikali tawala. Tulipopata uhuru tukaamua kuwa serikali yetu haitakuwa na dini. Na hivi ndivyo ilivyo hadi sasa.

Kwetu sisi ambako idadi ya waumini wa dini kuu mbili hazitofautiani sana, kuwepo kwake kunaweza kusababisha wengine nao wadai upendeleo vile vile na baadhi ya waislamu kushinikiza kuwa ipewe haki sawa na Mahakama za serikali. Hii itatufanya wengine tuone kuwa tunaanza kuelekea kwenye utawala wa sheria.

Natofautiana nawe katika swala la rufaa. Kwa mtazamo wangu ni lazima Mahakama ya Rufaa ya taifa iwe juu ya mahakama zote zinazotambuliwa ili kuhakikisha kuwa haki za kikatiba za mwananchi yeyote hazikiukwi.
 
Sasa utaona kitu ambacho watu wanataka siyo Kadhi (kwani tayari wapo na wanatambulika kisheria) lakini wanachotaka ni kuwa Kadhi awe Hakimu pia.


Nimekusoma Mkuu,

Sasa kwa mtazamo wako unadhani jambo hili ni baya?,na linaweza kuhatarisha amani ya taifa?[/QUOTE]

Sanda binafsi siamini kama kuwepo kwa Mahakama za Kadhi kutaharisha amani ya Taifa. That is on principle. Hata hivyo, Mahakama ya Kadhi ya aina gani Waislamu wa Tanzania wanaitaka ndilo lilipo Tatizo.

a. Je iwe kama ya Israeli na India?
b. Je iwe kama Nigeria Kaskazini?
c. Je iwe kama ya Sudani
d. Je iwe ni ya kwetu wenyewe yenye kuangalia mazingira na historia ya nchi yetu?
e. Je iwe na mfano wa Saudi Arabia?


Lakini suala kubwa ambalo siyo rahisi kujibiwa ni suala la sheria.

Sasa watu wengi hawajui ni kuwa kitabu cha sheria za Kiislamu ambazo zingetumika katika Mahakama ya Kadhi kilishamalizwa/almost done tangu mwishoni mwa miaka ya sitini. Sheria zilizochaguliwa zilihusisha wasomi wa dini ya Kiislamu wa madhehebu mbalimbali na kupata ushauri pia kutoka nje wakiwamo wanasheria maarufu toka India.

Lakini mabadiliko katika Uislamu hasa baada ya mapinduzi ya Irani na kuibuka kwa wimbi la Waislamu wenye msimamo mkali na vikundi vya kighaidi vyenye kutumia dini vinafanya mjadala wa Kadhi leo hii kuwa mgumu kweli.

Ndio maana mimi naamini uanzishwaji wa mahakama hizo wakiachiwa waislamu wenyewe itakuwa vizuri sana kwani katika ya matunda yake mazuri ni kuwa itawalazimisha Waislamu kukaa pamoja kuzungumza na kujadiliana juu ya mambo wanayokubaliana kuliko ilivyo sasa ambapo kuna mgawanyiko mkubwa maoni hususan suala la ibada na usimamiaji wa mali na amri ya mwisho.

Waislamu waandae mchakato wa kuanzisha mahakama hizo na wakubaliane jinsi ya kuzisimamia na kuchangisha fedha za kuendesha n.k
 
Ukiangalia utaona katika nchi ambazo ni secular na zimeruhusu mahakama ya kadhi ni kuwa wingi wa waumini wa dini nyingine (Israel,wayahudi;India, wahindu; Kenya,wakristu; Afrika ya Kusini, wakristu n.k) wanawapa safety net ya kuweza kuhakikisha kuwa haki za wasio waislamu haziwi affected.


Hapa umetumia mifano mibaya; Mahakama za Kadhi zilikuwepo katika Palestina kabla ya Taifa la Israeli kuundwa 1948. Eneo linalokaliwa sasa na Israeli lilikuwa likikaliwa na waarabu na kwa miaka mingi likiendeshwa kwa sheria za Kiislamu. Hivyo Israeli haikutengeneza uwepo wa Mahakama za Kadhi bali ulizikuta na kuzitambua na kuziwekea mipaka yake.

India vivyo hivyo, Mahakama za Kadhi zilikuwepo kabla ya kuundwa kwa Taifa la India tunavyolifahamu sasa na kabla ya kutengana kwa India na Pakistani. Kuna maeneo ya India ambayo yalikuwa na Waislamu wengi (Pakistani ya wakati huo na majimbo yanayokaribiana nayo kama Kashmir inayogombewa). Waingereza walipoenda huko walizikuta na waliziacha zifanye kazi zake japo kama Waisraeli walizipunguzia nguvu. Baada ya kuundwa kwa India ya sasa, Wahindi waliamua kuwa secular state na hivyo walizipiga marufuku na hata hivi sasa haziko kisheria lakini maamuzi yake katika ngazi za chini yanaachiliwa kusimama.

Afrika ya Kusini na kwenyewe zimetambulikana kwa sababu moja kubwa tu nayo ni kuwa kulikuwa na jamii ya Waislamu kwenye maeneo machache ambao walitaka kuongozwa Kiislamu na baada ya uundwaji wa Katiba mpya ya Afrika ya Kusini vitu vingi viliruhusiwa na hivyo kuifanya Katiba yao kuwa one of the most liberal in the world. Wa South wanafahama juu ya kunyanyaswa na kutengwa na wamejitahidi sana kuondoa kitu chochote kinachomfanya mtu awe duni.

Kwa Kenya nao ni mfano mbaya kwa sababu Mombasa, Lamu, Malindi, Mijikenda n.k na Ukanda wa Pwani ya Afrika ya Mashariki (Tanga, Dar-es-Salaam, Bagamoyo, Kilwa na visiwa vya Zanzibar) ulikuwa na utawala wa Kiislamu kwa miaka mingi. Na Mahakama za Kadhi zilikuwepo kabla hata ya Mjerumani kuja, na zilikuwa zimezama hata sehemu za ndani ambako Uislamu ulikuwa umeenea. HIvyo Mahakama hizo kama ilivyokuwa India na Israeli hazikuanzishwa kwa ruhusa ya Muingereza, zilikubaliwa kuendelea kwani zilikuwepo tayari.

Na hii ndiyo hoja kubwa kwa WAislamu kuwa Mahakama za Kadhi siyo kitu kigeni katika Afrika ya Mashariki, zimewahi kuwepo, na zimewahi kuwepo wakati wa wamisionary wakifanya kazi. Historia inaonesha kuliwahi kutokea migongano lakini leo hii tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuzirudisha mahakama hizi bila kuwa na matatizo yeyote yale.

Hapa kwetu kabla ya uhuru dola ilishikwa na utawala ambao ulikuwa wa kikristu ( Malkia akiwa ndiye kiongozi wa Church of England) kwa hiyo kutokuwa na wasiwasi kuwa wafuasi wake watakuwa affected au hizo mahakama zitakuwa na ubavu wa kwenda nje ya sheria za serikali tawala. Tulipopata uhuru tukaamua kuwa serikali yetu haitakuwa na dini. Na hivi ndivyo ilivyo hadi sasa.

Kwetu sisi ambako idadi ya waumini wa dini kuu mbili hazitofautiani sana, kuwepo kwake kunaweza kusababisha wengine nao wadai upendeleo vile vile na baadhi ya waislamu kushinikiza kuwa ipewe haki sawa na Mahakama za serikali. Hii itatufanya wengine tuone kuwa tunaanza kuelekea kwenye utawala wa sheria.

Natofautiana nawe katika swala la rufaa. Kwa mtazamo wangu ni lazima Mahakama ya Rufaa ya taifa iwe juu ya mahakama zote zinazotambuliwa ili kuhakikisha kuwa haki za kikatiba za mwananchi yeyote hazikiukwi.
[/QUOTE]
 
Kadhi kwelikweli, nahisi kunawatu katika dini wanaona mambo hayaendi mpaka wapate nguvu ya ziada,ila sidhani kama serikali imeshindwa kazi yake maana kama ni muongozo wa waislam si quran inatosha na mashehe sasa hiyo mahakama ni watu wanataka kuanzisha vitega uchumi maana inaonekana mahakama zinaongoza kwa rushwa so nadhani njaa zinasumbua watu.labda tu! wangesema ni kesi ipi ambayo imeshindwa kutatuliwa na serikari? Waamie uarabuni basi.
 
Just curious, will Mahakama ya Kadhi work under which denomination guidance? will it be Sunni, Shia, Ahmadiya, Bohora or there is a general agreement that as long as Quran is the key piece of doctrine behind the court, then the individual intepretation of the laws or Quran itself based on denomination becomes invalid?
 
Reverend.. hilo lilishaamuliwa zamani sana; wanazuoni wa Kiislamu hata wanasheria wa kawaida watajifunza sheria za Kiislamu kama wanavyojifunza civil law. Tofauti kubwa ni kuwa wakati sheria zetu nyingi msingi wake ni Katiba, sheria za Mahakama ya Kadhi msingi wake ni Qurani.

Wanasheria wake watajifunza sheria hizo pasipo kujali imani yao kama vile hatuulizi mwanasherie wetu ni wa chama gani au ana mlengo gani wa kushoto as long as anatumikia sheria zetu kwa mujibu wa kiapo chake.
 
Reverend.. hilo lilishaamuliwa zamani sana; wanazuoni wa Kiislamu hata wanasheria wa kawaida watajifunza sheria za Kiislamu kama wanavyojifunza civil law. Tofauti kubwa ni kuwa wakati sheria zetu nyingi msingi wake ni Katiba, sheria za Mahakama ya Kadhi msingi wake ni Qurani.

Wanasheria wake watajifunza sheria hizo pasipo kujali imani yao kama vile hatuulizi mwanasherie wetu ni wa chama gani au ana mlengo gani wa kushoto as long as anatumikia sheria zetu kwa mujibu wa kiapo chake.


labda kwa kuongezea tu hili la kwako,Qurani ni MOJA tu.
Sasa ukiwa Shia,Sunn na kadhalika utafata hiyo hiyo(imekua ikifatwa toka enzi na enzi na sheria zake hazibadiliki)
Tatizo lina kuja kwenye Tafsili,sasa hapo ndio inakuja umuhimu wa kuwa na KADHI ambaye ni Mjuzi wa sheria hizo za Qurani.
 
Back
Top Bottom