Jumla ya Wachezaji 26 Wasajiliwa Wakati wa Dirisha Dogo la Usajili

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JUMLA ya wachezaji 26 wamesajiliwa na klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara
katika dirisha dogo lililofikia ukomo juzi tayari kwa kuanza mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 15.
Wakati dirisha dogo la usajili likifungwa, kuna timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi hiyo zimeshindwa kuongeza wachezaji wapya kutokana sababu mbalimbali.

Klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo zilikuwa kwenye vita ya kuwania wachezaji, tayari zimekwishaanika majina ya nyota wao waliowasajili.

Yanga imemsajili mshambuliaji raia wa Zambia, Davies Mwape, na Juma
Seif ‘Kijiko’ kutoka JKT Ruvu, wakati watani zao Simba wameimarisha
safu ya ushambuliaji kwa kumtwaa mshambuliaji mwenye nguvu Ally Ahmed
Shiboli kutoka maafande wa KMKM Zanzibar na kumrejesha beki wake Meshack Abel aliyekuwa African Lyon kwa mkopo.

African Lyon wao wamesajili wachezaji wanne ambao ni Shabani Aboma, Zahoro Pazi, John Njama na Hamis Yusuf huku Majimaji ya Songea ‘Wanalizombe’ wakiwatwaa Patrick Betwel, Yahaya Shaban, Kasim Kilungo, Mohamed Kijuso na Ulimboka Mwakingwe.

Toto African ya Mwanza, nayo imeongeza wachezaji watano ambao ni Malegesi Mwangwa, Kamana Bwiza, Mussa Omary, Evans Paul na Saidi Manga, huku
Kagera Sugar ikiwanasa Steven Mazanda na Juma Seif kutoka Gor Mahia ya Kenya, wakati Mtibwa Sugar imembeba Salum Sued pekee.

Matajiri wa Azam FC na Maafande wa Polisi Dodoma, wamegoma kusajili na
kubakiwa na wachezaji walioanza nao mzunguko wa kwanza wa Ligi hiyo,
iliyoanza kutimua vumbi Agosti 21 mwaka huu.

Majina ya wachezaji hao yanatarajiwa kuthibitishwa na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), leo ili kubaini wale ambao usajili wao ulikumbwa
na kasoro kabla ya kuanza kwa Ligi hiyo
 
Back
Top Bottom