Jumatano maandano makubwa zanzibar nzima yakiongozwa na makamanda wa ukawa

Nimesikia kuna tshirt zina bendera na chata ya tanganyika kwanza. Je,ni kweli au zuga?
 
Wehu wakikutana sijui tutapata mchanganyiko gani haya acha yapuyange majitu yasiyojielewa yenye uchu wa madaraka watachoka na hayo mandamao yao.

Ccm ndio wenye uchu wa madaraka navili kudhihirisha hilo rasimu ya katiba imependekeza serikali ndogo wakaona ikipitishwa nafasi zao zitakuwa mashakani ndio maana wakaamua kuiponda na kuwalaani walioratibu ile rasimu na kuanza kubandika maoni ya ccm amabayo hayajakusanywa kutoka kwa wananchi
Sasa hapa nani mroho wa madaraka kama sio ccm wanaobadilisha maoni ya wananchi kwa manufaa yao.
 
Katiba Mpya inatengenezwa BUNGENI au BARABARANI?

""Jibu la swali lako utalipata siku wananchi wote tutakapotinga hapo ikulu na kuzidai funguo za ikulu,Muda huo LUKUVI,WASIRA,NCHEMBA,NDUGAI,SERUKAMBA n.k watakuwa wanapigia stori zao SEGEREA kama si THE HAGUE (GWANTANAMO).
 
Makamanda tabora tumewasbr kwa ham sana make hao mafsad mkiwalegezea kamba itatengenezwa katba yao na siyo ya waTanzania
 
Uzuri ni kwamba kuna The Hague.Hakuna mharifu atakayesalimika.Nadhani CCM waanze kujiandaa kuwafuata akina Ruto na Kenyatta.
Mkuu huko The Hague hawaangalii uhalifu usiokuwa na maslahi na Wazungu! Kama ilikuwa inafuata haki mpaka sasa M7, PK, Bush Sr & Jr, Obama, Blair, Perez, Netanyahu, Mkapa ungekuta wameshatinga mahakamani! Ile imewekwa kama sehemu ya No Fly Zone program kwa Viongozi wasiotaka kuingia mikataba kama walivyofanya serikali ya CCM! ... Wazungu wanaipenda serikali yetu iliyoko madarakani usipime! Hata Jeshi likiamua kuua nusu yetu wao watashangilia kwani watapunguza kugharamikia uzalishaji wa virusi vya UKIMWI na EBOLA kwaajili ya kutupunguza ....
 
Nafikiri wote hapa wameshindwa kusimamia issue!Katiba sio lazima naona tulipofika panatosha afadhali huu mchakato ukaishia hapa maana at last kuna watu watapoteza maisha na mali zao kwa ajili ya interest za watu flani hapa kuna hidden agenda kwa pande zote mbili ukawa na tanzania kwanza!Normally hawa politicians wanawatumia raia kwa interest zao hapa kuna watu wanajua serikali tatu watapata mamlaka na kuna watu wanajua serikali tatu ulaji wao unakuwa mashakani so scape goat ni mtanzania!!!!!
 
Mimi ngoja nije na ushauri wa hekima kwa serikali yangu tukufu:-

****Mithali 23:13, Usimnyime mtoto wako mapigo; Mithali 20:30, Michubuko ya fimbo husafisha uovu; Na mapigo hufikilia ndani ya mtima. Mithali 13:24, Yeye asiyetumia fimbo yake, humchukia mwanaye; Bali yeye ampendaye humrudi mapema. Mitahli 29:15, Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa, humuaibisha mamaye.
 
Mpka kieleweke Mara hii Zanzibar kwanza tanganyika kwanzaaaaaa bunge la intarahamwe Mara hii kaeni pembeni
 
Hivi imekuwaje CHADEMA wakaungana na "CCM B?" , au U-CCM B wa CUF umeshaisha?Dr.Slaa na Mbowe mliwaaminisha wafuasi wenu kuwa CUF imefunga ndoa na CCM, na NCCR MAGEUZI sio tena bali ni NCCR MANUNUZI kwakuwa MBATIA amepewa hela na CCM ili aue upinzani! Nashangaa Leo mnasema Mmeungana na hizi tuhuma hazisemwi tena!
Katika siasa hakuna uadui wa kudumu ila mkijikuta mko pamoja katika kupigania maslahi ya wananchi huwa ni jambo jema, huwezi kuacha kushirikiana na mwenzako kisa tu huyu ni CUF au NCCR. hata wana CCM wanaojitambua katika masuala fulani fulani mbona tunakuwa nao pamoja kwa mfano sasa hivi tupo pamoja kwenye sirikali3 na mtani wetu Kris Lukosi mwingereza!
 
Katika siasa hakuna uadui wa kudumu ila mkijikuta mko pamoja katika kupigania maslahi ya wananchi huwa ni jambo jema, huwezi kuacha kushirikiana na mwenzako kisa tu huyu ni CUF au NCCR. hata wana CCM wanaojitambua katika masuala fulani fulani mbona tunakuwa nao pamoja kwa mfano sasa hivi tupo pamoja kwenye sirikali3 na mtani wetu Kris Lukosi mwingereza!
Watangazieni wananchi kuwa CUF sio CCM B tena.
 
Jamani tusishabikie hili suala kisiasa! mambo ya vyama yawekwe kando! kila mwenye ufafanuzi mzuri wa muundo upi wa serikali unaotufaa tuutumie, tumpe nafasi ya kumsikiliza! UKAWA wameamua kuiga mfano wa CCM ambao wamegawanyika makundi mawili kwenda mikoani kuunga mkono muundo wa serikali mbili, hotuba ya JK, Na miaka 50 ya muungano! Kinana alizindua rasmi mikutano hiyo pale mwembe yanga!
Sasa wanapotokea wtz wengine wanaotaka kufanya kampeni za aina hiyo wasionekane kuwa ni wachochezi! maana Tanzania ni yetu sote! HOFU YETU NI! NINI? Waamuzi wa mwisho ni sisi wenyewe! tutachambua pumba na mchele! Mwisho wa siku tutatofautisha pumba ni zipi na mchele ni upi!! hakuna sababu ya kuzomeana na kupeana majina mabovu! MUNGU TUPE AMANI NA MIOYO YA KUSTAHIMILIANA DAIMA! TUEPUSHE NA YULE MWOVU!!
 
Mkuu,fuatilia mambo yanavyokwenda. Ili katiba mpya ipatikane(ambayo ccm wanai push iwe ya serikali mbili),ni lazima zipatikane theluthi mbili za wajumbe wa zanzbar na theluthi mbili za wajumbe wa bara. Sasa kwa bara wanaweza kubahatisha kupata(sababu wabunge wa ccm na wajumbe mapandikizi ni wengi) ingawa pia sio 100% sure sababu baadhi ya ccm na baadhi ya mapandikizi wanataka s 3(ref:Mtikila,Sarungi,Lembeli at al). Lakini kwa Zanzbar hawawezi kupata kamwe kama wajumbe wa kambi ya upinzani wamejitoa bungeni(sababu upinzani wote na 70% ya ccm hawataki kusikia s2). Sasa upinzani umeona bora uchochee kuni kule kwenye urahisi.Ni mahesabu tu
Tanganyika inadaiwa zanzibar! Uhuru wa tanganyika upatikane zanzibar? kwa nn sio dodoma kigoma tabora songea iringa au mara?
Mtikila unakwenda kuidai tanganyika yetu zanzibar?
 
nashindwa kuielewa serikali. unampaje kazi fundi akujengee nyumba na unamlipa na kulala usingizi. anakwambia nyumba tayari unakurupuka kuhamia na kuanza kulalama nyumba mbovu!! wataalam waliobakia bungeni minus ukawa wanatoa hoja zenye mashiko za takwimu. kwa nini tume haikupewa input hii katika draft zao za awali kabla ripoti haijakuwa public
 
Back
Top Bottom