Jukwaa la Wahariri lamfungia Mkuchika; latoa ripoti ya Tarime

KubwaJinga, naona umegwaya. maneno mengiiiii.... Mkjj keshatoa sababu yake ya kutofanya hivyo, But they've dared you in your own capacity, namba ya simu na donge nono juu, lakini naona umeishia kujing'ata meno tu mkuu....ya Pilato tumwachie Pilato...
 
ha ha ha ha

Umeshaanza "kujibaraguza" sasa wakati ulikuwa umeshaahidi kutoa info zako ili hii interview ifanyike. Mara ohh unataka skype, zip code, kelele nyingi kumbe hakuna kitu. Kumbuka kuwa ukimaliza hii interview ya Mbowe inabidi pia unipe mimi information zako - jina, simu nk ili nikuhoji kuhusu madai yako dhidi ya watu wa Tarime uliyotoa hapa wakati wa msiba wa Wangwe na hasa hasa wakati wa uchaguzi wa Tarime.

Magabe,
Itabidi ukajifunze kiswahili. Inaelekea hufahamu maana ya 'kujibaraguza' ndio maana umeupachika huo msamiati pasipo ili mradi tu na wewe uonekane umeutumia.

Naona na uzushi bado hujaacha. Bandika hapa hayo madai niliyotoa dhidi ya watu wa Tarime ili kila mtu auone otherwise huo mdomo wa uzushi ufunge.

 
It seems like Mbowe is now easly availlable for interview, what were the obtacles then??

I'll be in NYC sometimes next week and will provide you with my number.

kelele nyingi kumbe debe tupu....mara unataka simu gani na sasa ishakuwa next week, ......... subira huvuta heri
 
KubwaJinga, naona umegwaya. maneno mengiiiii.... Mkjj keshatoa sababu yake ya kutofanya hivyo, But they dared you in your own capacity, namba ya simu na donge nono juu, lakini naona umeishia kujing'ata meno tu mkuu....ya Pilato tumwachie Pilato...

Steve,
Mbona uko mbio mbio ku-conclude?? Mimi sio wa kushinda kwenye mtandao kama MMJJ. Mahojiano lazima yafanyike lakini ni kulingana schedule yangu na ya huyo mkuu kama.

Kwa kuanzia, ninakaribisha maswali kwa yeyote anayetaka swali lake liulizwe. Tuma kupitia JF PM. Hapa haabudiwi mtu yeyote.
 
Magabe,
Itabidi ukajifunze kiswahili. Inaelekea hufahamu maana ya 'kujibaraguza' ndio maana umeupachika huo msamiati pasipo ili mradi tu na wewe uonekane umeutumia.

Naona na uzushi bado hujaacha. Bandika hapa hayo madai niliyotoa dhidi ya watu wa Tarime ili kila mtu auone otherwise huo mdomo wa uzushi ufunge.


yeleyele yele yele nyingi!

Toa number yako ya simu hapa au nitumie kwenye PM, mimi nitakupigia simu na nitakuhoji na kurekodi mahojiano hayo. Sauti yako na demeanor yako na kila kitu unachosema kitarekodiwa na kisha kitawekwa hapa. Standard wewe unayotaka kuweka kwa watu wengine (ulianza na Wangwe) kama Mbowe na wengine, basi nawe utapewa hiyo hiyo standard.

Hayo ya "kujibaraguza" na "kuwashwa" ni maneno yako uliyoyatumia hapa na sasa unayapata tu back mwenzangu. Kuruka ruka kwingi, na maneno mengi kumbe hakuna kitu.

Nasubiria ufanye hiyo interview ya Mbowe na kisha yangu dhidi yako itafuata. Au kama unataka kufanya interview na mimi basi ufanye hivyo ili mimi nawe wote tutoke nyuma ya computer zetu na kuweka maneno yetu kwenye line na record za jamiiforum.

Okay?
 
Steve,
Mbona uko mbio mbio ku-conclude?? Mimi sio wa kushinda kwenye mtandao kama MMJJ. Mahojiano lazima yafanyike lakini ni kulingana schedule yangu na ya huyo mkuu kama.

Kwa kuanzia, ninakaribisha maswali kwa yeyote anayetaka swali lake liulizwe. Tuma kupitia JF PM au kubwajinga@gmail.com. Hapa haabudiwi mtu yeyote.

Toa number yako ya simu! inahitajika sauti yako na maneno yako. Nani ajuaye labda utanunua mtu akujibie maswali yako? Naona unataka kufanya kila kitu kama Sara Palin (huku ukibatiza wengine usara palini) kwa kutaka kujificha ili watu wasipate kila kitu unachofanya (nani ajuaye labda utakuwa na mtu hapo anakupa majibu kama sara palin afanyavyo na John McCain?)
 
Magabe,
Ukimaliza kubwabwaja fanya ubandike hapa hayo madai niliyotoa dhidi ya watu wa Tarime ili kila mtu ayaone. Otherwise nakukumbushia tena huo mdomo wa uzushi upumzishe.
 
It seems like Mbowe is now easly availlable for interview, what were the obtacles then??

I'll be in NYC sometimes next week and will provide you with my number.

At last ile week iliyoahidiwa imefika..... natumaini hii interview ya Mbowe itafanyika wiki hii.
 
It seems like Mbowe is now easly availlable for interview, what were the obtacles then??

I'll be in NYC sometimes next week and will provide you with my number.

Naona hii "next week" imepita (na sasa imekuwa last week) bila hii interview (baina ya mwanachama machachari kubwajinga na Mheshimiwa Mbowe ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi na wasomaji wa forum hii) kufanyika..... ndugu yetu kubwajinga umepotelea wapi tena?
 
Naona hii "next week" imepita (na sasa imekuwa last week) bila hii interview (baina ya mwanachama machachari kubwajinga na Mheshimiwa Mbowe ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi na wasomaji wa forum hii) kufanyika..... ndugu yetu kubwajinga umepotelea wapi tena?

Wakati mwingine majina huelezea tabia za watu ie kubwajinga
 
Jukwaa la Wahariri limechukua maamuzi kadhaa kuhusiana na kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Habari kutoka Dar-es-Salaam zinasema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya jitihada zote za kuitaka Wizara hiyo kubatilisha (rescind) uamuzi wake wa kulifungia gazeti hilo kushindikana.

Maamuzi yaliyochukuliwa na Jukwaa hilo ambalo linawakusanya Wahariri wa magazeti nchini ni haya yafuatayo:

a. Kuanzia jana kutoandika habari zozote zinazomhusu Kapt. George Mkuchika kama Waziri wa Habari kwa muda wa siku tisini. Uamuzi kama huo uliwahi pia kuchukuliwa huko nyuma dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Omar Ramadhani Mapuri ambaye naye alisusiwa na vyombo vya habari baada ya kuonekana amehalalilsha matumizi ya mabavu kwenye kuwadhibiti waandishi wa habari waliokuwa wameenda kuripoti na kupiga picha sakata la Jeshi la Magereza na wananchi waliohamishwa kwa nguvu kutoka nyumba zao baada ya Jeshi hilo kuzichukua kwa nguvu.

b. Kumuandikia Rais Kikwete barua ya kumtafa afikiria uteuzi wake wa Kapt. George Mkuchika kama Waziri wa Habari nchini. Wahariri wamedai kuwa Bw. Mkuchika amekuwa kikwazo cha uhuru wa habari na itakuwa ni kwa maslahi ya Taifa kama atahamishwa au kupangiwa jukumu jingine.

c. Kufungua kesi ambayo itazuia kuendelea kutumika kwa baadhi ya sheria (kama ile ya Magazeti ya 1976) kutokana na ukweli kuwa tayari mapendekezo ya mswada wa sheria ya Uhuru wa Habari yameshawasilishwa kwa Mkuchika na mojawapo ya sheria ambazo zinalalamikiwa ni hiyo. Kimsingi wanataka kuhakikisha mahakama inazitangaza sheria hizo kuwa ni kinyume na Katiba na hivyo kutaka hatimaye kupitishwa kwa sheria mpya ya Uhuru wa Habari.

d. Kufanya maandamano makubwa ambapo yatahusisha waandishi wa habari na mashabiki wa vyombo huru vya habari wakiwa wamejifumba vitambaa midomoni kuashiria kunyamazishwa kwa vyombo vya habari nchini. Haya yatatangazwa lini na wapi.

e. Kuanza kukampeni kwa wafadhili, mabalozi, na taasisi za kimataifa juu ya uvunjaji wa haki ya uhuru wa maoni ambao umeanza kuonekana Tanzania na hivyo kutishia demokrasia yetu.

Jukwaa la Wahariri latoa ripoti ya Tarime

Wakati huo huo, Jukwaa hilo la Wahariri limetoa ripoti yake kuhusu madai na habari iliyotolewa kutoka Tarime mara baada ya kifo cha Mhe. Chacha Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Bw. Freeman Mbowe aliokolewa na Polisi baada ya kutishiwa na mapanga. Habari hiyo iliyotolewa kwenye magazeti kadhaa ikiwa imefanana karibu neno kwa neno ilionekana imeleta utata na kizaa zaa hasa baada ya kudaiwa kuwa ilikuwa imehusisha plagiarizing (kukopi maneno ya mtu mwingine neno kwa neno na kuyafanya kama ya kwako).

Tume iliyoundwa na Jukwaa hilo ikiongozwa na Bw. Saed Kubenea imetoa taarifa hiyo na kuhitimisha mambo kadhaa. Miongoni mwa mambo ambayo yametajwa ni kuwa:

a. Hakukuwa na mapanga yeyote yaliyokuwa yameoneshwa hadharani kiasi cha kusababisha madai kuwa alikuwa nusura Mbowe auawe na hivyo kulazimika kuokolewa na Polisi.

b. Hakukuwa na tukio hilo la majaribio ya kumdhuru Bw. Freeman kama lilivyoripotiwa.

c. Habari zote zilikuwa zimeandikwa na mwandishi mmoja.

(to be updated)
Twalikumbuka Jukwaa lililokuwa na MENO siyo hili la akina Balile
 
Back
Top Bottom