Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Jukwaa la Wahariri limechukua maamuzi kadhaa kuhusiana na kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Habari kutoka Dar-es-Salaam zinasema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya jitihada zote za kuitaka Wizara hiyo kubatilisha (rescind) uamuzi wake wa kulifungia gazeti hilo kushindikana.
Maamuzi yaliyochukuliwa na Jukwaa hilo ambalo linawakusanya Wahariri wa magazeti nchini ni haya yafuatayo:
a. Kuanzia jana kutoandika habari zozote zinazomhusu Kapt. George Mkuchika kama Waziri wa Habari kwa muda wa siku tisini. Uamuzi kama huo uliwahi pia kuchukuliwa huko nyuma dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Omar Ramadhani Mapuri ambaye naye alisusiwa na vyombo vya habari baada ya kuonekana amehalalilsha matumizi ya mabavu kwenye kuwadhibiti waandishi wa habari waliokuwa wameenda kuripoti na kupiga picha sakata la Jeshi la Magereza na wananchi waliohamishwa kwa nguvu kutoka nyumba zao baada ya Jeshi hilo kuzichukua kwa nguvu.
b. Kumuandikia Rais Kikwete barua ya kumtafa afikiria uteuzi wake wa Kapt. George Mkuchika kama Waziri wa Habari nchini. Wahariri wamedai kuwa Bw. Mkuchika amekuwa kikwazo cha uhuru wa habari na itakuwa ni kwa maslahi ya Taifa kama atahamishwa au kupangiwa jukumu jingine.
c. Kufungua kesi ambayo itazuia kuendelea kutumika kwa baadhi ya sheria (kama ile ya Magazeti ya 1976) kutokana na ukweli kuwa tayari mapendekezo ya mswada wa sheria ya Uhuru wa Habari yameshawasilishwa kwa Mkuchika na mojawapo ya sheria ambazo zinalalamikiwa ni hiyo. Kimsingi wanataka kuhakikisha mahakama inazitangaza sheria hizo kuwa ni kinyume na Katiba na hivyo kutaka hatimaye kupitishwa kwa sheria mpya ya Uhuru wa Habari.
d. Kufanya maandamano makubwa ambapo yatahusisha waandishi wa habari na mashabiki wa vyombo huru vya habari wakiwa wamejifumba vitambaa midomoni kuashiria kunyamazishwa kwa vyombo vya habari nchini. Haya yatatangazwa lini na wapi.
e. Kuanza kukampeni kwa wafadhili, mabalozi, na taasisi za kimataifa juu ya uvunjaji wa haki ya uhuru wa maoni ambao umeanza kuonekana Tanzania na hivyo kutishia demokrasia yetu.
Jukwaa la Wahariri latoa ripoti ya Tarime
Wakati huo huo, Jukwaa hilo la Wahariri limetoa ripoti yake kuhusu madai na habari iliyotolewa kutoka Tarime mara baada ya kifo cha Mhe. Chacha Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Bw. Freeman Mbowe aliokolewa na Polisi baada ya kutishiwa na mapanga. Habari hiyo iliyotolewa kwenye magazeti kadhaa ikiwa imefanana karibu neno kwa neno ilionekana imeleta utata na kizaa zaa hasa baada ya kudaiwa kuwa ilikuwa imehusisha plagiarizing (kukopi maneno ya mtu mwingine neno kwa neno na kuyafanya kama ya kwako).
Tume iliyoundwa na Jukwaa hilo ikiongozwa na Bw. Saed Kubenea imetoa taarifa hiyo na kuhitimisha mambo kadhaa. Miongoni mwa mambo ambayo yametajwa ni kuwa:
a. Hakukuwa na mapanga yeyote yaliyokuwa yameoneshwa hadharani kiasi cha kusababisha madai kuwa alikuwa nusura Mbowe auawe na hivyo kulazimika kuokolewa na Polisi.
b. Hakukuwa na tukio hilo la majaribio ya kumdhuru Bw. Freeman kama lilivyoripotiwa.
c. Habari zote zilikuwa zimeandikwa na mwandishi mmoja.
(to be updated)