Prof. Lengo la muungano ilikuwa ni chanzo cha kuunda umoja wa afrika,
kwa maana nchi nyingine zingejiunga baadaye, zambia ilionyesha nia lakini baada ya kuyaona masharti "ambayo ni zanzibar pekee iliyakubali" haikuwa tayari kujiunga, na haikutokea nchi nyingine ya afrika kujiunga.
Prof. Rais wa zanzibar amekuwa mjumbe wa baraza la mawaziri, hakuwa na uchaguzi ispokuwa kukubali akiisoma picha iliyompata aboud jumbe (watu wamecheka kidogo)
Prof. Ibara inatoa mamlaka kwa bunge kutunga sheria ambayo inapaswa kuelekeza kuwa hiyo sheria inapaswa kutumika zanzibar tu. Prof. Anashangaa, Kama jambo husika ni la muungano vipi sheria ielekeze jambo kipekee wakati jambo lenyewe lipo kwenye hati ya makubaliano!!!
Prof. Msumari wa mwisho kwa jeneza, ilitokea kesi ikasajiliwa znz mahakama ya rufaa, ikaletwa mahakama ya rufaa tanganyika, ikakaliwa, kwa mwendelezo wake hukumu ilikuja toka kuwa zanzibar si nchi, kwa hiyo hapawezi kutokea uhaini huko zanzibar
Prof. Ali hassan Mwinyi alipata kusema bungeni kuwa tuna serikali mbili kuelekea moja.
Anamaliza kwa kusema hakuna ugumvi kati ya wananchi wa zanzibar na tanganyika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.