Juice kwa kiswahil 2iteje?

tafsiri yake ni sharubati/sharobati. Niliwahi kusikia mjadala huu kutoka kwa wataalam wa lugha ya kiswahili toka baraza la kiswahili la taifa.
 
Swali moja majibu kibao. Kazi kweli kweli.

Mimi mamlaka zangu zote zinasema kuwa Juice ni juisi/ maji ya matunda!

Hiyo ya juice kuitwa sharubati kwangu ni mpya na sijawahi kuiona katika mamlaka yoyote yale.

Sharubati niijuayo mimi kwa Kiingereza ndiyo sherbet. Wale ambao wamewahi kula/kunywa sherbet watajua kuwa sherbet si juice.

Sasa iweje juice iwe sharubati/ sherbet?

Juice ni juisi kama ilivyo Police na Polisi au Schule (Kijerumani) na Shule!

Labda aje mtu na kuniambia kuwa hiyo fasili/ tafsiri ni mpya lakini kwa sasa mamlaka zote za kimaandishi ambazo nimezirejea zinaonyesha kuwa juice ni juisi/ maji ya matunda.
 
sio sharobati,ni sharubati,limenyumbuliwa kutoka neno la kiarabu sharbat.
 
Kwa mujibu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, TUKI.
juice n 1 maji ya matunda/nyama n.k.; juisi (of grated coconut) kasimile, tui. 2 digestive/gastric ~ maji- tumbo. 3 (colloq) mafuta; umeme; gesi. juicy adj 1 -enye maji mengi. 2 (colloq) nayovutia (kwa sababu inaongelea tabia/kashfa za mwingine) give me all the juicy details leta umbeya wote. juiciness n.
 
Unaweza pia ukatuwekea tafsiri ya 'sherbet' kwa Kiswahili?
 
Namwunga mkono TZ1. KIswahili chenye kujiheshimu kitatumia "maji ya k.m. machungwa, tofaa, nazi, parachichi n.k. "Juisi" kwangu ndio mfano wa kutohoa kubaya sana kutoka Kiingereza ambako si lazima hata kidogo.
 
Back
Top Bottom