Jonijoo ni mtangazaji anaeongoza kuzipa media hasara. Ni mtangazaji mzigo


Alianzia kuonekana pale Times Fm lakini wakubwa hakuwashawishi kumpa kipindi kikubwa hawakuridhika na kiwango chake.

Baadae akatimkia Wasafi FM akapewa kipindi cha Block 89 akafeli kipindi kikafa ilikuwa hasara tu kipindi kilijaa kelele wadhamini hakuna.

Akaletwa Lil Ommy pale Wasafi na akaja na kipindi kipya na ilikuwa jonijo awe msaidizi wa Lil Ommy akakimbia akimuogopa Lily ommy atamficha.

Akakimbilia EFM kwa Majizo. Pale akapewa kipindi cha empire akiwa na B Dozen akuonesha lolote alishindwa Ku add value kipindi kikakosa sponsors listeners wachache Majizo akakifuta kipindi.

Amejaribu kumamishia mchana lakini hali ile ile kipindi hakina mvuto hakina listeners hakuna sponsors. Nacho kimefeli ni hasara tu.

Kwa sasa alichobakiza ni misemo tu ya kukopi kwenye bajaj au malori sijui wahuni sio watu.

Nafikiri ndio mtangazaji mzigo kuwai tokea kwenye urban radio stations.
Idea za Vipindi vya Jonijo, kwa Africa vinaweza kufanya Vizuri South africa, na sio Tanzania, Watanzania wana aina ya Vipindi vyao, kama Dadaz cha east africa, na Vipindi vingine vya Umbeya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom