Leadership is different from project management. Our crisis partly stems from the fact that we have been electing project managers instead of leaders! And the difference is you need money to successfully manage a project, but you need ideas to be a good leader!
Leadership is different from project management.
Our crisis partly stems from the fact that we have been electing project managers instead of leaders! And the difference is you need money to successfully manage a project, but you need ideas to be a good leader!
Huyu jamaa nilikuwa indifferent sana kwake lakini kadri siku sinavyokwenda nazidi kuamini Urais ni kazi kubwa sana kwake kama ana hiyo ndoto..
Mwanzoni tulijua kuwa wewe ni mtu makini kume tumekosea. Nadhani hata wanaokutumikisha wanajua kuwa wewe si makini na ndio maana wanakuwekea spidi gavana na kukuambia uache ubabe. Mwanzoni nilidhani wamekuonea kumbe walikuwa sahihi. Upo kama roboti. Nimegundua hili kutokana na matamshi na kauli zako. Barabara zote nchini unazijua wewe. Vifungu vyote vya sheria umevikariri wewe. Hizo sheria ni kwa ajili ya binadamu lakini wao/sisi sio programmed kama wewe.
Juzi hapa mkizindua barabara pale Dodoma, Pinda alikupiga dongo kuwa Rais alikupeleka uvuvi, na kule unajua idadi ya samaki nchini. Rais akaona bora akurudishe ujenzi. Tatizo lako mkuu unamtumikia kafiri kupitiliza, hadi unampa kero.
Wewe ni mchapakazi sawa, lakini yawezekana huna maadili ya kazi. Hakuna mtanzania anayekuwazia urais. Wanakuwazia uwaziri tu kwa kuwa watanzania wanajua unajua kutumika.
Achana kabisa na siasa zako za maji taka. Sio kila unapotoa neno hadharani usifie chama chako na kuponda upinzani. Kwa taarifa yako, unaowahutubia ni wapinzani. Sasa unapoponda viongozi wao na harakati za upinzani, wanakuchukia kweli. Wanakuoanisha na majina yako.
Tatizo lako mkuu unatupa mawe hovyo kiasi cha kuwatwanga na wazazi wako pia. Nakufananisha na Abunuwasi kukata tawi ulilokalia. Hilo tawi ni wananchi. Mpita njia akikuambia kuwa unafanya kosa kwani utaanguka, unamkejeli. Utakapoanguka utamkimbilia aliyekuambia ukweli kumwomba utabiri zaidi, angalia asijekwambia utakufa lini.
Achana na upinzani kwani ni jeshi kubwa kwa sasa. Una kashfa nyingi tu tunazozifahamu na nyingine zitafahamika. Una kashfa ya kuuza nyumba za serikali. Una kashfa za kumpa kimada wako nyumba ya serikali. Una kashfa ya kunyanyasa staff wako kwa kuletewa majungu na wapambe wako. Una kashfa ya ubabe, n.k, n.k. Fanya kazi, kiongozi kwani huijui kesho. Kazi ya kubwabwaja mwachue nape. Kaajiriwa kwa kazi hiyo. We kazi yako miundombinu. Usiwe kama mzazi anayewapa wanae mahitaji kwa masimango. Wenzako umeshwasikia wanabwabwaja hovyo? Time will tell
Urais kwa sasa huchaguliwa kwa kura za wengi na haupewi na mtu, Urais wa kupewa ulikuwa wa Nyerere, yeye ndiye aliepewa kwenye sahani bila kuchaguliwa. Upo hapo ulipo? ni nani alimchaguwa Nyerere kuwa Rais, na yeye akampasia kibaraka wake, MMwinyi na Mkapa. Kikwete kautolea jasho, na kama huyo Magufuli anauwezo na yeye autolee jasho.[/QUOTE]
Kikwete hakuutolea jasho alitumia mabilioni ya pesa zilizochangishwa na kundi lake lililojiita la mtandao wakiwemo Lowassa, Membe na wengineo. Walichangisha pesa hizi kutoka kwa mafisadi mbali mbali hasa wa kidindi akina Jeetu, Manji, etc na kuzitimia kuwahonga tena kwa hongo ya foreign currencies (US Dollars au British pounds) ili wampitishe yeye kama mgombea wa Magamba badala ya Salim ambaye alikuwa ni chaguo la wengi. Mkapa naye kwa sababu anazozijua yeye mwenye na baada ya kuona mgombea aliyemtaka Abdalla Kigoda kupigwa chini akadandia behewa la mtandao na hivyo kusaidia katika kumchafua SAS ili asichaguliwe kama mgombe wa magamba. Kwa hiyo hakuna ukweli wowote kwamba Msanii Kikwete ameutolea jasho Urais bali ukweli ni kwamba alitumia njia za haramu kuingia Ikulu.
urais kwa sasa huchaguliwa kwa kura za wengi na haupewi na mtu, urais wa kupewa ulikuwa wa nyerere, yeye ndiye aliepewa kwenye sahani bila kuchaguliwa. Upo hapo ulipo? Ni nani alimchaguwa nyerere kuwa rais, na yeye akampasia kibaraka wake, mmwinyi na mkapa. Kikwete kautolea jasho, na kama huyo magufuli anauwezo na yeye autolee jasho.
huyu ndio kiongozii anayegawa majukumu ofisini na kuhitaji mrejesho mbele ya media, tena kwa madoidoMimi huwa nawa-admire wazazi wa Magufuli,ni vichwa aisee!Jina la Pombe linasadifu kabisa tabia ya huyu robot!
Safety last ni safety first, umenena!Hafai kuwa Rais hata pm hawezi .Magufuli anatofauti gani na Lyatonga mrema.
Safety last ni safety first, umenena!
watajeni hao mnaotoa sifa zao kama mwenzenu mleta hoja sio mnazungukazunguka na kusema hafaiWanaJf;
Ni vizuri tutofautishe Mtendaji na Kiongozi. Magufuli ana sifa ya Utendaji lkn siyo Uongozi na ndiyo maana hata maamuzi yake mengine yanasababisha utendaji udorore kwa walio chini yake. Yeye ni mtu wa kupewa kitu cha kukamilisha na si kiongozi wa kuweza kung'amua lipi jema na lipi baya. Rejea hata maamuzi ya kuuza nyumba za Serikali, sawa ni kweli Baraza la Mawaziri lilipitisha hayo maamuzi na yeye kama Waziri husika akawa mtekelezaji. Lkn kama angekuwa mtu ambaye ni Creative angeweza kuona nini yatakuwa madhara ya maamuzi hayo kwa Uchumi wa Tanzania. Magufuli ni sawa na PROJECT MANAGER kama alivyosema Dr. Kitila Mkumbo. Magufuli ana tabia kama za Mbwa wa Mwiindaji ambaye ukienda naye mawindoni, then unamshtua Sungura au Swala kwenye kichaka, then unamruhusu kumfukuza yule mnyama ili amkamate na kukupa kitoweo. Magufuli hata post ya uwaziri Mkuu haumfai, kwani siyo mbunifu. Hawa siyo aina ya viongozi tunaowahitaji kwasasa. Tanzania kwasasa tunahitaji Kiongozi Mbunifu mwenye uwezo wa kund'amua mambo ya msingi na creative kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Pia huyo kiongozi awe MZALENDO NA JASIRI na mwenye VISION. Hatuhitaji viongozi aina ya JK ambao hawakuwa/hawana na VISION nyingine tofauti na kutaka tu kuwa RAIS bila kujua kwamba je huo URAIS ATAUFANYIA NINI?