John Pombe Magufuli unatuchefua

..nashangaa kwanini mpaka leo haburuzwi kupelekwa mahakamani kama Basil Mramba na Daniel Yona.

..kwanza, kuna hasara ya bilioni 15 iliyosababishwa na uamuzi wake wa kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza.

..pili, kuna hasara ya mabilioni mengine iliyosababisha na uamuzi wake wa kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa.

..tatu, kuna suala la kutumia madaraka yake vibaya "kuwauzia" ndugu na vimada nyumba za serikali.

..nne, kuna suala la kulidanganya bunge kwamba uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ilikuwa na faida na siyo hasara kama wale waliopinga uamuzi huo walivyokuwa wakidai.

..tano, matumizi mabaya ya madaraka yake kuingilia mradi wa ujenzi wa barabara na kulazimisha barabara hiyo ipitie jimboni kwake.
 
Unajua katika Mawaziri walio na "balls" wakiwa convinced na hoja iliyo na tija na kutenda kuhusu hoja hiyo.....Magufuli ni mmojawapo....and he is a straight forward man......kama alikuwa mislead......hilo ni suala jingine.....si kama Lowassa (often times with hidden agendas)

Hata leo ukiwa na wazo zuri la kujenga nchi mpigie simu/mwandikie halafu utaona matokeo yake.........

..nashangaa kwanini mpaka leo haburuzwi kupelekwa mahakamani kama Basil Mramba na Daniel Yona.

kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa laizembea au alifanya makosa yalifanyika kwa utashi wake......hao uliowataja walifanya maamuzi wakijua kuwa ni makosa na ni matumizi mabaya ya ofisi zao...........

......kwanza, kuna hasara ya bilioni 15 iliyosababishwa na uamuzi wake wa kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza.....

Root ya tatizo lile mbona hulizungumzii?..........Unajua watu waliokuwa responsible na root ya tatizo waliishia wapi...........na wengine wameishia kupewa hata ubunge na wengine madaraka mbali mbali............

..pili, kuna hasara ya mabilioni mengine iliyosababisha na uamuzi wake wa kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa.

Pamoja na kuwa sikulipenda wazo la kuuza nyumba za serikali......however,..........Unajua Serikali ilikuwa inapoteza pesa ngapi kwneye zile nyumba?

..tatu, kuna suala la kutumia madaraka yake vibaya "kuwauzia" ndugu na vimada nyumba za serikali.

Je waweza kututajia majina ya hao vimada na ndugu zake ili kuondoa mzizi wa fitina.........?

......nne, kuna suala la kulidanganya bunge kwamba uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ilikuwa na faida na siyo hasara kama wale waliopinga uamuzi huo walivyokuwa wakidai........

Ni muhimu ukapata data za uhakika kuhusu suala hili ili kujua ukweli kuwa tuliapata hasara au lah...........

.......tano, matumizi mabaya ya madaraka yake kuingilia mradi wa ujenzi wa barabara na kulazimisha barabara hiyo ipitie jimboni kwake.....

Hili si kweli....hakulazimisha barabara kupitia jimboni kwake...........ila aliongezea scope ya kazi ili barabra ifike jimboni kwake.......
 
Urais kwa sasa huchaguliwa kwa kura za wengi na haupewi na mtu, Urais wa kupewa ulikuwa wa Nyerere, yeye ndiye aliepewa kwenye sahani bila kuchaguliwa. Upo hapo ulipo? ni nani alimchaguwa Nyerere kuwa Rais, na yeye akampasia kibaraka wake, MMwinyi na Mkapa. Kikwete kautolea jasho, na kama huyo Magufuli anauwezo na yeye autolee jasho.

mbona unapenda kumwandama Marehemu ambae hawezi kujitetea?ata dini yetu hairuusu.ulikuwa wapi wakati yupo hai kusema unayosema!...mwache mzee wetu apumzike..

NB:siyo Nyerere aliyekuferisha mtihani wa la saba,ni kichwa chako tu!!
 
Mwanzoni tulijua kuwa wewe ni mtu makini kume tumekosea. Nadhani hata wanaokutumikisha wanajua kuwa wewe si makini na ndio maana wanakuwekea spidi gavana na kukuambia uache ubabe. Mwanzoni nilidhani wamekuonea kumbe walikuwa sahihi. Upo kama roboti. Nimegundua hili kutokana na matamshi na kauli zako. Barabara zote nchini unazijua wewe. Vifungu vyote vya sheria umevikariri wewe. Hizo sheria ni kwa ajili ya binadamu lakini wao/sisi sio programmed kama wewe.

Juzi hapa mkizindua barabara pale Dodoma, Pinda alikupiga dongo kuwa Rais alikupeleka uvuvi, na kule unajua idadi ya samaki nchini. Rais akaona bora akurudishe ujenzi. Tatizo lako mkuu unamtumikia kafiri kupitiliza, hadi unampa kero.

Wewe ni mchapakazi sawa, lakini yawezekana huna maadili ya kazi. Hakuna mtanzania anayekuwazia urais. Wanakuwazia uwaziri tu kwa kuwa watanzania wanajua unajua kutumika.

Achana kabisa na siasa zako za maji taka. Sio kila unapotoa neno hadharani usifie chama chako na kuponda upinzani. Kwa taarifa yako, unaowahutubia ni wapinzani. Sasa unapoponda viongozi wao na harakati za upinzani, wanakuchukia kweli. Wanakuoanisha na majina yako.

Tatizo lako mkuu unatupa mawe hovyo kiasi cha kuwatwanga na wazazi wako pia. Nakufananisha na Abunuwasi kukata tawi ulilokalia. Hilo tawi ni wananchi. Mpita njia akikuambia kuwa unafanya kosa kwani utaanguka, unamkejeli. Utakapoanguka utamkimbilia aliyekuambia ukweli kumwomba utabiri zaidi, angalia asijekwambia utakufa lini.

Achana na upinzani kwani ni jeshi kubwa kwa sasa. Una kashfa nyingi tu tunazozifahamu na nyingine zitafahamika. Una kashfa ya kuuza nyumba za serikali. Una kashfa za kumpa kimada wako nyumba ya serikali. Una kashfa ya kunyanyasa staff wako kwa kuletewa majungu na wapambe wako. Una kashfa ya ubabe, n.k, n.k. Fanya kazi, kiongozi kwani huijui kesho. Kazi ya kubwabwaja mwachue nape. Kaajiriwa kwa kazi hiyo. We kazi yako miundombinu. Usiwe kama mzazi anayewapa wanae mahitaji kwa masimango. Wenzako umeshwasikia wanabwabwaja hovyo? Time will tell

Mm nahisi kuna mkono wa kisiasa wa kuchafuana baada ya kusoma maoni ya watu
 
Huyu jamaa anatembea na idadi kubwa sana ya wanahabari kwenye ziara zake,wanalipwa posho na serikali kinyume na utaratibu,lengo ni ili aandikwe na kutangazwa na kila chombo cha habari,hii inafanya watu wengine waone yeye ni wa pekee sana katika utendaji,ni kweli anachapa kazi lakin maamuzi yake ya ukurupukaji yanaharibu future yake
 
Hakuna mtu asiyekuwa na mapungu kama mwanadamu..huyu jamaa katika mawaziri wanaofanya kazi zinaonekana huyu ni number one..tuache habari za CCM na CDM,Tanzania bila nguvu ile nchi aiendi hata kidogo..

hasa upande wa miundombinu sababu kila kona kumeoza hakufai. Natamani kuona barabara za bongo ziko kama za Tokyo
Mpeni Hongera zake pale anapostaili na ushauri pale anapokosea.
Hakuna mtu anayelikataa hili!lakini watu wanasikishwa na uropokaji wake,ambao unawatia shaka watanzania na hasa wale wanaopima mapaya na mazuri ya mtu kwa haki!
 
kamwe tusidanganywe na hawa viongozi wanaotafuta umaarufu katika majukwaa ya kisiasa kama akina Magufuli. Hii tabia ya kujidai kupiga simu mbele ya waandishi wa habari majukwaani na kujidai kuwa mkali kwa watu amabao wako chini ya mamlaka yake ni kujitafutia the so called cheap popularity. Hebu tujiulize kuna hatua gani zinazochukuliwa baada ya kupigiano simu majukwaani. Si ni miradi hii hii tunazidi kuona inazidi kusuasua siku, miezi hata miaka? Kama wanataka tuwaamini basi tuone hatua zikichukuliwa kwa watu hawa walioshindwa kutimiza wajibu wao sio kuoneshwa mikwara tu ya kupigiana simu majukwaani halafu baada ya hapo every thing remains as usual.
 
Tatizo ni mtandao wa kifisadi,tatizo sio mtu binafsi mimi huwa nawaambia watu wengi hiki kitu,hili lazima tutafakari,kama unaingia madarakani kwa pesa zilizopatikana kifisadi utawezaje kuwakemea au kukataa matakwa ya mafisadi waliofinance uchaguzi wako,hivyo ni wazi tunahitaji mabadiliko mazima na si kuhangaika na majani ya gugu huku tukiacha shina
 
huyu Mrema type nani ampe urais? Hafai hata kuwa waziri mkuu.Mpenda sifa na mtaka makuu
 
Hakuna dhambi kubwa aliyoitenda ambayo wafanyakazi wa nchi hii hawatamsamehe kama ile ya kuuza nyumba za serikali kwa vigogo waliokuwepo madarakani enzi za utawala wa Mkapa. Hivi sasa watumishi wa uma wananyanyasika kuhusu mahali pakuishi huku wakiona nyumba za serikali alizoziuza Magufuli zikiwa zinapangishwa kwa bei ya kuruka huku waliozinunua wakiwa wamestaafu au kuhama katika miji husika. Kama kweli ana ndoto ya Uraisi arejeshe kwanza nyumba alizoziuza na atubu dhambi hiyo. PIA WITO KWA WANA JF WOTE NA WAPENDA HAKI ZA WAFANYAKAZI KOTE NCHINI ANZENI KAMPENI YA BILA KUKOMA YA NCHI NZIMA YA KUTAKA NYUMBA ZA SERIKALI AMBAZO AKINA MAGUFULI WALIZIUZA ZIREJESHWE HARAKA
 
ni kweli kuwa watanzania hawana hiyana. Ni wepesi kusamehe na kupotezea. Cha msingi anayetubu na atubu kivitendo, kama ulivyopendekeza. Kitendo cha kutuma watu humu kumsafisha kiaina inamuongezea mauzauza, na huo uwaziri pengine nxt time atausikia
 
Hakuna mtu asiyekuwa na mapungu kama mwanadamu..huyu jamaa katika mawaziri wanaofanya kazi zinaonekana huyu ni number one..tuache habari za CCM na CDM,Tanzania bila nguvu ile nchi aiendi hata kidogo..

hasa upande wa miundombinu sababu kila kona kumeoza hakufai. Natamani kuona barabara za bongo ziko kama za Tokyo
Mpeni Hongera zake pale anapostaili na ushauri pale anapokosea.

Tunafahamu anamudu kazi yake kwa kiwango cha kutosha,anapostahili sifa huwa tunampa,anapochemsha naye tunamwambia
Ameonyesha kwamba siyo jasiri kwa viwango vya uwajibikaji wa kutukuka,angeachia ngazi pale alipozuiwa kutekeleza wajibu wake wa kiutendaji
 
Mwanzoni tulijua kuwa wewe ni mtu makini kume tumekosea. Nadhani hata wanaokutumikisha wanajua kuwa wewe si makini na ndio maana wanakuwekea spidi gavana na kukuambia uache ubabe. Mwanzoni nilidhani wamekuonea kumbe walikuwa sahihi. Upo kama roboti. Nimegundua hili kutokana na matamshi na kauli zako. Barabara zote nchini unazijua wewe. Vifungu vyote vya sheria umevikariri wewe. Hizo sheria ni kwa ajili ya binadamu lakini wao/sisi sio programmed kama wewe.

Juzi hapa mkizindua barabara pale Dodoma, Pinda alikupiga dongo kuwa Rais alikupeleka uvuvi, na kule unajua idadi ya samaki nchini. Rais akaona bora akurudishe ujenzi. Tatizo lako mkuu unamtumikia kafiri kupitiliza, hadi unampa kero.

Wewe ni mchapakazi sawa, lakini yawezekana huna maadili ya kazi. Hakuna mtanzania anayekuwazia urais. Wanakuwazia uwaziri tu kwa kuwa watanzania wanajua unajua kutumika.

Achana kabisa na siasa zako za maji taka. Sio kila unapotoa neno hadharani usifie chama chako na kuponda upinzani. Kwa taarifa yako, unaowahutubia ni wapinzani. Sasa unapoponda viongozi wao na harakati za upinzani, wanakuchukia kweli. Wanakuoanisha na majina yako.

Tatizo lako mkuu unatupa mawe hovyo kiasi cha kuwatwanga na wazazi wako pia. Nakufananisha na Abunuwasi kukata tawi ulilokalia. Hilo tawi ni wananchi. Mpita njia akikuambia kuwa unafanya kosa kwani utaanguka, unamkejeli. Utakapoanguka utamkimbilia aliyekuambia ukweli kumwomba utabiri zaidi, angalia asijekwambia utakufa lini.

Achana na upinzani kwani ni jeshi kubwa kwa sasa. Una kashfa nyingi tu tunazozifahamu na nyingine zitafahamika. Una kashfa ya kuuza nyumba za serikali. Una kashfa za kumpa kimada wako nyumba ya serikali. Una kashfa ya kunyanyasa staff wako kwa kuletewa majungu na wapambe wako. Una kashfa ya ubabe, n.k, n.k. Fanya kazi, kiongozi kwani huijui kesho. Kazi ya kubwabwaja mwachue nape. Kaajiriwa kwa kazi hiyo. We kazi yako miundombinu. Usiwe kama mzazi anayewapa wanae mahitaji kwa masimango. Wenzako umeshwasikia wanabwabwaja hovyo? Time will tell
kwanza unatuchefua na nani?exclude watu hapo ni wewe mwenyewe unachefuka,pia wewe ndio una siasa chafu una lolote kwanza umetumwa wewe ni mtimanyongo wako na roho ya korosho nyoka wa mdimu ndimu uli akija mtu kuchuma unamng'ata. kwa magufuli kuweka siasa katika hotuba hakuna kosa kwani ndio hali halisi lazima akifagilie cham chake CCM JUU, hata angekuwa waziri wa nccr au cdm lazima angesifia chama chake usikatae nature ya siasa.kama kashafa hakuna ambae hana kashfa na hauwezi pendwa na kila mtu ila kashfa zinatofautiana kam wanawake ni suala binafsi hata .....anao na unajua tena zaidi ya kumi sembuse magufuli?
 
kifupi sijatumwa na mtu. Na wewe umetumwa na nani? Au wewe ndiye yule kimada?
 
Kazi anafanya, its okey lakin ANACHOCHEFUA ni pale, almost kila akizindua miundombinu lazima akashifu upinzan..... na ole siku hiyo awepo jk ndo atakashifu km kapewa catalyst... Nampa pole km anadhan yeye ni all Tanzanians Tanzanian.
 
Na Hajawahi kuomba msamaha kwa kuiba nyumba za watz na kuwapa Kimada na Mdogo wake. SI SAHIHI KIONGOZI WA SERIKALI KUTUMIA EVENTS ZA KISERIKALI KUKIKAMPENIA CHAMA CHAKE ASUBIRI WKT WA KAMPENI, hiyo si Demokrasia hatuoni nchi nyingine wakitaja Vyama vyao ktk event za kiserikali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom