John Pombe Magufuli unatuchefua

naona kuna harakati za kumsafisha baada ya madongo ya uzi wa majuzi. Huyo hafai kwa lolote. Ngoja nitaifufua tena ile thread
 
wananchi wangekuwa wanashiriki katika kuchagua viongozi ingewezekana lakini wananchi wanaonyesha tu mfano wa kupiga kura na kile kinachoongelewa na wananchi katika sanduku la kura kinapuuzwa na wenye mamlaka ya kusimamia upigaji kura. mia
 
mkuu Dr anamweleza Mkandarasi Yeah yeah nini,maneno mengi kuliko kazi hahahahaha

watu kama hawa bana hawawezi pewa nafasi kubwa kama Uraisi maana upo uwezekano wa kutomwekea Raisi mstahafu kinga ya kutoshitakiwa
Dr bana huwa hana mzaha ktk kazi,ingawaje anamapungufu yake,lakini kiukweli hatuwezi mfananisha na mawaziri wengine waliobaki

naweza mfananisha na SOKOINE


Dr Magufuri pamoja na utumishi uliotukuka na kutokuwa na kashifa yeyote yeye pamoja na Mizengo Pinda hawafai kuwa marais wa nchi maana hakuna sehemu yeyote wala mahala popote hawa viongozi wawili wamesimama kukemea ufisadi wa viongozi wakubwa hadharani matokeo yake wamejikita kimya wakiwa kama opportunists wakisubiri nao wajiingize katika kinyang'anyiro cha urais cha 2015. Wkati hisia za watanzania na nchi yote kwa ujumla zinaongelea wizi wa mabilioni ya fedha ukifanywa na viongozi wakubwa wa serkali Magufuri na Pinda wamekaa kimya kana kwamba hawaoni, hawasikii, hawafahamu, hawaelewi, hawajui, hawaogopi na wala hawachelei hisia za watanzania dhidi ya serikali ya chama chao tawala.

Sokoine angekuwepo sio kwamba tu angekemea ufisadi hadharani bali angelitekeleza kwa vitendo na watu kama Edward Lowassa, Rostam Aziz, William Ngereja, Mustapha Mkullo, Khamis Mgeja mwenyekiti CCM Shinyanga, Mabina mwenyekiti CCM Mwanza, Jairo na genge la mafisadi na wezi wote wa mali za umma wangekuwa hawako madarakani na wako mahakamani wana kesi za kujibu kwa hiyo Magufuri asifananishwe na Sokoine huo ubavu hana iwapo alilazimishwa na mkapa kuuza nyumba na akauza? Sokoine alimkatalia Nyerere waziwazi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Barongo na Sebabili wa Shinyanga lazima waende ndani na hakuna kuachiwa na alifanya hivyo wakatiwa ndani, na akiwa njiani kwenda Morogoro kujua Mzindakaya anafanya madudu gani pale ili na yeye amuweke ndani akapatwa na mauti pale Dakawa na hiyo ndiyo ilikuwa pona ya Mzindakaya, Mkuu wa mkoa wa Morogoro wakati ule
 
Kwa wasiomfahamu Magufuli ni mtu mwenye roho mbaya,kama msaga sumu, kwanza kabisa, kauza nyumba za umma, kaweka alama za x kwenye nyumba za watu,mpaka vijijini. Nina uhakika hizo barabara hazitajengwa hata kwa miaka 50 ijayo. Mjue alama x inagofya,inatia na pressure. Ameweka faini kubwa kwa magari yanayozidisha uzito, ingawa wastani wa uzito wa barabara zetu ni tani 54, magari yanayobeba uzito wa tani 10,yakizidisha uzito ni shs 70000 kwa @ tani...alipopewa waziri wa nyumba na makazi alinyanganya watu viwanja huko boko na bunju kwa visingizio vya kutoendelezwa,wakati serekali haijaweka miundo mbinu, kama kituo cha polisi,kituo cha afya, mali nk... Angalia hasara aliyolitia kwa kiherere cha kukamata samaki akiwa waziri wa maji na uvuvi..almaarufu samaki wa magufuli, gharama ya kuwaifadhi inalingana sawa na thamani ya samaki wenyewe! Huyu bwana kwa taarifa yenu hapendi kuona maendeleo ya watu..
 
Hata yeye ni gamba hafai.aliuza hovyo nyumba za serikali na sasa nchi inaingia gharama kubwa kulipia watumishi wake hotelini.
 
@Huyu Magufuri hafai kabisa na wala watanzania tusijaribu hata kumfikiria. Kifupi watanzania hatuhitaji mwana CCM yoyote kuja kuiongoza nchi yetu tena. Mabaya waliyotufanyia kwa miaka 50 yametosha. Na haya ni baadhi tu ya maovu ya Magufuli aliyowafanyia Watanzania: 1/Hasara ya uuzaji nyumba za Serikali(vizazi vyote vitamkumbuka) 2/Yuko tayari kuipigania CCM ibaki madarakani hata kwa hila (eg.Kampeni Igunga,mijadala bungeni nk.) 3/Hana msisimamo wowote wa maana kwenye mambo ya msingi yanayowagusa watanzania wengi kwa sasa (eg.Muswaada wa Katiba mpya,Posho,Ufisadi,ugumu wa maisha,Uuzwaji mali za umma,Uporaji kwenye madini,Ukandamizwaji wa harakati za kidemokrasia,nk) 4/Ni mtu wa ujanjaunja tu,Visasi,Ubabe nk. @Kama ikitokea watanzania tukalogwa na kumchagua Magufuri aje kuwa rais basi tutakuwa tumeamua haya; 1/Tuendelee kuwa chini ya kongwa la utumwa wa CCM kwa miaka mingine 50. 2/Kuendeshwa kidikteta kwa Zaidi ya miaka 30 tena na mtu mmoja (Atakuwa kama Museveni,Mugabe,Albashiri)
 
Saint Ivuga... are you serious au unapima maji??
  1. vigezo vya uongozi si kubwabwaja, maana alitakiwa ajue hayo kabla hata ya kufika site/project
  2. umesema apewe, apewe na nani?
  3. unadhani tatizo letu kwa sasa ni nini?? ni strategist, leader au a wheen n' spanner guy?
we need a visionary leader anayejua watanzania wanataka nini na sio wanachama wake wanataka nini
 
mkuu Dr anamweleza Mkandarasi Yeah yeah nini,maneno mengi kuliko kazi hahahahaha

watu kama hawa bana hawawezi pewa nafasi kubwa kama Uraisi maana upo uwezekano wa kutomwekea Raisi mstahafu kinga ya kutoshitakiwa
Dr bana huwa hana mzaha ktk kazi,ingawaje anamapungufu yake,lakini kiukweli hatuwezi mfananisha na mawaziri wengine waliobaki

naweza mfananisha na SOKOINE

kandarasi mwongo kweli kapigiwa simu kajifanya yupo saiti..hahhaha kakamatwa anajifanya yeah yeah
 
APEWE!?
ZIMEKUWA PIPI?
Kama akiwa waziri aliuza nyumba za serikali,akiwa rais si atauza nchi mwanaharamu huyu?
mkataeeeeeeee!!!
huyu wa sasa hivi mnbona anawakumbatia mafisadi na kucheka cheka na huyu ndio richmond baba lao lakini si mlimrudsha ikulu?
 
Saint Ivuga... are you serious au unapima maji??
  1. vigezo vya uongozi si kubwabwaja, maana alitakiwa ajue hayo kabla hata ya kufika site/project
  2. umesema apewe, apewe na nani?
  3. unadhani tatizo letu kwa sasa ni nini?? ni strategist, leader au a wheen n' spanner guy?
we need a visionary leader anayejua watanzania wanataka nini na sio wanachama wake wanataka nini

wewe hujui kuwa ccm wanapeana urais?
 
Sokoine angekuwepo sio kwamba tu angekemea ufisadi hadharani bali angelitekeleza kwa vitendo na watu kama, Rostam Aziz, Jairo na genge la mafisadi na wezi wote wa mali za umma wangekuwa hawako madarakani na wako mahakamani wana kesi za kujibu. Sokoine alimkatalia Nyerere waziwazi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Barongo na Sebabili wa Shinyanga lazima waende ndani na hakuna kuachiwa na alifanya hivyo wakatiwa ndani, na akiwa njiani kwenda Morogoro kujua Mzindakaya anafanya madudu gani pale ili na yeye amuweke ndani akapatwa na mauti pale Dakawa na hiyo ndiyo ilikuwa pona ya Mzindakaya, Mkuu wa mkoa wa Morogoro wakati ule
Du!, kumbe ile ajali ambayo mpaka kesho, inaacha maswali mengi bila majibu, sasa naanza kupata majibu!. Sumbawanga Kiboko!,
 
WanaJf;
Ni vizuri tutofautishe Mtendaji na Kiongozi. Magufuli ana sifa ya Utendaji lkn siyo Uongozi na ndiyo maana hata maamuzi yake mengine yanasababisha utendaji udorore kwa walio chini yake. Yeye ni mtu wa kupewa kitu cha kukamilisha na si kiongozi wa kuweza kung'amua lipi jema na lipi baya. Rejea hata maamuzi ya kuuza nyumba za Serikali, sawa ni kweli Baraza la Mawaziri lilipitisha hayo maamuzi na yeye kama Waziri husika akawa mtekelezaji. Lkn kama angekuwa mtu ambaye ni Creative angeweza kuona nini yatakuwa madhara ya maamuzi hayo kwa Uchumi wa Tanzania. Magufuli ni sawa na PROJECT MANAGER kama alivyosema Dr. Kitila Mkumbo. Magufuli ana tabia kama za Mbwa wa Mwiindaji ambaye ukienda naye mawindoni, then unamshtua Sungura au Swala kwenye kichaka, then unamruhusu kumfukuza yule mnyama ili amkamate na kukupa kitoweo. Magufuli hata post ya uwaziri Mkuu haumfai, kwani siyo mbunifu. Hawa siyo aina ya viongozi tunaowahitaji kwasasa. Tanzania kwasasa tunahitaji Kiongozi Mbunifu mwenye uwezo wa kund'amua mambo ya msingi na creative kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Pia huyo kiongozi awe MZALENDO NA JASIRI na mwenye VISION. Hatuhitaji viongozi aina ya JK ambao hawakuwa/hawana na VISION nyingine tofauti na kutaka tu kuwa RAIS bila kujua kwamba je huo URAIS ATAUFANYIA NINI?
 
Sain Ivuga,

kwa nini umechagua kunihribia krismasi yangu ya kujiliwaza kihivo hivo nyumbani bila senti mfukoni? Kamwe usitusingizie eti tulimrudisha Mhe Kikwete Magogoni wakati unajua fika kwamba kura moja tu ya Jaji Lewis Makame ndio iliokua mfadhili wa huu utawala haramu.

Usinilaumu lolote kuendelea madarakani kwa kiongozi yeyote mpenda UFISADI na MAFISADI huko CCM!!!!!!!!!!

huyu wa sasa hivi mnbona anawakumbatia mafisadi na kucheka cheka na huyu ndio richmond baba lao lakini si mlimrudsha ikulu?
 
Sain Ivuga,

kwa nini umechagua kunihribia krismasi yangu ya kujiliwaza kihivo hivo nyumbani bila senti mfukoni? Kamwe usitusingizie eti tulimrudisha Mhe Kikwete Magogoni wakati unajua fika kwamba kura moja tu ya Jaji Lewis Makame ndio iliokua mfadhili wa huu utawala haramu.

Usinilaumu lolote kuendelea madarakani kwa kiongozi yeyote mpenda UFISADI na MAFISADI huko CCM!!!!!!!!!!

ninaweza kuthibitisha jinsi mlivyomrudisha jk magogoni ..ila ngoja nikupotezee kwa sababu naweza nikaiharibu sikukuu yako. na hutakiwi kushangaa kwani Lowasa yupo njiani ..najua magufuli hawezi kwenda popote
 
Kwa mtaji wa Tume ya Uchaguzi ambayo watendaji wake wanateuliwa na Rais, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, hakuna haja ya kupiga kura. Ni kupoteza wakati. Tumeshindwa kuipata Katiba Mpya, tususie uchaguzi mkuu ujao. Waache waende wakasimame wenyewe na sisi tuunde Serikali Mbadala, ya kuongoza nchi. Kama wanataka TUASI, bora TUASI, kieleweke! NOW THIS IS SEDITION! YES! Mimi Mchochezi!
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom