TANZIA John Mwankenja auawa kwa risasi

Poleni sana wananchi wa Rungwe na Serikali isifanye haraka kutamka sababu za kuuwawa kwake na wala isitumie opportunity hii kukiharibia chama kingine
 
RIP, Vyovyote iwavyo tunalaani mwananchi yeyote yule kuuwawa kwa kisingizio chochote kile. Hasa mwananchi huyo akiwa ni raia asiyekuwa na silaha na kutishia maisha ya wengine, iwe kwenye mgodi, maandano ya amani au hata nyumbani. Tuwaache polisi wafanye kazi yao kama walivyofanya kwenye vifo vya raia wengine waliouwawa kwa mtindo huu mfano Prof Jwan Mwaikusa, katibu wa CCM kata ya Isamilo, etc. Any speculation will not serve the justice to Mwankenja.
 
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, Ninyi watu sio Mapolisi wala wapelelezi kwa nini mnakimbilia sababu za kisiasa wakati makada wote karibu ni wafanyabiashara! je ukikuta kuna dhuluma kati yao hapo vipi au ukikuta anaweka kauzibe kwenye ulazi wa wanamagamba hapo vipi!?
 
Poleni sana wafiwa wote, ukweli maafa ya viongozi wa kisiasa kwa sasa yamekuja juu sana, sababu za msingi bado hazijafahamika, na wanao paswa kutupa ukweli wa hili ni polisi, sasa wao wakikaa kimya matokeo yake ndo haya kuwa ni mambo ya kisiasa, kila mmoja anaamka na majibu yake.

Hili lisifanyiwe masikhara kwakuwa matokeo yake yatakuwa na madhara makubwa, naomba polisi wafanye kazi yao vilivyo kisha watupe matokeo, maana huku bado CHADEMA wanaomboleza CCM tena yamewakuta ambayo yamewakuta mara kadhaa.

MUNGU BARIKI SIASA ZA TANZANIA MUNGU BARIKI WATANZANIA AMINA.B
 
poleni sana wana Rungwe na wana CCM kwa ujumla....!! Bwana alitoa na Bwana ametwa jina la Bwana lihimidiwe.....!!!
 
Poleni wanarungwe na familia yake. Naomba mungu wauaji wajulikane ili tujue sababu zake
 
Poleni sana ndugu zetu kwa msiba huu mzito.hivi
idadi ya madiwan wa cdm na ccm katika halmashauri hiyo
iko vp cdm wanaweza kuchukua hiyo halmashauri?
 
Wakati CHADEMA wanabadilisha rangi za bendera yao na kuweka rangi nyekundu ndani ya bendera mpya, watu wengi tulikuwa hatujawaelewa .

Ila hivi sasa kwa yanayo jidhihirisha ni wazi kabisa maana ya rangi hiyo inaonekana wazi. Kwani matukio ya hivi karibuni ya kutaka kumuua Mh. Mbunge wa Tarime kwa kumpiga mawe , na jana kumpiga risasi Mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe, yaonekana kabisa kuna mkono wa CHADEMA na kuna kikosi maalum cha mauaji kimeundwa kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyomo kwenye bendera yao ya alama nyekundu ambayo ni mauaji na umwagaji damu

RIP Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe.
Kule Mwanza yale masuala ya aliyekuwa meya wa jiji la Mwanza kwa tiketi ya CCM kesi haijamalizika, sasa CCM Rungwe nako mambo yanatokea! Kuna nini ktk utawala wa CCM!????
 
Nimeamini kwa nini wabunge a kishinda awakai uko
loh kama mnauana wenyewe kwa wenyewe mbunge si mna msharobaisi kabisa
 
Nimezipata habari muda huu,kuwa katibu mkuu wa CCM wilaya ya Rungwe-Mbeya,bwana John Mwakenja,ameuawa na watu wasiyojulikana ofisini kwake.
Na jeshi la polisi mkoani humo,wanasema kifo hicho kinasadikiwa kuwa kimetokana na sababu za kisiasa na tayari wamewakamata watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo,pasipo kuwataja majina yao kwa sababu za kiusalama.
 
kwa sababu yoyote ile iwe ya kisiasa, mapenzi, thuluma , ulozi, unafiki, majigambo, ukabila, imani,rangi, jinsia kwa yote hayo hakuna hata moja linalohalalisha haki ya kutoa uhai wa binadamu mwingine. wahalifu watafutwe na sheria ichukue mkondo wake.
 
Kazi ya chadema hiyo!siasa zao za kumwaga damu zishaanza kufanya kazi!naionea huruma tz kwa kile kinacholetwa na cdm
 
R.I.P Mwakenja. Basi utasikia mara CDM! Hawana mpango huo! Wanaamini kwa kile wanachokisema na ni sahihi, ni wananchi kuchagua wenyewe tu. Hebu tusubiri vyombo vya usalama viseme, si viko kazini tangu jana? Tusiwa pre-empty police wa Mbeya na wana usalama wengine, na yule mkuu wa Mkoa Mwakipesile, au kashahamishwa? Vifo vya hivi mara nyingi ni kulipizana kisasa, tusubiri nani alikuwa na kisasi naye na anashukiwa kufanya hivyo. Ninaamini serikali yetu ikiamua kufanya jambo inaweza, tusubiri.
 
Back
Top Bottom