John Kaduma!

Sawa sawa kabisa na ndani yake ilipatikana makala ya stanslaus katabalo ikihusu loliondo.akiita loliondo-gate.wapo wengi tu kuna emmanuely kibiki yo man.

Stan Katabalo alikuwa gazeti LA Mfanyakazi
 
Sina uhakika ni lini alifariki lakini hadi mwishoni mwa mwaka 1999 nilikuwa najua kuwa alikuwa amefariki, huenda ni mwaka huo ama kabla.

Nachojua hakuwahi kubadili jina. Jina Mohammed Hussein lilikuwa ni la kumshabikia aliyewahi kuwa mchezaji nyota wa Bandari ya Mtwara, Yanga na Simba, Mohammed Hussein "Mmachinga." Wakati John Kaduma akichora jarida la Tabasamu, crew ya jarida hilo ilikuwa ikijipigia chapuo kuwa inatumia mtindo wa wachezaji uwanjani wa 4-4-2 waliokuwa wakiuita "Samba Msele" na ndiyo maana John Mathias Kaduma alijipa jina la mcheza mpira. Majina mengine ya bandia ya John Kaduma yalikuwa,

  1. Fogasta
  2. John Black
  3. Baba Jack (Jina la bintiye Jacqueline)
  4. Tanzania One

Wimbi la Kitintale nakumbuka aliyechora ni Chrisantus Katembo (Chris Katembo). Wakati huo naona Kaduma hakuwa na amani katika Sani hasa baada ya kufariki Said Mbwana Makatta Bawji aliyekuwa kiongozi na mtunzi wa Hadithi Mahiri kama Maji Mazito na Kizaizai iliyokuwa na akina Mayuku, Zumo, Mzee Ole, Obi, Linda na Seba.

Kaduma ameathiri sana mtindo wa uchoraji wa wasanii wengi wa Tanzania, miongoni mwao ni mimi. Nafikiria namna fulani ya kurudisha nguvu/kumbukumbu zake japo kidogo but in a modern way.

Tunawamiss Born Town, Bush Stars, Makwekwe. Tunawamiss Ndumilakuwili (Profesa), Madenge, Kipepe, Bob Mazish, Lodi Lofa, Pimbi, Mzee Mwalubadu, Kizibao, Wanzuki n.k.

Tunakumbuka kosa alilofanya Mzee Mwalubadu kulazimisha Kizibao apangwe matokeo yake akasababisha penati iliyofanya Bush Stars wafungwe. Siku hiyo Ndumilakuwili hakusema "Yan Kibadachi, Yan Shodan Kataa!"

RIP John M. Kaduma.
Maelezo mazuri na historia nzuri sana,kumbe Chris Katembo nae kaanza uchoraji muda mrefu?RIP Kaduma.
 
R.I.PJOHN KADUMA familia ya ndg John ipo Iringa kama kuna mtu anataka kujua habari zake zaidi mama yake mzazi bado yupo hai anaishi Frelimo
 
Hakuna kama John Kaduma. Hata waliomtangulia akina Philip Ndunguru (Mchoraji wa mwanzo kabisa wa Sani) hawakuwa na uwezo kama wake. Never. Akina madenge wa siku hizi wabaaaaya.

BTW, nafanyia kazi namna ya kurudisha nguvu za akina madenge, lodilofa etc kwa kizazi cha sasa na cha miaka ya 80 kwa njia inayosisimua zaidi. Likely kuanzia mwaka 2016 naweza kuwa katika hatua muafaka. "Niko kambini najifua." Tuombe uzima.
Mzee vipi hii ahadi?
 
Mtuhumiwa kwangu mimi ni riwaya ya pili kwa ukali kutoka kwa Tuwa ikitanguliwa na Mkimbizi.
Nilicheki na Tuwa na kumueleza juu ya kuiweka Mtuhumiwa katika kitabu,kipindi hicho ndio alikua anaandaa riwaya yake ya UTATA lakini aliahidi ataifanyia kazi ishu.
Msachi tu kwenye facebook,chapa Husein Tuwa na mambo yataenda...you know wha i'm sayin'!!!?
Nilikipata hicho kitabu cha Mtuhumiwa mwaka 2016
 
Hakuna kama John Kaduma. Hata waliomtangulia akina Philip Ndunguru (Mchoraji wa mwanzo kabisa wa Sani) hawakuwa na uwezo kama wake. Never. Akina madenge wa siku hizi wabaaaaya.

BTW, nafanyia kazi namna ya kurudisha nguvu za akina madenge, lodilofa etc kwa kizazi cha sasa na cha miaka ya 80 kwa njia inayosisimua zaidi. Likely kuanzia mwaka 2016 naweza kuwa katika hatua muafaka. "Niko kambini najifua." Tuombe uzima.
Kaka ahad ni den,mpaka sasa kwako huo mwaka haujafika?!,sisi wa zaman enzi izo tunakusubiria sana
 
Hakuna kama John Kaduma. Hata waliomtangulia akina Philip Ndunguru (Mchoraji wa mwanzo kabisa wa Sani) hawakuwa na uwezo kama wake. Never. Akina madenge wa siku hizi wabaaaaya.

BTW, nafanyia kazi namna ya kurudisha nguvu za akina madenge, lodilofa etc kwa kizazi cha sasa na cha miaka ya 80 kwa njia inayosisimua zaidi. Likely kuanzia mwaka 2016 naweza kuwa katika hatua muafaka. "Niko kambini najifua." Tuombe uzima.
Maneno yanaishi boss tupe mrejesho ulifanikiwa ama kutofanikiwa vipi hapa. Huu ni mwaka 2020.
 
Kumbukizi,
R.I.P my role model J.Kaduma
IMG_20190923_074251.jpg
 
Kipindi hicho nipo Darasa la 3B ilikuwa mwendo wa kuvizia kwa wakubwa kitaani maana ilikuwa mwendo wa kuazimishana wenyewe kwa wenyewe, sie kina bichkoma kulisoma hadi ulifume mchagoni au juu ya kabati
mtaa mzima kuna kopi moja inazunguka au ukute kipande cha gazeti kimefungiwa maandazi ukifika hom unaweka maandaz kushoto unaanza kulipitia tartibu.
 
Mkuu umetisha...hiyo 1986 kwenda 87.

Hapo kuna dokta love pimbi, lodi lofa, kipepe na mzee sani mwenyewe, ndumila kuwili kule pembezoni na mzee sukununu kama sijakosea.

Hizo graphics sio za marehemu Ndunguru ? Yuwapi Mkuu Magembe R. Malima atupitishe hiz flashback.
Philip Ndunguru alikufa mnamo Februari 28, 1986 kabla toleo hili la Sani halijatoka. Hizo graphic ni za Ibra Washokera...
 
Collins Mdachi naye alishatangulia mbele ya haki nadhani 2014. Huyu Magembe R. Malima sijui kapotelea wapi? Hii ndiyo shida ya JF mtu ambaye ana connection na mwenzake humu "AKIAGA" hatutakuja kujua.
Ni kweli Collins Mdachi amekufa. Wapo pia wachoraji wengine waliokuwa maarufu ambao pia wameshakufa kama Katti Ka-Batembo. Huyu alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Wachoraji Comics Tanzania (Tanzania Popular Media Association "TAPOMA")...
 
Back
Top Bottom