John Cheyo: Mazungumzo ya maridhiano kuendeshwa kwa gredi yaani ya 'ukubwa' wa vyama viwili tu siyo sahihi

Kila mjadala wa katiba ukifika mnaanza kutisha watu mara mabeberu, mara ushoga utaingizwa kwenye katiba mara muungano utavunjwa!! Why? Mbona mara ya mwisho mlifuta maoni yote ya Warioba mkaweka yenu? Kwani mtashindwa kufuta hizo "ajenda" za mabeberu?

Mnapoingia mikataba ya kifisadi na mabeberu mnatumia katiba Gani? Ila ikitakiwa kubadilishwa mnakua wakali!!

Sijapinga.

Nimo kwenye kusindikiza wenzetu kwenye Kwaresma.

Ajenda, Katiba, wala iwe nini ni baada ya kufungua kifungo.

Amani ikutawale
 
Vishindo vikubwa vya BAWACHA Sumbawanga, mfano wa ukubwa wa CHADEMA kanda ya Nyasa

 
Kiukweli CDM wamejitahidi sana kwa sasa ndio chama pekee cha upinzani kimeweza na kinaweza kufanya shughuli zake za kisiasa mahali popote na muda wowote na mambo yakaenda vyedi, kongele zenu makamanda
 
Toka Kijiji cha Tamasenga, Rukwa

WAZEE WA SUMBAWANGA WANENA MAZITO YA FARAJA KWA UJIO WA VIONGOZI WA CHAMA CHA CHADEMA NGAZI YA TAIFA



Wazee wa Sumbawanga watoa baraka zao na kuhimiza wananchi wote, wake kwa waume wafike kumkaribisha Mh. Freeman Mbowe na ujumbe wake atapoingia katika viunga vya mji wa Sumbawanga kuelekea katika mkutano mkubwa wa hadhara mjini Sumbawanga Rukwa.
 
23 February 2023

LIVE : MAPOKEZI YA FREEMAN MBOWE SUMBAWANGA RUKWA

 
24 February 2023
JIMBO LA KWELA, RUKWA

MAPOKEZI YA CHADEMA JIMBO LA KWELA ALIPOWASILI MWENYEKITI MBOWE NA UJUMBE WAKE

 
17 February 2023

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki



Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?

Anaongeza kuwa ustaarabu wa kisiasa uwe katika nyanja zote na siyo lugha tu. Hili la ukubwa na huyu mtawala haikubaliki hivyo baraza la vyama la siasa lipewe hatamu na jukumu la kuongoza mazungumzo yatayojumuisha vyama vyote badala ya vyama viwili kujifungia chumbani bila wananchi kushirikishwa na ushirikishwaji ndiyo people's power ya wale rafiki zetu.

Mkongwe huyo wa siasa anasema maisha ni magumu ni katika mifuko yao wananchi inayosababishwa na bei ya mafuta kupanda. Hivyo hii ya serikali kuamua kuagiza mchele kutoka nje haitasaidia kupunguza bei ya mchele dukani.

Jibu la kukabiliana na mfumuko wa bei ni kutumia neno moja tu ruksa la rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na hivyo bulk procurement ya wachache kuagiza (kununua) mafuta ndiyo mzizi wa mfumuko wa bei /root cause ya mfumuko wa bei unaonufaisha wanunuzi wachache wa mafuta kupitia bulk procurement.

Ruksa ya Mzee rais Ali Hassan Mwinyi kuacha milango wazi kwa kila kitu ndiyo jibu endelevu / sustainable la kukabiliana na mfumuko wa bei hivyo EWURA na TBS wabaki kuwa wasimamizi wa ubora wa bidhaa na baada ya hapo bei ya mafuta itakuwa chini ya Tshs 2,000 kwa lita na hili litapelekea mfumuko wa bei wa kila kitu nchini kwenda chini na maisha kuwa nafuu.

Wafanyabiashara wa vitu na bidhaa zote hata mafuta lazima wawe wengi na ndiyo unafuu kwa maisha ya wananchi utapatikana, hii zimamoto ya kusimamia bei ya mafuta au kuagiza mchele toka nje kukabiliana na ughali wa maisha siyo suluhisho la kudumu.

John Cheyo mfanyabiashara wa siku nyingi anasema watanzania zaidi ya nusu hawaishi mashambani, bali wanaishi mijini na shamba lao ni mifukoni hivyo mchele toka Katavi, Shinyanga na Mbeya kuwa juu kwa walaji wa mijini unasababishwa na bei ya juu ya nishati ya mafuta ya dizeli na siyo vinginevyo pia wala ruzuku haitasaidia jibu ni neno ruksa kuruhusu biashara huria ya wafanyabiashara wengi wa biashara za ndani na nje.

Mzee John Cheyo anafurahishwa na waziri wa kilimo Hussein Bashe kutoyumbishwa na mbinyo wa kelele za kutoa bei elekezi kwa mazao ya wakulima au kufunga mipaka wakulima kuuza soko la nje. Mazao ni Mali ya wakulima anasisitiza Mzee John Cheyo na hiyo ndiyo sera ya UDP ya kuwajaza mapesa watanzania ikiwemo wakulima.
CHEYO amezeeka! Lakini akili yake ilizeeka zamani sana

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
24 FEBRUARY 2023
Tunduma, Tanzania

WALIOKUWA WAFUNGWA WA KISIASA AMBAO NI WANACHAMA WA CHADEMA WAPIGA PICHA NA MWENYEKITI WA TAIFA FREEMAN MBOWE

Wafungwa wa kisiasa ambao ni wanachama wa CHADEMA leo wamepanda jukwaani ili watu wapenda haki kote nchini Tanzania na ulimwenguni waweze kuwaona.


Wanachama hao walifunguliwa kesi za kutunga kuelekea uchafuzi wa uchaguzi serikali za mitaa 2019 na uchanguzi mkuu wa 2020 chini ya awamu ya tano ya utawala wa CCM uliokuwa ukiongozwa Rais John Pombe Magufuli.

Wananchi wa Tunduma na viongozi wa CHADEMA walipiga mayowe ya kulaani unyama na udikteta huo baada ya kuwaona live / mubashara waliokuwa wafungwa wa kisiasa walipopanda kwa zamu jukwaa kuu kutokana na wingi wao.

LIVE : KUNDI KUBWA LA VIONGOZI KANDA YA NYASA CHADEMA WAHANGA WA KESI ZA KUTUNGA WAPANDA JUKWAANI

 
24 February 2023
Tunduma, Songwe
Tanzania


UMATI WA WANA-WANCHI WALIOFURIKA KTK MKUTANO WA HADHARA WA CHADEMA TUNDUMA


Mwenyekiti wa CHADEMA taifa pamoja na viongozi wa chama wakiongozana taifa na wa kanda wakiendelea na ziara ya kazi za chama katika mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa ambayo ni kanda ya CHADEMA Nyasa
 
24 February 2023
Tunduma, Tanzania

MAKUMI YA WAFUNGWA WA KISIASA WALIOACHIWA WAPANDA JUKWAANI KUONESHA UDHALIMU WA CCM AWAMU YA 5



Makundi ya wana CHADEMA waliokuwa wahanga wa kutengezewa kesi wakati wa utawala wa awamu ya 5 na kufungwa jela kwa kubambikiwa kesi zisizo na ukweli wapanda jukwaa kuu wananchi na jumuiya ya kimataifa wapate kujua ukatili uliokuwepo ktk kutumia mfumo wa haki jinai vibaya dhidi ya wanasiasa wa upande wa upinzani.
 
Mbunge Aida Kenani awakaribisha viongozi wa CHADEMA taifa na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika ziara hiyo ya Kanda ya Nyasa

 
25 February 2023
Mlowo, wilaya ya Mbozi
Songwe
Tanzania

Freeman Mbowe : Wanachama wa CCM tumepigika wote, njooni mjiunge na CHADEMA

 
CHADEMA yagusia kilimo cha kahawa Mbozi na vyama vya ushirika



Pascal Haonga akizungumza katika mkutano wa hadhara awapa ripoti viongozi wa CHADEMA taifa na kanda jinsi CCM ilivyofeli kuweka mikakati ya kuinua wakulima wa kahawa
 
CUF - Walioondoka na baba warejee, kuimarisha umoja CUF 2023



CUF waanza kazi ya kuimarisha chama kwa kuhimiza walioondoka sasa warudi nyumbani .... team mkakati ya CUF ipo kazini kuhakikisha chama kinaibuka imara zaidi ..
 
MKUTANO WA HADHARA, ACT WAZALENDO WAMWEKA WAZI BWANA MKUBWA ALIYEKWAMISHA MAENDELEO YA ZANZIBAR


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, aweka wazi jinsi mambo yalivyobadilika baada ya mama kuchukua hatamu za uongozi maana kabla ya hapo vikwazo vilikuwa lukuki.

Mipaka ya nchi kwa ajili ya mafuta na gesi, dhahabu kukimbiliwa na bwana plea bargain ambaye sasa ni jaji, nchi ya Zanzibar kukosa mamlaka ya kukopa au uwekezaji kwa sababu ya yule bwana mkubwa, sasa mama kaingia hakuna vikwazo ila tunasikia kelele mama kwa kutupatia mgao sahihi
.
 
08 March 2023
Moshi, Kilimanjaro
Tanzania

MKUTANO WA BARAZA LA WANAWAKE CHADEMA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Mgeni rasmi Mh. Rais Samia Hassan akiwazawadia BAWACHA zawadi baada ya kupewa zawadi maalum toka BAWACHA

Mengineyo yaliyojiri:
Hotuba nzito zatolewa kuhusu Tanzania mpya anayoiongoza Rais Samia Suluhu Hassan. Matumaini makubwa yanaendelea kujitokeza na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliye mgeni rasmi asema hali hii mpya tuilinde na kamwe tusiruhusu kurudi kule tulikotoka heshima ya nchi ikaporomoka

 
31 July 2023
Ngara, Biharamulo
Tanzania

FREEMAN MBOWE - IMEBAKI MBIO ZA FARASI WAWILI, KWA KUWA VYAMA VINGINE VIMESHINDWA



Vyama vingine vya kisiasa vimeishiwa pumzi ya kufanya siasa mfano CUF Prof. Haruna Lipumba , ACT-Wazalendo ya Zitto Kabwe , TLP, UDP ya John Cheyo n.k vimesalimu amri kwa CCM na kutegemea Baraza la Vyama vya Siasa kujaribu kufifisha chama cha CHADEMA.

Hayo yameonekana wazi moto wa kazi ya kisiasa ya Operasheni +255, Okoa Bandari na Katiba Mpya ya CHADEMA ilivyoitikisa chama dola kongwe cha CCM na kuanza kutaka kuhariri maneno gani yatumike kwa wanasiasa kulingana na kamusi mahususi ya kipekee ya CCM isiyotambilika na vyombo rasmi vya kukuza na kuenzi lugha na maneno ya kiSwahili sanifu ya kamusi za TUKI wala BAKITA
 
Back
Top Bottom