Mwenyekiti wa Chama cha UDP anasema hakuna chama cha upinzani ambacho ni kikubwa kuliko vingine.
"Tunaona kuna chama tawala na kuna chama kinajiita sisi kikubwa!, hakuna chama cha upinzani kikubwa kuliko vingine, namshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutaka mchakato wa Katiba mpya uwe Shirikishi maana hatutafuti katiba ya vyama viwili"
"Wanapoanza kuzungumza kwenye mikutano kwamba kuna vyama vingine ni vyama vya mfukoni mara vyama vya namna gani, mara kuna vyama vimeolewa na CCM hii sio sawa, sisi kama UDP hilo tunaona litatugawa".
"Njia nzuri ya kufikia mchakato wa Katiba mpya ni kufuata maelekezo ya Mhe. Rais Samia aliyotoa, kwamba mchakato uwe shirikishi, wote tushirikishwe, na wananchi ndio wapewe kipaumbele sio chama kimoja wala viwili." - Mzee John Momose Cheyo.