JK ziarani Brazil kwa siku tano (Source TBC1 habari)

4.jpg

Rais Jakaya Mrisho kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kulia ni Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman. Picha na habari: Ikulu.

Rais Jakaya Mrisho kikwete amewasili Brazil Jumapili Aprili 15, 2012 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano.

Katika ziara hiyo Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais mstasafu wa nchi hiyo Mheshimiwa Inacio da Silva Lula na viongozi waandamizi wa nchi hiyo.

Katika ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi zinazoshiriki katika Mpango wa Ubia wa Uwazi Serikalini (Open Government Partnership-OGP) utakaofanyika mjini Brasilia chini ya Uenyekiti wa Rais Rousseff na kuhudhuriwa na wajumbe wapatao mia nne (400) kutoka serikalini, Asasi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Kimataifa.

Ubia wa Uwazi Serikalini au kwa kifupi OGP, ni mpango uliozinduliwa Septemba 2011 mjini New York, Marekani kwa lengo la kuwapa wananchi nafasi ya kushiriki katika kuamua mambo yanayowahusu, kupitia vyama visivyo vya Kiserikali na vya Kijamii.

Ubia huu unashirikisha kwa usawa wawakilishi wa serikali kwa upande mmoja na wawakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali za Kijamii kwa upande mwingine. Nchi ya Brazil kwa kushirikiana na Marekani imekuwa mstari wa mbele katika kusukuma ubia huu.

Rais Kikwete anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, asubuhi mara tu baada ya hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na Mwenyekiti wa mkutano huo Rais Dilma Rousseff wa Brazil, ambapo ataelezea maendeleo iliyofikia katika kuandaa mpango kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi kama ilivyokubaliwa katika kikao kilichofanyika Disemba 2011.
Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 20 Aprili, 2012.
 
Hivi tuongeapo serikali haina pesa kabisa kwani haya matumizi mabaya ya fedha yatakwisha lini?
hivi kama asingeenda kwani ingekuwaje ukizingatia huu wakati mgumu hasa kifedha tulio nao kama Taifa
Kuna sababu gani ama faida gani kwa Taifa kwa Kikwete kuenda na mkewe? mnijuze tafadhari.......................
 
Kuna tetesi mmoja kati ya vasco na max ni punga,so wanaenda kupungana na kukumbushiana
 
lu9.jpg

Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha nchini Brazil alipokwenda kumsalimia Rais kwenye hotel ya Tivoli jijini Sao Paulo
 
jamaa ameenda Brazil kwenye mkutano gani? marais na wakuu wengi wa marekani ya kaskazini, kusini na kati wako Cartagena, Colombia kwa mkutano wa nchi hizo, na yeye hausiki na mkutano wa nchi hizo. Sasa nakua sielewi ameenda anakutana na nani mzito huko Brazil badala ya kwenda waziri mmoja kule?
 
[h=3]Ziara ya Kikwete Brazil haina tija kwa taifa kama mambo yenyewe ni haya.[/h]Chanzo; mpayukaji blog

Rais Jakaya Kikwete akishuhduia mkewa akisalimiana na kocha wa zamani wa timu ya taifa Maxio Maximo. Rais na kocha wapi na wapi jamani?
Katika pita pita yangu kwenye vyombo vya habari nchini, sikuona mahali ilipo taarifa ya rais Jakaya Kikwete aliyeko nchini Brazil ukiachia mbali makala moja toka Sao Paolo iliyoandikwa kwenye Mjengwa Blog ambako picha hii imetoka. Habari inaongelea upuuzi mtupu eti jinsi ya kuwa na timu nzuri ya taifa. Hiyo si kazi ya rais ni kazi ya waziri wa michezo hata vilabu vya michezo. Kwanini rais asifute wizara ya michezo akaiweka chini ya ofisi yake ili angalau tujue rais wetu ni rais na waziri wa michezo?
Ukisoma ile makala ambayo bila shaka Anna Nkinda aliyeiandika ameandamana na rais, unapata kichefuchefu.
Nilichojifunza ni kwamba rais wetu hana jipya wala la maana la kuandikwa na vyombo vya habari. Maana nijuavyo, rais wa nchi ni alama ya nchi. Popote awapo lazima umma wa wananchi ujue anachofanya na yuko katika hali gani. Kuna uwezekano kuwa rais yuko Brazil akifanya mambo ya hovyo kama hiyo picha juu inavyoonyesha. Nadhani ndiyo maana magazeti ya Tanzania hayana muda wa kufuatilia kuandika anachofanya rais. Sasa inashangaza hata hao waandishi wa habari wanaolipwa na kuandamana na rais wanafanya kazi gani kama hawana hata habari za kutuma nyumbani? Kwa maana hiyo huu ni ushahidi kuwa rais wetu ni wa hovyo kweli kweli.
 
So what kama obama ameenda?kutoka DC hadi brazil ni km kutoka Dar hadi Pretoria.Obama akisafiri am sure he doesn't use more thatn $ 100,000(150mil) kwenda brazil.mheshimiwa anatumia 300mil ka nchi kenye uchumi mbovu. huu ungwana kweli?
 
Back
Top Bottom