JK wapambe wake wanamdanganya nae anadanganyika!

Kwami huyu Mh. hasomi magazeti au hata baadhi ya taarifa za habari haangali, ina maana hata taarifa za habari huwa anasaidiwa kuangaliziwa kisha anachambuliwa zilikua zinasemaje?? Japo vyombo vyetu vingi vya habari hazipo wazi na huru, ila kwa kiwango hicho hicho vimeweza kuchora picha nzima ya maisha duni na hali mbaya za watanzania ina maana yeye hazioni kupitia vyombo hivyo???
 
Kwa hali iliyopo sasa nchini,
huna budi kusema Rais hana wasaidizi kabisa,
kwani mambo hayaeleweki na hao wasaidizi hakuna wanachokifanya kumsaidia JK[/QUOTE

Rais anatakiwa kuwa mtu wa kuchukua hatua na si kusaidiwa. Rais wetu si juha kusema hawezi kufikiria. Hivi ata kulipa DOWANS ili watanzania wafe nayo rais anahitaji kusaidiwa hapo?
 
sasa unauliza nini,
bila shaka majibu unayo wewe mwenyewe, au
unataka tuseme useme ni wapinzani hao.

Kagame alisaidiwa au anasaidiwa na nani? Gadaffi je? Rais hana uwezo wa kufikiria au vipi mpaka asubiri kusaidiwa?
 
nchi ipi uliwahi kuona Rais anajifanyia mambo yake mwenyewe bila washauri ni kama na wewe umedanganywa na mwalimu aliyekufundisha somo la uongozi

Kwahiyo ata akishauriwa kuuza nchi anakubali kwakuwa kashauriwa? Au unasema ukiwa rais uwezo wa kufikiria unukabidhi kwa watu?
Je, unataka kusema rais wetu hana uwezo wa kuchagua au kuteua washauri wazuri kama viongozi wengineo duniani? Usisahau kuwa rais wa TZ katiba inampa madaraka zaidi ya Dikteta yaani ni Mungu mtu.
 
sura za wafuasi wa chadema zinaonekana kuwa na njaa kali ni rahisi kuyumbishwa hata kama njaa yao sio ya kusababishwa. kuna njaa za aina mbili ya kujisababishia na kusababishwa

Rais wetu naye vp kuhusu kudanganywa na nyinyi mnaomsaidia. Unataka kutuambia kuwa nae yuko kundi unalolisema hapa?
 
Sijapata kuona rais muongo kama JK, aliwadanganya watu wa goms mabomu kuwa mtalipwa punde tu akaapa sasa hivi anakula kuku kasahau, ahadi nyingi harafu anateleza. Harafu kila siku mnasingizia wasaidizi wake. MIMI niliwahi kusikia kuwa JK si wasaidizi ila anataka kusikia anachotaka yeye tu na kufanya anachopenda yeye tu. na ndo maana wasaidizi wanampa anavyovitaka.
 
Kwami huyu Mh. hasomi magazeti au hata baadhi ya taarifa za habari haangali, ina maana hata taarifa za habari huwa anasaidiwa kuangaliziwa kisha anachambuliwa zilikua zinasemaje?? Japo vyombo vyetu vingi vya habari hazipo wazi na huru, ila kwa kiwango hicho hicho vimeweza kuchora picha nzima ya maisha duni na hali mbaya za watanzania ina maana yeye hazioni kupitia vyombo hivyo???

Nadhani ukiwa rais kupitia CCM basi unapofuka na kuwa kiziwi maana huyu JK alikuwa ni moto wakati anakampaini kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza. Aliahidi kuvunja mikataba mibovu ila la kushangaza hajawahi kuvunja ata mmoja ila kuongeza mingi mibovu kabisa ukiwemo huu wa reli ya kati kwa wa Hindi.
 
Sijapata kuona rais muongo kama JK, aliwadanganya watu wa goms mabomu kuwa mtalipwa punde tu akaapa sasa hivi anakula kuku kasahau, ahadi nyingi harafu anateleza. Harafu kila siku mnasingizia wasaidizi wake. MIMI niliwahi kusikia kuwa JK si wasaidizi ila anataka kusikia anachotaka yeye tu na kufanya anachopenda yeye tu. na ndo maana wasaidizi wanampa anavyovitaka.

Nakuunga mkono. Hili linawezekana hapo kwenye red.
 
Hicho unachotaka wewe ndo huyo RAHISI asichotaka, yaani kufanya kazi mwenyewe. Jamaa ni bonge la mvivu, sasa wewe unataka afanye kazi ipi ambay anaweza?

mlituingiza porini.

Juzi kwenye kumpokea Prince, na yeye alikuwa anamfunga kamba prince wa watu kuwa sasa Tanzania imeendelea sana, sasa wewe unataka wasaidizi wake wamwambie nini?
 
kosa lake mwenyewe kama mkuu wa kaya. Ye mwenyewe amewahi kuwa mtendaji anajua wanadanganya vp... Baada ya kuchukua nchi alitakiwa awe anaingia front. Sasa kalagabaho!
 
Kuna watu humu ndani wanaongea mambo bila kufikiri vizuri. Vijana wanapokuwa jobless na wananjaa huwa ni 'time bomb'. Vijana hao ndio husababisha uhalifu kuongezeka katika jamii kama vile udokozi( ukibaka), wizi na hata ule wa kutumia silaha ili wapate mlo. Kibaya zaidi hao ndio hufanya tusilale kwa amani majumbani mwetu. Na hata ukipaki gari lako unahofia kung'olewa power window na taa. Na hao ndio huwa chanzo cha political instability. Kwa hiyo ukishiba usimcheke aliye na njaa. Jambo la msingi ni kumsaidia aondokane na dhiki aliyonayo kama inawezekana. Wengi wetu tunaowadharau wenye njaa humu kwenye jukwaa ni sisi tunaowaibia hao hao tunaowadharau kupitia dhamana tulizokabidhiwa. Ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom