omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
Wakuu hapa tusidanganyane, Rais Kikwete, alinunua media zote na vyombo vyote muhimu vya taifa ikiwa ni pamoja na Usalama wa Taifa chini Mkurugenzi ya mstaafu wa huko, na mwishoni alimnunua mpaka rais Mkapa, aliyetumia madaraka yake kumpitisha kwa nguvu,
Kikwete pia aliwanunua mpaka waalimu wa Mlimani, aliwanunua mpaka baadhi ya wa-Tanzania wenzetu waliokuwepo BBC London, hawa kwa kushirikiana kwa pamoja walituhadaa wananchi wa Tanzania tena bila aibu kuwa wamefanya Polls ambazo zinaonyesha Kikwete tu ndiye anayetakiwa kuwa rais, lakini toka awe rais hatujasikia wakifanya Polls tena kutuambia anything else kuhusu taifa letu, au hata huyo rais alipo na Polls leo.
Kaka u can do better than this mediocrity generalization/conclusions)samahani kwa kutumia maneno mazito).
Kuhus MEDIA unajua wazi kuwa sio JK aliyehusika kwa karibu na hili. Ilikuwa ni shughuli ya LOWASSA na ROSTAM kwa manufaa yao wenyewe. Vilevile sio wote waliokuwa wakimremba JK walinunuliwa. Wapo waliokuwa wakiamini wazi kuwa ndiye anayewafaha na hawakuwa wakifanya waliyoyafanya kutokana na kununuliwa kama unavyodai. Lakini kumbuka JK aliuzika sio kwa uwezo wake lakini kwa kuwa mbadala wa "mwarabu" Salim, "Kikongwe" Malecela "aliyelaaniwa na Mwalimu", "FISADI ama ZERO" Sumaye, "Mlevi na rafiki ya MKAPA" Kigoda na propaganda zengine za kweli na zisizo za kweli....
Kuhusu wasomi na hapa nasema tena kuwa si kweli JK alikuwa na uwezo wa kuwanunua wasomi hasa wale wa MLIMANI. Kama ni suala la REDET mimi nimekuwa karibu na shughuli zao na hata ile opinion poll iliyofanyika kabla ya uchaguzi wa 2005. Si kweli zoezi lile halikufanyika kisomi. Hatua zote za kisomi zilifuiatwa na wala zoezi hii halikumhusisha Prof Mkandala pekee ambaye ndiyo amekuwa kinara wa tuhuma kuwa wasomi walikuwa wanatumiwa na JK. Zoezi la kujua maoni ya watanzania lilifuata hatua zote za kisomi. Tatizo ni ukaribu wa JK na Prof Mkandala (na UKADA wake kama walivyo wasomi wengine) wakati ule na hata hivi sasa ambao ulipelekea kujenga taswira ya kumbeba JK....
Kuna wasomi kama Prof CHACHAGE ambaye alikuwa na mategemeo makubwa na JK. Katu huwezi kuniambia kuwa Prof Chachage niliyemjua mimi naye pia alikuwa amenunuliwa na vijisenti vya JK. Wapo walikuwa wakiamini kwa dhati kuwa JK ni mwakilishi wa wanyonge na angekuwa na uwezo mkubwa wa kushughulikia madhila ya wanyonge wenzake. Wapo waliokuwa wakiamini kuwa JK ni mjamaa asilia ambaye angeweza kuirudisha CCM kutoka katika mikono ya Walalakheri na kuwawezesha walalahoi kurudisha sauti yao katika chama hicho. Prof Chachage alikuwa mmoja wa hawa na katu imani yake kwa JK halikuwa eti kwa kuwa alinuliliwa.....Namtumia Prof Chachage kama mfano wa wasomi ambao walimuunga mkono JK kwa dhati kutokana na imani waliyokuwa naye juu yake na sio eti walinunuliwa......wapo wengi wengine..
Tanzanianjema