JK tazama mwezio huyu

Wakuu hapa tusidanganyane, Rais Kikwete, alinunua media zote na vyombo vyote muhimu vya taifa ikiwa ni pamoja na Usalama wa Taifa chini Mkurugenzi ya mstaafu wa huko, na mwishoni alimnunua mpaka rais Mkapa, aliyetumia madaraka yake kumpitisha kwa nguvu,

Kikwete pia aliwanunua mpaka waalimu wa Mlimani, aliwanunua mpaka baadhi ya wa-Tanzania wenzetu waliokuwepo BBC London, hawa kwa kushirikiana kwa pamoja walituhadaa wananchi wa Tanzania tena bila aibu kuwa wamefanya Polls ambazo zinaonyesha Kikwete tu ndiye anayetakiwa kuwa rais, lakini toka awe rais hatujasikia wakifanya Polls tena kutuambia anything else kuhusu taifa letu, au hata huyo rais alipo na Polls leo.

Umasikini wetu wa-Tanzania na njaaa kubwa tuliyonayo ya kudumu, ndiyo vimetufikisha hapa tulipo na uongozi wa taifa letu wa Ze-Comedy, Ohhh yeah now we are stuck, hata hao waliokuwa wakijikomba kwake Kikwete ili wapate madaraka leo hawana raha tena maana wanajua fikakuwa hawana heshima mbele ya jamii, wananchi hatuwaheshimu kabisaa, leo rais Kikwete aliyekua bingwa wa kukutana na wananchi hata magengeni sasa anawakimbia wananchi wale wale kulikoni?

Kikwete aliyekuwa bingwa wa kukutana na wananchi kwenye kila kona ya US, leo hataki kabisaa na wasaidizi wake ni wakali kama pili pili ukiwatajia hilo la rais kukutana na wananchi, kulikoni? Huyu ndiye aliyewanunua wanamuziki kina Ally Choki na Muumini Munir, kila kukicha kwenye nyimbo zao hawakuisha kumtaja taja kwamba Kikwete ni mtu wa watu, mtu wa watu my fooot! sasa mtu wa watu anakimbia vipi tena hao hao watu ambao zamani alikuwa mtu wao? Au alikuwa anataka madaraka tu sasa hawahitaji tena?

Mheshimiwa Rais Kikwete, umetufikisha mahali ambapo tumejaribu sana kupakwepa kupafikia, na tumejaribu sana kukataa kuwa tupo napo, tumejaribu sana kukutetea kuwa upewe muda, we have done everything kujaribu kukupa nafasi ili urekebishe taifa letu, lakini sasa umefika wakati hatuwezi kukudanganya tena, kwamba kinachoendelea kwenye utawala wako ni aibu kubwa sana kwa kijana kama wewe kutufikisha wananchi kwenye this junction where sasa tunakosa uaminifu na kiongozi yoyote, kuanzia wewe mwenyewe mpaka wanaokuzunguka, simply ni kwamba wote mnanuka rushwa na uwezo mdogo sana wa kuongoza taifa letu.

Haya maneno ya Zuma, they are coming tena soon maana inaonekana huenda wananchi wa taifa hili tukamhitaji shetani Lowassa, ili kukuondoa kwenye kura za huko ndani ya CCM, huwezi kumlaumu mtu yoyote ila ni wewe mwenyewe na tamaa yako ya kusifika na uongozi ambao umeshindwa kuonyesha matendo enough ya kutuaminisha wananchi kwamba una-deserve another term, umeanza kukimbia wananchi huko US na UK, sasa unaanza kuwakimbia wananchi hata wa Mbeya tu? I mean how low can it get na uongozi wako? Maandamano ya Ma-Albino, hukuyajua kabla hujaenda Mbeya kuwa yatakuwepo? Serikali nzima ya Tanzania haiwezi kuwapokea hao ndugu zetu mpaka iwe wewe tu? Toka lini hiyo? Mbona Tabora watoto 19 viongozi wa baadaye wa taifa hili walipokufa mbona hukwenda?

Unajua ndugu zangu wananchi wa Tanzania, kama hatuwezi kuamka sasa tunakwenda down na huu utawala wa Ze-Comedy, ingawa wengine hatushangai sana kwa sababu tulionya mapema kuwa wananchi wa taifa hili we were about to make the worst mistake ever ambayo tutalipia sisi na watoto kwa vizazi vingi vijavyo, na here we are tumepotea!

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Wote mnaomfananisha JK na Obama mnakosea pale mnapoenda mbali zaidi.
Mwambie JK aende pale Berlin,German akapull crowd na yeye.
Obama ana world wide movement...Awe Rais asiwe rais movement yake itabaki pale pale...Ni kama movement ya MLK nk.
JK yeye hapo bongo ni maneno matamu na ulaghai wa ccm...JK alikuwa yuko karibu na wananchi na hata mimi mwenyewe kukumbana na JK na kumpungia maeneo flani flani hapo bongo ilikuwa ni kama norm...Watu walimwona ni mtu wa watu kutokana na hilo alitakiwa kuja na sera tu na mambo ntolee.
Jamii ya wamarekani na bongo ni mbili tofauti...Hata ukiwa na wamarekani kwenye somo la historia ama hata mtaani tu kwenye stori za kawaida unasikia tu we bombed this we killed Saddam we give them freedom,we are fighting the terrorists and so forth.
Hapo bongo ni stori za tofauti...Tulipata uhuru 1961,nchi iliuzwa,UKIMWI unauwa sana,malaria ni balaa,Kipindu pindu chauwa 20 Dar nk.
Jamii hizo zina mindset ya tofauti na kwasababu mtu kama Obama anarelate na wananchi wa aina tofauti duniani kote na hapo utashangazwa ni kivipi watu wenye historia za tofauti waweze kumwelewa na kumshabikia.
Mnaomfananisha JK na Obama kwenye hili naomba mjuwe pia kuwa Obama akija hapo Bongo...Rais ama Non Rais...Atapull nyomi si kidogo.....Hilo liko wazi....JK nayeye anaweza hilo hapa USA?
JK yeye aachane na siasa zisizoona mbele...Obama hata asiposhinda respect yake duniani itabaki pale pale.
 
"Mkapa kamaliza fresh maana hakuna aliyetegemea anaweza kutimiza aliyokuwa ameahidi. kwanza kila mtu aliamini hata Urais hatouweza kwamba tungekuwa tunaongozwa na Nyerere kupitia Mkapa. hiyo imemuwezesha kutulia na kuweza kujipanga na kutimiza zaidi ya 80% ya alivyotaka kufanya."

Endeleaaa kaeleza yote vizuri lakini katibua kwa kumtaja Mkapa eti ni mfano wa "usafi" wa utawala wake. Hivi tumeshasahau:
a) Mkapa hakustahili kuwa mgombea Urais mwaka 1995 ila tu Nyerere alimpora JK (sio siri). Ndio maana kuna hisia kwamba Mkapa ilibidi ampiganie JK amshinde SAS "kulitoa hilo ndonge ktk mtima wake" na kulipa fadhila alizokapewa in a silver plate. Ukweli kuwa alibebwa na Nyerere miaka yake minne ya awali upo pale pale – politically Mkapa was unknown and unpopular B4 his nomination.

b) Sijui Endeleaaa kapata wapi takwimu za mafanikio ya 80% kwa Mkapa lakini taarifa zisizo na ubishi (undisputable facts) ni kuwa:
Awamu ya Mkapa ndio iliyoongoza idadi ya MAFISADI akiwepo na yeye mwenyewe;
- Ununuzi wa Rada (idadi ya Airlines imepungua JNIA badala ya kuongezeka tofauti na walivyokatarajia - Gulf Air, Oman Air, Air India haziji Dar tena!)
- Mikataba mingi ovyo ya madini enzi yake
- Scramble for EPA loot
- Ujenzi wa Twin Towers (jamanii, eti tunahitaji hayo ma-sky scrappers wakati barabara ya Lindi kwenda Masasi kuna DARAJA DOGO LA NANGOO, WILAYA YA MASASI LINACHUKUA MIAKA SABA HALIJATENGENEZWA (ipo diversion yenye daraja la muda la mbao na hapo mtoni palishaua watu ktk basi)
- RICHMOND, TICTS, ATCL, TRC, n.k. ni kinara wake
c) Ni awamu ya Mkapa iliyoshuhudia Bongo kutoa wakimbizi na kwenda kuishi ktk mahema kule Mombasa (Refugees) baada ya Askari wake kuwaua kwa maksudi (in cold blood) Wapemba 27. Yaani Wabongo tuliyanyamazia mauaji hayo lakini tunapiga kelele vifo vya watoto 19 awamu ya JK (hii ni double standard)!
d) Huyo huyo Mkapa ndiye aliyepiga marufuku kuingiza TZ, kusoma, kuchapisha au kusambaza kitabu cha Dr. Hamza Mustafa Njozi cha "Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania" na kuwanyima Wananchi uhuru wa kujua taswira ya maudhui yaliyoandikwa na mzalendo mwenzao.
e) Mkapa ndiye aliyeanzisha "kuzungumza" na Wananchi kila mwisho wa mwezi kupitia TV na radio. Huko sio kuzungumza jamani bali ni kuhutubia au kusoma taarifa kwa watazamaji/wasikilizaji kwani yule wa upande wa pili hawezi kumjibu Rais ama kumwuliza swali. Ni Alhaji Mwinyi pekee ktk Awamu zote 4 aliyekuwa anazungumza na Walalahoi pale CCM ofisi ndogo Mtaa wa Lumumba na kuwasikiliza "live" matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi mda huo huo. Kwa hili, NANI KAMA MZEE RUKSA?
f) Tahadhari kuh mada ya Kitila Mkumbo: kumlinganisha Obama na JK kutokana na kadamnasi ya wasikilizaji sio kipimo sawia. Wote wawili kuna wanaowapenda sana sana lakini pia wapo wanaowakosoa kwa nia njema (criticise), wanaowahujumu ndani ya vyama vyao kwa sababu moja au nyingine (hypocritics) na wapinzani ndani na nje ya vyama vyao wasiolisifia jema lo lote (haters). Nasaha ninayotoa ni hii: It's too early to congratulate Obama - plse leave him to rest in peace. AMEN!
 
Wakuu hapa tusidanganyane, Rais Kikwete, alinunua media zote na vyombo vyote muhimu vya taifa ikiwa ni pamoja na Usalama wa Taifa chini Mkurugenzi ya mstaafu wa huko, na mwishoni alimnunua mpaka rais Mkapa, aliyetumia madaraka yake kumpitisha kwa nguvu,

Kikwete pia aliwanunua mpaka waalimu wa Mlimani, aliwanunua mpaka baadhi ya wa-Tanzania wenzetu waliokuwepo BBC London, hawa kwa kushirikiana kwa pamoja walituhadaa wananchi wa Tanzania tena bila aibu kuwa wamefanya Polls ambazo zinaonyesha Kikwete tu ndiye anayetakiwa kuwa rais, lakini toka awe rais hatujasikia wakifanya Polls tena kutuambia anything else kuhusu taifa letu, au hata huyo rais alipo na Polls leo.

Umasikini wetu wa-Tanzania na njaaa kubwa tuliyonayo ya kudumu, ndiyo vimetufikisha hapa tulipo na uongozi wa taifa letu wa Ze-Comedy, Ohhh yeah now we are stuck, hata hao waliokuwa wakijikomba kwake Kikwete ili wapate madaraka leo hawana raha tena maana wanajua fikakuwa hawana heshima mbele ya jamii, wananchi hatuwaheshimu kabisaa, leo rais Kikwete aliyekua bingwa wa kukutana na wananchi hata magengeni sasa anawakimbia wananchi wale wale kulikoni?

Kikwete aliyekuwa bingwa wa kukutana na wananchi kwenye kila kona ya US, leo hataki kabisaa na wasaidizi wake ni wakali kama pili pili ukiwatajia hilo la rais kukutana na wananchi, kulikoni? Huyu ndiye aliyewanunua wanamuziki kina Ally Choki na Muumini Munir, kila kukicha kwenye nyimbo zao hawakuisha kumtaja taja kwamba Kikwete ni mtu wa watu, mtu wa watu my fooot! sasa mtu wa watu anakimbia vipi tena hao hao watu ambao zamani alikuwa mtu wao? Au alikuwa anataka madaraka tu sasa hawahitaji tena?

Mheshimiwa Rais Kikwete, umetufikisha mahali ambapo tumejaribu sana kupakwepa kupafikia, na tumejaribu sana kukataa kuwa tupo napo, tumejaribu sana kukutetea kuwa upewe muda, we have done everything kujaribu kukupa nafasi ili urekebishe taifa letu, lakini sasa umefika wakati hatuwezi kukudanganya tena, kwamba kinachoendelea kwenye utawala wako ni aibu kubwa sana kwa kijana kama wewe kutufikisha wananchi kwenye this junction where sasa tunakosa uaminifu na kiongozi yoyote, kuanzia wewe mwenyewe mpaka wanaokuzunguka, simply ni kwamba wote mnanuka rushwa na uwezo mdogo sana wa kuongoza taifa letu.

Haya maneno ya Zuma, they are coming tena soon maana inaonekana huenda wananchi wa taifa hili tukamhitaji shetani Lowassa, ili kukuondoa kwenye kura za huko ndani ya CCM, huwezi kumlaumu mtu yoyote ila ni wewe mwenyewe na tamaa yako ya kusifika na uongozi ambao umeshindwa kuonyesha matendo enough ya kutuaminisha wananchi kwamba una-deserve another term, umeanza kukimbia wananchi huko US na UK, sasa unaanza kuwakimbia wananchi hata wa Mbeya tu? I mean how low can it get na uongozi wako? Maandamano ya Ma-Albino, hukuyajua kabla hujaenda Mbeya kuwa yatakuwepo? Serikali nzima ya Tanzania haiwezi kuwapokea hao ndugu zetu mpaka iwe wewe tu? Toka lini hiyo? Mbona Tabora watoto 19 viongozi wa baadaye wa taifa hili walipokufa mbona hukwenda?

Unajua ndugu zangu wananchi wa Tanzania, kama hatuwezi kuamka sasa tunakwenda down na huu utawala wa Ze-Comedy, ingawa wengine hatushangai sana kwa sababu tulionya mapema kuwa wananchi wa taifa hili we were about to make the worst mistake ever ambayo tutalipia sisi na watoto kwa vizazi vingi vijavyo, na here we are tumepotea!

Mungu Ibariki Tanzania.

mkulu napomgeza maneno yako ya busara...laiti haya maneno yangefika mezani kwa mkulu....ze comedy....kimsingi nakubaliana nawee na hata 2005 kwenye uteuzi wa ccm ,wengi tuliliona tatizo kwa kikwete lakini tatizo sauti zetu hazikupenya masikio ya wanachama waliokuwa wakichagizwa na hadi watumishi wa MUNGU walionunuliwa kwa bei rahisi ili kutuambia kuwa KIKWETE NI CHAGUO LA MUNGU!!
 
Jamani mpeni prezidaa wetu muda kidogo, he has been vere busy making crucial decisions so far, like deciding to change the motor blocade from mercedes benz to BMWs and X5's, or what suit to wear with chris Tucker and Boyz II Men appearances... He will soon come around.
 
Wakuu hapa tusidanganyane, Rais Kikwete, alinunua media zote na vyombo vyote muhimu vya taifa ikiwa ni pamoja na Usalama wa Taifa chini Mkurugenzi ya mstaafu wa huko, na mwishoni alimnunua mpaka rais Mkapa, aliyetumia madaraka yake kumpitisha kwa nguvu,

Kikwete pia aliwanunua mpaka waalimu wa Mlimani, aliwanunua mpaka baadhi ya wa-Tanzania wenzetu waliokuwepo BBC London, hawa kwa kushirikiana kwa pamoja walituhadaa wananchi wa Tanzania tena bila aibu kuwa wamefanya Polls ambazo zinaonyesha Kikwete tu ndiye anayetakiwa kuwa rais, lakini toka awe rais hatujasikia wakifanya Polls tena kutuambia anything else kuhusu taifa letu, au hata huyo rais alipo na Polls leo.

Umasikini wetu wa-Tanzania na njaaa kubwa tuliyonayo ya kudumu, ndiyo vimetufikisha hapa tulipo na uongozi wa taifa letu wa Ze-Comedy, Ohhh yeah now we are stuck, hata hao waliokuwa wakijikomba kwake Kikwete ili wapate madaraka leo hawana raha tena maana wanajua fikakuwa hawana heshima mbele ya jamii, wananchi hatuwaheshimu kabisaa, leo rais Kikwete aliyekua bingwa wa kukutana na wananchi hata magengeni sasa anawakimbia wananchi wale wale kulikoni?

Kikwete aliyekuwa bingwa wa kukutana na wananchi kwenye kila kona ya US, leo hataki kabisaa na wasaidizi wake ni wakali kama pili pili ukiwatajia hilo la rais kukutana na wananchi, kulikoni? Huyu ndiye aliyewanunua wanamuziki kina Ally Choki na Muumini Munir, kila kukicha kwenye nyimbo zao hawakuisha kumtaja taja kwamba Kikwete ni mtu wa watu, mtu wa watu my fooot! sasa mtu wa watu anakimbia vipi tena hao hao watu ambao zamani alikuwa mtu wao? Au alikuwa anataka madaraka tu sasa hawahitaji tena?

Mheshimiwa Rais Kikwete, umetufikisha mahali ambapo tumejaribu sana kupakwepa kupafikia, na tumejaribu sana kukataa kuwa tupo napo, tumejaribu sana kukutetea kuwa upewe muda, we have done everything kujaribu kukupa nafasi ili urekebishe taifa letu, lakini sasa umefika wakati hatuwezi kukudanganya tena, kwamba kinachoendelea kwenye utawala wako ni aibu kubwa sana kwa kijana kama wewe kutufikisha wananchi kwenye this junction where sasa tunakosa uaminifu na kiongozi yoyote, kuanzia wewe mwenyewe mpaka wanaokuzunguka, simply ni kwamba wote mnanuka rushwa na uwezo mdogo sana wa kuongoza taifa letu.

Haya maneno ya Zuma, they are coming tena soon maana inaonekana huenda wananchi wa taifa hili tukamhitaji shetani Lowassa, ili kukuondoa kwenye kura za huko ndani ya CCM, huwezi kumlaumu mtu yoyote ila ni wewe mwenyewe na tamaa yako ya kusifika na uongozi ambao umeshindwa kuonyesha matendo enough ya kutuaminisha wananchi kwamba una-deserve another term, umeanza kukimbia wananchi huko US na UK, sasa unaanza kuwakimbia wananchi hata wa Mbeya tu? I mean how low can it get na uongozi wako? Maandamano ya Ma-Albino, hukuyajua kabla hujaenda Mbeya kuwa yatakuwepo? Serikali nzima ya Tanzania haiwezi kuwapokea hao ndugu zetu mpaka iwe wewe tu? Toka lini hiyo? Mbona Tabora watoto 19 viongozi wa baadaye wa taifa hili walipokufa mbona hukwenda?

Unajua ndugu zangu wananchi wa Tanzania, kama hatuwezi kuamka sasa tunakwenda down na huu utawala wa Ze-Comedy, ingawa wengine hatushangai sana kwa sababu tulionya mapema kuwa wananchi wa taifa hili we were about to make the worst mistake ever ambayo tutalipia sisi na watoto kwa vizazi vingi vijavyo, na here we are tumepotea!

Mungu Ibariki Tanzania.

Mkuu tuko pamoja
Uliyoyasema ni ukweli mtupu
 
Jamani mpeni prezidaa wetu muda kidogo, he has been vere busy making crucial decisions so far, like deciding to change the motor blocade from mercedes benz to BMWs and X5's, or what suit to wear with chris Tucker and Boyz II Men appearances... He will soon come around.

Hivi wewe ndugu yangu bado unadanganyika na propaganda za kina Kingunge na Makamba eti mpaka sasa bado una matumaini ya Rais kupewa muda ndipo atawachukulia hatua wezi wa epa,matapeli wa richmond,atawapa watanzania ajira milioni moja alizoahidi,atautafutia mpasuko wa kisiasa zanzibar suluhisho la kudumu,atarudisha nyumba za serikali zilizoporwa nk
Hivi huo muda ni muda gani hasa mnaoutaka wakati tulimchagua kwa kipindi cha miaka 5 na aliahidi kuyatekeleza hayo yote na sasa anaelekea ukingoni mwa ngwe yake?
 
Wtz sometimes huwa wananichosha utashangaa 2010 anapeta na chama chake.
 
Watanzania wenzangu,

Tulipanda bangi hapo 2005 na sasa tunavuna bangi. Hatuwezi kupanda bangi na kuvuna mahindi.

Yanayotekea sasa yalishaonekana wakati wa kampeni za uchaguzi 2005 hivyo hakuna cha kushangazaa wala kipya.
Listi ya Jakaya ilijulikana na mpaka sasa inajulikana ( Ni mafisadi tupu) kwani ndiyo waliompa support ya hali na mali ya kwenda Ikulu, na sasa ndiyo wanaongoza nchi jinsi watakavyo na Kikwete yupoyupo tu.
 
Hivi wewe ndugu yangu bado unadanganyika na propaganda za kina Kingunge na Makamba eti mpaka sasa bado una matumaini ya Rais kupewa muda ndipo atawachukulia hatua wezi wa epa,

Unajua ishu zingine huhitaji kuwa Professor, kujua ukweli wake na pumba zake, unapoongelea Kikwete, Makamba, Msekwa na Kingunge unachosema exactly ni kwamba,

Katika miaka zaidi ya 45 ya uhuru wa nchi hii Tanzania, leo 2008 hawa viongozi wanne ndio the best vichwa vya kutuongoza wananchi Millioni 40, does that make sense?
 
Jamani siasa zina misimu wakulu wangu, JK alinufaika na kalizmatik pawa aliopewa na mungu ktk uchaguzi wa 2005, kwani hata Mwita yule UVCCM alipokuwa Rais wa DARUSO alipingana na VC wa sasa wa UDSM kuhusiana na JK kuwa the best candidate kwa CCM 2005 lakini alishindwa kutokana na nguvu za mvuto wa JK by then lakini CCM nayo ilihitaji Rais wa aina hiyo kwa wakati ule hivyo haikuwa rahisi kuwakosa ama JK au SAS. Ndiyo siasa na Demokrasia wakuu wangu. Mabadiliko ya America yanayopigiwa sasa ni ama Black au Mama akae Jumaba jeupe,hawazungumzi haya hadharani ila mioyo yao inataka na ni wajibu wa vyama vyao vikuu kujibu kiu hizo kwa kuwaletea wagombea wenye sura hizo.

Nikubaliane na yeye JK kuwa ilimchukua 10yrs kuipata fursa aliyonayo sasa hivyo hii inathibitisha hoja yangu ya huko nyuma tulipokuwa tunalumbana juu yake, nilibainisha kuwa 1995 JK hakuwa chaguo halisi la wana CCM maana wao wana CCM walikuwa radhi SAS au Edward Lowasa waichukue nchi toka kwa mzee Mwinyi, 1995 mzee Mwinyi alitamani amkabidhi nchi hii JSM lakini tayari JKN alishamzidi nguvu huku akisaidiwa na UVCCM ya kaka yangu John ambaye sasa ni M/kiti CCM Dsm, ni wao waliotumwa na Mwalimu wamfuate Salim Ethiopia lakini SAS akakataa na hapo ndipo interest ya vijana ikahamia kwa mwanaharakati mwenzao Edward, naye akijua mvutano wa udini uliomo ndani ya CCM akaona ni vema amhusishe na JK ktk pattern yao ya kusaka nchi, aliiamini sana nguvu ya UVCCM na kuwa mwalimu ni mmoja wa mashabiki wa machaguo ya vijana kwa kuangalia kupanda kwa SAS, Hamad na wengineo, hapo ndipo unapoona timu ya akina Mkuchika,Makinda na wengineo wakijipenyeza na kushamiri, JKN akagundua game hiyo na kisayansi akajitenga nao akisubiria dakika ya kuwashughulikia akina Guninita, akaanza kwa ku disco Edward na kumpa chati CD huku akiwapa moyo UVCCM kwa ujio wa JK, kumbukeni 95 nchi ilishaingiwa na udiniudini na manung'uniko yasiyo na kichwa wala miguu, JKN alishajua hilo na alijua wazi kwa kumtosa JSM na Edward UVCCM hatakuwa na la zaidi ya kumuunga mkono JK na hapo ndipo mtego ulimsurubu mzee Mwinyi na baadhi ya vigogo wa CCM kwani walijikuta wanaingia mtegoni na kuelekeza mapenzi ktk imani zao zaidi kuliko itikadi za chama chao, JKN akabaki yeye pekee ndie msimamizi wa itikadi ya CCM na hapo akawa amewapata wana usalama kiurahisi na kuifanya kazi ya kumptisha Ben William Mkapa mtu ambaye hakuwa na kundi ndani ya CCM na wala kukubalika miongoni mwa mwa waTZ, haikuwa ngumu kuzipata kura za Zenj ambazo zilihamishwa toka kwa CDM kuja BWM ktk raundi ya pili. Ikumbukwe pia ktk Halmashauri kuu CDM ndiye aliyeongoza akifuatiwa na JK na BWM, baada ya hapo kampeni chafu kati ya JK na CDM zikajitokeza na JK akasimama hadharani akimshutumu Lawrence Mutazama Gama kuwa anamhujumu in favor of CDM automatically BWM akathibitika kuwa ni mtu asiye na makundi ndani ya CCM na kwa hali ya nchi ilivyokuwa na CCM yenyewe iliaminika dhahiri kuwa huyu anafaa kuibeba nchi na kuiunganisha.

Siasa za msimu zilimpa fursa Ben William Mkapa nchi na siyo hujuma dhidi ya JK au CDM kama tunavyoamini.

JK amepewa nchi ktk hali hiyohiyo, umma uliridhika sana na Ben anavyoiacha nchi, kwa wakati ule tuliamini na bado tunaamini kuwa dunia ni kijiji kimoja hivyo kiongozi wa diplomasia na mvuto kwa umma ni moja ya njia bora kabisa ya kuipeleka nchi yetu mbele, nani aliyekuwa na mvuto wa kidiplomasia zaidi kati ya JK na SAS? 10 yrs foreign under Mkapa, karisma pawa yake kwa umma hata kama magazeti yasingelijiingiza bado JK ali stand better chance kwa mvuto zaidi ya SAS ila si ktk diplomasia hapo SAS alikuwa juu, SAS alizidiwa ktk hilo kwa nguvu ya ziada ya BWM iliyomfanya JK akubalike sana miongoni mwa umma.

Tujifunze kukubali nguvu za wakati na pengine kukabilina nazo ili jamii iuone ukweli halisi wa mambo kabla na tuache nge--- nge .

Pengine tujiulize ktk hali ya Zenj , SAS angefanya nini kama rais wa TZ? Ni nani aliyekuwa na nafasi nzuri kuikabli hali hiyo kati ya SAS na JK?

Mvuto wa waisalamu ktk uchaguzi 2005, ni nani alikuwa bora zaidi kati ya SAS na JK?
Angalieni na mchnago wa wakristo ktk uchaguzi ule walimkubali nani zaidi kati ya JK na SAS?

Tuangalie pande zote za shilingi positively na negatively kama tunataka kujenga.
Siku njema wakuu
 
Hapana. Mwanzo wake JK haukuwa kama wa Obama. Obama unajua anasimama wapi. JK aliwalaghai Watanzania kwa lugha rahisi rahisi ya maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kasi mpya ari mpya etc.

kwakweli ni dhambi kumfananisha JK na Obama. Obama anaweka mambo yake wazi kwa kuchanganua jinsi gani akavyoleta mabadiliko uko US. lakini JK alikuwa anatuimbia wimbo tu wa Ari mpya......
kwa kweli nashukuru sana sikumpigia kura, maana ningekuwa najilaumu sasa.
 
Ndugu zangu,

Katika hili suala naomba kuwaomba mkubali ukweli kwamba watanzania wote tunapaswa kubeba lawama na wala si Jakaya pekee yake.
Jakaya alipokuwa anaomba kura ama ridhaa ya watanzania kwenda Ikulu tuliona na kusikia wazi mapesa yakimwagwa kama njugu kila kona ya Tanzania.
Jakaya amekuwa mtumishi wa serikali kwa muda mrefu na wala hajawahi kuwa mfanyabiashara mashuhuri, sasa kwanini tusijiulize mapema wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba huyu Jakaya anapata wapi mapesa ya kumwaga kama njugu?. Jakaya alinunua kura zetu kwa maana kwamba tuliuza haki zetu kimsingi na kwa sasa hatuna haki tena ya kumuuliza anafanyia nini kura zetu alizonunua. Je na yeye akianza kuwauliza watanzania mlifanyia nini mapesa aliyowapa wakati wa kampeni mtamjibu nini?.

Hapa napenda kuwaeleza kwamba tuwe makini sana katika kuchambua, kupendekeza na kuchagua viongozi wa ngazi za juu. Tusibabaike na sauti nzuri, wala ahadi tamutamu, wala sura, wala pesa, wala kujuana.

Yanayotea katika uongozi wa Tanzania kwa sasa ni lawama zinatuhusu watanzania wote. Kama kweli tumechoka na kuelewa makosa yetu basi tuige mfano wa wana Tarime na Mbeya ili 2010 uwe ndiyo mwisho wa Chama Cha Mafisadi kutawala Tanzania.

SO totally agree with but mwisho wa mafisadi kutawala??? mh mh dont think so.
 
Big crowd doesn't means that people will cast their vote for you. I think Dems wenyewe wanahofia Bradly effect.
Mimi naofia another watergate scandal kwenye campaign finance. Milion 150,000 a month?
Hey where is the money coming from?
 
sakata la mawe mbeya ni wzi wananchi wamemchoka rais na wal si kitu kingine kama anvyodai salva
 
Tuangalie pande zote za shilingi positively na negatively kama tunataka kujenga.
Siku njema wakuu

Kuhusu mwaka 1995, Mwalimu aliwekeza nguvu zake zote kwa SAS. Hakuwa amejiandaa kukabiliana na upande wa pili yaani hakutegemea kuwa SAS angeweza kukataa. Ukisoma Rai ya Jenerali kwenye ile Makala ndefu aliyoiita Barua Ndefu kwa JK. Kuna mahali aliandika JK aliwahi kuitwa Ikulu ambapo aliwakuta Mwalimu na Mzee Mwinyi. Huko ndiko alikoambiwa akachukue fomu. Kama maelezo haya ya Jenerali Ulimwengu ni yakweli basi Mwalimu alikuwa 'akitapatapa' nani awe Rais baada ya SAS kumbwaga. Swali ninalojiuliza ni LINI na KWANINI Mwalimu alikuja badili msimamo na kuamua kumuunga mkono BWM maana naambiwa ilichukuwa masaa mengi hadi usiku wa manane BWM kukubali kuchukua fomu baada ya mwalimu kuwatuma wajumbe wake wamfuate BWM pale Selenda Bridge Club. Ukiondoa mahusiano yao mengine lakini ikumbukwe Ben ndiye alikuwa akionekana kila siku Msasani kwa Mwalimu kupeleka 'Umbeya' wa yaliyokuwa yakijadiliwa Bungeni kuhusu kuanzishwa Serikali Tatu na ishu za lile kundi la G55!

Leo nilikuwa nafuatilia magazeti redioni. Naona Salva Rweyemamu kaibuka tena na kusema JK hakuwa na ratiba ya kuhutubia Uwanja wa Sokoine! Hivi jamani JK na kundi lake wanatuonaje sisi Watanzania! Hivi huyu Salva Rweyemamu ni MZIMA WA AKILI KWELI?!! (Nakumbuka aliwahi kujadiliwa humu kwamba ni Mtanzania au si Mtanzania na uhusiano wake na kina Jimmy Minani na kina Nkurunzinza?) Nadhani JK kama anataka kufanya jambo la maana amrudishe kule Gazeti la Uhuru, tena huko akawe Mhariri wa Michezo maana hiyo kazi anaiweza na tena kama anaongelea Simba ili wakashindane na mwenzake James Nhende ambaye ni mzuri akiwa anaongelea Yanga!

Maelezo ya Salva hayatamsaidia kabisa JK. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kupitia vyombo vya habari vya Mbeya na hasa Redio (Mbeya FM, Generation FM, Bomba FM) alinukuliwa akisoma ratiba ya Rais JK siku moja kabla ya ziara yake. Mkuu wa Mkoa alitamka kuwa siku ya mwisho JK angehutubia Wananchi pale Sokoine. Haya, Rais JK mwenyewe aliposimamishwa na lile kundi pale Mwanjelwa aliwaomba wale wananchi wachague wawakilishi wao na angeongea nao pale Sokoine. Haya, Uwanja wa Sokine umekuwa ukifanyiwa ukarabati mdogomdogo ikiwemo kuchonga barabara kuzunguka Uwanja! Nimeambiwa juzi wananchi walianza kujaa Uwanjani tangu saa mbili asubuhi, walichoambulia ni kutazama mechi kati ya Prisons na Polisi Morogoro!

Hata kama tulishakuwa Mabwege siku za nyuma, JK na wapambe wake waache kutufanya Mazuzu kiasi hiki! Ptuu!! Tumechoka ila ngoja tuishie hapa isije ikaonekana kuwa tunarusha mawe 'kimtindo' halafu wakatumwa akina Tossi kutusaka ukizingatia kuwa na sisi tumo humo humo kwenye New Komedi Gavamenti!
 
Back
Top Bottom