JK; Nimekubali Kuwa Ben Mkapa Ni Simba Ingawa Hangurumi!

yawezekana kweli nkapa ni simba maana jk ni yanga damdam kwa maana hiyo hivyo ni v2 tofauti.
 
Baada ya wanamtandao kumfitinisha Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa mwaka 2005 huku wakipandikiza chuki dhidi ya Mkapa kwa madai kuwa alikuwa hamtaki Kikwete chuki ambazo zimewahi hata kuandikwa na magazeti nchini , ikiwa ni mwaka wa sita akiwa madarakani rais Jakaya Kikwete amewaambia wasaidizi wake Mkapa ni simba ingawa haungurumi kwa maana ya kutopenda kujionyeshajionyesha. Kubadili mtazamo kwa Kikwete dhidi ya Mkapa ndiyo kunaelezwa kuwa ndiyo kiini cha mzee Ben Mkapa kurejea kwa kasi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa, na siyo hivyo tu lakini pia inaelezwa tayari Kikwete ameanza kuandaa mkakati wa kuhakikisha Mkapa anakuwa Mwenyekiti wa CCM kwa mara nyingine tena ili kumaliza makundi hasimu ndani ya chama hiko lakini pia ili kuivusha salama CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Hii track imerekodiwa studio gan ili tupate moyo wa kuickliza coz mkapa amechuja kwenye game kitambo(HANA MVUTO)..
 
kama rais aliyemaliza vipindi vyake viwili kwa mujibu wa katiba na kuendelea kutunzwa kwa posho inayotokana na kodi za wananchi Mkapa hakupaswa kuendeleza ushabiki wa kisiasa tena kwa kuponda vyama vya Upinzani.

Back
Top Bottom