Jk kwa kuwa umeboronga kwenye uchumi, heshima imebaki kwenye katiba

Mdomo Mwepesi

Member
Apr 19, 2011
67
93
Ni dhahiri kabisa kuwa ameshindwa kuinua uchumi wa nchi na badala yake ameendelea kuudidimiza. Katika hali hiyo hakuna kitu chochote cha maana atakachokumbukwa na Watanzania na hata kizazi kijacho. Nafasi aliyobaki nayo ni kuongoza mchakato wa kupatikana kwa katiba INAYOKIDHI MATAKWA YA WATANZANIA na siyo kundi fulani. Hayo ndiyo yatakuwa mafanikio yake kwa kipindi chake cha miaka 10 ya urais na si vinginevyo. Na ataweza kukumbukwa na kuheshimiwa kwa hilo tu.
 
Back
Top Bottom