Rais Samia, Tunaomba usimame kwenye chumba kimoja na siyo kwenye mstari

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,075
Katika watu waliompongeza sana Samia, toka siku za mwanzo ni vyama vya upinzani na wale wanaopenda demokrasia na utawala wa haki na sheria.

Katikati ya pongezi hizo, mara utawala wa Rais Samia ukamkamata Mbowe na kumbambikia kesi ya ugaidi kwa vile tu alisema kuwa CHADEMA itaendelea kudai katiba na hawatatii kauli ya Rais Samia kuwa harakati za katiba zisimame kwanza mpaka ajenge uchumi.

Kukamatwa kwa Mbowe na kisha kumbambikia kesi ya ugaidi, kuliwafanya watu kurudi nyuma na kujiuliza kama kauli za Samia kutaka kujenga Taifa lenye demokrasia, haki na utawala wa sheria zilikuwa ni kauli thabiti au porojo. Tukio lile liliwarudisha nyuma Watanzania wengi na kuanza kwenda kwa tahadhari na utawala huu wa Rais Samia.

Baada ya kumwachia Mbowe, kisha kuwaachia wanachama na viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliokuwa wamebambikiwa kesi, kuwaachia waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi, kuwalipa mafao waliotumikia nchi wakitumia vyeti visivyo vyao katika kutafuta elimu, imani ya wananchi ilianza kurejea tena kwa Rais Samia. Kisha Rais Samia akakubali kuwa twende kwa pamoja katika kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Mara akavuruga tena kwa kulikabidhi jukumu la kupatikana katiba mpya kwa kada wa CCM, bwana Mutungi, mtu ambaye wakati wote ametumika kuvuruga vyama vya siasa. Kumpa jukumu la kupatikana katiba mpya msajili wa vyama mvurugaji wa demokrasia, na mamluki wa CCM aliye na jukumu la kuua vyama vya upinzani vyenye nguvu, kuliwafanya watanzania wengi kutilia mashaka dhamira ya Rais Samia katika kuipata katiba mpya iliyo nzuri inayoendana na matakwa ya wananchi wote.

Katikati ya mashaka haya makubwa, utawala wa Rais Samia, kwa siri ukaamua kuipatia kampuni ya DP haki za yendeshaji bandari zote za Tanzania kupitia mkataba wa kimagumashi unaopora mamlaka ya nchi.

Katikati ya ubaya huu, Rais Samia amemfukuza kazi DC na DED ambao waliamua kuhamisha pesa toka eneo ambalo lina wananchi wengi wanaounga mkono siasa za upinzani na kuzipeleka pesa hizo kwenye eneo waliloamini kuwa lina wananchi wengi wanaoiunga mkono CCM. Rais Samia, akaona tendo hilo siyo sahihi, amewafuta kazi mara moja. Lakini wapo ambao hawakuelewa, wakasema kuwa DC na DED wamefukuzwa kazi na Samia kwa sababu kuna wanaCCM wamerudisha kadi za CCM. Lakini ukweli ni kwamba DC na DED walihamisha pesa ya miradi toka eneo linaloaminika kuwa na wananchi wengi wanaounga mkono vyama vya upinzani. Hivyo wale wanaCCM wa eneo hilo, nao wakachukia, na kuamua kuzirudisha kadi za CCM. Na kwenye hili Rais Samia ametenda haki, na anastahili pongezi.

Kuna wakati Rais Samia anatuweka katika dilemma na kuzisumbua nafsi zetu. Nafsi yangu inapata ugumu sana ninapomnenea mtu ubaya wakati pengine siyo amefanya mabaya lakini siyo mbaya kwa sababu hana dhamira mbaya.

Je, haya ambayo hayapendezi, kama haya ya bandari, yamefanyika kwa sababu Rais ana dhamira mbaya? Au alikuwa na dhamira njema lakini wabaya wakampeleka vibaya? Haya mambo ya kuwakamata wanaoukosoa mkataba mbaya wa bandari, na kuwabambikia makosa ya uhaini, yalikuwa ni maagizo ya Rais Samia au ni wale wabaya wanaomwingiza Rais kubaya wakati wote?

Ili tusipate shida, na wala tusimhukumu Rais kimakosa, tunamwomba Rais asimame ndani ya chumba na siyo kwenye mstari unaogawanya. Kama kuna vyumba viwili: kimoja ni cha utawala bora na kingine ni cha Utawala wa Fitina, basi Rais asimame kwenye chumba kimojawapo, na wala siyo kwenye mstari unaogawanya ili tutoe hukumu ya haki.

Hakuna mwenye chuki kwa Rais eti kwa sababu ni Mzanzibari, au eti kwa sababu ni mwanamke au eti kwa sababu ni muislam. Masikitiko na makasiriko yetu ni kwa yale yanayotendeka yanapoonekana yapo kinyume na maslahi ya Taifa la leo na la kesho.

Kama Rais kweli yupo na wananchi, na analitakia mema Taifa letu, atengebeze mazingira sahihi kwa haraka ya upatikanaji wa katiba, na siyo kuwa katika hali ya NATAKA SITAKI, kama ilivyo sasa.

Mkataba wa bandari ni mbaya, wanaosema ni mzuri, wengi wao ni watu wanafiki, wanaoamini kuwa kwa kusema hivyo wanamfurahisha Rais. Huu mkataba mbaya wa bandari, kama haubadilishwi au kufutwa ndio utakaofuta mema mengi ya Rais Samia.
 
Samia hana credibility ya kumchukulia hatua mtu yeyote anayekosea kwenye serikali yake, kwasababu kama ni makosa, basi hakuna kosa kubwa tulilofanyiwa watanganyika kama lile alilotufanyia yeye la kuzitoa bandari zetu zote kwa mwarabu aziendeshe milele.

- Hivyo kabla hajawachukulia hatua wengine wote, anatakiwa kwanza ajitazame yeye, asiwaonee hao wadogo.

Baada ya kukosea, na kutambua hilo, kwa kujua hana majibu ameamua kutunyamazia, kwa maana nyingine ameamua kujigeuza bubu na kuziacha bandari zetu zote ziende mikononi mwa mwarabu milele, huyu ni kiongozi mjinga asiyejua kuwajibika kwa anaowaongoza.
 
Katika watu waliompongeza sana Samia, toka siku za mwanzo ni vyama vya upinzani na wale wanaopenda demokrasia na utawala wa haki na sheria.

Katikati ya pongezi hizo, mara utawala wa Rais Samia ukamkamata Mbowe na kumbambikia kesi ya ugaidi kwa vile tu alisema kuwa CHADEMA itaendelea kudai katiba na hawatatii kauli ya Rais Samia kuwa harakati za katiba zisimame kwanza mpaka ajenge uchumi.

Kukamatwa kwa Mbowe na kisha kumbambikia kesi ya ugaidi, kuliwafanya watu kurudi nyuma na kujiuliza kama kauli za Samia kutaka kujenga Taifa lenye demokrasia, haki na utawala wa sheria zilikuwa ni kauli thabiti au porojo. Tukio lile liliwarudisha nyuma Watanzania wengi na kuanza kwenda kwa tahadhari na utawala huu wa Rais Samia.

Baada ya kumwachia Mbowe, kisha kuwaachia wanachama na viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliokuwa wamebambikiwa kesi, kuwaachia waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi, kuwalipa mafao waliotumikia nchi wakitumia vyeti visivyo vyao katika kutafuta elimu, imani ya wananchi ilianza kurejea tena kwa Rais Samia. Kisha Rais Samia akakubali kuwa twende kwa pamoja katika kupata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Mara akavuruga tena kwa kulikabidhi jukumu la kupatikana katiba mpya kwa kada wa CCM, bwana Mutungi, mtu ambaye wakati wote ametumika kuvuruga vyama vya siasa. Kumpa jukumu la kupatikana katiba mpya msajili wa vyama mvurugaji wa demokrasia, na mamluki wa CCM aliye na jukumu la kuua vyama vya upinzani vyenye nguvu, kuliwafanya watanzania wengi kutilia mashaka dhamira ya Rais Samia katika kuipata katiba mpya iliyo nzuri inayoendana na matakwa ya wananchi wote.

Katikati ya mashaka haya makubwa, utawala wa Rais Samia, kwa siri ukaamua kuipatia kampuni ya DP haki za yendeshaji bandari zote za Tanzania kupitia mkataba wa kimagumashi unaopora mamlaka ya nchi.

Katikati ya ubaya huu, Rais Samia amemfukuza kazi DC na DED ambao waliamua kuhamisha pesa toka eneo ambalo lina wananchi wengi wanaounga mkono siasa za upinzani na kuzipeleka pesa hizo kwenye eneo waliloamini kuwa lina wananchi wengi wanaoiunga mkono CCM. Rais Samia, akaona tendo hilo siyo sahihi, amewafuta kazi mara moja. Lakini wapo ambao hawakuelewa, wakasema kuwa DC na DED wamefukuzwa kazi na Samia kwa sababu kuna wanaCCM wamerudisha kadi za CCM. Lakini ukweli ni kwamba DC na DED walihamisha pesa ya miradi toka eneo linaloaminika kuwa na wananchi wengi wanaounga mkono vyama vya upinzani. Hivyo wale wanaCCM wa eneo hilo, nao wakachukia, na kuamua kuzirudisha kadi za CCM. Na kwenye hili Rais Samia ametenda haki, na anastahili pongezi.

Kuna wakati Rais Samia anatuweka katika dilemma na kuzisumbua nafsi zetu. Nafsi yangu inapata ugumu sana ninapomnenea mtu ubaya wakati pengine siyo amefanya mabaya lakini siyo mbaya kwa sababu hana dhamira mbaya.

Je, haya ambayo hayapendezi, kama haya ya bandari, yamefanyika kwa sababu Rais ana dhamira mbaya? Au alikuwa na dhamira njema lakini wabaya wakampeleka vibaya? Haya mambo ya kuwakamata wanaoukosoa mkataba mbaya wa bandari, na kuwabambikia makosa ya uhaini, yalikuwa ni maagizo ya Rais Samia au ni wale wabaya wanaomwingiza Rais kubaya wakati wote?

Ili tusipate shida, na wala tusimhukumu Rais kimakosa, tunamwomba Rais asimame ndani ya chumba na siyo kwenye mstari unaogawanya. Kama kuna vyumba viwili: kimoja ni cha utawala bora na kingine ni cha Utawala wa Fitina, basi Rais asimame kwenye chumba kimojawapo, na wala siyo kwenye mstari unaogawanya ili tutoe hukumu ya haki.

Hakuna mwenye chuki kwa Rais eti kwa sababu ni Mzanzibari, au eti kwa sababu ni mwanamke au eti kwa sababu ni muislam. Masikitiko na makasiriko yetu ni kwa yale yanayotendeka yanapoonekana yapo kinyume na maslahi ya Taifa la leo na la kesho.

Kama Rais kweli yupo na wananchi, na analitakia mema Taifa letu, atengebeze mazingira sahihi kwa haraka ya upatikanaji wa katiba, na siyo kuwa katika hali ya NATAKA SITAKI, kama ilivyo sasa.

Mkataba wa bandari ni mbaya, wanaosema ni mzuri, wengi wao ni watu wanafiki, wanaoamini kuwa kwa kusema hivyo wanamfurahisha Rais. Huu mkataba mbaya wa bandari, kama haubadilishwi au kufutwa ndio utakaofuta mema mengi ya Rais Samia.

Hata mtu mwenye dhamira nzuri kuna angle anawekwa hawezi fanya lolote, kuamua kunyamaza maana yake ana dhamira njema, anajua anakosea na hana cha kuelelezea, Hakuna jambo gumu hapo kuelewa. Huyu Mama hana roho mbaya, ni mtu mwema, Ni hao wanaume wa chama wanampotosha.
 
Anaongozwa na Wapuuzi, Haongozi Wapuuzi , tunajitambua.

Hatutakaa Kimya
 
Back
Top Bottom