Jk kukakutana na mke wa mandele bondeni

POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
2,400
katika ziara yake nchini South Africa, Jk ameenda kumtembelea mke wa Nelson Mandela ili kuwajulia hali. Ok je hii ilikuwepo kwenye ratiba ya ziara yake? kurugenzi ya mawasiliano Ikulu katika " taarifa Kwa umma" hakukuwa na ratiba ya kuona familia ya Mzee Madiba.
Hii imekaaje wakuu?:bange:
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni maalum katika mjadala wa kimataifa kuhusu Visheni Mpya ya Kilimo katika Afrika (Achieving Africa's New Vision for Agriculture) utakaofanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini, kesho, Jumatano, Mei 4, 2011.
Rais Kikwete pia atatembelea Kituo cha Kimataifa cha Biashara (World Trade Centre) mjini humo humo kuona maandalizi yanayofanywa kwa ajili ya kuanzisha kituo kama hicho nchini Tanzania.
Aidha, kesho hiyo hiyo, Rais Kikwete atashiriki katika mjadala maalum wa maandalizi ya kuanzishwa kwa Soko la Mazao nchini (Commodity Exchange) ambalo maandalizi yake yanafanywa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB).
Rais Kikwete atashiriki katika shughuli hizo muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Tanzania ikiwa sehemu ya ushiriki wake katika Mkutano wa Uchumi Duniani – Kanda ya Afrika (World Economic Forum-Africa) unaofanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini.
Mwaka jana, mkutano huo ulifanyika mjini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika nje ya mji wa Cape Town katika historia yake.
Rais Kikwete ameondoka nchini leo, Jumanne, Mei 3, 2011, kwenda Cape Town kwa ajili ya mkutano huo wa siku mbili ambako pia atashiriki katika shughuli nyingine tatu kuhusu uchumi na maendeleo.
Washiriki wengine wa mkutano wa Visheni Mpya ya Kilimo katika Afrika, ambako Rais Kikwete atakuwa mgeni maalum, ni pamoja na viongozi mbalimbali duniani wa serikali, biashara na uchumi, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyokuwa ya kimataifa, wasomi na vyama vya wakulima duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03 Mei, 2011
 
Kawaida yake ****** ni hiyo kufanya mambo ambayo hayako kwenye ratiba zake. Na anapokuwa nje ya nchi ndio utalii huo maana siku nyingi hajatoka nilidhani nae kajivua gamba kumbe hata akijivua gamba anabaki yuleyule si mwingine
 
Huyu Jamaa kwetu ni kama Paka aliyesimika mikucha yake mgongoni, tutalia sana, tujuta sana,
tutalalamika sana lakini hatobabadirika ng'o
 
kwani kuna ubaya gani jamani mna mnakua sasa hata hamna hoja mnakua mnapinga tu vitu hovyo,yule ni binadamu hakuna ubaya wowote kama aliona kapata hata dakika 5 asiende kujulia hali watu basi kazi,iko siku hata akienda kumcheki mzazi wake mtasema,dah kuongoza nchi za kiafrika!!!!!!!
 
kwani kuna ubaya gani jamani mna mnakua sasa hata hamna hoja mnakua mnapinga tu vitu hovyo,yule ni binadamu hakuna ubaya wowote kama aliona kapata hata dakika 5 asiende kujulia hali watu basi kazi,iko siku hata akienda kumcheki mzazi wake mtasema,dah kuongoza nchi za kiafrika!!!!!!!
Kwani Mandela na mke wake Graca wameachana siku hizi? Kwa nini msiseme JK alienda kumjulia hali Mzee Mandela? Na kumjulia hali mtu hasa mzee na mtu wa heshima kama Mandela ni kosa? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Hivi wakuu wengne huwa wanachepuka kwenda kumsalimia mama Maria Nyerere bila kuwepo kwenye ratiba?
 
Back
Top Bottom