Elections 2010 JK: Elimu bure haiwezekani, ila kompyuta kwa kila mwanafunzi inawezekana

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,692
20,452
JK amekuwa akiwabeza wapinzani wake kuwa wanatoa ahadi ya kutolewa elimu bure wakati haitekelezeki. Lakini ni JK huyo huyo ambaye siku si nyingi alisema atatoa computer (desktop) kwa kila mwanafunzi nchini na laptop kwa kila mwalimu. Nadhani amesahau kwamba alichoahidi ni kigumu kutekelezeka kuliko wanachoahidi wenzake sasa. Kuweka computer kutahitaji computer set yenyewe, kiti na meza kwa ajili ya kuwekea computer (bila kujali kama kila mwanafunzi wa sasa anakalia dawati au la!), miundombinu km vile umeme kwa ajili ya kuendesha computer (sina hakika km aliwauliza TANESCO umeme umeishia wapi), solar panel zenye Watts za kutosha (iwapo hawatatumia umeme wa TANESCO, na sina uhakika kama aliuliza power consumption ya CRT desktop pekee), mafundi wa kuzifunga, maintanance costs na walimu wa kuwaelekeza wanafunzi walau namna ya kuzitumia.
Swali langu: Iwapo aliahidi computer + laptop, kwa nini awashangae wanaoahidi elimu bure? Kipi ni rahisi kutekelezeka, computer/laptop AU elimu bure?
Gharama ya jumla ya matumizi ya computer/laptop per student/teacher haiwezi kumsomesha mwanafunzi mmoja mmoja wa sekondari na chenji zao zikabaki kwenda kuwachangia wale wachache wa elimu ya juu?

Katika majibu yake, ndipo Rais Kikwete alipogusia kuhusu mpango huo Tanzania Beyond Tomorrow ambao alisema kuwa utahakikisha katika kipindi cha miaka mitano kila mwalimu anakuwa na laptop, yake na baada ya hapo kila mwanafunzi atakuwa na kompyuta yake.
'Wanasema watatoa elimu bure, hayo yote sisi tulishayajaribu. Tulikuwa na elimu bure, afya bure, yakatushinda na sera hiyo ilibadilishwa chini ya Mwalimu Nyerere," alieleza Kikwete na kuongeza: "Sisi shule za kata tu, zinatusumbua, sijui wao watawezaje kutoa elimu bure?"
 
Back
Top Bottom