Asubuhi ya leo nilikuwa kwenye daladala nikitokea Kinondon nikielekea Ilala,ndani ya daladala ile dereva alifungulia TBC Fm mjadala uliokuwepo ni wa watu kupiga simu na kuchangia suala la uhaba wa mafuta, wengi walitoa ushauri kuwa wauzaji wafungiwe leseni,,,,,,kwa kuwa kipindi kilikuwa ukingon kikaisha, mara mtangazaj akacheza hotuba ya Nyerere ambapo nyerere alikuwa akikemea juu ya masuala ya rushwa na jinsi wafanyabiashara wanavyokwepa kodi na the way wanavyoiweka serikal viganjani.
Abiria wote walinyamaza,,,,,punde mtangazaj akacheza hotuba ya RAIS KIKWETE, ntajitahid kumnukuu"Tangu mwaka 2001 mpaka sasa Tanzania ni miongon mwa nchi 20 ambazo uchumi wake unakua kwa Kasi", miguno ikaanza na vicheko, akatokea jamaa mmoja ambae alikaa na mwanajesh aliyekuwa akitabasamu tu,"HUYU ANATUZINGUA".
Yule jamaa aliongea huku amekunja sura, mara hotuba ya JK ikaendelea namnukuu"Watu huwa hawataki kujikubali, sasa kama hujikubali itakuwaje??"
Kilichofuata hapo tena si kuisikiliza hotuba bali ni zogo kwenye daladala, kila mtu akiibeza ile hotuba, yule mwanajesh nilimsikia akisema"HUYO NDIO KIKWETE BWANA".
Nikabaki najiuliza mbona hotuba ya Nyerere hawakuikejeli? Maana Nyerere alisema "SERIKALI CORRUPT HUWA INAWAOGOPA WAFANYABIASHARA, SERIKALI CORRUPT HUWA HAIKUSANYI KODI BALI HUWAONEA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO, WALE WAKUBWA INAWAACHA NA HATA IKIWAAMBIA WANASEMA AH ATATUFANYA NINI HUYU?"
Haya alosema mzee Nyerere ndio yanayotokea leo kuhusu mafuta yanaendana na hiki kipande cha hotuba.