JK azua mtafaruku kwenye daladala

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Asubuhi ya leo nilikuwa kwenye daladala nikitokea Kinondon nikielekea Ilala,ndani ya daladala ile dereva alifungulia TBC Fm mjadala uliokuwepo ni wa watu kupiga simu na kuchangia suala la uhaba wa mafuta, wengi walitoa ushauri kuwa wauzaji wafungiwe leseni,,,,,,kwa kuwa kipindi kilikuwa ukingon kikaisha, mara mtangazaj akacheza hotuba ya Nyerere ambapo nyerere alikuwa akikemea juu ya masuala ya rushwa na jinsi wafanyabiashara wanavyokwepa kodi na the way wanavyoiweka serikal viganjani.

Abiria wote walinyamaza,,,,,punde mtangazaj akacheza hotuba ya RAIS KIKWETE, ntajitahid kumnukuu"Tangu mwaka 2001 mpaka sasa Tanzania ni miongon mwa nchi 20 ambazo uchumi wake unakua kwa Kasi", miguno ikaanza na vicheko, akatokea jamaa mmoja ambae alikaa na mwanajesh aliyekuwa akitabasamu tu,"HUYU ANATUZINGUA".

Yule jamaa aliongea huku amekunja sura, mara hotuba ya JK ikaendelea namnukuu"Watu huwa hawataki kujikubali, sasa kama hujikubali itakuwaje??"

Kilichofuata hapo tena si kuisikiliza hotuba bali ni zogo kwenye daladala, kila mtu akiibeza ile hotuba, yule mwanajesh nilimsikia akisema"HUYO NDIO KIKWETE BWANA".

Nikabaki najiuliza mbona hotuba ya Nyerere hawakuikejeli? Maana Nyerere alisema "SERIKALI CORRUPT HUWA INAWAOGOPA WAFANYABIASHARA, SERIKALI CORRUPT HUWA HAIKUSANYI KODI BALI HUWAONEA WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO, WALE WAKUBWA INAWAACHA NA HATA IKIWAAMBIA WANASEMA AH ATATUFANYA NINI HUYU?"

Haya alosema mzee Nyerere ndio yanayotokea leo kuhusu mafuta yanaendana na hiki kipande cha hotuba.
 
Kasi ya maendeleo inayoonekana na kina Shimbo peke yao sidhani kama nchi tunafaidika na chochote ni siasa za uongo na tarakimu ya uchumi zilizfochakachuliwa, ni maendeleo gani yanayozungumziwa bila watu?
 
Sasa hivi watanzania tunangoja nini? Hv hatuoni mifano ya nchi za Africa ambao wameamua kujitoa kwa ajili ya vizazi vyao vya baadae? Huyu jamaa (JK) si tulimweka wenyewe?

Sasa unadhani wa kumtoa? Ni sisi wenyewe....tuingieni mtaani jamani, tunaweka kambi pale magogoni siku 2 tu anaachia ngazi. Au mnataka mpaka mambo yawe mazito zaidi ndo mshtuke? Huyu mkwele amesha shndwa kuendesha hii nch tusingoje hyo miaka 4 ijayo ni mingi sana wakuu.

Kama kweli tunataka mabadiliko basi tunabid tudai na sio kuchekeana wana jamii....mi nashaur kuwa tuendelee kupeana habari ya maandamano kupinga utawala wa huyu jamaa ili j3 wiki ijayo tuingie barabarani. Au mnadhani kwa kupiga domo tv hapa jf ndo matatizo yetu yatakwisha? We need to fight....lets rise up people.
 
hivi ana elimu gani? maana kwa situation ilivyo na anavyoongoza nchi ingekuwa amesoma hata std II angeshajiuzulu
 
Kila mtanzania mwenye akili timamu na asiyenufaika na ufisadi wa serikali hii ana hasira na huyu mtawala mbovu. Wengine tulionya mapema kuhusu kumuachia mtu huyu aendelee kwa miaka mitano mingine baada ya kuonyesha wazi kwamba hafai. Ni mbabaishaji asiyejua alikwenda Ikulu kufanya nini.
 
Mi nasikitikia kura yangu kiukweli roho inaniuma kumpa kura raisi wa aina ya kikwete. Hivi hajui nchi anavyoingiza nchi porini?
 
Ahsante sana Mkuu Bajabiri kwa habari hii. Kuna watu huandika hapa kwamba Kikwete ni bora kuliko Mwalimu katika utendaji. Huu ni ushahidi mwingine wa kuonyesha jinsi Kikwete alivyo bomu tena la hali ya juu katika uongozi.
 
hivi ana elimu gani? maana kwa situation ilivyo na anavyoongoza nchi ingekuwa amesoma hata std II angeshajiuzulu
<br />
<br />
hana elimu ya maana... digrii yake almost adisco... na docrorial ya kuzawadiwa alipewa na chuo gani sijui..
 
Kuna usemi niliusoma hapa JF unasema nchi nyingine wana Rais Tanzania tuna ****** sasa ndo naamini huu usemi
 
Shukran mkuu kwa mada hii. Licha ya michango mingi kuonyesha kukerwa na kukatishwa tamaa na jinsi viongozi walivyotuacha. Mie nitajikita kwa kwenye upana wa tatizo. Kwa sasa kuna malumbano yanaendelea baina ya Meya Masaburi na wabunge wawili (Mtemvu na Zungu).

Nionavyo ni kuwa kweli tupo kwenye msiba na maafa makubwa, hasa kwa malumbano yanayoashiria hakuna wa kuwachukulia hatua japo kila mmoja inaonyesha anashiriki katika kuibomoa nchi hii.

Walikuwa wapi siku zote wasitoe kero zao mpaka leo wamekatana ndio wajito kimasomaso kwenye media kutiana vitisho. Sioni mwenye nafuu na lililobaki ni moja tu, "Kuwakataa". Tuendelee kuwasiliana mpaka siku ifike ya kufikisha ujumbe
 
mda umefika watanzania tuingie street na kumtoa mkwele as nchi imemshinda na ufisadi ndio unaongza...wadanganyika tuamke tuingie street and push the guy out..
 
Shukran mkuu kwa mada hii. Licha ya michango mingi kuonyesha kukerwa na kukatishwa tamaa na jinsi viongozi walivyotuacha. Mie nitajikita kwa kwenye upana wa tatizo. Kwa sasa kuna malumbano yanaendelea baina ya Meya Masaburi na wabunge wawili (Mtemvu na Zungu).

Nionavyo ni kuwa kweli tupo kwenye msiba na maafa makubwa, hasa kwa malumbano yanayoashiria hakuna wa kuwachukulia hatua japo kila mmoja inaonyesha anashiriki katika kuibomoa nchi hii.

Walikuwa wapi siku zote wasitoe kero zao mpaka leo wamekatana ndio wajito kimasomaso kwenye media kutiana vitisho. Sioni mwenye nafuu na lililobaki ni moja tu, &quot;Kuwakataa&quot;. Tuendelee kuwasiliana mpaka siku ifike ya kufikisha ujumbe

Mrangi wewe sijui wa goima, masange, haubi, chandama, au jangalo. By the way pointi yako nyuri lkn sio mahala pake its better ukaanzsha thread yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom