JK awazundua Watanzania 'ULOFA wenu' ndio unawawaliza!

Huyo ndio Rais wa wote, inabidi umsikilize sana na maneno yake yamelenga kfundisha nyie mnaorubuniwa kwa bia mbili mbili na kipande cha kuku kwa ulofa wenu.

malofa ni wote wanaoupigia chapuo undumilakuwili wa jk.....you inclusive.
 
watu wazima wamesombwa na mafuso toka vijijini,wakafungiwa uwanja wa Kirumba,wakapewa pilau na pombe na leo wameshinda wanashangilia... kama siyo ulofa ni nini sasa?
Jamani chipukizi ni watoto wa shule za msingi...leo nimeshangazwa na kuwaona wazee wakifanya uchipukizi....kweli Kuna wananchi wenzangu wengi tu ambao ni MALOFA
 
JK ametoboa jinsi viongozi wa CCM wanavyoowamaliza Watanzania....kwa kuwafanya 'malofa' na kuwaibia haki ya kupata viongozi wasio na dira, mafisadi. JK akihutubia katika Miaka 35 ya Chama Cha Mafisadi, Kirumba Mwanza mchana huu, ameweka wazi 'ujinga wa watanzania' na hasa kudanganywa katika kufanya maamuzi katika kupiga Kura, pale alipofikia hatua ya kurejea kauli ya kudhalilisha aliyowahi kuitamka aliyewahi kugombea Jimbo la Ukonga, Marehemu Ukiwaona Dito wa Muzuzuri (Ditopile), pale aliposema kuwa tatizo la watanzania ni 'ULOFA WAO' maana huwa wanakubali kupelekwa kukesha guest, wanaacha wake au waume zao na watoto majumbani wamelala, mwishowe wanagawiwa sh. 1,000 au 2,000 tu na vipapatio vya kuku, wanakubali kuwapigia kura viongozi wabovu, waliooza. JK kasisitiza kuwa Dito alikuwa 'mkweli', kuwaambia watanzania kuwa 'malofa', aliwapasha ukweli! Pamoja na yote hayo, JK alizidi kuwafumbua macho wasikilizaji na Watanzania wote kuwa kwa kauli aliyotoa Dito ya kuwa 'Malofa', wapiga kura walikasirika, walimkimbia ktk mikutano yake, alikosa kura ktk chaguzi zote zilizofuata....!

Na yeye JK kwa kafikia kuhalalisha kuwa Dito 'aliwapashma ukweli' Watanzania kuwa ni 'MALOFA', tunalo la kubisha?? Naomba kuwasilisha!

PAMOJA DAIMA! (Source: Tiibisii)

Muongo huyo, mbona hiyo mbinu ndiyo utumiwa na chama chake kila chaguzi na hajawai lalamika!

Hapo anaanza kuogopa wenye hela kushinda chaguzi za ndani ya chama! Ni vigumu ccm kufanya chaguzi bila kutawaliwa na fedha.

Vuneni mlichopanda.
 
kaamua kupambana na wahafidhina wenzie?
Ukiiangalia statement yenyewe jinsi ilivyo ni kwamba it is time to think and act differently. Asichosema ni kuwa kama kura zitapigwa, atakayeshinda ndiye atapewa mamlaka ya kuongoza bila kuchakachua?
 
JK bwana, unajua alipoongea na DK Slaa akashangaa sana kwanini mtu mwenye akili kama huyu hajawa Raisi!
Akawasikiliza kina Tundu Lisu, John Mnyika akashangaa mbona kina Ole sendeka, Magufuli, Simbachawene takataka kabisa kwa hawa jamaa! Ndo yanamtoka sasa!

Mkuu ni kwavile natumia simu, vinginevyo ningekugongea like!
 
Namfagilia sana JK. Wakati mwingine yaweza kuwa washauri ndo wanamharibia. Ila ninamuomba JK aache historia. Asikumbatie chama chake. Akumbatie utanzania zaidi. Kuwa mwenyekiti wa chama isiwe tatizo. Mbona Kaka Lyatonga alikuwa na mgombea urais hapo 2010 na bado akampigia JK KAMPENI? Maana aliona huyo wa kwake ni kilaza. Hapo ndipo nitakamilisha furaha yangu na JK. He is trying to be a good leader now na aendelee kuwa. Mwai walimboa chama chake na akahamia kingine na he is still the presidaa. Big up JK Na karibu sana Mwanza.

Akili zake na zako hazipishani kabisa!
 
Huyo ndio Rais wa wote, inabidi umsikilize sana na maneno yake yamelenga kfundisha nyie mnaorubuniwa kwa bia mbili mbili na kipande cha kuku kwa ulofa wenu.


Sindionyie mnaorubuniwa na khanga, kapero na Tshirt za India na china bila kusahau bukubuku
 
Sure maana ndivyo wengi wa watanzania tulivyo ndiyo maana hata sasa wanatuona mapoyoyo....
 
Nadhani 'akili yake' inamchemka angalau kwa sasa, anaona upepo unavuma!. Mara Davos 2012, wachangiaji wamempupua, akirudi ndani, akina Pinda na Makinda wanajitangazia 'miposho' wakimchomekea kuwa tayari kahalalisha! Akihema, anakumbuka kauli ya leo (ktk gazeti Mwananchi) Mhasham Askofu Methodius Kilaini, (Askofu Mkuu, Jimbo la Bukoba), aliposema kwa hali ya sasa "Tanzania ipo pabaya sana, inahitaji Rais kama Kagame, atakayeiongoza nchi kwa 'fimbo ya chuma' pasipo kuwaonea haya au aibu viongozi walafi, mafisadi na waharibifu wa rasilimali za umma". Tena anakumbuka miswada miwili imepigwa chali, na Wabunge wengine wamejipanga kumlambisa mchanga ktk miswada mingine ijayo, naona inabidi atembee na glass ya maji uhai au juice kila aendapo kupunguza 'presha'...

My take: Kama kweli anafanyia kazi kauli zake, awafukuze mafisadi zake na wale anaodhani wanakwamisha movement zake za ki-magamba magamba, aache kilalama! Tunanjuaga JK, Kama yeye...Hakunaga! anaegemea kulalama ahurumiwe..!
hajakaa sawa anasikia Tunduma Waziri amepofolewa mawe na wananchi, Jimbo la Uzini Chadema ndiyo wanalichukua hivi hivi anaona kimsingi mambo ni magumu sana
 
Back
Top Bottom