JK awazundua Watanzania 'ULOFA wenu' ndio unawawaliza!

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
JK ametoboa jinsi viongozi wa CCM wanavyoowamaliza Watanzania....kwa kuwafanya 'malofa' na kuwaibia haki ya kupata viongozi wasio na dira, mafisadi. JK akihutubia katika Miaka 35 ya Chama Cha Mafisadi, Kirumba Mwanza mchana huu, ameweka wazi 'ujinga wa watanzania' na hasa kudanganywa katika kufanya maamuzi katika kupiga Kura, pale alipofikia hatua ya kurejea kauli ya kudhalilisha aliyowahi kuitamka aliyewahi kugombea Jimbo la Ukonga, Marehemu Ukiwaona Dito wa Muzuzuri (Ditopile), pale aliposema kuwa tatizo la watanzania ni 'ULOFA WAO' maana huwa wanakubali kupelekwa kukesha guest, wanaacha wake au waume zao na watoto majumbani wamelala, mwishowe wanagawiwa sh. 1,000 au 2,000 tu na vipapatio vya kuku, wanakubali kuwapigia kura viongozi wabovu, waliooza. JK kasisitiza kuwa Dito alikuwa 'mkweli', kuwaambia watanzania kuwa 'malofa', aliwapasha ukweli! Pamoja na yote hayo, JK alizidi kuwafumbua macho wasikilizaji na Watanzania wote kuwa kwa kauli aliyotoa Dito ya kuwa 'Malofa', wapiga kura walikasirika, walimkimbia ktk mikutano yake, alikosa kura ktk chaguzi zote zilizofuata....!

Na yeye JK kwa kafikia kuhalalisha kuwa Dito 'aliwapasha ukweli' Watanzania kuwa ni 'MALOFA', tunalo la kubisha?? Naomba kuwasilisha!

PAMOJA DAIMA! (Source: Tiibisii)
 
Nukuu yake hiyo inabidi tuitafakari kwa makini sana tusije tukaistafsiri tofauti ikawa sivyo yeye alivyotaka itufikie.....ika JK mjanja sana maana dhana ya kuvua gamba ameibadilisha tofauti na alivyosema akiwa dodoma!!!siasa ni mchezo wa ujanja ujanja sana
 
Nadhani yuko sasahihi kabisa, wakati mwingine ni lazima awakilishe ujumbe kwa mifano, nadhani hapo suala kubwa ilikuwa ni kuwananga wabunge wa CCM kule bungeni, hasa akirejea ktk suala zima la Katiba. Kwa hilo nami nampongeza kwa kusema ukweli.
 
hata hao sungusungu waliojaza uwanja wa kirumba kama si pilau kofia na flani walizopewa wasingekuja leo, kwa hiyo anawaambia watz waache ufala
 
  • Thanks
Reactions: FJM
JK bwana, unajua alipoongea na DK Slaa akashangaa sana kwanini mtu mwenye akili kama huyu hajawa Raisi!
Akawasikiliza kina Tundu Lisu, John Mnyika akashangaa mbona kina Ole sendeka, Magufuli, Simbachawene takataka kabisa kwa hawa jamaa! Ndo yanamtoka sasa!
 
Hapo kawatumia salaam wabunge wa magamba, kwani wao wanapigania posho tu bila kuangalia maslahi na kipato cha mlala hoi. Si ameona jinsi walivyokataa bills mbalimbali kule mjengoni?? na ameshasoma kwamba wanajiandaa na kuupinga musuada wa marekebisho ya katiba....kisa kawageuka kuhusu mshiko
 
Jk anajua yeye ukomo wa uraisi ni 2015,Anatuasa tusiwe malofa tena kwa kudanganywa na Lowasa na vijisenti vyake,ila why hakusema haya 2010 mwanzoni?
 
Namuunga mkono 100% .waTanzania-tuna matatizo ya akili hasa tunapoona chakula wakati wa kampeni!
 
Nadhani 'akili yake' inamchemka angalau kwa sasa, anaona upepo unavuma!. Mara Davos 2012, wachangiaji wamempupua, akirudi ndani, akina Pinda na Makinda wanajitangazia 'miposho' wakimchomekea kuwa tayari kahalalisha! Akihema, anakumbuka kauli ya leo (ktk gazeti Mwananchi) Mhasham Askofu Methodius Kilaini, (Askofu Mkuu, Jimbo la Bukoba), aliposema kwa hali ya sasa "Tanzania ipo pabaya sana, inahitaji Rais kama Kagame, atakayeiongoza nchi kwa 'fimbo ya chuma' pasipo kuwaonea haya au aibu viongozi walafi, mafisadi na waharibifu wa rasilimali za umma". Tena anakumbuka miswada miwili imepigwa chali, na Wabunge wengine wamejipanga kumlambisa mchanga ktk miswada mingine ijayo, naona inabidi atembee na glass ya maji uhai au juice kila aendapo kupunguza 'presha'...

My take: Kama kweli anafanyia kazi kauli zake, awafukuze mafisadi zake na wale anaodhani wanakwamisha movement zake za ki-magamba magamba, aache kilalama! Tunanjuaga JK, Kama yeye...Hakunaga! anaegemea kulalama ahurumiwe..!
 
Namfagilia sana JK. Wakati mwingine yaweza kuwa washauri ndo wanamharibia. Ila ninamuomba JK aache historia. Asikumbatie chama chake. Akumbatie utanzania zaidi. Kuwa mwenyekiti wa chama isiwe tatizo. Mbona Kaka Lyatonga alikuwa na mgombea urais hapo 2010 na bado akampigia JK KAMPENI? Maana aliona huyo wa kwake ni kilaza. Hapo ndipo nitakamilisha furaha yangu na JK. He is trying to be a good leader now na aendelee kuwa. Mwai walimboa chama chake na akahamia kingine na he is still the presidaa. Big up JK Na karibu sana Mwanza.
 
Good JK ss washikishe adabu hao vilaza magamba wenzako inaonekana ujio wa chadema hapo ikulu umekufungua macho
 
Hapo hapo anasema uongozi wa machinga mwanza wakutane naye waseme wanata kusaidia nini? Nao malofa?

Hivi wakati wa camapign 2010 ccm waliahidi nini kwa hawa machinga? na wamefanya nini tangu uchaguzi uishe?
 
kweli ni malofa,mataaaaaaahira wa kufikiri.waliochagua magamba woooote kwa pilau,kofia,vitambaaa na bubu buku walizokuwa wakipewa ni maloooooooofaaaa!
 
Ahahahahahah,Asante sana president kwa kuwazindua wasiofahamu, hapo unamaanisha kabisa kwamba walioipigia kura CCM ni malofa, heri yangu mimi ambaye sijawahi kupigia kura Magamba.
 
Nina mashaka na kauli yake, hasa nikizingatia mandhari ya alikotamka yale maneno, jimbo lile linaongozwa na mtu kutoka chama gani, asijekua amelenga ujumbe huo kuwafikia wapiga kura wa Mwanza mjini
 
Back
Top Bottom