Rais Kiketwe, kiongozi anapoenjoy maisha chini ya JPM wakati watanzania wanalia

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
Image result for Kikwete na magufuli kwenye ndege

leo nimetazama tena hii picha ya mh JK akisafiri kwenda SA na mh JPM. ukitazama kwa macho ya juujuu wawili hawa kusafiri pamoja unaweza kudanganyika na kuishia kufurahia na kusifia kwamba tuna taifa la viongozi wanaopendana. na kwa kuwa uzoefu unaonesha sisi ni watu tunaosahau mapema sana na kudanganyika kirahisi, basi kufikiri kunakomea hapo na ndio mana makuhadi wa uongozi wa JPM walihakikisha picha kama hizi tunazipata.

ukweli ambao watanzania hatuujadili ni kwamba madhara makubwa tunayopata sasa kama taifa chini ya uongozi wa uditekta wa magufuli umesababishwa na JK kwa sehemu kubwa sana kabla na baada ya JPM kuwa rais.

kwanza JK aliongoza nchi kidhaifu sana kiasi kwamba kila mtu akajiona naye anaweza kuwa rais. na hii ikapelekea ccm kupata idadi kubwa ya waliochukua fomu kuliko wakati wowote ule. yeye ndio alimfanya JPM ambaye hajawahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi ajione anaweza kuwa mwenyekiti wa taifa wa ccm na rais. tena sio rais wa kutuongoza bali wa kutunyoosha.

jambo lingine ni ukweli kwamba JK ndio aliyesimamia kura za wananchi kuchakachuliwa na kuhakikisha JPM anashinda ili asionekane alikidhoofisha chama. cdm walichemsha kutowawekea wananchi mtu mwenye uwezo wa kutosha lakini haikuhalilisha hata kidogo kuibiwa kura. bado alichaguliwa na msingi wa demokrasia ni kuheshimu maamuzi ya wapiga kura.

mutakumbuka kuna mtoto wa JK alikua na ujasiri wa kujirekodi kabla hata ya matokeo kutangazwa kwamba watu wakijifanya wanafanya fujo kukataa matokeo baba yake atatatuchapa. wale wasiokumbuka hili tazama hapa .

kwa wanaotazama mambo kwa mapana yake, mtoto wa rais hawezi kuwa na kebehi kwa taifa kwa mtindo huu kama hajui baba yake anasimamia na anafanya nini.

JK ni moja wa watu waliopata maumvu ya uongozi wa JPM mwanzoni kabisa hasa baada ya mtandao wa watu wake kuondolea kila alipokua kawapachika: usalama, ndani ya ccm, jeshini, polisi, mashirika ya uma, na kwingineko. maslahi ya familia yake yaliathirika pia. mutakumbuka ziara kadhaa za JK na Mkapa hapa ilkulu na tukawa tunaambiwa ni mazungumzo tu na JK akitoka anatabasamu na kusema anapompongeza rais. wenye uelewa wa mambo walijua nini kiko nyuma.

JPM alipoona uhusiano na JK ambaye alikua bado ana nguvu kisiasa ndani ya chama unaharibika alimua KUMHONGA JK kwa kumpa mke wake ubunge. yani kati ya wanwake mamilioni wenye uwezo na uongozi ndani ya ccm JPM akamwona mama salma kikwete ndio maridadi kuliko wote kupewa ubunge wa kuteuliwa na rais. nafasi za ubunge wa kuteuliwa na rais ziliwekwa kikatiba kama fursa ya rais kuteua watu wanaoweza kumsaidia majukumu yake pale ambapo watu anaowahitaji wako nje ya bunge. sasa watanzania tujiulize. mama salma kateuliwa ili afanikishe nini kwenye nchi hii? kafanikisha nini tangu ateuliwe?

JK kaendelea kula bata huku akikosa kabisa roho ya utu na ukweli. kama kiongozi mzee ambaye alitakiwa kutoa kauli mambo yanapokwenda ovyo, amemua kuwa mnafiki ili yeye na familia yake wandelee kula bata. ana hasara gani bwana hata kama ninyi munalia? yeye anaishi ikulu pale msoga (muliofika munapajua kulivyo), watoto wake wako vizuri, na nyumbani kwake anaweza kutisha bunge kama spika maana ana mbunge wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa. analindwa, na lift kwenye ndege anapewa. wakati wengi wanalia na maumivu, yeye hajawahi hata kutetea watanzania wanaoteswa, kufungwa, kupotezwa, au kuumizwa.

kibaya kwa sasa anajipa na kupata umaarufu kwa udhaifu wa JPM. anajua watu wanaumia na wangetamani mbadala. anafurahi anaposikia tunasema tunamkumbuka pamoja na madudu yote aliyofanya. anajua sisi ni wasahaulifu. anajua yeye sio mwenzetu. kwanza yeye anajulikana duniani na bado anasafiri kila mara. kwa nini bana!!

Na ssisi badala ya kukumbushwa alipotufikisha, anavyoendelea kutokua msaada, na kumtaka kuwajibika kama kiongozi mzee, sasa tunamwona ni dalii naye anatuenjoi. niwakumbushe tu kua unaposikilizia maumivu ya #MfumoJiwe / #MfumoMagufuli kumbuka mastamaindi wa mfumo huu ni JK.

tuwe wajasiri kumkumbusha wajibu wake. pamoja na yote anaweza kurekebisha baadhi ya makossa na taifa hili likamkumbuka kwa mema zaidi ya mabaya. kuna vizazi vyake baada yake hivyo atawacha atapowaacha wanaolia. hatuna chuki naye kwa makosa yake maana hatuwezi kuyabadili. yalishatokea.

ila tumtake awe kiongozi na mzee. huyu rais katili na dikteta alikua waziri wake na ni yeye alimpa uraisi kwa nguvu. hivyo awajibike sasa kumwambia ukweli na kumkemea kama baba wa taifa JKN alivyofanya kwa mwinyi na mkapa na wakawa na adabu.

Sam
 
Sidhani hyo clip ya mwanae kama iliwekwa na huyo mtoto ,labda alikua akifanya utani kwa mwenzie
mambo mengine sio ya kumlaumu jk watoto wana mambo mengi.
 
Endelea kujidanganya huku umejifunika shuka huko kwenu ushagoni ukiamka utakuta watu wanajadili mambo ya kujikwamua kiuchumu na sio zile story za kulia lia buda.
 
Halafu akisimama majukwaani kuhutubia anajifanya analaumu watangulizi wake!
 
Endelea kujidanganya huku umejifunika shuka huko kwenu ushagoni ukiamka utakuta watu wanajadili mambo ya kujikwamua kiuchumu na sio zile story za kulia lia buda.
Lumumba imewakaririsha kwamba kila anayeongea hoja kinyume nanyi hana la kufanya. fikiria vizuri na tumia akili
 
sidhani hyo clip ya mwanae kama iliwekwa na huyo mtoto ,labda alikua akifanya utani kwa mwenzie
mambo mengine sio ya kumlaumu jk watoto wana mambo mengi
Watoto wangapi wa maraisi wamewahi kufanya hayo? halafu anafanya hivyo kitoto na hakuna maelezo yoyote yanayotolewa na familia wala baba kuomba radhi kwa jamii!! kweli?? yeye mwenyewe alisema za kuambiwa changanya na zako
 
Mada dhaifu, iliyoandikwa kwa mtazamo dhaifu na baya zaidi ktokujua hata mambo madogo tu. Hivi unataka JK amwambie nini Raisi? Yeye ndo anayesaini maslahi yake. Unakumbuka Jiwe alivyomwambia Sheni kuhu maslahi ya Maalim Seif? Aidha kwenye mikutano ya CCM hakuna umwamba kwa rais aliyeko madarakani. Wao husema CCM ina wenyewe. Mwisho nakumbusha kuwa JK ni rais mstaafu, hivyo safari za nje zipo kisheria.
Z
 
Kwa hiyo unachothibitisha ni kwamba anatetea na yuko kimaslahi binafsi Zaidi na hiyo inafanya hawezi kusimama kwa maslahi ya umma. nawe nikukumbushe pia kwamba maslahi ya viongozi hayategemei huruma ya rais bali yamewekwa na kusimamiwa na sharia za nchi.
 
Hili kusimamiwa na sheria linawezekana pale ambapo sheria zenyewe zinaheshimwa. Bahati mbaya hili kwa sasa halipo. Imekuwa bahati mbaya unalaumu kwa mambo ambayo ama hayapo au ni tofauti na hayo unayodai.
 
Muwe mnajitahidi kuja na hoja na mijadala yakujenga Taifa letu kimaendeleo, sio kuzileta zile zile ambazo tumeshazijadili ila kwa style nyingine.

Yaani badala ya kuwa na mijadala ya msingi kama Taifa, tunakuwa tukijadili personalities na udaku tu.
tatizo kubwa ni wewe stroke kutokuleta mijadala ya msingi hadi isiyo ya msingi inaibuka
 
Image result for Kikwete na magufuli kwenye ndege

leo nimetazama tena hii picha ya mh JK akisafiri kwenda SA na mh JPM. ukitazama kwa macho ya juujuu wawili hawa kusafiri pamoja unaweza kudanganyika na kuishia kufurahia na kusifia kwamba tuna taifa la viongozi wanaopendana. na kwa kuwa uzoefu unaonesha sisi ni watu tunaosahau mapema sana na kudanganyika kirahisi, basi kufikiri kunakomea hapo na ndio mana makuhadi wa uongozi wa JPM walihakikisha picha kama hizi tunazipata.

ukweli ambao watanzania hatuujadili ni kwamba madhara makubwa tunayopata sasa kama taifa chini ya uongozi wa uditekta wa magufuli umesababishwa na JK kwa sehemu kubwa sana kabla na baada ya JPM kuwa rais.

kwanza JK aliongoza nchi kidhaifu sana kiasi kwamba kila mtu akajiona naye anaweza kuwa rais. na hii ikapelekea ccm kupata idadi kubwa ya waliochukua fomu kuliko wakati wowote ule. yeye ndio alimfanya JPM ambaye hajawahi kuwa hata balozi wa nyumba kumi ajione anaweza kuwa mwenyekiti wa taifa wa ccm na rais. tena sio rais wa kutuongoza bali wa kutunyoosha.

jambo lingine ni ukweli kwamba JK ndio aliyesimamia kura za wananchi kuchakachuliwa na kuhakikisha JPM anashinda ili asionekane alikidhoofisha chama. cdm walichemsha kutowawekea wananchi mtu mwenye uwezo wa kutosha lakini haikuhalilisha hata kidogo kuibiwa kura. bado alichaguliwa na msingi wa demokrasia ni kuheshimu maamuzi ya wapiga kura.

mutakumbuka kuna mtoto wa JK alikua na ujasiri wa kujirekodi kabla hata ya matokeo kutangazwa kwamba watu wakijifanya wanafanya fujo kukataa matokeo baba yake atatatuchapa. wale wasiokumbuka hili tazama hapa .

kwa wanaotazama mambo kwa mapana yake, mtoto wa rais hawezi kuwa na kebehi kwa taifa kwa mtindo huu kama hajui baba yake anasimamia na anafanya nini.

JK ni moja wa watu waliopata maumvu ya uongozi wa JPM mwanzoni kabisa hasa baada ya mtandao wa watu wake kuondolea kila alipokua kawapachika: usalama, ndani ya ccm, jeshini, polisi, mashirika ya uma, na kwingineko. maslahi ya familia yake yaliathirika pia. mutakumbuka ziara kadhaa za JK na Mkapa hapa ilkulu na tukawa tunaambiwa ni mazungumzo tu na JK akitoka anatabasamu na kusema anapompongeza rais. wenye uelewa wa mambo walijua nini kiko nyuma.

JPM alipoona uhusiano na JK ambaye alikua bado ana nguvu kisiasa ndani ya chama unaharibika alimua KUMHONGA JK kwa kumpa mke wake ubunge. yani kati ya wanwake mamilioni wenye uwezo na uongozi ndani ya ccm JPM akamwona mama salma kikwete ndio maridadi kuliko wote kupewa ubunge wa kuteuliwa na rais. nafasi za ubunge wa kuteuliwa na rais ziliwekwa kikatiba kama fursa ya rais kuteua watu wanaoweza kumsaidia majukumu yake pale ambapo watu anaowahitaji wako nje ya bunge. sasa watanzania tujiulize. mama salma kateuliwa ili afanikishe nini kwenye nchi hii? kafanikisha nini tangu ateuliwe?

JK kaendelea kula bata huku akikosa kabisa roho ya utu na ukweli. kama kiongozi mzee ambaye alitakiwa kutoa kauli mambo yanapokwenda ovyo, amemua kuwa mnafiki ili yeye na familia yake wandelee kula bata. ana hasara gani bwana hata kama ninyi munalia? yeye anaishi ikulu pale msoga (muliofika munapajua kulivyo), watoto wake wako vizuri, na nyumbani kwake anaweza kutisha bunge kama spika maana ana mbunge wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa. analindwa, na lift kwenye ndege anapewa. wakati wengi wanalia na maumivu, yeye hajawahi hata kutetea watanzania wanaoteswa, kufungwa, kupotezwa, au kuumizwa.

kibaya kwa sasa anajipa na kupata umaarufu kwa udhaifu wa JPM. anajua watu wanaumia na wangetamani mbadala. anafurahi anaposikia tunasema tunamkumbuka pamoja na madudu yote aliyofanya. anajua sisi ni wasahaulifu. anajua yeye sio mwenzetu. kwanza yeye anajulikana duniani na bado anasafiri kila mara. kwa nini bana!!

Na ssisi badala ya kukumbushwa alipotufikisha, anavyoendelea kutokua msaada, na kumtaka kuwajibika kama kiongozi mzee, sasa tunamwona ni dalii naye anatuenjoi. niwakumbushe tu kua unaposikilizia maumivu ya #MfumoJiwe / #MfumoMagufuli kumbuka mastamaindi wa mfumo huu ni JK.

tuwe wajasiri kumkumbusha wajibu wake. pamoja na yote anaweza kurekebisha baadhi ya makossa na taifa hili likamkumbuka kwa mema zaidi ya mabaya. kuna vizazi vyake baada yake hivyo atawacha atapowaacha wanaolia. hatuna chuki naye kwa makosa yake maana hatuwezi kuyabadili. yalishatokea.

ila tumtake awe kiongozi na mzee. huyu rais katili na dikteta alikua waziri wake na ni yeye alimpa uraisi kwa nguvu. hivyo awajibike sasa kumwambia ukweli na kumkemea kama baba wa taifa JKN alivyofanya kwa mwinyi na mkapa na wakawa na adabu.

Sam[/QUOTE
ukweli asio kuwa na akili ataongea mengi hivi unataka kumfananisha makufuli na kikwete. kikwete hafikii makufuli hata nusu yake makufuli kafanya mazuri mengi na wala sio dictetor
 
kosa la kiufundi lililofanyika kwenye uchaguz 2015 nipale viongo watu waliokua wamewaona dhaifu kuhusika au kushiriki kumleta kiongoz mpya ...alafu patokee miujiza uyo kiongoz mpya awetofaut na alete mabadiliko yatakayo onyesha udhaifu wa aliyepita .......hili swali au hii hali itaendelea mpka tujue nijinsi gan yakutengeneza viongoz na kuwaandaa na sio kupachikana ....by the way kinachofanyika saiv ndicho kilichopangwa kufanyika na kitakachofanyika badaye tunaweza kukibadilisha au kukiacha kifanyike kama inavyopaswa kwasababu matokeo ya Leo nimazao ya mbegu tulizozipanda jana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom