JK Awafunga goli watanzania, wao washangilia!

Kitila hata mimi nilijisikia hivyo hasa kabla ya kusoma tamko lenyewe. Nadhani Rais anapoteza nafasi kubwa sana ya kuamsha taifa! yaani kama kuna mtu kajaliwa kila kitu mezani na anashindwa kutumia sijui kama atatokea mwanasiasa mwingine Tanzania atakayekuwa na "mambo yaliyomkalia sawa" kama JK.
 
Asante MKJJ kwa samari yako hiyo; binafsi sijaiona ripoti hiyo, labda leo jioni. Hata hivyo nilikuwa na wasiwasi sana kufuatia tamko la Luhanjo lililokuwa katika lugha za jumla jumla. Kudai Balali kafukuzwa kazi wakati yeye mwenyewe alishatangaza kujiuzulu siyo adhabu kabisa; huyu mtu anatakiwa akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo.

Je, wakati J. K. I. Kwete anasema wakuu wa majeshi washughulike kuyakamata makapuni yaliyokula njama za kuiibia Benk, je ana maana hata Mkono Advocates? Maana inajulikana kuwa nao walichota sana pale BoT.
 
Kichuguu,
Hawa hawatamkamata Balali. Hiyo ripoti ni whitewash. Hawataki ukweli ujulikane. They wish he was dead!
 
Asante MKJJ kwa samari yako hiyo; binafsi sijaiona ripoti hiyo, labda leo jioni. Hata hivyo nilikuwa na wasiwasi sana kufuatia tamko la Luhanjo lililokuwa katika lugha za jumla jumla. Kudai Balali kafukuzwa kazi wakati yeye mwenyewe alishatangaza kujiuzulu siyo adhabu kabisa; huyu mtu anatakiwa akamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo.

Je, wakati J. K. I. Kwete anasema wakuu wa majeshi washughulike kuyakamata makapuni yaliyokula njama za kuiibia Benk, je ana maana hata Mkono Advocates? Maana inajulikana kuwa nao walichota sana pale BoT.

mzee ukiingia kwenye http://www.klhnews.com pale juu kuna "Pics and Docs" unaweza kupata nakala yenyewe ya tamko katika pdf..

or Download it here: Tamko
 
Yeah nimeshapata preview ya baadhi ya magazeti mengine yanasema "JK Amng'oa Balali"...

Huko Tanzania kwani waandishi wengi wanasifia serikali ili labda watapewa ulaji, wanasahau nafasi yao katika jamii! Tushukuru kuwa magazeti kama mwanahalisi na raiamwema angalau yanafanya objective journalism kwani mengine yote ni extension ya TBC ya Tido Mhando!
 
Aaaaah jamani, tunategemea nini wakati system ndio ileile, iliyolifanya li-nchi lenye utajiri kama hili kuwa moja katika nchi masikini duniani! Mimi binafsi sishangai kwa yanayojiri kwani system ni ileile, hamkumbuki Mkuu Nyerere alivyong'atuka, hiyo hiyo BoT iliwaka moto na hakikubaki kitu na hakuna kilichofanyika. Sasa cha kushangaa ni nini? lakini ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka, kama haya yote yana mwanzo, basi na mwisho upo tuu, Shah wa Iran ni mfano wa karibu. Jee hamjui system ni nini?
 
Aisee mwanakijiji nakubaliana na hoja zako. Mimi mwenyewe baada ya kulisoma hilo tamko la serikali (Naomba nisiite Report) kuhusu bank kuu. Kusimamishwa na kuteuliwa kwa kwa gavana mpya nilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza na nadhani mengi pia umeuliza.

1. Taarifa inasema uteuzi wa balali umesitishwa lakini tuko hewani ni kwanini na alihusika je, na ni hatua gani uchukuliwe dhidi yake na alishirikiana na nani katika hilo.

2. Kuteuwa boodi ya wakurugenzi ambayo ilikuwepo wakati wa ufisadi ni danganya toto kwani nadhani baadhi yao ni questinable pia mfano katibu mkuu Hazina (Grey Mgonja ni mmoja wa bodi member na moja kwa moja anahusika pia na hii issue ya BOT kutokana na nafasi yake je hii si danganya toto? http://www.bot-tz.org/AboutBOT/Board_Members.htm

3. Nadhani ukipitia sheria ya mademi ya Taifa ya 1977 iliyofanyiwa marekebisho 2003 kama sikosei na ukipitia mkakati wa madeni wa taifa utagundua kuna utata kati ya kazi ya kitengo cha madeni ya Nnje kilichopo Bank kuu na kilichopo Hazina kwa Mwasibu mkuu wa Serikali. Hata taarifa zao na figures zina tofautiana. Niliposoma hii sheria nimegundua pia kuwa Bank kuu ili ifanye malipo idhini hutolewa na kamati ya madeni ya taifa ambayo Mgonja ndie mwenyekiti na hii ndio naona kuwa hii bod ya sasailitakiwa kuvunjwa mara moja ili kutoa nafasi ya maamuzi huru.

4. Kunaswala umegusia kuhusu bank kuu na wizara ya Fedha. Kama sikosei Benk kuu ni huru na nadhani Governor yeye hawajibiki kureport kwa Katibu mkuu wala waziri wa fedha. Jaribu kufuatila sina uhakika lakini nadhani inatakiwa hivyo ili kuweza kufanya kazi Fisical policy na monetary policy vizuri.

5.Siju mzee kuhusu swala la kuhire Scotland yard inakuwa je hapo. Kidogo linanipa utata najua Kenya walifanya lakini hapa naona bado ni vyombo vya ndani vinaweza kutumika pia kwa hili.

6.Umetoa wazo zuri sana kuwa baada ya kusitisha malipo ya EPA ilibidi kitengo cha madeni ya nnje cha bank kuu kivunjwe kabisa. Na wahusika wote wa ngazi zote wachukuliwe hatua za kisheria. Kwanza kama sasa hivi watuhumiwa wote wangesimamishwa kazi kwanza

Mimi bado nipo gizani jamani. Hivi kuhusu hiuzo pesa kurejeshwa inakuwa je? maana unaonekana kuwa baadhi ya makampuni wala hayajawahi kusajiliwa. a stll confused hapo.

Niliongea na jamaa wa ndani ya Bank anasema hii EPA ndio account ya kulipia hata shule za watoto wa wakubwa wanaosoma nnje ya nnchi.

****** sijui na swala la ujenzi wa majengo nalo hapo inakuwa je.



Hii nadhani ilikuwa ni nafasi nnzuri sana kwa JK kurudisha imani kwa wa danganyika na kutoa fundisho kwa watendaji wengine.

Lakini nikitoa hitimisho langu naomba nijiunge na wa Tz wengine kushangilia bao la mkono kwani pia ni hatua muhimu hii iliyochukuliwa na serikali japo ni kutokana na shinikizo la wafadhili. Mabadiliko ni taratibu na tunasubiri kuona hatua zaidi zinachukuliwa.

http://news.yahoo.com/s/afp/20080109/wl_africa_afp/tanzaniaeconomybankcorruption_080109223025
 
Mkjj mimi nadhani hatujafungwa goli. Tukiishinikiza siri kali iwafukuze kazi na kuwakamata wale wote watendaji wa BOT waliohusika kwa namna moja au nyingine katika wizi huu mkubwa basi Muungwana hatakuwa na jinsi ila kufanya hivyo.

Huyu Balalli na ugonjwa wake kama alidhani uraia wake wa Marekani utamsaidia kutorudishwa nyumbani katika wizi mkubwa alioufanya basi ameula wa chuya. Muungwana akinyanyua uzi na kumuomba Condoleeza kumrudisha huyu jamaa ili akajibu tuhuma nzito basi Marekani haitasita kufanya hivyo.

Tukiamua kukaa kimya kama kawaida ya kichwa cha mwendawazimu hata akinyolewa vibaya kiasi gani huwa hatii neno, basi tutakuwa tumefungwa goli. Lakini tukipiga kelele pamoja na nchi za wafadhili, mashirika ya kimataifa basi Muungwana atakuwa amewekwa kwenye kona na hana pakuchomokea.

Kumbuka ukaguzi wa tuhuma za BOT usingefanyika kama siyo shinikizo za nchi wafadhili na mashirika ya kimataifa. Wakiamua kutia sauti zao tena pamoja na sauti za Watanzania basi hakuna ujanja.

Tusikubali hawa mafisadi toka BOT wakatoroka nchi kama yule mhindi wa rada na aliyejipatia kiharamu milioni $12 zetu, ni lazima wakamatwe mara moja na mali zao zote zifilisiwe mara moja ikiwemo Ballali.
 
Mwanakijiji kwa kiasi fulani naweza kuungana na wewe, lakini kwanza naona tuwe na subira kidogo au kwanza tuione hiyo ripoti, tusitoe lawama bila kwanza kuiona ripoti yenyewe, nakujua rais amevaa viatu gani. Huenda ni issue ngumu inayoweza kuyumbisha serikali nzima na kudestabilize mambo mengi.
Kwa haraka haraka hayo Makampuni kuyafuatilia inaonekana kama ni "game of chasing a ghost" hakuna lolote la maana litakalopatina kutokana na hatua hiyo. Hata hivyo Bodi ya BOT ina uwezo gani wa kuwachukulia hatua wahusika, au ni hatua za kusema wewe uliiba milioni 5 adhabu yako kapumzike, na wewe uliidhinisha hii adhabu yako utasimamishwa kwa miezi 6,
Kuna nyingine itakuwa interesting, Kama Balali (as US citizen/resident) akitakiwa na ikashindikana kumpata, itakuwa issue nyingine ya mtanzania mwenye uraia wa kigeni kupewa kazi nyeti, na kushindwa kumwajibisha kwa kuwa na uraia wa nchi nyingine...........
Wakati mwingine unaweza kuona kama ni mazingahombwe tu, how can you send the acused to deal with another acused on the same case, inatia mashaka kidogo!
Lakini ni vizuri kwanza tusibiri kwanza kuiona ripoti yenyewe halafu ndio tuone hayo mambo yenyewe, na kama busara alizotumia JK ni appropriate!
 
Mnkjj, kanikurupusha kutoka kwenye umati wa watu unaomshangilia Mkuu wao... kwa uamuzi mchungu aliofanya.
Kitu kimoja kipo dhahiri... Balali hawezi 'kuiba' kiasi cha shilingi bil133 peke yake. Hili si suala la benki kuu... fedha zililipwa kuelekea kipindi cha kampeni za uchaguzi, uchaguzi ukamweka Mkuu kwenye kiti?
Kuna mtu anaweza kutibu kizunguzungu? Sasa naona maluweluwe!
 
Mi pia siwaelewi kama mnasubiri waende mahakamani, wakati huku uswahili kwetu. Mtu akiaba twangapepeta anakula tairi, akikwapua buku anakula kiberiti. Sasa mtu kaiba kiwanda cha simu na matrekta, kwani hatujui wanakaa wapi hawa manyang'au. Tukimwachia Kiwete awezi kushika dumu la mafuta mwenyewe, yeye alichofanya ni kuita kelele za mwizi tu, mbio za kuwafukuza hana. Na sisi tukitulia tusifanye tunalopaswa kufanya, ndio kwaheri mwalimu hiyo. Magazeti huku kwetu kama kawa, pambio kwa kwenda mbele.
Waendelee na usanii wao lakini ushindi kwetu ni lazima, kwa mawe, kwa vijiko, hata kwa meno. Kila mtu afanye anachopaswa kufanya basi. Siku zao zinahesabika
 
Hizi ni SANAA na zipo to stay for the following 7 yrs.
JAMAA AMEFUZI KWENYE KILE CHUO CHAO CHA WATOTO WA MJINI,hivi hamshanga kuna jmaa hapa Nchini amewapiga changa la macho Wafanyabiashara wa Ki-israel mabiloni na bado yupo mtaani kama kawaida,hivi hii inchi ingekua na viongozi wa ukweli ukweli si jamaa wangerudishiwa mapesa yao baada ya jamaa PAPA TP kufirisiwa.
 
Asante Mwanakijiji.

Ikumbukwe kuwa suala la uchunguzi wa BoT walilazimishwa kufanya ndio maana hawakutaka kuunda kmati teule ya bunge kama alivyopendekeza Dr. Slaa.

Walijua mengi zaidi yangejulikana kwa umma kama kamati ingeundwa. Si nia yao kushughulikia tatizo hili kwa moyo wa dhati kabisa.

Wanataka kujisafisha mbele ya wafadhili na umma wa watanzania.Wananchi ndio unatakiwa kushinikiza zaidi ili hatua madhubuti zaidi katika mambo yote yanayoenda ndivyo sivyo.

Kila la kheri wana JF
 
TUJIKUMBUSHE

Januari 9, 2008
Kupitia taarifa inayotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Rais Jakaya Kikwete anatangaza kutengua uteuzi wa Balali kuwa Gavana na kuagiza hatua zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika na ubadhirifu uliogunduliwa kwenye EPA. Anamteua Beno Ndullu kuwa Gavana mpya wa BoT.
Januari 7, 2008
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anamkabidhi Rais Kikwete ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Ernst & Young.

Desemba 23, 2007
Kampuni ya Ernst & Young inakabidhi ripoti ya uchunguzi wake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, ambaye anaahidi kuifikisha kwa rais katika wiki ya kwanza ya mwaka 2008.

Desemba 20, 2007
Inaripotiwa kuwa Gavana Balali ameandika barua ya kujiuzulu akiwa nje ya nchi, Ikulu na Wizara ya Fedha zinasema kuwa hazina taarifa.

Desemba 19, 2007
Meghji anatetea kuchelewa kwa ripoti ya BoT.

Desemba 4, 2007
Freeman Mbowe anafungua Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA na kueleza kushangazwa na ukimya wa serikali kuhusu ripoti ya uchunguzi wa ubadhirifu ndani ya BoT.

Desemba 01, 2007
Dk. Willibrod Slaa anaelezea kukerwa na usiri wa ripoti ya ukaguzi wa hesabu za BoT.

Novemba 29, 2007
Ukaguzi wa hesabu za BoT unakamilika na inaelezwa ripoti hiyo kufika kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Septemba 22, 2007
Wafadhili wanadai ufafanuzi wa tuhuma za ufisadi zinazoihusu BoT.

Septemba 20, 2007
Hali ya Gavana Balali inaripotiwa kuendelea vizuri.

Septemba 16, 2007
Wananchi wataka msimamo wa tuhuma za BoT na nyinginezo kutoka kwa Rais Kikwete.

Septemba 15, 2007
Dk. Slaa anahutubia mkutano wa hadhara Mwembe Yanga, Temeke, kisha anataja orodha ya waliowaita mafisadi wanaotafuna nchi, akimjumuisha na Balali.

Septemba 14, 2007
Afya ya Gavana Balali inagubikwa na utata, lakini inaelezwa kuwa yuko nje ya nchi kwa matibabu.

Septemba 11, 2007
Kampuni ya Ernst & Young iliyoteuliwa kupitia hesabu za BoT katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ili kubaini ukweli kuhusu ubadhirifu wa fedha, inaanza kazi.

Septemba 09, 2007
Inaripotiwa kuwa hali ya Gavana Balali si nzuri, hivyo amepelekwa nje ya nchi kwa uchunguzi na matibabu.

Agosti 19, 2007
CHADEMA inajibu mapigo ya Spika dhidi ya Slaa na hoja ya BoT.

Agosti 18, 2007
Spika anamtuhumu Dk. Slaa kuwa ameghushi nyaraka alizotaka kuzitumia dhidi ya BoT na kutishia kumshitaki.

Agosti 16, 2007
Dk. Slaa anachomoa hoja binafsi ya BoT bungeni akidai kuwapo kwa dalili za kukosekana kwa nia njema, hasa baada ya Mbunge mwenzake, Zitto Kabwe, kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge baada ya kuwasilisha hoja yake iliyokataliwa na wabunge wa CCM. Anaahidi kuipeleka kwa wananchi na kwa wafadhili, lakini pia anadai kutishiwa maisha.

Agosti 12, 2007
Yaelezwa kupitia katika vyombo vya habari kuwa Balali anapaswa kustaafu kazi Juni mwaka 2008, kitakapokwisha kipindi chake.

Agosti 6, 2007
Dk. Slaa awasilisha hoja binafsi bungeni ya kutaka Bunge liunde kamati teule kuichunguza BoT.

Julai 26, 2007
Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi yapitisha mahesabu ya BoT ya mwaka 2005/2006, baada ya kuridhishwa na majibu ya Gavana Balali.

Julai 13, 2007
Wapinzani watoa hoja za kumshangaa Balali na kusisitiza hoja za kumtaka ajiuzulu.

Julai 12, 2007
Gavana Balali aitisha mkutano na wanahabari na kupinga shinikizo la kumtaka ajiuzulu kwa manufaa ya umma akisema hatajiuzulu kamwe, kwani hakufanya kosa lolote.

Julai 12, 2007
Balali anapunguziwa mzigo, rais anateua manaibu gavana watatu kumsaidia.

Julai 9, 2007
Viongozi wakuu wa vyama vinne vya upinzani vya NCCR Mageuzi, CHADEMA, TLP na CUF wazungumza na wanahabari na kueleza wasiwasi wao kuwa serikali inamlinda Gavana Balali dhidi ya kashfa anazokabiliwa nazo.

Julai 2, 2007
Waziri Mkuu ahitimisha mjadala wa ofisi yake bungeni na kukiri kuwa tuhuma za BoT ni nzito na kueleza dhamira ya serikali kutumia kampuni ya kimataifa kuzichunguza na kuzitolea majibu.

Aidha awataka wapinzani Hamad Rashid na Dk. Slaa kuachana na hoja ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ya Bunge.

Juni 29, 2007
Serikali kupitia kwa Waziri wa Madini na Nishati inamsafisha mke wa Gavana Daudi Balali, aitwaye Anna Mug anda, kuhusu tuhuma za yeye kutumia nafasi ya mumewe na kisha kuwa mkurugenzi katika moja ya makampuni ya madini ya dhahabu hapa nchini.

Juni 28, 2007
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed, aliambia Bunge kuwa kiasi cha dola milioni 800 kimepotea BoT na kueleza kushangazwa na hatua ya serikali kupinga Bunge kuunda kamati teule.

Juni 27, 2007
IMF inatoa taarifa kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wake, Murilo Portugal, ikitaka uwazi uwepo katika suala la kuichunguza BoT.

Juni 26, 2007
Mjadala unatanuka kuhusu tuhuma za ufujaji fedha BoT, na safari hii Mbunge wa CCM, Ole Sendeka, anataka iundwe tume ya kuichunguza BoT, huku Dk. Slaa akisisitiza kuhusu suala hilo katika mjadala wa hotuba ya waziri mkuu.

Juni 25, 2007
Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa anatoa tuhuma nzito za ubadhirifu ndani ya BoT bungeni na kutaka Gavana wa Benki Kuu, David Balali ajiuzulu.

Juni 15, 2007
Bunge la Bajeti linakaa na bajeti ya mwaka 2007/08 inasomwa na Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji.
 
Mwanakijiji nakupongeza kwa uchambuzi mzuri uliotoa, naungana na wengine kukuomba kwamba huo uchambuzi utolewe kwenye gazeti ili watanzania wengi waupate, taratibu ipo siku wataelewa somo.

Kama ww Mkjj, binafsi simwelewi kabisa huyu msanii JK jamani. Aliyofanya COSTECH kumwondoa Mkurugenzi na kuiacha bodi iliyopaswa kumsimamia ikaachwa kuendelea na kazi, ni kichekesho kisichomithilika hivi jamani is our President serious kweli na haya maigizo yote? Na structure ya BOT kama sikosei nayo ni utumbo wa ajabu, kama nakumbuka vizuri gavana ndio chairperson wa bodi-hii sijui ni managment ya ulimwengu gani masikini. Kungekuwa na njia JK anapaswa kushinikizwa BOT nzima ifanyiwe overhaul.
 
Nafikiri kuna masuala mengi yanayohitaji kuangaliwa kisheria na ndiyo maana Mwanasheria Mkuu ametajwa kusimamia kadhia hii. Isingewezekana rais akatoa amri au majibu au maelekzo kwa kila suala. Ndiyo maana kaamuru asasi kadhaa ikiwemo na CAG washirikiane kuonyesha njia.
Kwa mfano, ukivunja EPA, unaweka nini badala yake? Je unahitaji kwenda bungeni tena kupitisha sheria nyingine itakayosimamia ulipaji madeni? Nadhani kuna mambo mengi ya kuangalia hapa ya kimuundo na kisheria. Huenda pia Gavana mpya akatumia fursa hii kupendekeza muundo mpya wa BoT kwa kuzingatia kuwa kabla ya uteuzi wake alikuwa "anajiandaa" kuikwaa nafasi hiyo (tulishamtabiria huko nyuma).

BTW, katika mabadiliko ya mawaziri yanayotarajiwa kutokea wakato wowote kuanzia sasa, kutakuwa na mawaziri wawili au watatu kutoka vyama vya ushindani!
 
Mzee Mwkjj, good analysis, and I am relieved that there are thinking people among us, maana jana nilikata tamaa jinsi baadhi ya watu na makanjaja walivyokuwa wanamsifia Msanii Mkuu!
Mi naomba niongeze kwamba kulikuwa na shinikizo kubwa sana ya wafadhili. Uozo wa BoT ulianza kuonekana kwa wafadhili including World Bank na IMF mwaka moja uliopita. Kwa wale wanaofanya kazi BoT wanaweza kuthibitisha kwamba malipo ya project za World Bank ambazo zilikuwa zinalipwa kupitia BoT yalisimamishwa mara moja DEcember 31st 2006 na suppliers na contractors wote walianza kulipwa directly from WB in Wahsington. BoT walilazimika kurudisha any outstanding na ilibidi kampuni ifuatilie from Washington. Hii issue nilielezwa na mtu aliyekuwa anafanya kwenye project moja kubwa funded by WB. Ditto for IFM. Sasa kama waandishi wetu wangefanya uchunguzi wangejua mapema that something is wrong. Nasikia pia other donor organizations and countries pia walikuwa wametoa deadline ya 31st December 2007 for action to be taken, na ndiyo maana Msanii Mkuu imebidi alete mazingaombwe.
- Point nyingine ni kuhusu ukweli kuhusu kampuni zilizohusika. RUmour in town has it that some of the recipients of this EPA (acha hiyo ya Deep Green etc) ni watu ambao wanadeal in illegal biashara and they were engaged in money laundering. Na ni watu ambao wanajulikana na wanazunguka nchi hii na Vogue zao! Sasa kampuni zilizotajwa kwenye EPA scandal ni hewa, watakamatwa na akina nani? Hapana ni kufanya international action they should be tracked down.
 
Aisee ni balaa tupu,na ndio maana mie sikupongeza Hatua hiyo,Nilishajua ni Usanii mtupu as usual,Jambo la Msingi ni Lazima CAG atuambie Hayo Makampuni yanamilikiwa na Nani.

Kwanini miezi sita ili wachukuliwe hatua ili khali ilishathibitika walihusika?ina maana Ripoti ni ya Uongo mpaka Wachunguzwe tena na Takukuru?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom