JK atabiria wapinzani kushika dola!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,797
12,239
Rais Kikwete jana akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni aliwataka wapinzani wajifunze utamaduni wa kusifu yale mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM ili nao wakipata madaraka wafanye mara tatu maana ni lazima wataendeleza pale alipoishia yeye.

Naye Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli akikubaliana na utabiri huo wa Rais alisema kuwa wanataka uzinduzi ufanywe na Rais Kikwete ili Rais mwingine ajaye asije kujivunia mafanikio hayo awe ametoka CCM au upinzani kwani fedha za ujenzi zimetafutwa na serikali ya awamu ya nne.

Wana JF je tunaweza kubashiri kuwa sasa serikali ya CCM imekubali yaishe? TAFAKARI!
 
utawala wa dola la nchi hii si mali ya CCM peke yao. iko siku na wao watatoka na wataingiza wale wanaoitwa wapinzani kwa sasa. so kwa mwenye hekima hili wala halimsumbui. ni mwenye upungufu wa hekima pekee ndiye awezae kuwaza kuwa CCM itatawala milele!!! hilo kwa ufupi halipo na hakuna chama cha kisiasa kitakachotawala milele!
 
Aisee!! Sijui mnaongea nini nyie,hivi nikisema kuwa kesho mchana kutakuwa na mwangaza utanipa hadhi ya mtabiri??nipo hapa ofisini kwangu natabiri kuwa mwisho wa mwezi huu ntapata mshahara!!mwisho»Jk ameona,si kuwa ametabiri,kwikwikwikwikwiiiii.
 
Ni mtazamo wako!
Rais Kikwete jana akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni aliwataka wapinzani wajifunze utamaduni wa kusifu yale mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM ili nao wakipata madaraka wafanye mara tatu maana ni lazima wataendeleza pale alipoishia yeye.

Naye Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli akikubaliana na utabiri huo wa Rais alisema kuwa wanataka uzinduzi ufanywe na Rais Kikwete ili Rais mwingine ajaye asije kujivunia mafanikio hayo awe ametoka CCM au upinzani kwani fedha za ujenzi zimetafutwa na serikali ya awamu ya nne.

Wana JF je tunaweza kubashiri kuwa sasa serikali ya CCM imekubali yaishe? TAFAKARI!
 
He is trying to read between the lines and came up with that logical argument.By the way, hzo ndio politics yote yawezekana.
Zamani wakiwa katika majukwaa ya siasa walikuwa wakitamba kuwa CCM ina hakika ya kuendelea kutawala kwa zaidi ya miaka 50 ijayo! Kwa sasa confidence hiyo hawanayo tena!
 
Kwa timu yake ya Nape, Mwiguru na Lusinde, hata mimi ningeweza kutabiri!!
 
Huo siyo utabiri isipokuwa ametumia kanuni inayosema, "Ishara ya mvua ni mawingu." kwa hapa Tz ishara ya kuondoka madarakani kwa CCM si mawingu tena bali mawe ya barafu yameanza kudondoka (mauwaji-Arusha, Singida, Mwanza, Igunga, Iringa, Mwaandishi wa habari, .... ). Na pia mwanzo wa ngoma ni lele, na lele imeshaanza, what then ....?
 
Upinzani kuchukua dola hakuhitaji utabiri wa JK na serikali yake na kama upinzani watasubiri huo utabiri watasubiri milele.
Wapinzani wanatakiwa kukaza buti ni kuindoka serikali ya CCM 2015 bila kujali kama JK alitabiri au hakutabiri....
 
Rais Kikwete jana akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni aliwataka wapinzani wajifunze utamaduni wa kusifu yale mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM ili nao wakipata madaraka wafanye mara tatu maana ni lazima wataendeleza pale alipoishia yeye.

Naye Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli akikubaliana na utabiri huo wa Rais alisema kuwa wanataka uzinduzi ufanywe na Rais Kikwete ili Rais mwingine ajaye asije kujivunia mafanikio hayo awe ametoka CCM au upinzani kwani fedha za ujenzi zimetafutwa na serikali ya awamu ya nne.

Wana JF je tunaweza kubashiri kuwa sasa serikali ya CCM imekubali yaishe? TAFAKARI!
Wapinzani bwana kwa kujikanyaga hamjambo, Na mtachonga sana wakati JK yeye kazi kwanza majungu no.
 
Tanzania itaendele kuwa chini ya utawala wa raisi kutoka upande wa CCM uchaguzi ujao wa 2015..kwani kuna watu amboa katika chama chao ni competitive kwa wapinzani na wanamvuto kwa jamii,aliyo sema JK nimawazo yake kama nguli wa siasa Afrika kwakuwa anajua Tanzania si yake peke yake wala ya CCM,kwani hata wakati wa chama kimoja Kinatawala ulikuwepo upinzani ndani yake..!!
 
Kwani wewe hapo kimekuuma nini? ina maana huwamini kuwa ZITTO ni zaidi ya SLAA?

acha propaganda wewe na haya mambo ya Zitto yamechuja siku hizi na yeye hana jipya kama enzi za Buzwagi na hauwezi ukamshindanisha na yeyote ndani ya CDM yupo Down siku hizi
 
Anajua anachokizungumza maana katika watu wenye ufahamu wa mambo ya ndani nchini kwetu na most informed person ni yeye....Anajua kwa 90% mpaka sasa CDM inachukua nchi na kwakua si mpenda mabavu anawaandaa wenzake ma-conservatives wakubali tu yaishe asije ishia kwenda the Hague na kuishi miserable life katika uzee wake....

Mheshimiwa Rais Taifa hili litakukumbuka kama utakubali kufanya smooth transition usije ruhusu wenye uchu wa madaraka wakakuchuza na mwisho laana kukuangukia ww wakati wao wakiwa wana starehe na familia zao...
 
Back
Top Bottom