JK atabiria wapinzani kushika dola!

Nadhani atakuwa anaanza kutumia busara, kwa kuwa njia peke yake ya kuepuka yeye na genge lake la magamba kutopelekwa the Hague, ni kukubali matakwa ya wananchi watakayosema kwenye sanduku la kura 2015, lakini akijifanya mkaidi na kuwatumia kina Mwema, Chagonja na Kamuhanda wake, atakuwa anajitafutia trip ya chapu chapu ya kwenda the Hague. Naamini hapendi yaliyomtokea mwenzake Charles Taylor!!

ukimaliza kuota kapige mswaki ukazurure.hapa tanzania hakuna kiongozi anaefanana wala kukaribiana na tylor
 
Moyoni wote wana ccm wanakubali na kukiri kuwa 2015 watakuwa wapinzani. Ila midomoni mwao wanakataa katakata kuwa 2015 upinzani unachukua nchi. Hongera kikwete na Magufuri kukiri hadharani kuwa ndivyo itakavyokuwa!
 
Nini maana ya Upinzani? Hakuna atakayesifia mazuri ya CCM, wajibu wa Upinzani ni kuanika maovu ya serikali ili wananchi waiadhibu uchaguzi ujao. JK yaonyesha ni MWAUPE au ndio HIVYO
 
Yani hawa viongozi wa ccm watajikuta wanaropoka yote bila kujijua mithili ya wale wanaonena kwa lugha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
acheni bange za kujificha uchochoroni nyie,kuna thred apa inasema chadema kuwa chama cha upinzani daima itafute
Mbona una jazba kiasi hicho??!! Au na wewe ni miongoni mwa wale mabilionea mlioficha mapesa yetu uswisi? Basi ni vyema mkazirudisha mapema, ili muepukane na mkono wa sheria, lakini mkisubiri2015, wakati CDM, imeingia madarakani, ni lazima mtaburuzwa mahakamani, ili muhukumiwe na kuzionja Segerea na Ukonga. Maana kwa sasa nyinyi hamuendi huko, badala yake, magerezani mnawajaza wapinzani kwa kesi zenu za kubabatiza!!
 
Rais Kikwete jana akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni aliwataka wapinzani wajifunze utamaduni wa kusifu yale mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM ili nao wakipata madaraka wafanye mara tatu maana ni lazima wataendeleza pale alipoishia yeye.

Naye Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli akikubaliana na utabiri huo wa Rais alisema kuwa wanataka uzinduzi ufanywe na Rais Kikwete ili Rais mwingine ajaye asije kujivunia mafanikio hayo awe ametoka CCM au upinzani kwani fedha za ujenzi zimetafutwa na serikali ya awamu ya nne.

Wana JF je tunaweza kubashiri kuwa sasa serikali ya CCM imekubali yaishe? TAFAKARI!
Kuna kitu inaitwa hoodwink, au tongue- in-cheek, please check it out.
 
acha kujipa matumaini hewa wewe.chama dola kife kirahisi hivo?mtasubiri sana

Inaelekea wewe jamaa, kutokana na jazba zako, inonekana umo kwenye system, kwa hiyo kutokana na hili joto la M4C, lilivyoshika kasi,limeshakuchanganya kabisa, lakini ngoja nikupe ushauri wa bure, mabadiliko nchini mwetu kwa sasa ni inevitable, na yamekuja kwa staili ya mafuriko ya gharika, sasa wewe unataka kuuchekesha, kwa kutaka kuyazuia mafuriko hayo kwa mchanga!! Ni jambo obvious kuwa huo mchanga utasombwa na vilivyomo ndani yake (MAFISADI) kwa hiyo hayo mayowe yako hayawezi kuzuia hizo changes za utawala zinazokuja!!
 
Mm nilishuhudia akisema wapinzani wasipinge kila kitu, km daraja wajenge ngazi ya 3 kwenda mbinguni sasa huo ni utabiri au jokes?
 
:flypig:wanajua kutiboa ni vigum mpaka pinda kazomewa c mchezo wana siasa za uchwara ndio maana mama yangu hawatoboi happo 2015 kwani kura zetu lazima tuzilinde ipasavyo kila idara na chopa :flypig:ndio zinaingia zicindikize kura na kuzilinda
:flypig:
 
"Fedha za ujenzi zimetafutwa na serikali ya awamu ya nne".
Ni sahihi zaid kusema "fedha za ujenzi zimekopwa na serikali ya awamu ya nne kulipwa na serikali ya awamu ya tano".
 
Rais Kikwete jana akizindua ujenzi wa daraja la Kigamboni aliwataka wapinzani wajifunze utamaduni wa kusifu yale mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM ili nao wakipata madaraka wafanye mara tatu maana ni lazima wataendeleza pale alipoishia yeye.

Naye Waziri wa ujenzi Dr. Magufuli akikubaliana na utabiri huo wa Rais alisema kuwa wanataka uzinduzi ufanywe na Rais Kikwete ili Rais mwingine ajaye asije kujivunia mafanikio hayo awe ametoka CCM au upinzani kwani fedha za ujenzi zimetafutwa na serikali ya awamu ya nne.

Wana JF je tunaweza kubashiri kuwa sasa serikali ya CCM imekubali yaishe? TAFAKARI!

i dont understand what you are talking about..................this guy is a smiling monster!!!
 
Upinzani kushika dola si swala la kutabiri ni swala la muda tu! Yaani kutabiri upinzani kushika dola ni sawa na leo Jumamosi utabiri kuwa kesho itakuwa Jumapili!
 
Back
Top Bottom