JK ashusha panga: Filikunjombe, Lembeli, Mkono, Bashe, Kingwangalla, Premji, Diallo watoswa

Ludewa

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
215
37
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM - NEC kimemalizika hivi punde huko Dodoma, huku wale wabunge wa CCM waliosaini fomu ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, majina yao yakiwa yamekatwa. wabunge waliokatwa majina yao kwa kosa la kumwadhibisha waziri mkuu ni Mhe. Deo Filikunjombe, ambaye aliomba nafasi ya UNEC wilaya ya Ludewa na mhe. Nimrodi Mkono aliyeomba Unec na Uenyekiti wa Wazazi Taifa.

My take: Mie nilidhani Filikunjombe na Mkono na wabunge wengine waliosaini ile fomu waliisaidia serikali ya CCM, loh kumbe kitendo kile kiliwaudhi wakubwa! ama kweli ccm ina wenyewe, akina Pindi Chana.

Zaidi:
Imeandikwa na Happiness Mtweve | Tanzania Daima | 26, Sept 2012

HATIMAYE Panga la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, limewashukia vigogo wa chama hicho na kuwatupa nje ya kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za uongozi wa jumuiya za chama na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Wakati panga hilo likiwashukia baadhi ya vigogo, Rais Kikwete ametoa kauli nzito ya kutaka wagombea waliopata kutoa kauli za vitisho dhidi ya chama hicho kufanya kile walichokusudia kukifanya.

Kikwete katika kauli yake hiyo alionekana waziwazi kukerwa na kauli za ‘patachimbika' au zile za kutishia kujitoa na kujiunga na vyama vya upinzani.

Akizungumza kwa ukali, Kikwete ambaye juzi alitamba akisema CCM haitakufa kama inavyotabiriwa na baadhi ya watu, alihitimisha kauli yake kwa kusema watu wenye kauli za namna hiyo walikuwa hawafai kuendelea kuwa wanachama wa chama hicho.

Panga la Rais Kikwete limewaangukia wagombea wenye nyadhifa zaidi ya moja serikalini na ndani ya chama pamoja na baadhi ya wabunge.

Wengine waliokatwa na vikao hivyo vya juu vya CCM vilivyomalizika jana mjini Dodoma, ni wagombea waliokuwa wakiibua malumbano na wakati mwingine kuikosoa CCM hadharani, makada waliojipambanua kama wapiganaji na wapambanaji wa ufisadi na baadhi ya wabunge walioweka saini zao bungeni kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ya kutaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ajiuzulu.

Habari kutoka ndani ya NEC, ziliwataja walioenguliwa kuwa ni pamoja na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana la CCM Taifa (UVCCM), Hussein Bashe.

Bashe na Kigwangalla ambao wamekuwa katika mvutano mkubwa wa kusaka madaraka ndani ya chama, majina yao yalipendekezwa kukatwa kuwania nafasi hiyo kuanzia kwenye sekretarieti, Kamati ya Maadili na Kamati Kuu kabla ya kuthibitishwa na NEC.

Makada hao wamekuwa kwenye mvutano wa kisiasa uliodumu toka mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu ambapo Bashe alienguliwa kuwania ubunge, Jimbo la Nzega na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Kigwangalla aliyeshika nafasi ya tatu. Nafasi ya pili ilichukuliwa na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Lucas Selelii.

Mbali ya hao, panga hilo limemkata Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.

Mgeja na Lembeli nao wamekuwa katika mvutano mkubwa ndani na nje ya chama. Uhasama wao unachochewa na kambi mbili kubwa zenye uhasama mkubwa.

Wengine waliokatwa ni Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na Mbunge wa Ludewa, Deo Filukunjombe.

Wabunge hao ni miongoni mwa waliotia saini kutaka Waziri Mkuu Pinda ang'oke. Duru za siasa zinasema kuwa msimamo wa wabunge hao kuhusu Pinda, ndio ulisababisha wakatwe kuwania NEC.

Athari za saini za kutaka kumng'oa Pinda ambazo zilisababisha Baraza la Mawaziri lipanguliwe na kuundwa upya, zimeonekana pia kumgusa Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, ambaye ametupwa nje kuwania nafasi ya uenyekiti wa wazazi CCM taifa.

Mkono ambaye ni wakili maarufu nchini, jina lake pia ni miongoni mwa majina yaliyokatwa katika vikao vya ngazi za chini na hivi karibuni alitahadharisha kuwa endapo hatarejeshwa na NEC, patachimbika.

Mbunge wa zamani wa Nyamagana, Antony Diallo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza aliyekuwa akitetea nafasi yake, Clement Mabina nao wamekatwa.

Akizungumza baada ya kufanya maamuzi hayo magumu, Rais Kikwete alisema anashangaa kuona baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho wakitaka kuuana kuingia NEC na kugeuza uchaguzi huo kuwa uwanja wa mapambano na kuwa na ndimi mbili.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo mjini hapa jana wakati akifunga kikao cha NEC.

Alisema hivi sasa wagombea wengi wamekuwa wakijitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na kung'ang'ania kupata ushindi kiasi cha wengine kufikia hatua ya kutoa kauli za vitisho kwa kusema wasipopata nafasi ‘patachimbika'.

"Inashangaza kuona kugombea NEC tu watu wanataka kuuana, wanakimbilia nini huko ndani?" alihoji Rais Kikwete.

"Ina maana watu hawa wanaonyesha dhahiri kuwa hawana nia njema na chama, bali wanaingia kwa maslahi yao binafsi, hivyo tuna kila sababu ya kuwakataa ili tujenge timu ya ushindi ambayo ndiyo nia yetu," aliongeza mwenyekiti huyo.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama kutogeuza uchaguzi huo kuwa uwanja wa fujo kwa kutumia silaha, majembe, ngumi na mikuki kwani hiyo ni fedheha kubwa kwa chama hicho.

Rais Kikwete alisema kama kuna wagombea ambao watajitoa ndani ya CCM na kuhamia chama kingine kutokana na majina yao kutopendekezwa, wajitoe.

"Hatuchagui wagombea wenye ndimi mbili ambao wanasema kama hatutapitishwa tutahamia chama kingine, hao tunawatakia kila la heri waende tu, kwani hawana nia njema na chama hiki," alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa ukali, alisema anajua suala la kuwaengua baadhi ya wagombea litazua mjadala, lakini nia ya chama ni njema katika kuleta sura mpya na uhai.

"Kufanya hivyo ni pamoja na kupata viongozi watakaokiletea chama ushindi katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2014 pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, hivyo lazima watu hao watambue kuwa kazi wanayoifanya ni kuunda timu ya ushindi wa chama na si wa watu.

"Najua kuna ndugu na marafiki ambao hawatateuliwa kutokana na kujaa kwa nafasi na mapungufu na madhaifu ambayo yalionekana baada ya Kamati ya Maadili kupitia majina yao, hivyo wasione kama wameonewa bali wajue kama ndio utaratibu wa chama wa kuhitaji viongozi shupavu, hodari na mwenye uwezo wa kukitetea na kukipigania chama na kukipa ushindi," alisema Rais Kikwete.

Aliwatahadharisha wagombea watakaotumia rushwa kwenye kampeni zao watambue kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wanafanya kazi yao muda wote, hivyo atakayekamatwa asije akamlaumu mtu.
baadhi ya majina ya waliopita kugombea ni haya:

CCM MWANZA
Anthony Diallo
Erenest Mabina
Zebedayo Athumani
Joseph Yaredi
Mashimba Hussein Mashimba

NYAMAGANA
Raphael Shilatu
Yahya Ibrahimu

SHINYANGA
Mwendapole hassan Ramadhan
Seja Alex
Dr.Maneno
Hamis Mgeja

majina zaid badae kidogo mtaletewa
 
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM - NEC kimemalizika hivi punde huko Dodoma, huku wale wabunge wa CCM waliosaini fomu ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, majina yao yakiwa yamekatwa. wabunge waliokatwa majina yao kwa kosa la kumwadhibisha waziri mkuu ni Mhe. Deo Filikunjombe, ambaye aliomba nafasi ya UNEC wilaya ya Ludewa na mhe. Nimrodi Mkono aliyeomba Unec na Uenyekiti wa Wazazi Taifa.

My take: Mie nilidhani Filikunjombe na Mkono na wabunge wengine waliosaini ile fomu waliisaidia serikali ya CCM, loh kumbe kitendo kile kiliwaudhi wakubwa! ama kweli ccm ina wenyewe, akina Pindi Chana.

CCM kama wee sio mshirika wa mafisadi huna chako
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM - NEC kimemalizika hivi punde huko Dodoma, huku wale wabunge wa CCM waliosaini fomu ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, majina yao yakiwa yamekatwa. wabunge waliokatwa majina yao kwa kosa la kumwadhibisha waziri mkuu ni Mhe. Deo Filikunjombe, ambaye aliomba nafasi ya UNEC wilaya ya Ludewa na mhe. Nimrodi Mkono aliyeomba Unec na Uenyekiti wa Wazazi Taifa.

My take: Mie nilidhani Filikunjombe na Mkono na wabunge wengine waliosaini ile fomu waliisaidia serikali ya CCM, loh kumbe kitendo kile kiliwaudhi wakubwa! ama kweli ccm ina wenyewe, akina Pindi Chana.

Tunashukuru kwa taarifa, ni habari njema maana ndiyo tuliyotegemea. Nasema habari njema kwa maana ya wanamageuzi ya kweli wanapokatwa majina yao watanzani tuko nyuma yao, na hakika uwanja ni mpana tu, na CCM watajutia nafasi za watu hao waliowakata katika jamii wanazowakilisha. Sikio la kufa halisikii dawa, ndio maana tunaona miti mingi inazidi kuteleza ambayo nyani amezoea kujishikila.

Waliokatwa majina yao hoja za msingi zinaeleweka kwa sababu ya kutolinda masilahi ya wasaliti wa taifa letu. Uwanja ni mpana na wazi, chagueni timu nzuri ambayo mtaongeza kasi ya mchezo kuchukua kombe.
 
Kwa hiyo ule mkwala wa Nimrod Nkono kwamba asipopitishwa patachimbika haujasaidia kitu? kudadadeki CCM, cjui ina gamba la mti gani wallah!

Mkwara wa Nimrod Mkono kwamba patachimbika si mjengoni Dodoma, subirini yatakayojilia na hatima za vuguvugu la mageuzi.
 
Msemaji wa haya ni Nape Nauye! Msipende kupewa taarifa potofu wakati kuna taarifa sahihi!
 
Imeandikwa na Happiness Mtweve | Tanzania Daima | 26, Sept 2012

HATIMAYE Panga la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, limewashukia vigogo wa chama hicho na kuwatupa nje ya kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za uongozi wa jumuiya za chama na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Wakati panga hilo likiwashukia baadhi ya vigogo, Rais Kikwete ametoa kauli nzito ya kutaka wagombea waliopata kutoa kauli za vitisho dhidi ya chama hicho kufanya kile walichokusudia kukifanya.

Kikwete katika kauli yake hiyo alionekana waziwazi kukerwa na kauli za ‘patachimbika' au zile za kutishia kujitoa na kujiunga na vyama vya upinzani.

Akizungumza kwa ukali, Kikwete ambaye juzi alitamba akisema CCM haitakufa kama inavyotabiriwa na baadhi ya watu, alihitimisha kauli yake kwa kusema watu wenye kauli za namna hiyo walikuwa hawafai kuendelea kuwa wanachama wa chama hicho.

Zaidi, angalia 1st post...
 
nahesabu siku za Mwakyembeee...,SIttaa...,sijui mgufuli.., hawa utawala ujao wanapumzishwa kwa umri am telling uuu. Na hv hawawezi piga ma deal ya nguvu ahahha watamaliza vyeo vyao na mshahara na marupupu chezeaa wasanii weyeee.

Mzalendo wa kweli hatakiwi CCM...,lbd mzalendo maneno na mzalendo wa kuegemea kundi mojawapo la watafuna nchi.

CCM inawenyewe kila siku mnaambiwa na wenyewe ndioo....sisiii...wanaitiaga kwa nguvu kweli kumbe chaguzi zinazokuja wanapunguzwaa na kuwa sio yao tena lol.....
 
Alama za nyakati hazizuiwi kwa matambiko wala mahoka, hilo ni pigo moja muhimu sana kwa ccm katika nyanja kuu mbili, siasa za uzee za kistarabu wamezitupa rasmi kwa kumtoa Mkono, na pili ni siasa za vijana zilizoanza kuleta sura muhimu isiyo ya kisultani baada ya kung'aa kwa nyota ya kisiasa ya Filikunjombe, sasa ni dhahi chama cha vijana kimeshikwa na Ridhiwani, Januari, na wengine wengi waikubalio IMLA
 
JK watanzania wangekupima kwa vigezo unavyowapima navyo wenzako wewe ungebakia kweli?

Hakuna kiongozi anayeongoza nchi kwa vitisho kama wewe kumbuka kauli zako wakati wa mgomo wa wafanyakazi!!

Unakumbuka kauli zako wakati wa mgomo wa madaktari?

Kuzushiana mambo hakuna mtu mzushi kama wewe JK, unakumbuka ulivyowazushia wenzako wakina Salim A Salim kuwa ni waarabu na uchafu mwingi uliowatupia wenzako ikiwemo kashfa za kutunga?

Suala la rushwa:
Serikali yako imejaa viongozi wala rushwa watupu ukiwemo wewe mwenyewe, wakati ulipokuwa waziri wa madini uligawa migodi kama njugu na pia ikiwemo suti uliyonunuliwa na yule mwarabu huko London.
 
Alama za nyakati hazizuiwi kwa matambiko wala mahoka, hilo ni pigo moja muhimu sana kwa ccm katika nyanja kuu mbili, siasa za uzee za kistarabu wamezitupa rasmi kwa kumtoa Mkono, na pili ni siasa za vijana zilizoanza kuleta sura muhimu isiyo ya kisultani baada ya kung'aa kwa nyota ya kisiasa ya Filikunjombe, sasa ni dhahi chama cha vijana kimeshikwa na Ridhiwani, Januari, na wengine wengi waikubalio IMLA

Nakwambia Yeriko shv kijana ukiwa mtetezi wa nchi yako kwa dhati kbs hauchukui muda CCM unafanyiwa zengwee kisa ni kulinda vijana wa kisultani. Kazi ipo na sita nae nashangaa anapiga makelel anasambabisha kina lembeli wanatolewa kafara wkt uspika tu alishindwa kuwazidi kete wapinzani wake na bado alikuwa hot je shv alivyochafuliwa kote CCM na CDM atauweza urais ...nae amalizie za mwisho mwisho na kina nape na mwakyembe wake
 
avatar9763_4.gif

Msemaji wa haya ni Nape Nauye! Msipende kupewa taarifa potofu wakati kuna taarifa sahihi!

4_%2BJK%2Bakisakata%2Bmuziki%2Bwa%2Bhamasa%2Bya%2BChama%2Bna%2BVijana%2Bwa%2BCCM.jpg

3_%2BJK%2Bakisakata%2Bmuziki%2Bwa%2Bhamasa%2Bwa%2BCCM%2Bna%2Bvijana%2Bwa%2BChama%2Bbaada%2Bya%2Bkuwasili%2Bnje%2Bya%2Bukumbi.jpg

Hii ndiyo CCM na mwenyekiti wake ni burudani tupu, hapo nchi itajengeka kwa mtindo huu?
 
politiki;

Umesema ukweli mtupu ndugu yangu maana kama kweli mbingu ipo Jk ataumbuka sana siku hiyo!

Lakini mkuu usisahau kwamba katika nchi hii CCM wana sera ya kuwafunga wezi wadogo na kuyafanya majambazi sugu kuwa watoa hukumu kwa wadokozi na raia wema huku yakishika nafasi za uwaziri, urais, makamu wa rais ubunge udiwani na vyeo vingi vya kichamachama ili mradi kutumia hicho chama kama kichaka; so usishangae kuona Kamuhanda ni kamanda wa polisi anaruhusu mauaji ya mtu asiye na hatia jiulize kama angekua ndio Jambazi ingeekuaje?

Hivyo amini tunaongozwa na majambazi na magenge ya wauaji yaliyopachikwa vyeo bandia vya kuongoza nchi hii
 
Last edited by a moderator:
najiuliza hivi Diallo kakosa nini mbona wamemtupa nje

halafu hii kauli ya " msipo nichagua/niteua naenda upinzani " mbona nasikia hata yeye aliitumia kumbe alikuwa anatishia tu

Yaani unauliza fisadi Diallo kakosa nini haujui vyombo vyake vya habari vinavyyooichafua CCM na kuipambaCDM mwanza...kwanza nae hana jipya huyo mafisadi alipokuwa waziri alituibia sn pale wizarani
 
anaye jua tafasiri ya maneno haya atupe hapa maana nadhani huu ni unabii kwao

'' MENE MENE TEKERI PERESI ''
 
Back
Top Bottom