Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Nauliza: Kutokana na yaliyojiri hivi karibuni -- hasa kile kiwewe kilichompata mgombea urais wa CCM kutokana na wimbi kali la nguvu za Dr Slaa -- kwanini mgombea huyo asiamuru kufutwa kwa kesi za Mramba, Mwakalebela na vigogo wengine wa chama hicho weanaokabiliwa na kesi mahakamani?
Kila mtu ameona ujasiri mkubwa aliofanya Rais Kikwete katika kuvunja maadili (ethics) kwa kuwanadi Mramba na Mwakalebela kwa kuwaambia wasitishike na lolote -- hatua ambayo wengi wanatafsiri kwamba kesi zinazowakabili si chochote au lolote, kwa nini asifupishe tu mambo na kuwafutia kesi sasa hivi, kuliko kuwafanyia Watz geresha kubwa? Anaogopa nini kufanya hivyo sasa hivi?
Kila mtu anajua huko mbeleni kesi hizi ama zitafutwa, au washitakiwa watashinda (kutokana na "matamshi ya JK"), au watasemehewa muda si mrefu baada ya kutiwa hatiani.
Uwezo anao. Katiba inamruhusu, anangoja nini? Anaogopa nini kuvunja maadili mengine katika haha zake za kutaka kumpiku mpinzani wake?