mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.(1)
Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini(2).
Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.(3)
Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu (4).
Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma.
Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu(5),
Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi, alisema Kikwete.(6)
.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.(7)
TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.(8)
CHANZO: NIPASHE
"Huku fedha zinatafunwa sana, maana ripoti zinaandikwa vizuri ila mambo hayajafanyika, mimi mwenyewe kule nyumbani kwangu waliandika kuwa wamejenga madaraja mawili, lakini kila wakati napita hapo sijawahi kuona hilo daraja waliloandika kuwa limejengwa, kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kutaka kuchunguza matumizi ya fedha aliandamwa kuanzia kule wilayani hadi huku juu Tamisemi, sasa inaonekana ninyi mnalea wezi acheni kabisa tabia hiyo," alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE
Kwanini mnaruhusu hali hii, wanaohusika wakishindwa kufanya hivyo washughulikiwe, msiwachekee watumishi wazembe maana mnasababisha malalamiko kila kukicha, alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE
"Lakini tukomeshe kabisa tatizo hili na hata mkitumia milioni 200 sioni tatizo cha maana nataka tukomeshe wizi huu, na kama hamna fedha za kufanya kazi hiyo semeni mimi nitawapa tu." alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE
<br />aisee, nyie acha tu tusimdharau babu!
big up JK
E bana, that was ridiculous but funny, nilim maindi lakini nikaishia kucheka.jana nilicheka sana...eti anasema.....'' ni nani anapaswa kuwapandisha watu vyeo?'' ghasia akajibu ni yule plae.....ni wewe? yaani unatakiwa ukiwa unafika ofisin computa yako inaflash tu majina ya wanaopaswa kupandishwa vyeo......computa mnazo jamani zitumieni vizuri''