JK: Amkaba koo Waziri Ghasia

Kumbe anayajua yote hayo? Alikuwa wapi miaka 5 iliyopita? Sasa itachukua miaka mingine 5 kukagua kama aliyoagiza yametekelezwa?
 
Mimi binafsi naona usanii at its best;

JK alishawahi kutuambia kuwa anawajua wauza unga na akawapa muda
akasema anawajua wa EPA warudishe
Juzi alisema tuwaachie TAKUKURU na Polisi wafanye kazi yao... leo anamwambia waziri usiwaachie hao watafanya kazi miaka na miaka... KUMBE ANAJUA TUKUTUKU NI WASANII EH? but is he ok with that, right??
Wherever he goes, he seems to haev all the solutions to our problems, alas, nothing has moved since 2005

Juzi kasema hawajui, hajui na hata kama wapo au hawapo yeye hawajui... then anasema ninawajua, najua mnafuga wezi mie najua... NINI HIKI JAMANI?:angry:

Usanii mpaka lini?:drum:
 
Picha za kuchonga na sinema mbalimbali za aina hii zitakua nyingi mno in town kujaribu kuonyesha kwamba JK kazinduka usingizi wa pono na kwamba eti sasa anaanza kuchapa kazi baada ya MAFISADI kufilisi nchi chini ya ufadhili wake.
 
Wapo wapi Kagoda, Deep Green na Meremeta? Kwa nao hawajatafuna mabilioni ya umma? Anataka kupendeza kwa kupulizia manukato mavazi yaliyochafuka? Kama yupo makini angedadisi pia ni watumishi wangapi wasio na sifa walioajiriwa kwa mlango wa nyuma na kupelekwa vituoni kwa staili ya "uhamisho" toka mamlaka vilizovunjwa au kupendekezwa kuvunjwa ikiwemo Tume ya Jiji
 
Kwa kweli naona aibu.
Huu ni aina gani ya utawala au uongozi?
Ni kale kale mchezo wa kuigiza tu.
Najutaaaa...........
 
Huyu Waziri Hawa Ghasia tangu wamtimue Prof. Baregu pale UD kwa kusema eti haitajiki aende huko wanapomthamini, wakati kuna tatizo la walimu alinitoa nyongo sana. Pia amekuwa akiwanyima contract ma-lectures wastaafu UD na SUA kwa sababu tu ni wapinzani, hata kama hizo fani zao hazina wakuzifundisha. Ninachoona huyu mama anajua kufanya visasi tu na siyo kazi. Ana jeuri huyoo, usipime!
 
Wahuni tu hao. Watu wengine hatujalipwa mishahara tangu Oktoba tulipoajiriwa halafu wengine wanacheka cheka hapa! Porojo tupu na usanii mwingi wakujionyesha kwenye vyombo vya habari.
 
mabilioni yanayotafunwa kutokana na mishahara ya watumishi hewa.(1)

Rais Kikwete alianza kumhoji Waziri Ghasia kwanini mabilioni ya fedha ya watumishi hewa yanaliwa na wahusika hawachukuliwi hatua zozote na wanaendelea kuwa kazini(2).

Baada ya kauli hiyo, Kikwete aliingilia na kuhoji kwanini wahusika wasitafutwe wakarejesha fedha hizo na kisha wakafikishwa polisi ili waandaliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani.(3)

Waziri Ghasia aliposimama na kumweleza Rais Kikwete kuwa polisi na Takukuru wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo, Kikwete aliingilia kati tena na kumweleza kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa wizara yake hivyo hawapaswi kuitupia mzigo Takukuru. “Hawa watumishi hewa wako wizara zote kwanini hamuwatafuti, maana fedha za umma zinazidi kupotea, Waziri hili liko ndani ya uwezo wenu msiwaachie Takukuru, mkiwaachia hao uchunguzi unaweza kukaa miaka na miaka huku wahusika wakiendelea kutafuna fedha za umma, mnaweza kusema mnaendelea na uchunguzi mkakuta wale wezi mnaowatafuta wengine wamekufa, wengine wameshastaafu (4).

Baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Waziri Ghasia alisimama na kuendelea kumweleza kuwa wizara yake imeanza mkakati wa kuwatafuta watu wanaolipwa mishahara ya watumishi hewa, lakini kabla hajafika mbali Rais Kikwete aliingilia tena kati na kumweleza kuwa watu hao wanafahamika kwa kuwa wako ndani ya utumishi wa umma. “
“Waziri haya mambo yako ndani ya mamlaka yenu na hampaswi kukasimu mamlaka yenu(5),

“Wizara zote na kwenye halmashauri wabaneni hawa watawatajia wezi hawa ila kama mnaona hamna mamlaka nao nipeni kazi hiyo mimi na Luhanjo (Katibu Mkuu Kiongozi) tutafanya kazi hiyo maana hakuna aliye juu yetu, tutapambana nao, hatuwezi kuacha fedha za umma zinaendelea kuliwa kama shamba la bibi,” alisema Kikwete.(6)
.
Katika hatua nyingine, Kikwete alithibitisha kuwa gharama za maisha zimezidi kuwa kubwa hivyo alimwagiza Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuangalia uwezekano wa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma ili kuwapunguzia makali ya maisha.(7)
TAMISEMI WANALEA WEZI
Akiwa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kikwete alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo ndio wamekuwa wakilea wezi wa fedha za umma kwenye halmashauri nyingi.(8)
CHANZO: NIPASHE

My take:
1. Kikwete kama waziri wa siku nyingi katika idara hajui kuwa pesa zinatafunwa hadi ashangae leo.
2. Yeye amewachukulia hatua gani wale wa Richmond, Kagoda, Meremeta, Tangold aliopelekewa majina na bunge
3. Jk amemfikisha nani mahakamani, na ile kamati yake ya kusimamia pesa za EPA imerudhisha kiasi gani
4. Mbona yale yaliyokuwa ndani ya uwezo wake hajafanya hata moja,na je si kweli yeye aliaachia watu wakastaafu wakiwa wezi
5. Kwanini Richomnd, EPA n.k alikasimu madaraka kwa Takukuru na tume ya luhanjo.
6. Haa!!! JK,shamba la bibi? lipi zaidi ya Richmond,EPA,Kagoda, Meremeta na Dowans. Please Mr President are you candid with your talk.
7. Kuongeza mishahara ni suluhisho la matatizo?, kipi bora kuongeza mishahara au kuzuia Inflation.Unataka twende sokoni na furushi
la pesa kununua mkate.! Uliwasiliana na wachumi wako kabla ya kusema haya Mheshimiwa Rais.
8. Haa! JK kuna mlezi wa wezi zaidi yako? hawa si wanafuata nyayo tu.

Conclusion: Huyu ndiye hasa JMK. Anajaribu kuonyesha kuwa anafanya kazi. Hakuna alichokisema ambacho yeye amewahi kufanya tofauti. Haya yote alipaswa kuongea na waziri wake katika vikao. Tulitaka tusikie mikakati ya kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi na si maswali na majibu.
Kama kawaida yake lengo lilikuwa kuonyesha kuwa anajali na anasilikiza shida za wananchi.
Utendaji kazi wa namna hii hautufikishi mahali popote. Huu ni usanii tu kuwalaumu mawaziri wake kwa kile asichokifanya. Yeye ndiye chanzo cha mfumuko wa bei, kulea wezi na utendaji mbovu. Kama angelikuwa makini Hawa Ghasia asingekuwa waziri tena, lakini si tunajua uwaziri ni suala la 'technical know who'
 
"Huku fedha zinatafunwa sana, maana ripoti zinaandikwa vizuri ila mambo hayajafanyika, mimi mwenyewe kule nyumbani kwangu waliandika kuwa wamejenga madaraja mawili, lakini kila wakati napita hapo sijawahi kuona hilo daraja waliloandika kuwa limejengwa, kuna wakati Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo aliwahi kutaka kuchunguza matumizi ya fedha aliandamwa kuanzia kule wilayani hadi huku juu Tamisemi, sasa inaonekana ninyi mnalea wezi acheni kabisa tabia hiyo," alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE

Bold nyeusi: Anajua kuna madaraja mawili hewa kila siku halioni sijui kwa miaka mingapi kachukua hatua gani? Hapa naona analalamika. Rais huyo!
Kwenye nyekundu: Mkuu wa wilaya Bagamoyo anachunguza ubadhirifu, anaandamwa hadi juu. "Rais" anashitaki au anajenga hoja gani hapa. Na yeye alinyamaza baada ya kuona Mkuu wa wilaya anaandamwa? Aliogopa? Kama anyemwandama ana nguvu kuliko rais, basi kikwete ana haki ya kuogopa.
Kwenye Bluu: "Rais" anaconclude kwa kukemea vikali! "acheni kabisa tabia hiyo"jamani" WanaJF huyu ni Rais au rahisi?
Anaongea kama mwananchi wa kawaida anvojadili politiks ya nchi hii akiwa viti virefu?
"Umri haujatimia" Mwalimu J.K. Nyerere.
 
“Kwanini mnaruhusu hali hii, wanaohusika wakishindwa kufanya hivyo washughulikiwe, msiwachekee watumishi wazembe maana mnasababisha malalamiko kila kukicha, alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE

1. Rais JK anza na mtumishi mzembe aliyeko mbele yako, Hawa Ghasia(jina lenyewe!). Mshughulikie. Mzembe atashughulikiaje wazembe wenzake?
2. Wewe Kikwete ni mtumishi mzembe namba moja. na watanzania hawakuchekei kama unvomtaka Hawa asiwachekee midebwedo wenzake. Ndo maana watanzania walikushughulikia Oct. 31, 2010, thanx to NEC ya Jaji na Kiravu, featuring uharamia wa taifa.
3. Mlio karibu na JK mpeni kioo ajitazame.
 
"Lakini tukomeshe kabisa tatizo hili na hata mkitumia milioni 200 sioni tatizo cha maana nataka tukomeshe wizi huu, na kama hamna fedha za kufanya kazi hiyo semeni mimi nitawapa tu." alisema Rais Kikwete.
CHANZO: NIPASHE

Mwizi anakabidhiwa feza ya maana apeleleze wizi alioufanya! MAFI YANGU
Agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Hamna lolote amini usiamini anajua kila kitu Jk. Haya ndio yale yakumwambia waziri wa sheria atoe tamko kuhusu katiba alafu kuona wananchi wamemkalia koo; akamgeuka akamwambia aseme ni tamko lake binafsi. Amini usiamini huu ni mchezo wakuigiza. Hili la waziri wa Sheria source ni mimi and I am confident with this information so mtu asihangaike kuuliza source nyingine. Huyu raisi si mwamini kabisa arghh!
 
Mkwere anafuta public popularity ili wadanganyika tujue kwamba eti kashaanza kupambana na ufisadi. Anajdanganya mwenyewe sio yetu macho na maskio.
 
jana nilicheka sana...eti anasema.....'' ni nani anapaswa kuwapandisha watu vyeo?'' ghasia akajibu ni yule plae.....ni wewe? yaani unatakiwa ukiwa unafika ofisin computa yako inaflash tu majina ya wanaopaswa kupandishwa vyeo......computa mnazo jamani zitumieni vizuri''
E bana, that was ridiculous but funny, nilim maindi lakini nikaishia kucheka.

Yani jamaa alivyoongelea kupandishana vyeo utadhani ni appointment za kukutana na mtu tu, utegeshe Windows Outlook ikukumbushe kwenye screen. Hakuna kuangali performance, kuandaa mshahara mpya, etc. etc. ni vuuup, leo Athumani is due for promotion, vuuuup, Athumani you are promoted!

Anyhow, tatizo kubwa na hii mikutano ya Kikwete nadhani ni kwamba Kikwete haendi na agenda yake, anasema anaenda kufuatilia utendaji wa maagizo yake lakini akifika pale anasikiliza hotuba ya Waziri halafu agenda inabadilika kwa kumlazimisha Kikwete kujibu ule utumbo alioongelea Waziri. Ndio sasa wanabaki kubishana kuhusu kutegesha komputa ya mpandisha vyeo imkumbushe kupandisha watu vyeo. Badala ya kuongelea vitu substantive kama vile TUCTA wanavyolia navyo.
 
Objectivity ya JF ni sawa na ya binti ambae ndio kwanza amevunja ungo. Full kuendeshwa na hormones....emotions dont build countries. Education, innovation, enterprise, good governance, rule of law, sound economic and fiscal policy, increasing the franchise, those are the things that build nations.Jazba, one sided pessimistic subjective perceptions do not. JK kwa hili muungeni mkono akishindwa ku enforce kwa watumishi wake basi ndio mmlaumu. Radicals never really achieve anything. Ask Maximillien Robespiere .
 
Back
Top Bottom