Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
WanaJF:
Baada ya kutafakari hotuba ya JK aliyotoa akiwa katika magwanda ya kijani hasa katika sehemu ile aliyojaribu kujisafisha kutokana na sakata la kampuni ya Dowans – ni dhahiri ameshindwa kukidhi kiu ya Watanzani wengi kuhusu kuhusika/kutokuhusika kwake katika sakata hilo.
Ameshindwa kukidhi kiu kwa sababu yeye tu ndiye alikuwa anazungumza – hakuna mtu wa kumuuliza -- maana kulikuwapo maeneo mengi alifunika funika tu au kupindisha ambapo kama kungekuwa na watu makini wa kumuuliza kutoa ufafanuzi, basi angenasa mtegoni bila ya wasiwasi wowote.
Mimi naona ili kukata mzizi wa fitina kabisa kabisa atafute angalau ka-ujasiri kidogo aitishe mkutano na waandishi wa habari ili alielezee sakata hilo na aruhusu kuulizwa maswali. Asichuje waandishi watakaohudhuria – kila chombo cha habari (TV, Radio na magazeti makubwa) yatume wanahabari wawili.
Akiweza kujieleza vizuri hapo ndipo tutajua kuwa hahusiki na sakata hilo (na si lazima awe hana hisa katika Dowans kama anavyong'ang'ania).