JK akataa stendi ya muda!

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,579
1,164
Raisi kikwete kawaagiza mkuu wa mkoa wa dar na menaja wa tanrods mkoa wampe majibu ndani ya wiki moja ni wapi itajengwa stendi mpya baada ya ile ya ubungo kuhamishwa.
Amekataa wazo lao la kujenga stendi ya muda pale chuo kikuu (udsm) na kuwaambia huko ni kufuja fedha za serekali.
Jk alikuwa anaweka jiwe la msingi ktk mradi wa mabasi yaendao kasi.
 
JK, hapo sawa!!!!!!!!!!!

Mimi niwasaidie kuchagua eneo,

Naamini Mbezi Luisi ni sahihi kwa sasa kwa sababu, pale kuna njia za kwenda sehemu nyingi( mfano, Goba mpaka mbezi Tanki bovu, Wazo, Luisi hadi Bunju, Luisi/Kinyerezi/Banana/tabata,), pia wakajenga stand nyingine kubwa kabisa pale Kongowe kwenye makutano ya kwenda Kigamboni na Mkuranga ili isaidie watu wa Mtwara/Lindi na Tunduru.

Naam kwa njia ya Bagamoyo Msata, wakawa na Stand yao kubwa kabisa Mapinga karibu na inapotokea njia itokayo Kibaha.
 
Siku zote raisi makini, anafanya maamuzi makini. Hongera jakaya.
 
Raisi kikwete kawaagiza mkuu wa mkoa wa dar na menaja wa tanrods mkoa wampe majibu ndani ya wiki moja ni wapi itajengwa stendi mpya baada ya ile ya ubungo kuhamishwa.
Amekataa wazo lao la kujenga stendi ya muda pale chuo kikuu (udsm) na kuwaambia huko ni kufuja fedha za serekali.
Jk alikuwa anaweka jiwe la msingi ktk mradi wa mabasi yaendao kasi.

Kufuja pesa ya ..... kama ni yeye kweli ambaye leo kakumbuka pesa ya serikali, basi kumbe iko siku waliokufa watafufuka!
 
Huenda kwenye ulaji huu hakuna mtu wake hivyo ameamua kujitoa kimasomaso. Mbona haoni ulaji wa Tanesco, IPTL, Dowans na madudu mengine mengi yenye kila baraka zake? Mbona haoni madudu ya WAMA na uagizaji mafuta nje ambapo kuna mkono wa watu wake wakiongozwa na Rahma Kharoos Kasiga aka Nyumba ndogo ya mkubwa wa inchi? Mambo mengine yanachekesha. Hata hivyo haiko mbaya hizo ndizo sanaa za mkuu mwenyewe. Yeye akifuja pesa ya umma kwa matanuzi ughaibuni si kufuja siyo?
 
Mimi niwasaidie kuchagua eneo,

Naamini Mbezi Luisi ni sahihi kwa sasa kwa sababu, pale kuna njia za kwenda sehemu nyingi( mfano, Goba mpaka mbezi Tanki bovu, Wazo, Luisi hadi Bunju, Luisi/Kinyerezi/Banana/tabata,), pia wakajenga stand nyingine kubwa kabisa pale Kongowe kwenye makutano ya kwenda Kigamboni na Mkuranga ili isaidie watu wa Mtwara/Lindi na Tunduru.

Naam kwa njia ya Bagamoyo Msata, wakawa na Stand yao kubwa kabisa Mapinga karibu na inapotokea njia itokayo Kibaha.

Mshkaji kwa mujibu wa maelezo yako, yao.
nekana umeinvest heavily maeneo hayo.
 
Huenda kwenye ulaji huu hakuna mtu wake hivyo ameamua kujitoa kimasomaso. Mbona haoni ulaji wa Tanesco, IPTL, Dowans na madudu mengine mengi yenye kila baraka zake? Mbona haoni madudu ya WAMA na uagizaji mafuta nje ambapo kuna mkono wa watu wake wakiongozwa na Rahma Kharoos Kasiga aka Nyumba ndogo ya mkubwa wa inchi? Mambo mengine yanachekesha. Hata hivyo haiko mbaya hizo ndizo sanaa za mkuu mwenyewe. Yeye akifuja pesa ya umma kwa matanuzi ughaibuni si kufuja siyo?

Dah!! Hili ndo tatizo la kukariri. Wengine wanaongelea issues, we unaongelea watu. Hebu tuache tujadili issues. Ebooo!!"
 
Naona hata wewe umeniangalia mimi badala ya kuangalia issue. Jaribu kuangalia issue utaona ni wapi umenoa ebo!
 
sasa naamini ipo siku wafu watafufuka..........

Ni kweli mkuu, mambo huwa yanabadilika.
Asili ya Binadamu ni kubadilika kadri mazingira yanayo mzunguka yanavyo badilika ili kukabiliana nayo.
Mabadilko chanya ni mazuri siku zote na yanakubalika.
 
hata mimi hili nimeliona mkuu.....
 
Mimi niwasaidie kuchagua eneo,

Naamini Mbezi Luisi ni sahihi kwa sasa kwa sababu, pale kuna njia za kwenda sehemu nyingi( mfano, Goba mpaka mbezi Tanki bovu, Wazo, Luisi hadi Bunju, Luisi/Kinyerezi/Banana/tabata,), pia wakajenga stand nyingine kubwa kabisa pale Kongowe kwenye makutano ya kwenda Kigamboni na Mkuranga ili isaidie watu wa Mtwara/Lindi na Tunduru.

Naam kwa njia ya Bagamoyo Msata, wakawa na Stand yao kubwa kabisa Mapinga karibu na inapotokea njia itokayo Kibaha.

kujenga hiyo stand moja tu rais amehoji cost implication!, sasa wewe waja na utitiri wa stand?! Si unachekesha?. Kwa maoni yangu stand kubwa ingejengwa kwenye bonde la jangwani kisha kuwe barabara nyingi za kutoa abiria nje ya mji، hivyo paitwe central bus station, period
 
Kwa jiji kubwa kama Dar ni lazima vituo vya huduma viongezwe na kupanuliwa. Ukienda Mbagala rangi 3 kuna terminal pale ya magari ya kusini, hapo hapo kuna terminal ya dala dala, ukienda Mbezi Luisi kuna terminal mpya ya dala dala na ile ya mwanzo imebadirishwa na kuwa sehemu ya kuogesha pick up.

Jiji la Dar sasa linaongeza inlet nyingine ya tatu, yaani Msata/Bagamoyo/Dar na hii inaongeza usalama na kupunguza msongamano zaidi njia ya Morogoro. Kuongeza Stand kubwa hakuepukiki mkuu. Miji yote ya zamani inahaha kupanua stand, sembuse Dar. Ni suala la wakati tu, na mimi nakuombea afya njema ili uzione hizo stand tatu mkuu.
 
Back
Top Bottom