JK ahaha kupandikiza kibaraka wake TUCTA

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174
Mgaya apata mpizani TUCTA

na Datus Boniface

amka2.gif
MJUMBE wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi nchini (TUCTA), Mussa Mnyeti ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Katibu Mkuu ndani ya chama hicho.
Hadi sasa nafasi hiyo inashikiliwa na Nicolas Mgaya, ambapo uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho unaratajiwa kufanyika Agosti mwaka huu.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mnyeti alisema nia, uwezo, na sababu anazo za kuwania nafasi hiyo.
“Uwezo, nia na sababu ninazo za kuwania na kuwa Katibu Mkuu wa TUCTA, kwa ajili ya maslahi ya wanachama na wafanyakazi wote nchini Tanzania, vijana nawaomba wanikubali katika hili kwa ajili ya malengo hayo yaweza kufanikiwa,” alisema.
Alisema sababu zilizomfanya kuwania ni pamoja na kuleta ushirikiano baina ya wafanyakazi na vyama vyao.
Alitaja sababu nyingine ni kupigania haki, maslahi pamoja na usawa wa wafanyakazi wa ngazi zote.
Katika maelezo yake alisema endapo akipata nafasi hiyo atapigania kima cha chini cha mshahara kiwe shilingi 315,000 ili kutimiza pendekezo la TUCTA.
Alisema pia atapunguza kodi za wafanyakazi kutokana na makato mbalimbali yanatofanywa katika mishahara yao.
Aidha aliahidi kuwapigia wafanyakazi kulipwa asilimia saba la pato la taifa.
 
Kweli JK ni kiboko.huku anawashawishi TUCTA wamkubali kwa kuwaahidi mishahara wafanyakazi bajeti ijayo na wao walivyo viruka njia wamemwalika katika sherehe ya MEI moSI.kumbe mwenzio anapanga kuwasarambatisha kwa kuwawekea mamluki.........poor TUCTA..............................................
 
PHP:
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mnyeti alisema nia, uwezo, na sababu anazo za kuwania nafasi hiyo.
   "Uwezo, nia na sababu ninazo za kuwania na kuwa Katibu Mkuu wa TUCTA,   kwa ajili ya maslahi ya wanachama na wafanyakazi wote nchini Tanzania,   vijana nawaomba wanikubali katika hili kwa ajili ya malengo hayo  yaweza  kufanikiwa," alisema.
   Alisema sababu zilizomfanya kuwania ni pamoja na kuleta ushirikiano baina ya wafanyakazi na vyama vyao.
   Alitaja sababu nyingine ni kupigania haki, maslahi pamoja na usawa wa wafanyakazi wa ngazi zote.
   Katika maelezo yake alisema endapo akipata nafasi hiyo atapigania  kima  cha chini cha mshahara kiwe shilingi 315,000 ili kutimiza  pendekezo la  TUCTA.

Tueleze rekodi yako ya kuwapigania wafanyakazi inasemaje????????????????????????????? Kabla ya wafanyakazi kuamini ahadi zako...............
 
PHP:
Alisema pia atapunguza kodi za wafanyakazi kutokana na makato mbalimbali yanatofanywa katika mishahara yao.
   Aidha aliahidi kuwapigia wafanyakazi kulipwa asilimia saba la pato la taifa.

Kwa hii si ni hoja tayari ipo mezani kwa serikali.........................mbona huna jipya??????????????????????????????????
 
Kwa nini ni kibaraka wa JK? CV yake tafadhali...
Kaka huyu alikuwa MKufunzi pale Monduli TC sijui kama ameacha, na alikuwa mkimbiza mwenge karibu muda wote alipokuwa pale TC. Pia ni kada wa CCM hata ukikutana naye utamkuta "amebeba Jembe na Nyundo {Joke)".
 
Jakaya anataka kupandikiza mamluki hapo TUCTA ili awe boya lake na wafanyakazi wasiwe na sauti ya kupigania hakizao; watakuwa wajinga sana wakimtosa Mgaya wakati huu!! Ajenda iko pale pale lazima kumtoa Nicholas na kumuingiza Mussa, mnaiona hiyo wanajanvi halafu jamaa anahubili kupiga vita udini wakati yeye kwa vitendo vyake ndio muasis i wa huo udini!
 
Ninamashaka na vyama vya wafanyakazi. Wanataka serikali ipunguze kodi katika mishahara ya wafanyakazi wakati vyama hivyo vinachota kutoka mishahara ya wafanyakazi makato ya kila mwezi bila kuwaonyeshea mapato na matumizi mwisho wa mwaka. vyama hivi vinapeleka wapi michango ya wafanyakazi?
 
Hawa nao nahisi pia ni mafisadi tu.Kila mwezi wanachukua fedha zetu lakini hata siku moja hawatuelezi ni namna gani wametumia,wezi tu!Kwanza mi nashangaa wananikata bila ridhaa yangu na faida yake wala siijui....UPUUZI MTUPU!
 
Musa Mnyeti chizi flani hivi, waliosoma UDSM kwa 2002 - 2006 watakuwa wanamkumbuka vizuri, kituko kikubwa alichowahi kukitoa ni pale alipochukua form ya kugombea uspika na akina msekwa na sitta akiwa mwaka wa tatu.
 
Basi kweli atakuwa ni mamluki.
 
Mhhh tusiharibu uchaguzi Huu mzito tusiponde mtu ili kumbeba Mgaya. Angalizo tu huyu wala simjui vizuri huyu Mnyeti lakini asibambikiwe vitu kunyoosha njia ya Mgaya ambaye nilisikia Pia ana uhusiano mzuri tu na baadhi ya Mafisadi
 
Basi kweli atakuwa ni mamluki.

Ndiyo na Hapana, ndiyo kwasababu hakuna linaloshindikana duniani lakini hapana kwakuwa kila mtu anamfahamu jinsi asivyo makini, hupenda kutafuta umaarufu usio wa lazima, kifupi anaonekana ni chizi zaidi. Alipo pewa kuongoza mbio za mwenge ilikuwa ni kumjaribu kwa kazi nyingine za chama lakini alichemka sana, chama kikamsusa ndio maana kaishia kwenye ualimu, vijana wenzake wengi wamepewa nafasi katika chama au kazi nyingine za maana.
 
Jakaya anataka kupandikiza mamluki hapo TUCTA ili awe boya lake na wafanyakazi wasiwe na sauti ya kupigania hakizao; watakuwa wajinga sana wakimtosa Mgaya wakati huu!! Ajenda iko pale pale lazima kumtoa Nicholas na kumuingiza Mussa, mnaiona hiyo wanajanvi halafu jamaa anahubili kupiga vita udini wakati yeye kwa vitendo vyake ndio muasis i wa huo udini!

JK ni mdini kwa vitendo na anatuhadaa wadanganyika kwa maneno .

Angalia uteuzi wake, majaji, wakurugenzi, wakuu wa vyuo, mawaziri and you name them. Kwa hiyo Jk anatuhadaa kwa maneno ili tusahau kuhoji kuhusu uteuzi wake

Angalia jinsi alivyowadanganya watanzania kuhusu maisha bora kwa kila mtanzania.= maisha bora yako wapi, leo kuna mfumuko wa bei.

Wafanyabiashara wanakumbatiwa, wanapigwa busu wakati watanzania wanaumia na bei mbaya ya sukari.

Sukari ni hitaji muhimu na lazima kwa masikini watanzania -
Watanzania tunaumia saaanaaaa.

Kukatwa kodi mara mbili mbili.... (PAYE na VAT) mfumuko wa bei na huku wafanyabiashara wanakwepa kodi na kuwanyonya watanzania.

Watz sasa tupo kwenye mchakato wa mageuzi ya kiuongozi. Viongozi tunaowataka ni waadilifu na wachapakazi na wala si viongozi wa kupachikwa pachikwa na umamuluki ndani yake. Tutataka kuona yeye anauweza uongozi kiasi gani zidi ya Mgaya vinginevyo akaendelee kukimbiza mwenge maana hatapata!
 
Na Mgaya mwambieni aje CDM tutampa cheo ngazi za juu maana ameonyesha anaweza kukaa pande za huku kidogo. Ila ndo kufulia kwake kunaanza. Malaria huanza taaaaaratiiibu
 
Hao wanaochagua viongozi tucta wakifanya kosa kumuacha Mgaya kiboko ya JK watakuwa wamekosea maisha yao yote!!Musa waachane nae kwa sasa maana anapandikizwa kuua Tucta!isiwe nguvu pia watauaa CWT kuweka watu wao....angalizo
 
Musa Mnyeti chizi flani hivi, waliosoma UDSM kwa 2002 - 2006 watakuwa wanamkumbuka vizuri, kituko kikubwa alichowahi kukitoa ni pale alipochukua form ya kugombea uspika na akina msekwa na sitta akiwa mwaka wa tatu.
Sahihisho mkuu, 2002 - 2006 kwa Msekwa na Sitta kusema walikuwa UDSM naona kama ni typing error vile. Weka vizuri hapo.
 
usahihi ni kwamba, Mnyeti aligombea uspika wa bunge la jamhuri yeye mnyeti akiwa mwaka wa tatu chuo. si kwamba wote walikuwa chuo na wakagomea uspika wa bunge la wanafunzi.
 
Jakaya anataka kupandikiza mamluki hapo TUCTA ili awe boya lake na wafanyakazi wasiwe na sauti ya kupigania hakizao; watakuwa wajinga sana wakimtosa Mgaya wakati huu!! Ajenda iko pale pale lazima kumtoa Nicholas na kumuingiza Mussa, mnaiona hiyo wanajanvi halafu jamaa anahubili kupiga vita udini wakati yeye kwa vitendo vyake ndio muasis i wa huo udini!
Una USHAHIDI NA ULICHO ANDIKA? TUWEKEE WAZI,USIPOTOSHE WENGI!
 
Back
Top Bottom