JK acha kuwaendekeza hawa madaktari wanaogoma

Great Thinkers & Sinkers,

Mimi naomba kuuliza tu! Hivi nyinyi mnaoshabikia madaktari kugoma kwa maana nyingine mnaunga mkono watanzania kufa bila kupata huduma za afya. Hizi siasa za namna hii zitawapeleka wapi?

Hivi kweli hapa watu wanadiliki kujiita 'Great Thinkers' kwa majadiliano hoja na matusi yanayotolewa humu.

Mtu akiwashinda kwa hoja mnasema katumwa huyu, oh mdini huyo, or CCM huyo hoo huyo %^$8^%£CHADEMA%£$£, Tuaache siasa za kipumbavu na kujadili vitu vya msingi. Watanzania wanakufa period! Au mnataka mpaka yawapate ndugu zenu wa karibu ndipo mtaoona umuhimu wa mgomo wa madaktari?

Kwa kushabikia mgomo wa madaktari mnashangilia kufa kwa watanzania! I don't see the logic here.

Swali langu kwenu Je ikitokea kuwa madaktari wanaendelea kugoma, na kila mtanzania atakayepoteza ndugu yake kwa kukosa huduma wakaamua kuangalia mambo yao binafsi, wakitoka tu kuzika ndugu yao wanatafuta daktari na kulipiza kisasi, je watakuwa wamekosea? kwani madaktari wanaishi miongoni mwetu. Hii haitakuwa njia sahihi hata kidogo na mungu apishe mbali isije kufika hapo tutumie hekima tuokoe maisha ya wantanzani. kwani Hatuna nchi nyingine nchi yetu nii tu, na pakiisha haribika usijidanganye kwamba utaenda uhamishoni. uhamishoni au ukimbizini siyo nyumbani.

Rudini kazini.
Sun Tzu mkuu wewe unaishi wapi wewe hamna anayeshabikia huu mgomo humu jf tuna tumia falsafa hii IF U CANT CONVINCE CONFUSE THATS ALL je kama serikali yako ingekuwa inajali afya za wanachi wake mpaka leo ungejirudia?

Wacha tu watu wafe sio wao wakwanza au wa mwisho kufa wote tutakufa nikutangulia tu ila wewe umeona watu wangapi wanapata ajali wanakufa kwakukosa huduma za haraka, kweli hospitali ya mhmbili CTSCAN haifanyi kazi?hospitali ambayo inaaminia tena ya taifa ya rufaa wewe unajua wagonja wangapi wamekufa sababu uchunguzi wa kina kutumia hichi kifaa umekosekana?

Usitetee hata madactari kuwepi haisaidii je unajua kwanini dr ulimboka kapelekwa nje sbbu kimekosekana kifaa chakuchunguza sumu iliyoonekana kwenye damu je ni watu wangapi wenye same problem na je wanaweza kwenda nje ya nchi usishabikie tuu nakulaani fungua ubongo wako ndugu.

Hhivi unajua kwenye mabango ya serkali wameandika huduma za mama na watoto bure fuatilia ujue kweli kama ni bure mjamzito usipkwenda na vifaa vyote mpaka bomba la sindano, gloves oxtocin husaidiwi, kweli hii ni serikali unajinunulia mpaka panadol unajifungua kwa shida unapelekwa wodini hamna kitanda unalala chini.

wakati wengine wanapitapita nandala zao mtotot ni mdogo hajaweza kucop mazingira ndugu yangu sun sijui unaishi wapi, ukiendelea kutuandikia ujinga watakutukana tu maana wanayaona hayo madactari wanaweza ila serikali imetupilia mbali afya za wananchi, lakini budget ya chai ya ikulu bil15 za hizihizi kodi zetu,naona ni bira kila atakayekufa kwa mgomo apelekwe pale ikulu.sinkers ni wewe mwenyewe.
 
Hivi serikali gani itaendelea kuwakubalia kila kitu hawa wahuni? kama hawataki kazi kwa nini wasijiuzulu kisha wakatafute kazi zingine. wananchi wanakufa kwa sababu dakatari ambaye serikali imemsomesha kwa gharama kede kede anataka alipwe milioni 4 kwa mwezi pesa ambayo serikali haina.

hawa jamaa ni wahuni na nadhani bora wakawa treated as such

Nomba sana serikali iwafukuze kazi hawa jamaa ili tuendelee mbele.

ndio sasa njooni mnitukane lakini nishatoa maoni yangu JF style...

Serikali ikikubali kua ni wahuni ina maana yenyewe ndio imewalea kufikia huko.

Lkn ni jambo zuri serikali ikabadiri mfumo mzima wa huduma za afya nchini ambapo serikali haitahusika na kuajiri madaktari.
 
Back
Top Bottom