JK aalika warembo wa Miss East Africa Ikulu

sijui lini atawaalika wasiojiweza wale viwete wa kule posta na ombaomba wote.kweli mambo ya urembo yameiteka TANZANIA kila kona miss kata ,miss tarafa sijui hadi kwa watoto sijui umiss

Kwani lazima rais aalike watu Ikulu ndiyo aonekane mzuri? Kama suala la kualika watu ni muhimu sana kwa Taifa basi awaagize mawaziri wafanye kazi hiyo pia kama sehemu ya kazi zao za kila siku. Huyu bwana anajichosha kwa kufanya kazi nyingi sana (ambazo si zake) lakini zenye tija kidogo au zisizo na tija kabisa. Na laiti angefanya hayo nchi ikiwa inakwenda vizuri. Ni sawa na dreva anayetelekeza gari lililokwama kwenye matope mazito na kwenda kunywa kahawa akibembelezwa na toto toka Makorora au Kwa Minchi - Tanga. It doesn't make any sense kwani hajamaliza hata kuandaa majibu ya akina Quares, Nkangaa, Butiku na wanzao.
 
Natamani sisi WASANII wachoraji tungealikwa kwa IKULU tukale vinono na tumnog'oneze muungwana nini tutaifanyia nchi yetu wakituwezesha.
 
Jamani kwa nchi ku host mashindano kama hayo ina manufaa kweli though hamuwezi kuyaona lakini kwa walio kwenye sector ya utalii ni rahisi saana kuona, kwakupitia hayo mashindano nchi inajulikana, ili kufanikisha hayo lazima kuwe na political support, alichokifanya JK sio kibaya hata kidogo la wala hakuwa na nia mbaya alifayanya kwa niaba ya watz wote

kwakutokwenda same mpaka leo kwahapo,,, binafsi naona sio vizuri kama kumbukumbu zangu ziko sahihi baada ya maafa ya same kuna kijiji kimoja Bagamoyo yalitokea mafuriko lakini hakuna mtu aliyekufa nadhani kesho yake JK aliwatembelea,,, kinachonishangaza ni kwanini hakwenda SAME pia??atakuwa na sababu lakini naamini alikuwa na uwezo wa kuwatembelea na kuwapa pole kama rais wao bila kuonyesha upendeleo wa wazi wazi


Hakuna manufaa yeyote kwa rais kuwaona. Maonyesho kama yameandaliwa vizuri then yatasaidia kuitangaza nchi. Kazi ya kue wahost ingefanya may be na Waziri (if imporatant) kama siyo bodi ya utalii kama kweli tunafikiri haya maonyesho yana faida kwa taifa. Lakini nionavyo mimi bodi ya utalii na wizara ya utalii hawana habari nayo ilipokuwa mkuu wa kaya ambaye kila mwaka lazima akutane na warembo. Tusubiri tuone kama ataialika timu ya mpira ya Ivory coast itakapopiga kambi bongo. Nafikiri hiyo itatutangaza kuliko hao ma-Miss.
 
kusema kweli rais wetu anashindana na Tiger Woods! na anamkaribia Belllusconi linapokuja suala la vimwana! Nani asiyekumbuka jinsi alivyokuwa "Never Miss" pale RELWE GEREZANI kwenye Netiboli ya NJE CUP!
Hiki ndio kidume bwana! Mwanaglie kwenye picha anavyotokwa udenda1
 
Hata Zuma aliwaalika warembo Ikulu na akawahutubia. Hakuna aliyehoji! Iweje Kikwete tuhoji? Tuwe straight forward, ama tumshauri kwamba tunapenda next time aalike watakaofanya vizuri kwenye hesabu nk or tunyamaze kimya kuliko kukosoa bila kutoa mbadala/suluhu ya hilo tunaloona ni tatizo.
 
Hata Zuma aliwaalika warembo Ikulu na akawahutubia. Hakuna aliyehoji! Iweje Kikwete tuhoji? Tuwe straight forward, ama tumshauri kwamba tunapenda next time aalike watakaofanya vizuri kwenye hesabu nk or tunyamaze kimya kuliko kukosoa bila kutoa mbadala/suluhu ya hilo tunaloona ni tatizo.

Tunahoji kwa kikwete kwa sababu ni rais wetu!!! Kwa nini tuhoji kwa zuma?? kwani zuma ndo rais wa TZ?? wasauzi juu yao kama hawahoji.
 
Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana (mmhmmhmmh)
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo Ni heri mama wewe
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

NO FURTHER COMMENTS ON THIS THREAD!!!
 
Nionavyo mimi Rais anaweza kualika watu wa aina mbalimbali Ikulu kwa sababu fulani. Nilicha na wasiwasi nacho ni frequency of visitations to the State House or his visits which I may call are not all that strategic. Mfano, kulikuwa na umuhimu gani kumchosha Rais kupokea Ambulance 2? tena sio ambulance 10, potelea mbali thamani yake. Kwa nini wasimpelekee hata angalau Waziri wa Afya basi? jamani wanamtia aibu Rais hata hao washauri wake. Ambulance 2? Shame!!!!
Rais anaweza kwenda kufanya ufunguzi wa vitu petty petty yani havina hata hadhi ya kufunguliwa na Rais. Pamoja na kuwa yeye anaridhia lakini washauri wake ndio wa kulaumiwa. Mwacheni afanye vitu more startegic jamani au apumzike.
 
Back
Top Bottom