Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Umekisoma? Kwani historia ni nini? Zifuatazo ndizo sura zake - Je, sio Historia hiyo au Propaganda sio Historia au sehemu ya Historia?

Chapter 3: Subjects and Citizens
Chapter 4: Personality and the Conception of the Völkisch State
Chapter 5: Philosophy and Organisation
Chapter 6: The Struggle of the Early Period – the Significance of the Spoken Word
Chapter 7: The Struggle with the Red Front
Chapter 8: The Strong Man Is Mightiest Alone
Chapter 9: Basic Ideas Regarding the Meaning and Organization of the Sturmabteilung
Chapter 10: Federalism as a Mask
Chapter 11: Propaganda and Organization
Chapter 12: The Trade-Union Question
Chapter 13: German Alliance Policy After the War
Chapter 14: Eastern Orientation or Eastern Policy
Chapter 15: The Right of Emergency Defense

Source: http://en.wikipedia.org/wiki/Mein_Kampf

- Nimekisoma sana mkuu tena kwa kufundishwa na mama mmoja m-Jew aliyepona pona kwenye mauaji ya Hitler, historia haiandikwi na watawala that is my point.

Respect.


FMEs!
 
mengi yameandikwa kwa sifa na kebehi lakini ukweli utabakia kwamba mwalimu katuachia mtihani mkubwa sana. Huu mtihani upo ndani ya maelezo yake na yale aloyafanya kwani katika kumsoma vizuri mwalimu tukubaliane kwamba mwalimu Nyerere hakuwa mtu mwenye maamuzi mazuri ktk MIRATHI..iwe familia yake ama Kitaifa kwani kosa kubwa la mwalimu pamoja na upendo wake kwa nchi yetu na wananchi wake ni ktk kukabidhi madaraka ya Uongozi.
Hivyo kuwadharau watu wengine na kuwaita wahuni hali chaguo lako ndilo linaonyesha uhuni zaidi nadhani bila shaka mwalimu alikuwa mhuni pia. Mimi siku zote nitalia na mwalimu ktk kuomboleza kwani ndiye aliyekabidhi madaraka ya nchi yetu kwa WAHUNI tunaowajua sisi. He meaned good hilo halina Ubishi lakini maadam tunakwenda chini, hayo namwachia Mungu..
Kawaita hao kina Malecela wahuni, Lowassa, Sitta na wengineo wengi tu kama wahuni, lakini alishindwa kuuona Uhuni wa wanae mwenyewe hao kina Mwinyi na Mkapa na kundi zima la mawaziri waliofuata walikuwa wahuni kupita kipimo chochote cha uhuni, hasa walipopata barehe ya uchaguzi wa mwaka 2000.
Hivyo sisi wananchi tumewaona wahuni wote ktk makundi tofauti na nadhani sisi wananchi ndio tyunaotakiwa kuandika vitabu kama hivi.
Na kama alivyosema FMES, ni kutokana na maamuzi yake ndio maana tupo hapa leo hii. Tanzania imekuwa nchi ya USANII, iuliyojaa madalali wauza nchi kama nyumba za Kariakoo. nchi yetu inanadiwa kama nyumba za Kariakoo na kama mtakumbuka niliwahi sema kila mageuzi ndani ya Kariakoo, hu refrect mikakati ya nchi nzima kiutawala. hapa ndipo tuliposimama leo hii ya kesho anayajua Mungu.

Binafsi nimechoka na hizi hadithi za Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na sijui JK...kwani nguvu ya taifa letu ni sisi wananchi wenyewe.. tulikubali hali hizo wakati ule na tunaendelea kukubali imani potovu ya kuabudu viongozi wetu kiasi kwamba wao wamefikia kuwa kama MIUNGU wetu..Haswa viongozi wanaelewa fika kwamba sisi wananchi tunawaogopa na sii kuwaheshimu, sisi ni watumwa ndani ya Uhuru kiasi kwamba hakuna tofauti ya kimaisha baina ya kuwa uhuru ama kutawaliwa kwa sababu ukiitazama tanzania kiuchumi ipo kwa maslahi ya watu wachache tu..Hivyo watawala wetu - iwe wazungu, waarabu ama waafrika weusi, haiwezi kuondoa maana halisi ya Utumwa wa mwananchi.
Hatma ya Tanzania haiwezi kutazamwa kwa kufuata hulka na tabia za viongozi kwa sababu Tanzania imejaa wasanii, wacheza sinema ambao wanasubiri tu role watakayo pangiwa kucheza..Ni muhimu sana kwa wananchi kuanza kujipanga Upya, kutazama watu na mazingira kulingana na wakati. Ya mwalimu yameisha pita, aloandika sii elimu bali matukio na fikra zake yeye..Na sii lazima iwe ndio ukweli wenyewe kwani tumeyaona kwa macho yetu wenyewe wahuni ni kina nani - Hao aloiwapa uonfozi wa nchi yetu ndio wahuni wa kweli!

- Bob vipi ndugu yangu umerudi maana nimekutwangia sana, maneno mazito sana haya.

Respect.


FMEs!
 
Nipo, nipo Boingo mkuu wangu nachukua Phd ya Udalali! maanake nimeisha pigwa changa la macho natafuta nauli hivi! bwaaa bwaa bwaaa!
 
..hii ni mara ya pili kukisoma kitabu cha Mwalimu Nyerere.

..nadhani kilichotokea kwa Mzee Malecela ni kosa la kiufundi tu, au tactical error, ktk kuhakikisha hoja ya Tanganyika inashindwa.

..Mwalimu angekuwa wa msaada mkubwa zaidi kama angekwenda kwenye chanzo cha matatizo ya huu Muungano wetu.

NB:

..kwa upande wangu nadhani wabunge 55 walikuwa wamekerwa na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikiendekezwa na utawala wa Raisi Mwinyi. rushwa na hujuma zile wakati mwingine zilionekana kama ni za Wazanzibari dhidi ya Tanganyika.

..baada ya hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, kulifuatia hoja nyingine binafsi ya Jenerali Ulimwengu, na Patrick Qorro na zote zilikuwa zimejielekeza ktk masuala ya rushwa na kukosekana kwa maadili ktk utawala wa Raisi Mwinyi.

- Mkuu umeshawahi kujiuliza kwa nini hawa wabunge wa G55 hawakushikwa na uhaini, maana that is exactly walichokuwa wanakifanya, na kwa nini Kaseka kiongozi wa hili kundi alipewa uwaziri baada ya hizi vurugu?

Respect.


FMEs!
 
- Nimekisoma sana mkuu tena kwa kufundishwa na mama mmoja m-Jew aliyepona pona kwenye mauaji ya Hitler, historia haiandikwi na watawala that is my point.

Respect.

FMEs!

Mkuu kama historia haiandikwi na watawala inaandikwa na nani? Wanahistoria wanasema historia huandikwa na washindi. Ndio maana historia ya Tanganyika kwa kiasi kikubwa imeandikwa na Wajerumani na Waingereza. Mpaka leo kitabu kikuu cha historia hapa nchini kinaitwa A MODERN HISTORY OF TANGANYIKA na kimeandikwa na Muingereza kwa jina John Iliffe.
 
Mkuu kama historia haiandikwi na watawala inaandikwa na nani? Wanahistoria wanasema historia huandikwa na washindi. Ndio maana historia ya Tanganyika kwa kiasi kikubwa imeandikwa na Wajerumani na Waingereza. Mpaka leo kitabu kikuu cha historia hapa nchini kinaitwa A MODERN HISTORY OF TANGANYIKA na kimeandikwa na Muingereza kwa jina John Iliffe.

- Ikiandikwa na watawala ndio matokeo yanakuwa kama hiki kitabu.

FMEs!
 
FMES halafu kumbuka Hitler hakuwa mtawala wakati anakiandika na tena hicho kitabu kwa kiasi kikubwa ndicho kilichomuuza wa Wajerumani mpaka wakamkubali - hebu soma rejea hii:

Hitler began the dictation of the book while imprisoned for what he considered to be "political crimes" after [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Beer_Hall_Putsch"]his failed revolution in Munich[/ame] in November 1923. Though Hitler received many visitors earlier on, he soon devoted himself entirely to the book. As he continued, Hitler realized that it would have to be a two-volume work, with the first volume scheduled for release in early 1925. The prison governor of Landsberg noted at the time that "he [Hitler] hopes the book will run into many editions, thus enabling him to fulfill his financial obligations and to defray the expenses incurred at the time of his trial."

Source: [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Mein_Kampf[/ame]
 
Companero,
Alichofanya Nyerere kinaweza kutafsirika vyovyote vile.. Sidhani kama ni busara kwako wewe kuandika historia ya maisha yako mwenyewe..kwa mfano ktk historia hiyo kama uliachana na mkeo mara nyingi mbaya atakuwa mkeo kumbe kulingana na watu wengine wanavyoiiona picha wanajua fika mkorofi ni wewe.
Kifupi historia ya nchi yetu inajiandika yenyewe hadi leo hii nachokiona ni MIMBA tu...
 
Historia lazima ihifadhiwe kwa maneno au maandishi. Tatizo letu ni kuwa historia yetu hatuihifadhi ipasavyo. Ndio maana tupo hapa tunagombania Kitabu cha Nyerere kama pipi. Hizi ni historia ambazo zinapaswa kuwa wazi kwa kila Mwananchi. Tunapaswa kuwa na kumbukumbu ya kitaifa kuhusu haya masuala. La sivyo mafisadi wa jana leo tutawaita wapiganaji! Afadhali sasa tunaanza kuamka, Azimio la Arusha nalo linachapishwa upya kwa Kiingereza na Kiswahili. Tukikumbuka tulipotoka hatuwezi kuacha huu upuuzi wa sasa uendelee! Tuhifadhi kumbukumbu za nchi hii, tumetoka mbali!
 
FMES,

..unless kuna kitu ambacho sikifahamu, lakini kwa uelewa wangu Wabunge wale walikuwa wanatumia haki yao ya kikatiba ndani ya Bunge la Jamhuri.

..kuhusu Njelu Kasaka kupewa Unaibu Waziri labda ilikuwa ni njia ya kumnyamazisha. wengine kama Sebastian Rukiza Kinyondo[r.i.p] alipewa wadhifa wa ukuu wa mkoa.

..nimeelekeza kwamba hawa G-55 walikuwa wamekerwa zaidi ya rushwa iliyokuwa inafanywa na Mwinyi na kundi lake. kwenye hoja yao walikuwa mpaka na malalamiko kwamba wa-Zenj wanateuliwa kushika nafasi zisizo za muungano. kuwapa G-55 madaraka ilikuwa ni njia ya kuwaingiza ktk kundi la wenye ulaji.

NB:

..binafsi ningependa sana kusoma hoja ya Tanganyika kama ilivyowasilishwa na Njelu Kasaka, na zaidi kupata hansard na kumbukumbu za mjadala huo bungeni.
 
Jamani, PM Malecela alikuwa nacheza strategy nzuri sana ya "" no blood in my hands"" na kwa kweli angeshinda kama sio Mwalimu kuona mchezo mzima.

Huwezi kushindwa kuitetea Serikali bungeni ukabaki PM, no way.
Huwezi kwenda kinyume na CCM, halafu bado ubaki kiongozi wa serikali ya CCM.

So JKN was right.

Mabavu ya kumleta Mkapa hiyo ni topic nyingine, na vile vile kutuletea Mwinyi wakati alikuwa hana uwezo hiyo nayo ni topic nyingine.
 
BBC wana tabia sana ya kufanya watu wanaowasikiliza na kuwasoma kuhisi kila wanachosema kuhusu Afrika na Zimbabwe ni kweli. Kuna mdau alienda Zimbabwe akashangaa kuikuta sivyo vile alivyokuwa anahisi kutokana na BBC. Alituma picha hizi:

http://udadisi.blogspot.com/2009/02/pamoja-na-vikwazo-air-zimbabwe-inatoa.html

http://udadisi.blogspot.com/2009/02/propaganda-balaa-eti-magari-yote-hamna.html

Lakini si ilitosha kumwambia kwa uzuri mzee wa watu Mtei kuliko kumwambia anahisia za Ki-BBC?
 
Lakini si ilitosha kumwambia kwa uzuri mzee wa watu Mtei kuliko kumwambia anahisia za Ki-BBC?

Kweli mkuu. Ni jazba tu maana kila kona nakutana na hizi hisia. Sasa huwa inaniuma napokutana nazo kwa wazee wetu ambao wanapaswa kutuonesha njia vijana tunaopumbazwa na vyombo vya habari. Nahisi hii iliniuma zaidi maana ndio kwanza nimetoka kukisoma kitabu cha Mzee wetu. Samahani kwa kuumiza hisia zenu.
 
FMES, ..unless kuna kitu ambacho sikifahamu, lakini kwa uelewa wangu Wabunge wale walikuwa wanatumia haki yao ya kikatiba ndani ya Bunge la Jamhuri.

Ndugu yangu nadhani unasahau kuwa Katiba ya wakati ule bado ilikuwa na 'schedule' ya 'party supremacy', yaani Katiba ya CCM ilikuwa imeingizwa ndani ya Katiba ya Nchi hivyo kwa kiasi kikubwa Chama kilikuwa juu ya Dola na Mihimili yake ndio maana Mwalimu Nyerere aliwawakia hao Wabunge waliokuwa wanapingana na Sera na Ilani ya Chama chao!

Nashauri kitabu cha Tanzania! Tanzania! cha Mwalimu nacho kiwekwe humu maana kinaelezea hoja hiyo ya Chama kushika hatamu dhidi ya G55. Kuna sehemu kinasema hivi:

"Ziko jitihada sasa hivi za kugombanisha Wabunge na chama chao kwa kutumia hadhi ya bunge...Mimi nasema kuwa ["Wabunge"] wanayo haki hiyo ["ya kuhoji Katiba, ambayo si maoni bali ndiyo sheria kuu ya nchi yetu"] na uhalali huo. Lakini wanajivua haki hiyo kwa kutumia hoja za kijinga. Ati Bunge likishatamka maoni yake, hata kama maoni hayo hayana uzito wa sheria, vyama vyote, pamoja na chama kinachotawala, lazima viyaheshimu maoni hayo au sheria hiyo, na vifute sera zao, hata kama uamuzi wa Bunge au Wabunge ni kinyume na sera zao. Na hata kama Wabunge hawakutumwa na wapiga kura kupitisha sheria hiyo. Hivi ninyi mnafikiri udikteta unaanzaje?"

Nadhani wanasheria wanaweza kulieleza hili suala la nguvu ya kikatiba ya chama kimoja vizuri. Ukipata muda pitia makala hii ya mwanasheria mahiri: http://www.kituochakatiba.co.ug/Maina99.htm. Au soma vitabu vya Msekwa maana alisifia sana kitendo cha kuipa nguvu ya kikatiba dhana ya chama kimoja kushika hatamu kuwa ni kitendo cha aina yake katika historia ya utungaji/uundaji Katiba duniani!
 
mkuu, nimekisoma kwa haraka sana,
lakini mbona kina Typo nyingi sana? ndo chenyewe au draft?
 
Back
Top Bottom