Jipatie nakala ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5 wa Kikwete

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Jamani, nasikia unasifiwa, unauzwa kuwa ni bora kuliko mipango mingine ya huko nyuma n.k Na kwamba ni mpango ambao tukiutekeleza utatupeleka kuwa taifa la kipato cha kati ndani ya muda mfupi tu. Najua uko katika print format, je kuna mtu ambaye anao katika digital format ili na sisi wengine tuangaze macho na kuukosoa? Naomba mnitumie (aliyenao) kwenye email ya hapa chini. Thanks.
 
Attachments

  • FiveYearPlanTZJune2011.pdf
    974.2 KB · Views: 411
Mtafute Dr Mipango kama unamawasiliano naye.Mpango bado unamapungufu kadhaa..Ila wanadai wanapokea maoni kwaajili ya kuuboresha.
 
Hakuna utekelezaji ndio maana hata hotuba ya waziri haijasema kuwa ametenga nini kwa ajili ya utekelezaji .
 
hapa kuan didli la kutaka kupiga pesa za wananchi, ccm(mabepari) kila kitu ni dili
 
Nchi zingekua zinaendelea kwa kupiga mdomo tu basi Tanzania tungekua tushapiga hatua kubwa zamani. Tatizo Tanzania kuongea kwingi lakini kutekeleza sifuri. Ahadi karibia zote za 2005 hazija kamilishwa, bado kuna zile za 2010. Hivi kweli tuna tegemea chochote kipya?
 
Unatofauti na mipango kama ile ya MKUKUTA, MKURABITA. au ni mueldelezo kinachobadilika ni lugha tu

Nijuavyo mimi hakuna mpango amabo kwenye makaratasi unaweza kuwa mbaya. tatizo siku zote ni utekelezaji
 
Aksante sana mkuu hii nitasoama soma week end vipengele vichache.

But kwa haraka haraka nimenagalia content sijaona neno Education. Vile vile binafsi ningeona serikali ina mpango wa mambo Housing kwa wnanchi wa vijijini na mijini.

Hatuwezi kuendelea kutegema watu binafsi wajenge nyumba na kuwa na mipango miji kwa nyumba za mishahara ya TGS. otherwise miji yetu itaendela kuwa vituko na ya wachache wenye makazi bora.

Ngoja nisome some vipengele vichache this weekdn hope nitakuwa na kitu cha kusifia nikirudi kuchangia.
 
Jamani, nasikia unasifiwa, unauzwa kuwa ni bora kuliko mipango mingine ya huko nyuma n.k Na kwamba ni mpango ambao tukiutekeleza utatupeleka kuwa taifa la kipato cha kati ndani ya muda mfupi tu. Najua uko katika print format, je kuna mtu ambaye anao katika digital format ili na sisi wengine tuangaze macho na kuukosoa? Naomba mnitumie (aliyenao) kwenye email ya hapa chini. Thanks.

Mwanakijiji nilidhani umepevuka kimawazo,kumbe you can still be swayed by cheap propaganda.Huu mpango wa miaka mitano wa serikali ya Kikwete is nothing but just another attempt ya kuwadanganya Watanzania.He is trying to show that anatujali, lakini ukweli ni kwamba anatengeneza njia kwa ajili ya mtu anayempenda 2015.Afterall hata kama mpango huo ungekuwa mzuri vipi,watu hawa hawana nia ya kweli ya kuwasaidia Watanzania.
 
Ndugu wananchi, msiwe na wasiwasi kabisa na mpango, huu wa miaka mitano, kwa hivi sasa ndio tuka katika maandalizi ya utekelezaji, hata ikifika 2015, hamjaona kitu, endeleeni kuvuta subira tuu, ila ili ufanikiwe kwa asilimia 100%, ni lazima 2015, mtupatie tena ridhaa ili tuendelee kuwapatia mipango hii mizuri mizuri ya maendeleo. Si mliuona MKUKUTA, ukaja MKURABITA hatimaye MKUMBITA, na sasa ndio mpango huu ambao hatujaupatia jina kamili.
 
Mtafute Dr Mipango kama unamawasiliano naye.Mpango bado unamapungufu kadhaa..Ila wanadai wanapokea maoni kwaajili ya kuuboresha.

Wanapokea maoni wakati Rais keshauzinduwa? what are they talking about?
 
Mwanakijiji nilidhani umepevuka kimawazo,kumbe you can still be swayed by cheap propaganda.Huu mpango wa miaka mitano wa serikali ya Kikwete is nothing but just another attempt ya kuwadanganya Watanzania.He is trying to show that anatujali, lakini ukweli ni kwamba anatengeneza njia kwa ajili ya mtu anayempenda 2015.Afterall hata kama mpango huo ungekuwa mzuri vipi,watu hawa hawana nia ya kweli ya kuwasaidia Watanzania.

Hakuna mtu mwenye matatizo kama ambaye amefumba macho yake hataki kuangalia au kutafuta ukweli. Wanasema "closed minded person". Ni vizuri kusoma na kupitia huu mpango mzima na kuupima on merit. Ndio tofauti ya kuwa msomi na kuwa msomaji.
 
Back
Top Bottom