Jinsi ya kumwita jini na kumuamrisha unavyotaka awe rafiki, mpenzi au msaidizi

JINSI YA KUMWITA JINN NA KUMUAMRISHA UNAVYOTAKA

Jinn ni kiumbe kama ulivyo wewe ameumbwa na anaishi na anakufa pia.Wanasaidiana na binadam kwenye mambo mengi na shughuli kadha wa kadha ila kwa leo sipo hapa kueleza jinsi ya kuumbwa kwao na vile wanavyoishi au vitu wanavyokula na maisha yao kwa ujumla kwa sababu imeshaalezwa mara nyingi tu hapa Jamiiforums maisha yao kiuhalisia ukitaka kufaham hivyo vitu waweza kutafuta THREADS nyingi tu ambazo zimewazungumzia hawa viumbe lakini hapa tutaelezana jinsi gani ya kuweza kumwita JINN na kumuamrisha utakavyo ikiwemo methods au formula za kutumia kwa mana hata ukimuhitaji binadam hawezi kuja tu mpaka umwite na hata kitu chochote kina taratibu zake pia ila cha ajabu binadam wengi wanawaogopa hawa viumbe lakini kiukweli wao ndio wanatuogopa sana sisi ila tu pale utakapomuonyesha kuwa UNAMUOGOPA utampa mwanya kwa sababu umemuonyesha wazi kuwa unamuogopa na hii ni kiumbe yoyote yule hata mbwa ukionyesha unamuogopa utaona matokeo yake,soma hapa JE WEE NI MUOGA sasa bila ya kupoteza muda hebu tujifunze...

JINSI YA KUMWITA JINN NA KUMUAMRISHA UTAKAVYO

HATUA YA AWALI

ANDAA VITU VIFUATAVYO ;-
I.] Mishumaa 3 MWEUPE,MWEKUNDU,MWEUSI.
II.]Bakuli Nyeupe ya Udongo (any size).
III.]Kioo cha kujitazamia.
IV.]Kiberiti cha njiti kipya.
V.]Pete aina yoyote.


MISHUMAA.
Mshumaa mweupe na mweusi inawakilisha UWEZOHURU NA TABIA YA JINN aidha ni muovu au ni mwema na pia huwakilisha ULIMWENGU wetu wa kibinadam na ULIMWENGU wao wa kijini.Na mshumaa wa tatu ambao ni MWEKUNDU humuwakilisha JINN

BAKULI JEUPE LA UDONGO.
Bakuli hili utalitumia kuweka zawadi yake pale atakapokuja liwe bakuli la udongo lisilo na maandishi wala michoro au marangi rangi.

KIOO CHA KUJITAZAMIA.
Kioo kinatakiwa kiwe kikubwa kiasi mfano wa karatasi ya A4 au zaidi kioo hiki kinatumika kuwakilisha ULIMWENGU MBILI wao na wetu hivyo kioo hutumika kuakisi ULIMWENGU WETU na ULIMWENGU WA KIJINI hivyo kinatakiwa kiwe kikubwa kiasi.

KIBERITI CHA NJITI SIO GAS LIGHTER.
Kiberiti kinatakiwa kiwe kipya kabisa hakijatumika hata kidogo hivyo ni bora ukanunua kiberiti dukani maalum kwa ajili ya kuwashia mishumaa yako.

PETE YA AINA YOYOTE ILE.
Pete inayoshauriwa kutumika hapa ni vizuri kama utapata pete ambayo inakuhusu nikiwa na maana uwe umeshaivaa angalau hii inapendeza zaidi kwa mana itatumika kuingiza uhusiano kati yako na JINN atakayekuja kwa sababu ataingia kwenye hiyo Pete kwa kuwa Pete hiyo inahusiana na wewe basi uhusiano wenu utajengwa kuanzia kwenye Pete hiyo.


HAKIKISHA UKO MSAFI
Hakikisha uko safi umeoga ila usitumie sabuni yenye harufu wala shampoo kama tulivyosema mwanzo kuwa harufu nyingine hawapendezewi nazo zinawarudisha tumia maji ya kawaida tu inatosha.

ANDAA ENEO LAKO VIZURI
Hakikisha umeshaandaa eneo lako kama ilivyoelekezwa hapo juu ukishaona lipo sawa.Vaa mavazi ya kawaida zingatia usivae mavazi yanayobana mwili wako uwe comfortable na mahali utakapotumia pawe kimya kabisa bila ya kelele au bughudha yoyote chomoa radio au television pia zima na hata mwangaza wa taa unashauriwa kuizima haihitajiki chumba kiwe na giza kabisa HAPANA kisiwe giza ila yahitajika kiwe na mwangaza wa asili tu unaotokana na jua.Hii ni ukweli kwamba viumbe hawa huogopa au hawapendi hivi vitu vya umeme ikiwemo Taa,Radio na hata TV kwa hiyo havina ulazima wa kuviwasha.


NINI CHA KUFANYA

-Kaa sehemu uliyoiandaa kwa ajili ya kufanyia zoezi lako miguu yako ikiwa umeikunja kwa mtindo wa X sio ukalie miguu halaf makalio yawe juu ya miguu hapana inatakiwa uikunje miguu ikiwa X na ukalie makalio kama wakaavyo wafanya meditation (cross legged).

-Weka kiberiti chako karibu na chukua kioo chako kiweke mbele yako kikutazame pamoja na mishumaa yako mitatu iweke kwa mpangilio kutoka kushoto kwenda kulia anza na MWEUPE,MWEKUNDU,MWEUSI ukitoka ulipokaa ifate mishumaa halaf kioo kiwe mbele kidogo hivyo mishumaa iwe inaonekana kwenye kioo.

-Bakuli ndio kitu kinachofuata hakikisha unaliweka katikati ya mshumaa mwekundu yani bakuli liwe mbele ya mshumaa mwekundu hivyo bakuli lako litakuwa katikati ya mishumaa na kioo kwa hiyo vyote viwe vinaonekana kwenye kioo.

-Pete au Saa hutumika kumnasa JINN utakayemuita na kumuamrisha na ataingia ndani ya Pete au Saa na inashauriwa sana sana hiyo Pete au Saa viwe vinahusiana sana na wewe yani uwe unaivaa au umeivaa japo mara kadhaa ili kuleta uhusiano wa karibu zaidi baina yako na JINN kupitia Pete hiyo kwa vile inahusiana na wewe.

Baada ya hapo unatakiwa kujiweka kweli hali ya ku-relax na kuwa huru kisha tazama kioo chako na ukiangalie wakati unaendelea kukiangalia unatakiwa kuvuta pumzi ndani,vuta kabisa pumzi kubwa na ya kutosha kabisa kisha ibane mpaka pale utakapoona mwenyewe kuwa unahitaji kuiachia basi iachie ila usiiachie kwa mara moja au kwa ghafla unatakiwa kuiachia taratiiiibu mpaka yote iishe,rudia tena kuvuta pumzi kwa jinsi hiyo mpaka uhakikishe kuwa umevuta mara 20 zote zikiwa ni pumzi ndefu kabisa (deep breaths).

BAADA YA MAANDALIZI HAYO,SASA ANZA

Hayo juu yalikuwa ni maandalizi,kujiweka sawa na kujitayarisha sasa waweza kuanza kwa kuchukua kiberiti chako na kuwasha mishumaa yako kwa kutumia NJITI MOJA TU na isizidi hiyo hivyo hakikisha umezima feni na sehem iliyopo imetulia na hakuna upepo,tumia NJITI MOJA kwa kuwasha kwanza mshumaa MWEUPE kisha MWEUSI halaf ipulize njiti yako kwa upepo wa taratiiibu tu mpaka izimike na uiweke pembeni.

Sasa ikiwa kama alama ya KITUKUFU ya kukutanisha na kuchanganya ZURI NA BAYA NA BAYA NA ZURI ili kuweka uwiano na usawa kati ya vyote viwili ili kutengeneza UWEZOHURU chukua mshumaa MWEUPE kwa mkono wako wa KUSHOTO na mshumaa MWEUSI kwa mkono wako wa KULIA yote kwa pamoja ili uwashe MSHUMAA MWEKUNDU hakikisha unagusanisha moto wa huku na huku kuwasha mshumaa wa katikati ambao ni MWEKUNDU .

Baada ya kuwasha mshumaa mwekundu rudisha mishumaa yako sehemu ilipokuwa mwanzo,ikiwa tayari yote inawaka sasa rudia kuisoma ile ARABIC PHRASE uliyoiandika ubavuni mwa mshumaa mwekundu kujikinga na shetani au JINN yoyote mbaya au muovu ili aje aliye mzuri na mwema tu,soma phrase hii mara 9 (NAMBA 9 NI NAMBA MUHIMU SANA,KATIKA DINI YOYOTE ILE JINN ANAYOFATA NI LAZMA KUWE NA UTATU MTAKATIFU,HIVYO 9 NI SAWA NA TATU YENYE UTATU NDANI YAKE AMBAYO NI SAWA UTATU MTAKATIFU) maneno unayotakiwa kuyasema mara 9 ni haya hapa tena "A'OO THU BILLAHI MIN ASH SHAITAN ARRAJIM" .

Mara tu utakapomaliza kusema maneno hayo yatawafanya MAJINI wasikie na watambue kuwa kuna kiumbe anawahitaji na anahitaji kuwasiliana nao na mara moja watakuwa tayari kuskiliza unachosema na KUTII kile utakachowaambia watakauwa tayari pia kukipokea bila ya kukipinga.

Hapo hapo utaanza kuskia hali tofauti kwenye mwili wako aidha utahisi kibaridi au kijoto kidogo au hali yoyote ambayo ni ya kawaida tu ikitokea hali hii USIOGOPE hiyo ni kawaida ni moja kati ya njia za MAJINI kukujulisha uwepo wao na kukujulisha kuwa tayari ameshafika hawezi kuja ukamuona LIVE hapana utahisi tu kuwa tayari dalili kuwa yupo chumbani.

Mwili wa binadam kwa kawaida una nishati ambayo JINN huipenda sana na nishati hiyo ni nywele na ndio mana unaweza hata ukachana nywele kwa shanuo la chuma na ukaona kama cheche hivi kwenye nywele au utaskia watu wakisema "NYWELE ZANGU ZIMESISIMKA" nywele zina nishati kwa kawaida sasa kwa kuwa JINN hupenda sana nishati hiyo hivyo basi HII ndio itakuwa zawadi ya kumpa,unywele mmoja.

Katika hali hiyo ya kuhisi uwepo wake tayari unatakiwa kumwambia maneno haya hapa "NAHITAJI KUZUNGUMZA NA WEWE KIFALME NDO MANA NIMEKWITA HAPA,NAKUZAWADIA NGUVU INAYOTOKANA NA MIMI KWA VILE UNAVYOTAMANI KWA KUBADILISHANA NA UWEZO WAKO" pindi usemapo maneno hayo chomoa unywele wako mmoja na uuweke kwenye bakuli lako kisha tulia kidogo kama sekunde tano hivi,sasa chukua Pete au Saa yako ambayo unataka wapi aingie kati ya hivyo viwili kama ni Pete haya chukua Pete yako pia uiweke kwenye bakuli lako kisha rudia maneno haya mara tatu "NAKUAMRISHA UINGIE KWENYE HII............UKAE HUMO NA UBAKI HUMO","NAKUAMRISHA UINGIE KWENYE HII............UKAE HUMO NA UBAKI HUMO","NAKUAMRISHA UINGIE KWENYE HII.............UKAE HUMO NA UBAKI HUMO" kisha tulia tena kwa sekunde tano.

Baada ya hapo nyanyua mshumaa wako MWEUPE upulize uzimike kisha nyanyua mshumaa MWEUSI pia upulize uzimike hii inawakilisha kuzima au kuondoa nguvu za UWEZOHURU alionao JINN na kukufanya wee kuwa MASTER wake au MKUU wake ukiwa unauacha mshumaa mwekundu ukiendelea kuwaka,chukua Pete au Saa yako ndani ya bakuli na uiweke pembeni ilipokuwa mwanzo halaf chukua unywele wako uliopo ndani ya bakuli kwa umakini kabisa uweke unywele huo au uunguze unywele huo kwenye moto wa huo mshumaa mwekundu unaoendelea kuwaka.

Mara tu utakapomaliza kuuunguza unywele huo basi zawadi itakuwa imeshafika mahala pake kwa kuunguzwa na moto wa mshumaa mwekundu kama tulivyoona mara ya kwanza kuwa mshumaa mwekundu unamwakilisha JINN hivyo kwa kumpa zawadi hiyo ataendelea kukaa na kubaki ndani ya Pete au Saa ambayo umemuarisha wewe aingie,ukishahakikisha kuwa nywele imeungua yote sasa nyanyua mshumaa mwekundu na uupulize uzimike,mwisho wa zoezi.

Zoezi lako limekamilika tayari na kama itakuwa ulifata kila kitu na kila hatua basi utakuwa tayari umeshamuweka JINN chini ya himaya yako akiwa ndani ya Pete yako au Saa uliyomuamrisha aingie.Kuna baadhi ya watu huanza kuhisi uwepo wa JINN mara tu anapomaliza zoezi.Kutokana na ukweli kwamba JINN huyo ni MPYA kwako basi atakuonea aibu na kukuogopa hivyo ataogopa kuja LIVE kwa kukuonea aibu au kukuogopa mpaka pale atakapokuwa na IMANI juu yako na KUKUAMINI ndipo atakapoamua kujitokeza LIVE na kuweza kumuona na mkaonana na kuwasiliana nae ana kwa ana.

Kama utapenda kumuuliza swali la aina yoyote ile basi baadhi ya JINNS huwa na njia zao tofauti wanazopendelea kutumia kuwajibu binadam,kama utamuuliza swali kabla ya kuanza kuonana nae basi tumia njia hii hapa chini;-

NJIA YA KWANZA
Chukua penseli kwa kutumia mkono wako ambao hauna nguvu kama mkono wako wa kulia ndio una nguvu basi tumia mkono wa kushoto shika penseli na weka kwenye mstari wa kwanza kabisa kwenye karatasi ambayo haijaandikwa kitu usiandike chochote,muulize swali kwa sauti kubwa kidogo iliyo na utulivu isiyo na ukali lakini utoe sauti na umuulize swali lako na muamrishe JINN WAKO auongoze mkono wako "KWA KUTUMIA MKONO WANGU NATAKA UUONGOZE UWEZE KUNIPA JIBU LA SWALI NILILOKUULIZA" kisha funga macho yako na anza kuisogeza penseli yako taratibu na kuchorachora kwenye karatasi yako ovyo ovyo tu bila ya kujua unachokichora au kukiandika mpaka karatasi yote iwe imejaa.Sasa fungua macho yako na angalia karatasi yako,kama JINN wako ni mwenye aibu sana atakupa jibu kwa maandishi ambayo yatakuwa nyuma ya michoro uliyoichora utaona alichokiandika na utaona jibu lako.Kama hana aibu basi atakupa jibu lako kwa kuandika sentensi zilizo wazi kabisa.

NJIA YA PILI
Njia nyingine wanayopenda kutumia majini kuwasiliana na WAKUU wao ni njia ya kutumia ULIMWENGU WA NDOTO kwa kuwa karibu sana na JINN na kukueleza yale uyatakayo dakika chache kabla ya kulala fanya MEDITATION kama ya dakika 10 au 15 juu ya maswali unayotaka akupe ufumbuzi muulize kwa HISIA ukiwa umetulia kwenye MEDITATION kabla ya kulala kisha ukimaliza tu panda kitandani ulale,haitachukua muda ukishapata usingizi JINN wako atakuja ndotoni kwa njia moja au nyingine na atakusaidia kukushauri na kukuongoza juu ya yale uliyomueleza kabla ya kulala.

Bila ya shaka baada ya kumtumia mara kadhaa na kukuamini akijua kuwa wewe ndio MKUU wake na kukuzoea atakuwa huru kuweza kujitokeza na kuja kwako ukamuona vile unavyotaka na mkawa mnawasiliana nae ana kwa ana.
Nyie watu ni hatari sana aisee!!, haya mambo nyie mnayatoa wapi.??
 
Majin ckuiz yamekua vbur kama nn ukiwaita wanajvuuuta kwel kwel n mmoja tu ukimuita anakuja tena umuekee halua
 
'unachosema ni kweli kabisa mkuu kwa sababu binadam wanatofautiana coz hata mi for the first time nakutana na JINN na kuonana nae ni alikuja MWENYEWE tu from nowhere tukaongea mambo mengi tu mengine sio ya kuweka hapa kuna siku akaniletea chakula ilikuwa ni pilau nikala kama kawaida alileta na juice pamoja na tambi ila tambi sikula coz pilau inapanda na juice bila shaka sikuwahi kula pilau tamu kama ile tangu nizaliwe akaniachia namba zake za simu tukawa tunawasilia nilikuwa sijamuonesha nyumbani kuna siku narudi nyumbani naambiwa kuna mgeni wako dada mmoja wa kiarabu alikuja hapa anaitwa JIHAN nilivyoskia hilo jina nikajua ni yeye na sikuwahi kumuonyesha home na mambo mengi tu si lazma kuyaweka hapa mkuu ila point ni kwamba alikuja tu mwenyewe bila ya kumwita baada ya muda nikapata tena rafiki alikuwa ni age met mwarabu flani hivi anaitwa VISHAL au BHAIJAN huyu nae alikuja mwenyewe tu badae ndo nikajua that he is not a human being na mengine mengi tu mkuu'
Heeh.!!
 
Ila nimesoma nanimejifunza kitu lakini paragraph ya 3 nimesoma Neno ALLAH hivi ni Yule mungu wetu waislamu au?
 
mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
je, una shida katika kazi au biashara?

je, unapata pesa lakini hukai nayo mkononi?

kwa matatizo haya na mengine mengi ni-PM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom