Jinsi ya kuchagua viongozi wa siasa kisayansi

Oct 11, 2015
49
35
JINSI YA KUCHAGUA VIONGOZI WA SIASA KISAYANSI

Mungu amenijalia kipaji cha maarifa ktk sayansi, pia mimi ni mwanafalsafa. Falsafa yangu ktk uchuguzi mkuu ni hii “SICHAGUI KIONGOZI KWA MISINGI YA CHAMA, NACHAGUA CHAMA KWA MISINGI YA KIONGOZI”.


Unaweza fikirini sentensi hiyo ya kifalsafa haieleweki lakini inaeleweka sana na imebeba uzito mkubwa sana wa kuchagua viongozi kifalsafa na kwa usahihi mkuu. Sentensi hiyo ya kifalsafa inamaanisha kwamba, “si chama kinachonifanya nichague kiongozi bali kiongozi ndo atanifanya nichague chama” yaani “nitamchagua KIONGOZI BORA bila kujali anatoka chama gani” yaani “yaani chama kikileta kuiongozi mbovu sitakichagua hatakama nakipenda kiasi gani”. Sentensi hizi za kifalsafa ni muongozo unaofaa sana kama ukiuzingatia ktk uchaguzi wa viongozi wetu wa siasa.
Tatizo kubwa la vijana wengi wamejaa ushabiki na kufata mkumbo bila kutafiti ubora na ubovu wa hicho wanachokishabikia. Lakini sisi kama wanafalsafa wa nchi hii lazima tutumie falsafa kimantiki (logically) na kwa weledi ktk kuchagua viongozi na mambo mengine. Kwa ujumla falsafa ni hekima ya maisha, moja ya sifa kubwa ya mwanafalsafa yoyote duniani ni “kupenda mafundisho yenye hekima, na kukosoa mafundisho yasiyo na hekima”.
Kupitia falsafa ya uchaguzi niliyoitoa hapo juu, utagundua kua “unatakiwa kuchagua kiongozi bora bila kujali katoka chama gani” pia “hutakiwi kuwa mtumwa wa chama cha siasa” mpaka kuchagua kiongozi mbovu eti kwasababu ameletwa na chama chako. Kama ni mzalendo (mpenda nchi yako) utanielewa vizuri na utakubaliana name kua nachoongea nikosahihi kifalsafa na kiuhalisia, namaanisha “usinywe sumu kwasababu baba yako ndo amekupa”, kama chama kinaleta mtu mbovu kataa hiyo sumu kwa manufaa ya nchi yetu, ikifika hapa falsafa yangu inasema “Tanzania kwanza, chama badae”, falsafa yangu nyingine inasema “nitakisalita chama kwa ajili ya Tanzania, na sitaisaliti Tanzania kwaajili ya chama”. Ndugu yangu mzalendo, chama kinaposimamisha viongozi wazembe, mafisadi, waongo n.k iokoe Tanzania kwa kukataa kuwachagua viongozi hao na kuchagua viongozi bora kwa ajili ya Tanzania bila kujali ni wachama gani.


Kifalsafa si busara kushabikia chama, na pia kua mwanachama wa chama cha siasa kama hunufaiki mojakwamoja kupitia chama hicho. Namaanisha kama huna maslahi ya mojakwamoja ktk chama, usikubali kua mwanachama bora uwe huru. Namaanisha hivi, “uwe mwanachama kama unamaslahi ya mojakwamoja ktk chama”.
Kwanini nasema si busara kushabikia chama cha siasa pia kua mwanachama (kama chama hakikunufaishi moja kwa moja)??

Jibu nirahisi sana. Kifalsafa na kiuhalisia ni kwamba “chama cha siasa ni MTAJI WA MWANASIASA KUFIKIA NDOTO ZAKE NA SI ZAKO” ndio maana mwanasiasa huhama chama kimoja kwenda kingine ili kutimiza ndoto zake na si zako. pia mwanasiasa huwatumia wanachama kama daraja la kufikia ndoto zake. Hivyo kama ulikua hunataarifa ni kwamba kama wewe ni mwanachama wa chama Fulani, kifalsafa na kiuhalisia wewe ni “daraja la mwanasisa kufikia ndoto zake na si zako”, yaani “wewe ni chambo cha mwanasiasa kupata samaki anaowahitaji” ndio maana si busara kushabikia chama au kua mwanachama kama huna maslahi ya moja kwa moja ktk chama. Hii ndo siri kuu kwanini mimi mwanafalsafa na mwanasayansi sina chama chochote, kwangu vyama vyote ni sawa, nachotaka ni KIONGOZI BORA bila kujali anatoka chama gani. Mwanafalsafa mwenzangu ni busara uyajue haya na kuwaelimisha wengine.

Tuje kwenye point yetu kuu. Nimesema mimi ni mwanasayansi kitaaluma pia Mungu wangu amenijalia kipaji cha hali ya juu ktk sayansi. Mpaka sasa hivi “NIMEGUNDUA SHERIA NANE ZA KISAYANSI” namaanisha “as a scientist I have discovered 8 scientific laws”. Kwa kadiri nitakavyoona inafaa nitatambulisha Law moja mpaka nyingine. Leo nitatumia sheria inayoitwa “Joachim first law of system” niliyoigundua mwenyewe kwa weledi nilojaliwa na muumba wa miisho ya ulimwengu. Sheria hii inaelezea mifumo yote duniani kwanzia cell as a system, mwili wa viumbe hai, machine mbalimbali, mtu binafsi as a system, familia, shule, kanisa, msikiti, chama, nchi, falme, makampuni, mashirika, n.k inaelezea siri ya mafanikio na kushindwa kwa mfumo wowote duniani, mbinguni na kuzimu.

Joachim first law of system states that “any system is controlled by its control center”. Maana yake “kila mfumo huongozwa na kitovu cha uongozi wa mfumo huo”. Yaani mfumo wowote unasehemu maalum ambayo huongoza mfumo mzima. Mfumo ni kitu tata kinachoundwa na sehemu mbalimbali zinazofanyakazi tofautitofauti zinazoongozwa na sehemu maalumu.


Mfano, mwili wako ni mfumo, maana unaundwa sehemu mbalimbali kama mikono, miguu, macho, masikio, pua, mdomo, tumbo, n.k ambapo viungo vyote hivyo huongozwa na sehemu maalum inayoitwa “UBONGO”. Ukiona mtu anakula kinyesi, anakunywa mkojo, anatukana hovyo, anatambea uchi na kufanya yanayofanana na hayo, tatizo si mwili wake unaofanya hayo bali ni “UBONGO ULIOAMURU MWILI UFANYE UCHAFU HUO”. Yaani mwili hufuata kile ubongo uachosema hata kama ni kibaya. Hivyo ukiona mtu anatembea uchi barabarani, tatizo si mwili kwamba umekataa kuvaa nguo, tatizo ni ubongo ulio-command hivyo. Ukiona mtu anatukana matusi, tatizo si mdomo, tatizo ni ubongo ulioamuru midomo itukane. Ukiona miguu inakwenda choo kilipo, mikono ikaanza kupakua kinyesi na kukiingiza mdomoni na kukila, tatizo si viungo hivyo bali ni ubongo ulioamuru hayo.



Kutokana na Joachim first law of system which states that “any system is controlled by its control center”, ukiona system inafanya vibaya, tatizo si system bali ni “system control center” inyoongoza system nzima, yaani ukiona mtu anatembea uchi, tatizo si mwili (system) bali ubongo (system control center). Ubongo ukipona utashangaa mtu yuleyule aliyekua anatembea uchi, anaacha mara moja na kuvaa nguo za heshima.

Niingie ndani zaidi. CCM imeiongoza nchi yetu kwazaidi ya miaka 50, lakini maendeleo tuliyonayo hayaridhishi. Namaanisha, ukilinganisha umri wa nchi yetu na rasilimali tulizonazo, tumepiga hatua lakini si kiasi cha kutosha.

Swali. Je, kwa nini CCM imeshindwa kutuleta maendeleo stahiki tangu ishike dora mpaka sasa????



Tatizo si CCM. Kisayansi, kifalsafa na kiuhalisia ukirejea sheria ya kisayansi inayosema “mfumo wowote huongozwa na kitovu cha uongozi wa mfumo” ni ukweli usiopingika kwamba CCM kama mfumo haijafanikiwa kuondoa umaskini, ufisadi, ujinga na maradhi nchini kwasababu ya aina ya “control center” au kitovu cha uongozi kilichokua kinaiongoza CCM kilishindwa kuiongoza ccm vizuri kuongoza nchi yetu.



Nipasue jipu. Tatizo si ccm bali anayeiongoza ccm. Nijenge hoja. Kwanini mwalimu alifanikiwa sana kiuongozi kama kitovu cha uongozi (system control center) wa nchi hii kama mfumo wakati waliomfatia yaani mwinyi, mkapa na mrisho hawakufanikiwa kiuongozi kama mwalimu???

Jibu ni rahisi sana. Nyerere alikua effective system control center of Tanzania akatengeneza effective system ya kupambana na ufisadi n.k ndio maana mwalimu alifanikiwa kuliko wenzake kwani yeye alikua effective zaidi kama control center wan chi ukilinganisha na wengine waliomfata. Yaani tatizo si mfumo bali ni Yule anayeuongoza mfumo, yaani nikitaka kujua kisayansi kabisa kiongozi ni effective kiasi gani naangalia mfumo anaoungoza ni effective kiasi gani. Namaanisha nikitaka nijue baba ni effective kiasi gani ktk malezi ya familia yake, “naanglia watoto wake wananidhamu kiasi gani”, nikitaka nijue mume ni bora kiasi gani “naangalia anamtreat mkewake kivipi” nikitake nijue mke ni bora kiasi gani “naangalia anamjali kiasi gani mume wake” naam nikitaka nijue nyerere ni effective kiasi gani “naangalia alipokua rais aliiongozaje Tanzania” yaani ufisadi ulitawala au uzalendo ulitawala? Naam ubora wa elimu ulikua chini au juu? Naam thamani ya shilingi ilikua chini au juu?? n.k. mwinyi, mkapa na mrisho nawapima kwa jinsi hiyohiyo nilivyompima nyerere kitaalamu kabisa. Yaani nikitaka nijue mrisho ni kiongozi bora kiasi gani naiangalia Tanzania ya leo, imejaa ufisadi au uadilifu, elimu imepanda ubora au imeshuka?? Thamani ya shilingi imepanda au imeshuka?? n.k. kanuni ni ileile nikitaka kujua Magufuli ni kiongozi bora au bora kiongozi “NAANGALIA wizara ya ujenzi ameiongozaje” kwa mafanikio au kwa ufisadi, naam nikitaka nijue lowasa ni kiongozi bora au ni bora kiongozi “NAANGALIA alipokua waziri mkuu aliitendea haki Tanzania au aliifanyia UFISADI”.

Naam hekima au falsafa inasema “ambaye ni mwaminifu ktk jambo dogo, hata kubwa pia atakua mwaminifu na asiyemwaminifu ktk jambo dogo hata kubwa pia hatakua mwaminifu”. Yaani anayekua mwaminifu ktk uwaziri hata urais pia atakuamwaminifu naam ambaye ni fisadi katika uwaziri mkuu, hata urais atakua fisadi papa.
Tuangalie mfano mwingine wa UONGOZI. Nikitaka nijue wewe ni dereva makini kiasi gani naangalia “UNAVYOLIONGOZA GARI BARABARANI” je, unazingatia kanuni za usalama barabarani au unaendesha hovyo hovyo??? Naam dereva mzembe, mrevi, asiyezingatia kanuni za usalama barabara atasababisha ajali kwa kugonga watu na magari, watu wasio na busara watalilaumu gari na kusema “hili gari ni baya sana linagonga watu na magari mengine!!!” lakini wenye busara na hekima (wanafalsafa) watasema “tatizo si gari bali NI DEREVA MZEMBE AMELIONGOZA VIBAYA”.



Naam gari lilelile likipata dereva mstaarabu, amequalify vizuri, anazingatia kanuni zote za usarama barabarani, utashangaa zile AJALI HAZITOKE. Hapa mtu asiye na busara atasema “lile gari limejirekebisha, linatabia nzuri haligongi watu tena” lakini mwenye hekima atasema “gari halina tabia nzuri bali limepata DEREVA ANAYELIONGOZA VIZURI NDIO MAANA HALISABABISHI AJALI”.



Namaanisha ajali za umaskini, ufisadi, ujinga na maradhi ambazo wapinzani wamekua wakisema zimesababishwa na ccm, kitaalamu ni kwamba zimesababishwa na ccm control center yaani mwinyi, mkapa na mrisho ambao hawakuiongoza ccm vizuri kama dereva wa kwanza yaani mwalimu. Tatizo la umaskini nchini na mengine, kitaalamu, kifalsafa, kisayansi na kiuhalisia yamesababishwa na mwinyi, mkapa na mrisho walioshindwa kuongoza vizuri gari la Tanzania. Naam mwalimu hatasaulika ktk historia nya TANZANIA kwasababu alikua dereva mstaarabu akaiongoza Tanzania na CCM kwa ujumla, hivyo tatizo sic cm ni mwenyekiti wa ccm, yaani tatizo si Tanzania bali rais wa TANZANIA anayeiongoza Tanzania yote.



Nani anafaa kua rais kati ya Magufuli na Lowasa?? Naam nani anafaa kua mbunge wa jimbo langu na nani anafaa kua diwani wa kata yangu kisayansi, kifalsafa na kiuhalisia???

Jibu ni rahisi sana hekima inasema “AMBAYE NI MWAMINIFU KTK JAMBO DOGO HATA KUBWA PIA ATAKUA MWAMINIFU, na ASIYEMWAMINIFU KTK JAMBO DOGO HATA KUBWA PIA HATAKUA MWAMINIFU”.


Ukitakaujue nani anafaa kua rais, mbunge, na diwani, hekima inasema usimsikilize anasema nini jukwaani kwani pale anatafuta UGALI WAKE hata kama ni fisadi kiasi gani atasema wananizingishia(naam hakuna mwizi anayeiba kisha kujitangaza kwa kusema ni mimi niliyeiba). Mwanasiasa akiwajukwaani hutua ahadi kama kichaa wa bangi naam atakwambia elimu bureeee, maisha bora kwa kila mtanzania ili umpe kula akishapata utashangaa MAISHA BORA YANAKUA MAISHA BARAA. USIDAGANYWE NA WANASIASA JUKWAANI, Muwamba ngoma huvutia kwake, hujinadi kwa ahadi kedekede, uonesha yeye ni masihi (hata kama ni fisadi MPAKA SHETANI ANAMSHANGAA!!!). Mwanasiasa atadanganya jukwaani ili akubalike na kumchafua mwezake ili asikubalike.

Ilikupona na hila ya wanasiasa, tumia hekima, naam nayo inasema “AMBAYE NI MWAMINIFU KTK JAMBO DOGO HATA KUBWA PIA ATAKUA MWAMINIFU, na ASIYEMWAMINIFU KTK JAMBO DOGO HATA KUBWA PIA HATAKUA MWAMINIFU”. Yaani nikitaka nijue magufuli anafaa kua rais au hafai naangalia wizara ya ujenzi aliiongizaje, kama ameshindwa kuongoza wizara atawezaje nchi yote, lakini kama aliongoza kwa umahiri mkuu hata nchi ni hivyohivyo. Kama lowasa alishindwa uwaziri mkuu ATAWEZAJE KUONGOZA NCHI NZIMA??


UKITAKA UJUE NANI NI RAIS, MBUNGE NA DIWANI, usimsikilize jukwaani atakudangfanya maana mwamba ngoma huvutia kwake, bali mchunguze ni mwaminifu kiasi gani ktk nyazifa ndogo alizotumikia au anazotumikia kwa sasa, kama anatumika kwa uaminifu mchague lakini kama ni fisadi, usimchague kwa manufaa ya nchi yetu tukufu. Hii ndo hekima.



Naelekea mwisho kabisa wa elimu hii mpya juu ya uchaguzi. Kama ni nyumba napiga bati sasa. Ukweli ni kwamba kutokana na maelezo ya kifalsafa, kisayansi na kiuhalisia, magufuli anafaa kua rais kuliko lowasa kwani amekua mtumishi mwaminifu san asana sana ukilinganisha na wenzake.



Wengi wanakubali hu ukweli. Lakini wanasema tatizo si magufuli bali ni chama chake kimejaa mafisadi na viongozi wasiowajibika. Hofu hii dhidi ya ccm imesababishwa na uongozi usioridhisha wa mwinyi, mkapa na mrisho. Niwatoe hofu, kisayansi, kifalsafa na kiuhalisia ni kwamba tatizo si ccm bali mwenyekiti wa ccm anayeiongoza, kizuri zaidi mrisho amemaliza muda wake na ameingia magufuli.



Niprove kisayansi kwamba ccm inawanachama waadilifu wengi sana kuliko mafisadi. Nitatumia topic ya probability ya mathematics, kuprove kwamba ccm inawanachama waaadilifu wengi sana kuliko mafisadi.
Nifate. Magufuli kiongozi mwadilifu, mzalendo, mpinzani mkubwa wa ufisadi na uzembe (mfano amefukuza wakandarasi zaidi ya 3,000 kwa makosa yao), kiongozi huyu wa aina yake amechaguliwa kwa asilimia 87.1% na wanachama wa ccm. Falsafa ya Kiswahili inasema “ndege wanaofanana huruka pamoja”, na kanuni ya kisayansi inasema “like dissolves like” hivyo ndani ya ccm kuna wanachama 87.1% wanaofanana na Magufuli ndo hao waliomchagua awemgombea wa urais kwani “ndege wanaofanana huruka pamoja” na chemistry inasema “like dissolves like”. Kisayansi ni kwamba probability ya wanachama waadilifu, wapinga ufisadi na wajibikaji ktk CCM ni 87.1% yaani ccm ina magufuli wadogo 87.1% na ndo waliomchagua magufuli huku 12.9% ni mafisadi ambao wengi wao sasa wamehamia chadema yaani lowasa, lostam azizi, masha, makongoro Mahanga, sumaye n.k hi indo 12.9% ya mafisadi ambao ndo walikichafua chama, na kukifanye kionekane si kisafi.

Je, magufuli akiwa rais atapata watu wajapakazi kama yeye wa kuunda baraza la mawaziri??.


Jibu ni ndiyo kwasababu ukireje matokeo ya NEC ni kwamba, kisayansi ndani ya ccm, kuna “MAGUFULI WADOGO” 87.1% ndo walimchagua apeperushe bendera ya ccm naam “ndege wanaofanana huruka pamoja” pia sayansi inathibitisha zaidi “like dissolves like”. Ukweli ni kwamba ndani ya ccm kuna wanachama wengi sana wapinga ufisadi, wawajibikaji, wazalendo kama magufuli ndo watashirikiana naye kutulete mabadiliko stahiki yunayoyahitaji na bora mabadiliko. Waadilfu wapo Samweli sita, deo filikunjombe, ana kilango, jenista Joachim mhagama, agrey mwanri,joseph ole sendeka, n.k siwezi kuwataja wote kwasababu ya muda.

MAGUFULI FOR CHANGE. MABADILIKO YA KWELI NI HAYA EE MWANANCHI.


MWISHO. Nimetumia maneno zaidi ya 2,000, masaa zaidi ya matano, sheria za kisayansi, ikiwemo sharia ya kisayansi niloigundua mwenyewe ile inayoelezea mifumo yote Dunia (pia ninazo sheria za kisayansi 7 nilizogundua mwenyewe), nimetumia falsafa yangu ya uchaguzi inayosema “sichagui kiongozi kwa misingi ya chama, nachagua chama kwa misingi ya kiongozi”, pia nimetumia concept za probability za mathematics for scientific proofs, nimetumia methali za Kiswahili, nimetumia weledi wa hali ya juu sana wa kisayansi nilojaliwa na muumba wa miisho uya ulumwengu(naam KWAKE IWE UTUKUFU), n.k. nimeenza kuandika mida ya saa mbili usiku na sasa ni saa saba usiku. Nimechoka, mgongo unauma, ninakumbuka shairi nilofundushwa o-level la “building a nation” kuna stanza inasema “the pain we get in building the nation” ni kweli haya ni maumivu tunayoyapata ktk kujenga TANZANIA our glorious nation, zaidi ya yote nalala saa saba usiku lakini kesho saa kumi na mbili inatakiwe niamke na kujiandaa kwenda shule ya St. WILLIUMS kufundisha wanafunzi bure kabisa JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAO.. Chakusikitisha zaidi kuna mbwa, nguruwe na wapumbavu wachache wataanza kunishambulia bila kujali gharama niloingia ikiwemo fedha (ukizingatia mimi ni mwanafunzi tu), watanirarua na kukanyagakanyaga maarifa haya adimu kama kichaa anavyochezea kinyesi naam “ATAKAYEPINGA UKWELI HUU USIOPINGIKA, AKAPIMWE AKILI”, hivyo sitashangaa vichaa wakishindwa kuelewa maarifa haya na kuanzakunishambulia, nikotayari kuwajibu kwa HOJA ZENYE NGUVU. Lakini wewe mzalendo wa kweli usiwe kama wao bali usome na wafundishe wengine bure kama nilivyoyanya kwako, ukiweza share na wenzako usiishie kulike. AMEEEEEN!!!!!!!!!!

KAMA HUJAELEWA UNARUHUSIWA KUULIZA KWA NIA YA KUJIFUNZA ZAIDI na si kuudhihirisha upinzani kichaa, naam MPUMBAVU AKINYAMAZA huhesabiwa ANAHEKIMA.

TAFADHARI USIUDHIHIRISHE UPUMBAVU WAKO. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA. AMENI.
 
bogus, chama ndicho kinachobeba falsafa na ilani ya uchaguzi, kuchagua ilani mbav ni kuchagua chama kibaya, na kuchagua chama kibovu kiongoz ni mbovu, chama ndicho hutoa dira kwa kiongoz nasi kiongoz kutoa dira kwa chama, chama ni system, leader is a standing figure withn a political party. jielewe dogo
 
Kitengo cha it cha Ccm mnahara sana na mbadooooo , Ccm haiwezi kuwaamulia raisi Watanzania
 
Back
Top Bottom