Jinsi ya kuandaa Business Plan kwa urahisi

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
Kwa maneno machache mno , Business plan ni andiko la kibiashara ambalo unaelezea wapi uliko kwa sasa, na wapi unataka kwenda (Future),ukielezea mikakati (strategies) utakayotumia kufika huko kwenye malengo (Goals) uliyojiwekea.

Business plan ya biashara moja hupishana na ya mwingine kulingana na ukubwa wa biashara (scale), rasilimali ilizonazo (resources), Eneo iliko (geographic) n.k

Kwa leo nakuletea Vipengele muhimu ambavyo kila Business Plan huwa navyo: (Nafanya rejea kwenye biashara ya kuuza vipodozi asilia)

1. PRODUCTS and SERVICES
Elezea vema ni nini unataka kuoffer kwa njia gani, matarajio nk
Hapa utaonesha bidhaa za ngozi na nywele asilia unazodeal nazo kwa majina, size, ujazo, n.k

2. MARKET ANALYSIS

Unatakiwa tuchambue masoko kwa kuyavunja katika vipengele mbalimbali kama wateja watarajia masoko kwenye hilo kundi pia sehemu kubwa tutajikita na wenye sifa zipi.

Mfano ukisoma watanzania , ni vyema utaje kundi (niche) mfano walioajiriwa . Hii itafanya tukianza marketing activities tudeal na kundi letu tu na si wengine kama wanafunzi n.k

3. MARKET STRATEGY
Hapa lazima uzungumzie mikakati gani ya kimasoko
unayo kuwafikia wateja wa zamani na pia kuwavuta wateja wapya. Mikakati kama ya bei, promo, ushindani lazima uguse

4. SWOT ANALYSIS
hapa inafahamika japo kuna room ya kuiboresha zaidi, kwa kifupi unapima nguvu za ndani ya biashara na udhaufu wako .Pia unapima vitisho toka nje na fursa zake.
Mfano nguvu zako: una access na mitaji

Udhaifu wako: HAuna muda wala ujuzi wa kuanzisha mradi (Hapo tafuta partner sahihi)

Vitisho toka nje: kuna ushindani

Fursa: Ni zama za internet, nusu ya Watanzania (milioni 30) unaweza kuwafikia ukiwa na ujuzi sahihi wa masoko mtandaoni (updated online marketing (siyo kupost whatsapp groups))

5. MANAGEMENT

Hapa kikubwa kujua gharama zake tutaweza kuzijua katika salary scale ya kampuni uliyojiwekea. Hapa tukijua idadi ya wafanyakazi tutaweza kujua vilevile gharama za kila mwezi

6. FINANCIAL HISTORY
. Inapendeza
uweke historia yako kimapato ulipofanya kwa small scale ili kuonesha inaingiza mapato. Kutaja aina ya wateja, bei za huduma, .Ungekuwa umeanza muda mrefu ningeshauri uambatanishe
statement ya miaka walau mitatu ya nyuma ambapo wataona faida/hasara za miaka mitatu mfululizo

7. FINANCIAL PLAN AND PROJECTIONS
. Hapa sasa inamaana nini unatarajia.

Umesema mnatarajia kupata labda hadi mil 250, sawa je ndani ya mwaka mmoja?miwili?mitano? Je inawezekana vp? Hapa
vile vile utaweka mambo kama BREAK EVEN ANALYSIS kuonyesha mauzo yatazidi gharama baada ya muda
gani. SALES FORECAST kuwa mkishaweka hiyo mil 100 mnatarajia mauzo kuongezeka kwa kiasi gani kwa mwaka. (%)

Mwisho unaweza onesha wadau mnaoshirikiana ,kwa vipodozi inaweza kuwa SIDO au TBS, n.k

Karibu kwa maswali na huduma ya business plan

0713 039 875
Dr Mussa Zaganza
Consultant
 
Back
Top Bottom