CANVAS Business Model

Jane Msowoya

JF-Expert Member
Aug 20, 2017
4,046
7,118
Heshima kwenu wakuu
Siku kadhaa nyuma niliweka andiko hapa lakutafuta mwekezaji kwenye biashara yangu, na nikapokea calls, SMS na Pms kadhaa zingine walitaka kujua nafanyaje fanyaje ili kuweza kuendeleza game na uzuri pia kuna wanaonifahamu physicaly so haikuwa ngumu kwao kuamini nilichoandika.

Mimi natumia CANVAS BUSINESS MODEL
Yenye vipengele 9, vipengele hivi kwa pamoja ndivyo vinavyobeba Biashara yako
1. Key Partners
Hawa ni watu ambao utashirikiana nao kufanikisha biashara yako mfano mimi naweza sema ni wauza malighafi, wakulima, nk

2. KEY ACTIVITIES
Hapa sasa biashara yako itakuwa inafanya nini? Mfano mimi nazalisha vipodozi.

3. KEY RESOURCES
Hapa ni vifaa gani au resources gani zitahitajika ili ufanikishe mfano mimi ni cash, machines, nk

4. VALUE PREPOSITION
Hapa sasa ni utofauti wako wewe na washindani wako, yaani utafanya nini ambacho kitaleta wateja kwako kutoka kwa washindani wako waje kwako.

5. CUSTOMER RELATIONSHIP
Hapa sasa ni mbinu gani utakazozitumia kuhakikisha unakuwa na mahusiano yasiyokoma na wateja wako, yaani wateja wasisahau uwepo wako kila watakapopata huduma.

6. CHANNELS
Utatumia channels gani kuwafikia tupo kwenye dunia ya tiktok ya IG ya websites nk so utatumia channel ipi (hapa uwe makini sana sana usije tumia whatsapp akati ni Biashara ya utalii)

7. CUSTOMER SEGMENT
Hapa sasa unamjua mteja wako ni nani mfano unauza madaftali ya watoto wa vidudu mtumiaji ni mtoto ila mteja wako ni mzazi (hapa nimuhimu sana kumjua mteja wako hapa ndipo utajua kipato cha mteja wako nk)

8. COST STRUCTURE
hapa sasa ndo utajua mwenendo mzima wa biashara yako na utatumia kiasi gani kuzalisha pisi ngapi,au kodi,mishahara nk

9.REVENUE STREAM
hapa ndo utajua sasa namna yakutengeneza pesa, yaani pesa itamzaaje mwenzake

LAKINI YOTE KWA YOTE
ZINGATIA FEEDBACK

Ni kipengele muhimu sana kwenye biashara yoyote ile,
Kuna aina mbili za feedback.

1. Feedback kutoka kwa wateja

2. Feedback kutoka kwa wazoefu wa biashara

Feedback kutoka kwa wateja zitakufanya ujue ni wapi unakosea kwenye bidhaa/huduma unayouza, wateja wanatarajia nini kutoka kwako, utaboreshaje huduma/bidhaa yako. Ndomana ni muhimu.

Feedback ya wazoefu wa biashara itakusaidia kukushape wew ambae unafanya biashara katika mipango yako, mbinu, uendeshaji, changamoto na utatuzi wake n.k. kuna muda unaweza kujiona uko sawa kwakila kitu kwasababu wew ndo muanzilishi wa biashara lakini kiuhalisia kuna vitu unakosea na kwasababu umejiwekea wewe ndo wewe huwezi kuskiliza thirdy party you will learn it in a hard way utachoma pesa mpaka uje kugundua kwamba ulikuwa unakosea sehmu ushaiva sana na hamu ya biashara huna tena so feedback from Outside is very important.

Jamani
Poleni kwa gazeti afu wale wajuaji wenzangu namie nilipokosea njooni msahihishe tu mimi sio mwalimu jamani just sharing kile ninachofanya mimi

Picha kwa udhamini sio kila Biashara ni startup
Salum Awadh

IMG_20231028_112351.jpg
 
Sina utaalamu wa mambo ya biashara, ila nilisoma uzi wako ule ukihitaji mwekezaji katika biashara yenu kwa thamani ya milioni kumi.

Ulisema pia biashara yenu kwa sasa ina thamani ya milioni 20.

Wazo langu kwa nini usitafute namna ya kupata mkopo wa hio milioni kumi then umiliki wa biashara ukawa mikononi mwenu asilimia mia moja.
 
Sina utaalamu wa mambo ya biashara, ila nilisoma uzi wako ule ukihitaji mwekezaji katika biashara yenu kwa thamani ya milioni kumi.

Ulisema pia biashara yenu kwa sasa inathamani ya milioni 20.

Kuna sababu kuu moja tu mkuu
Sili RIBA

Ila nikipata nafasi nitakuja na mawili matatu ya kwanini investor kuliko kukopa.
 
Kuna sababu kuu moja tu mkuu
Sili RIBA

Ila nikipata nafasi ntakuja na mawili matatu ya kwanini investor kuliko kukopa
Sijajua ni kwa muktadha gani unakataa riba, lakini pia siwezi kuhitilafiana nawe kwa hilo, hata hivyo unaweza kuwa na sababu za msingi na za kutosha kwanini mwekezaji badala ya mkopo.
Naomba ukijaliwa utujuze.
 
Riba ni dhambi kubwa sana kwa Imani yangu ya dini

Ni sawa na kulala na mzazi wako
SubhanaAllah
Ndio sababu kuu nyingine ni kawaida tu kwa sisi wenye ndoto za kumiliki biashara kubwa investors muhimu si unaona HISA zinauzwa huko DSE
 
Riba ni dhambi kubwa sana kwa Imani yangu ya dini

Ni sawa na kulala na mzazi wako
SubhanaAllah
Ndio sababu kuu nyingine nikawaida tu kwa sisi wenye ndoto zakumiliki biashara kubwa investors muhimu siunaona HISA zinauzwa huko DSE
Kwenye maswala ya imani hauna lawama, imani inapaswa kuheshimiwa sana.
Ingawa najua kuna taasisi za kibenki zinazotoa mikopo kwa kuzingatia imani au dini ya aina fulani.
 
Heshima kwenu wakuu
Siku kadhaa nyuma niliweka andiko hapa lakutafuta mwekezaji kwenye biashara yangu, na nikapokea calls,SMS na Pms kadhaa zingine walitaka kujua nafanyaje fanyaje ili kuweza kuendeleza game na uzuri pia kuna wanaonifahamu physicaly so haikuwa ngumu kwao kuamini nilichoandika

Mimi natumia CANVAS BUSINESS MODEL
Yenye vipengele 9, vipengele hivi kwa pamoja ndivyo vinavyobeba Biashara yako
1. Key Partners
Hawa ni watu ambao utashirikiana nao kufanikisha biashara yako mfano mimi naweza sema ni wauza malighafi,wakulima,nk

2.KEY ACTIVITIES
hapa sasa biashara yako itakuwa inafanya nini? Mfano mimi nazalisha vipodozi

3. KEY RESOURCES
hapa ni vifaa gani au resources gani zitahitajika ili ufanikishe mfano mimi ni cash,machines,nk

4. VALUE PREPOSITION
Hapa sasa ni utofauti wako wewe na washindani wako, yaani utafanya nini ambacho kitaleta wateja kwako kutoka kwa washindani wako waje kwako

5. CUSTOMER RELATIONSHIP
Hapa sasa ni mbinu gani utakazozitumia kuhakikisha unakuwa na mahusiano yasiyokoma na wateja wako, yaani wateja wasisahau uwepo wako kila watakapopata huduma

6. CHANNELS
utatumia channels gani kuwafikia tupo kwenye dunia ya tiktok ya IG ya websites nk so utatumia channel ipi (hapa uwe makini sana sana usije tumia whatsapp akati ni Biashara ya utalii)

7. CUSTOMER SEGMENT
Hapa sasa unamjua mteja wako ni nani mfano unauza madaftali ya watoto wa vidudu mtumiaji ni mtoto ila mteja wako ni mzazi (hapa nimuhimu sana kumjua mteja wako hapa ndipo utajua kipato cha mteja wako nk)

8. COST STRUCTURE
hapa sasa ndo utajua mwenendo mzima wa biashara yako na utatumia kiasi gani kuzalisha pisi ngapi,au kodi,mishahara nk

9.REVENUE STREAM
hapa ndo utajua sasa namna yakutengeneza pesa, yaani pesa itamzaaje mwenzake

LAKINI YOTE KWA YOTE
ZINGATIA FEEDBACK

Ni kipengele muhimu sana kwenye biashara yoyote ile,
Kuna aina mbili za feedback.

1. Feedback kutoka kwa wateja

2. Feedback kutoka kwa wazoefu wa biashara

Feedback kutoka kwa wateja zitakufanya ujue ni wapi unakosea kwenye bidhaa/huduma unayouza, wateja wanatarajia nini kutoka kwako, utaboreshaje huduma/bidhaa yako. Ndomana ni muhimu.

Feedback ya wazoefu wa biashara itakusaidia kukushape wew ambae unafanya biashara katika mipango yako, mbinu, uendeshaji, changamoto na utatuzi wake n.k. kuna muda unaweza kujiona uko sawa kwakila kitu kwasababu wew ndo muanzilishi wa biashara lakini kiuhalisia kuna vitu unakosea na kwasababu umejiwekea wewe ndo wewe huwezi kuskiliza thirdy party you will learn it in a hard way utachoma pesa mpaka uje kugundua kwamba ulikuwa unakosea sehmu ushaiva sana na hamu ya biashara huna tena so feedback from Outside is very important.

jamani
Poleni kwa gazeti afu wale wajuaji wenzangu namie nilipokosea njooni msahihishe tu mimi sio mwalimu jamani just sharing kile ninachofanya mimi

Picha kwa udhamini sio kila Biashara ni startup
Salum AwadhView attachment 2797417
Niliapia sitokuja kuongelea kitu chochote serious humu JF zaidi ya pombe na ngono ila ngoja leo nikushauri kitu sababu nimeona sana mabandiko yako na sijui kwanini yananiangukia

Nimefanya kazi za kuallocate funds kwenye startups kutoka kwenye foundations kadhaa nje na ndani ya nchi. Wengi ni wanasiasa kama wewe(usiishie kusoma hapo, vuta pumzi tuendelee). Wanalenga kutoa first impression kwa maneno mataam lakini biashara zao ni zero. Startups nyingi zinakufa hata kama walipewa funds sababu executives na founders ni wanasiasa tu, wanajua theory ya biashara na maneno mazito ya kutongoza investors ila hawajui kuendesha biashara kutokana, kutumia data, takwimu na saikolojia ili kufanya biashara iwe profitable zaidi.

Siku hizi nikisikia neno startup nataka hadi kutapika. Cheki kuna waghana flani walipata hadi usd 86 million wanajiita DASH ila kampuni limekufa, nenda kwa jirani zako JUMIA wako wapi sasahivi? Startups za hapa Tanzania ndo sitozitaja sababu founders lengo lao ni kupata funds wakanunue brevis wajenge nyumba then wafunge biashara.

Sasa mimi nakuomba kitu kimoja tu. Takwimu za biashara zako katika makundi haya.

1)Zitakazonifanya NIWEKEZE kwenye biashara yako
2)Zitakazonifanya NISIWEKEZE kwenye biashara yako.

Hapo kwenye takwimu nataka zote ambazo unatumia kwenye biashara yako kama vile customer follow ups, leads to client ratio, stock turnover, na statistics zote (kama una utimamu wa biashara utajua namaanisha zipi)
lkn pia ambatanisha financial statements za toka mwaka ulioanza kufanya business hadi mwaka huu.

Nitumie PM na kama nitapenda ninachokiona nina 15million hapa cash imekaa inasubiri kufanyiwa starehe tu, nitawekeza nusu kwenye biashara yako. Ukiona risk kunitumia nambie nikupe calendar yangu uchague siku tuonane ofisini kwangu, nitakua na cash ww uje na hizo data.

Good luck sweetheart.
 
Naungana nawe, ingawa general mikopo inafaida zake lakini katika faida kuna changamoto kubwa pia.
Wakati mwingine ni bora kuwa mbali nayo.

Natumaini njia unayotumia ni bora , wakati mmoja utakua kwenye kilele cha mafanikio.
 
Niliapia sitokuja kuongelea kitu chcht serious humu JF zaidi ya pombe na ngono ila ngoja leo nikushauri kitu sababu nimeona sana mabandiko yako na sijui kwa nn yananiangukia

Nimefanya kazi za kuallocate funds kwenye startups kutoka kwenye foundations kadhaa nje na ndani ya nchi. Wengi ni wanasiasa kama wewe(usiishie kusoma hapo, vuta pumzi tuendelee). Wanalenga kutoa first impression kwa maneno mataam lkn biashara zao ni zero. Startups nyingi zinakufa hata kama walipewa funds sababu executives na founders ni wanasiasa tu, wanajua theory ya biashara na maneno mazito ya kutongoza investors ila hawajui kuedesha biashara kutokana, kutumia data, takwimu na saikolojia ili kufanya biashara iwe profitable zaidi.

Siku hizi nikisikia neno startup nataka hadi kutapika. Cheki kuna waghana fln walipata hadi usd 86 million wanajiita DASH ila kampuni limekufa, nenda kwa jirani zako JUMIA wako wp sshv? startups za hapa tz ndo sitozitaja sababu founders lengo lao ni kupata funds wakanunue brevis wajenge nyumba then wafunge biashara.

Sasa mm nakuomba kitu kimoja tu. Takwimu za biashara zako katika makundi haya.

1)Zitakazonifanya NIWEKEZE kwenye biashara yako
2)Zitakazonifanya NISIWEKEZE kwenye biashara yako.

Hapo kwenye takwimu nataka zote ambazo unatumia kwenye biashara yako kama vile customer follow ups, leads to client ratio, stock turnover, na statistics zote (kama una utimamu wa biashara utajua namaanisha zipi)
lkn pia ambatanisha financial statements za toka mwaka ulioanza kufanya business hadi mwaka huu.

Nitumie PM na kama nitapenda ninachokiona nina 15million hapa cash imekaa inasubiri kufanyiwa starehe tu, nitawekeza nusu kwenye biashara yako. Ukiona risk kunitumia nambie nikupe calendar yangu uchague siku tuonane ofisini kwangu, nitakua na cash ww uje na hizo data.

Good luck sweetheart.
Wazee mpo nondo hadi naogopa,
 
Sina utaalamu wa mambo ya biashara, ila nilisoma uzi wako ule ukihitaji mwekezaji katika biashara yenu kwa thamani ya milioni kumi.

Ulisema pia biashara yenu kwa sasa inathamani ya milioni 20.

Wazo langu kwa nini usitafute namna ya kupata mkopo wa hio milioni kumi then umiliki wa biashara ukawa mikononi mwenu asilimia mia moja.

The first day nimeona uzi wake nikasoma nikaishia hapo nikaenda kusoma upuuzi wa kina rikiboy kule MMU wanavyokulana kimasihara.

Kuna point kubwa sana hapo. Investor yyt anaejitambua hawezi kuweka hata mia kwa hio doubt pekee.

Kama hataki kupata mkopo inamaanisha moja kati ya hizi assumptions ziko sahihi.
1)Biashara haina credit score/history nzuri.
2)Biashara haina assets (hio thamani ya 20m sijui kaipataje)
3)Biashara ina deni sugu hvo hawezi pewa mkopo tena.
4)ANAOGOPA MIKOPO* (anaogopa kudefault)

Hio 4 ni njia nyingine ya kusema huamini kwenye biashara yako, sabab kama unaogopa mkopo (ambao unaweza pata kwa hadi 10%) ni kwamba una hofu utapoteza dhamana unazoweka.

Siandiki hivi kuwa negative, lengo langu ni kumsaidia mtoa mada sababu nimedeal sana na issue kama hizi
 
Niliapia sitokuja kuongelea kitu chcht serious humu JF zaidi ya pombe na ngono ila ngoja leo nikushauri kitu sababu nimeona sana mabandiko yako na sijui kwa nn yananiangukia

Nimefanya kazi za kuallocate funds kwenye startups kutoka kwenye foundations kadhaa nje na ndani ya nchi. Wengi ni wanasiasa kama wewe(usiishie kusoma hapo, vuta pumzi tuendelee). Wanalenga kutoa first impression kwa maneno mataam lkn biashara zao ni zero. Startups nyingi zinakufa hata kama walipewa funds sababu executives na founders ni wanasiasa tu, wanajua theory ya biashara na maneno mazito ya kutongoza investors ila hawajui kuedesha biashara kutokana, kutumia data, takwimu na saikolojia ili kufanya biashara iwe profitable zaidi.

Siku hizi nikisikia neno startup nataka hadi kutapika. Cheki kuna waghana fln walipata hadi usd 86 million wanajiita DASH ila kampuni limekufa, nenda kwa jirani zako JUMIA wako wp sshv? startups za hapa tz ndo sitozitaja sababu founders lengo lao ni kupata funds wakanunue brevis wajenge nyumba then wafunge biashara.

Sasa mm nakuomba kitu kimoja tu. Takwimu za biashara zako katika makundi haya.

1)Zitakazonifanya NIWEKEZE kwenye biashara yako
2)Zitakazonifanya NISIWEKEZE kwenye biashara yako.

Hapo kwenye takwimu nataka zote ambazo unatumia kwenye biashara yako kama vile customer follow ups, leads to client ratio, stock turnover, na statistics zote (kama una utimamu wa biashara utajua namaanisha zipi)
lkn pia ambatanisha financial statements za toka mwaka ulioanza kufanya business hadi mwaka huu.

Nitumie PM na kama nitapenda ninachokiona nina 15million hapa cash imekaa inasubiri kufanyiwa starehe tu, nitawekeza nusu kwenye biashara yako. Ukiona risk kunitumia nambie nikupe calendar yangu uchague siku tuonane ofisini kwangu, nitakua na cash ww uje na hizo data.

Good luck sweetheart.
Huu ni ukweli usiopingika, actually Startups ni kachimbo kapya ka watu kupigia hela lakini pia sio Founders wote. Kuna baadhi wako smart sana tu kwenye solutions zao, nimekutana nao baadhi, wana visions lakini bahati mbaya wanazokutana nazo baada ya kupata Investors, investors wanakuja kama kutake over na kuanza kurun biashara kama wanavyoona wao kwakuwa wanapower ya capital kitu ambacho kinapelekea mpaka founders visions zinakufa, ukifatilia cases nyingi ziko hivo mpka hata kwa Elon Musk alvoanzisha Paypal. Ila all in all kuna Real people who want to solve real problems na kuna wapigaji kwa mgongo wa Startups na NGOs.
 
Kagusa maeneo yangu

Mimi nikija kuangalia biashara ya mtu naweza jua huyu anatoboa au hatoboi au ni pump and dump scheme. Kkoo pale nimesaidia wengi sana, ila hapa jf hizi fake ids zinatupa freedom ya kuwa wehu na kudharaulika pia
Mmmh kweli mkuu huo utaalamu muhimu sana kuwa nao, umeiva sana kwenye business models?
 
Huu ni ukweli usiopingika, actually Startups ni kachimbo kapya ka watu kupigia hela lakini pia sio Founders wote. Kuna baadhi wako smart sana tu kwenye solutions zao, nimekutana nao baadhi, wana visions lakini bahati mbaya wanazokutana nazo baada ya kupata Investors, investors wanakuja kama kutake over na kuanza kurun biashara kama wanavyoona wao kwakuwa wanapower ya capital kitu ambacho kinapelekea mpaka founders visions zinakufa, ukifatilia cases nyingi ziko hivo mpka hata kwa Elon Musk alvoanzisha Paypal. Ila all in all kuna Real people who want to solve real problems na kuna wapigaji kwa mgongo wa Startups na NGOs.
Ndo maana huyu kaambiwa akachukue mkopo.

Chukua mkopo bakiza ownership yako na control. Lkn kwa nn hawataki mikopo? Mkopo ni mgumu kupata kuliko kuuza shares. Kuuza shares ni rahisi kufanya pump and dump. Kama mtu kweli anaamini kwenye biashara yake (achana na wanaaoanza kabisa) na case ya mleta mada (20m valuation) hakuna sababu yyt ya kukimbia mkopo unayoweza nishawishi nayo unless kwa point nilizosema hapo juu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom